Hosea 3:1-5, Hosea 4:1-19, Hosea 5:1-15 NEN

Hosea 3:1-5

Upatanisho Wa Hosea Na Mkewe

3:1 Hos 1:2; 2Sam 6:19Bwana akaniambia, “Nenda, ukaonyeshe upendo wako kwa mke wako tena, ingawa amependwa na mwingine naye ni mzinzi. Mpende kama Bwana apendavyo Waisraeli, ingawa wanageukia miungu mingine na kupenda mikate mitamu ya zabibu kavu iliyowekwa wakfu.”

Basi nilimnunua huyo mwanamke kwa shekeli kumi na tano3:2 Shekeli 15 za fedha ni sawa na gramu 170. za fedha, pia kwa kiasi kama cha homeri moja na nusu3:2 Homeri moja na nusu ni kama lita 330. ya shayiri. 3:3 Kum 21:23Kisha nilimwambia, “Utaishi nami kwa siku nyingi, hupaswi kuwa kahaba au kuwa na uhusiano wa karibu na mtu yeyote, nami nitaishi na wewe.”

3:4 Hos 2:11; 13:11; Dan 11:31; Amu 18:14-17, 23-24; Mao 2:9; Kum 28:6; Zek 10:2; Kut 25:7Kwa maana Waisraeli wataishi siku nyingi bila kuwa na mfalme wala mkuu, bila kuwa na dhabihu wala mawe matakatifu, bila kisibau wala sanamu. 3:5 1Sam 13:14; Eze 34:23-24; Kum 4:30; Yer 50:4-5; Isa 9:13; 10:20; Hos 5:15; Mik 4:1-2; Za 18:45Baadaye Waisraeli watarudi na kumtafuta Bwana Mungu wao na Daudi mfalme wao. Watakuja wakitetemeka kwa Bwana na kwa baraka zake katika siku za mwisho.

Read More of Hosea 3

Hosea 4:1-19

Shtaka Dhidi Ya Israeli

4:1 Mit 10:21; 24:2; Mik 6:2; Isa 1:3; Ay 10:2; Yer 2:9; 7:28; 51:5; Hos 2:20Sikieni neno la Bwana, enyi Waisraeli,

kwa sababu Bwana analo shtaka

dhidi yenu ninyi mnaoishi katika nchi:

“Hakuna uaminifu, hakuna upendo,

hakuna kumjua Mungu katika nchi.

4:2 Isa 59:3; Hos 5:2; 6:2; 7:1; 11:12; Eze 22:2-9; 1Fal 21:16Kuna kulaani tu, uongo na uuaji,

wizi na uzinzi,

bila kuwa na mipaka,

nao umwagaji damu mmoja

baada ya mwingine.

4:3 Yer 4:25, 28; 9:10; Amo 8:8; Isa 15:6; 33:9; Sef 1:3Kwa sababu hii nchi huomboleza,

wote waishio ndani mwake wanadhoofika,

wanyama wa kondeni, ndege wa angani

na samaki wa baharini wanakufa.

4:4 Kum 17:12; Eze 3:26“Lakini mtu awaye yote na asilete shtaka,

mtu yeyote na asimlaumu mwenzake,

kwa maana watu wako ni kama wale

waletao mashtaka dhidi ya kuhani.

4:5 Eze 7:19; 14:7; Hos 2:2Unajikwaa usiku na mchana,

nao manabii hujikwaa pamoja nawe.

Kwa hiyo nitamwangamiza mama yako:

4:6 Mit 10:21; Hos 2:13; 8:1-12; Mal 2:7-8watu wangu wanaangamizwa

kwa kukosa maarifa,

“Kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa,

mimi nami nitakukataa wewe

usiwe kuhani kwangu mimi;

kwa kuwa umeacha kuijali sheria ya Mungu wako

mimi nami sitawajali watoto wako.

4:7 Hab 2:16; Hos 9:11; 13:6Kadiri makuhani walivyoongezeka,

ndivyo walivyozidi kutenda dhambi dhidi yangu,

walibadilisha utukufu wao kwa kitu cha aibu.

4:8 Isa 56:11; Mik 3:11; Hos 14:1Hujilisha dhambi za watu wangu

na kupendezwa na uovu wao.

4:9 Isa 24:2; Yer 5:31; Hos 8:13; 10:10; 12:2Hata itakuwa: Kama walivyo watu,

ndivyo walivyo makuhani.

Nitawaadhibu wote wawili kwa ajili ya njia zao

na kuwalipa kwa matendo yao.

4:10 Mik 6:14; Isa 55:2; Hos 7:14; 9:17; Eze 22:9; Law 26:26“Watakula lakini hawatashiba;

watajiingiza katika ukahaba

lakini hawataongezeka,

kwa sababu wamemwacha Bwana

na kujiingiza wenyewe

4:11 Isa 28:7; Hos 5:4; Mit 20:1; Law 10:9; 1Sam 25:36katika ukahaba,

divai ya zamani na divai mpya,

ambavyo huondoa ufahamu

4:12 Yer 2:27; Ufu 17:2; Hab 2:19; Isa 44:20; Hes 15:39; Za 73:27wa watu wangu.

Hutaka shauri kutoka kwa sanamu ya mti

nao hujibiwa na fimbo ya mti.

Roho ya ukahaba imewapotosha,

hawana uaminifu kwa Mungu wao.

4:13 Isa 1:28; Hos 2:13; 10:9; Yer 2:20; Amo 7:17; Rum 1:28Wanatoa dhabihu juu ya vilele vya milima

na sadaka za kuteketezwa juu ya vilima,

chini ya mialoni, milibua na miela,

ambako kuna vivuli vizuri.

Kwa hiyo binti zenu wamegeukia ukahaba

na wake za wana wenu uzinzi.

4:14 Mwa 38:21; Hos 9:10; Mit 10:21“Sitawaadhibu binti zenu wakati

wanapogeukia ukahaba,

wala wake za wana wenu

wanapofanya uzinzi,

kwa sababu wanaume wenyewe huandamana na malaya

na kutambikia pamoja na makahaba

wa mahali pa kuabudia miungu:

watu wasiokuwa na ufahamu

wataangamia!

4:15 Hos 9:15; 12:11; Amo 4:4; Yos 7:2“Ingawa umefanya uzinzi, ee Israeli,

Yuda naye asije akawa na hatia.

“Usiende Gilgali,

usipande kwenda Beth-Aveni4:15 Beth-Aveni maana yake Nyumba ya Ubatili (au Uovu), jina lingine la Betheli kwa dhihaka.

Wala usiape,

‘Hakika kama Bwana aishivyo!’

4:16 Isa 5:17; 7:25; Kut 32:9; Yer 31:18Waisraeli ni wakaidi,

kama mtamba wa ngʼombe ambaye ni mkaidi.

Ni jinsi gani basi Bwana anaweza kuwachunga

kama wana-kondoo

katika shamba la majani?

4:17 Mt 15:14Efraimu amejiunga na sanamu,

ondokana naye!

4:18 Mik 3:11; 7:3Hata wakati wamemaliza vileo vyao

wanaendelea na ukahaba wao,

watawala wao hupenda sana

njia za aibu.

4:19 Hos 12:11; 13:15; Isa 1:29Kisulisuli kitawafagilia mbali

na dhabihu zao zitawaletea aibu.

Read More of Hosea 4

Hosea 5:1-15

Hukumu Dhidi Ya Israeli

5:1 Hos 6:9; 9:8; Ay 10:12; Yer 5:26“Sikieni hili, enyi makuhani!

Kuweni wasikivu, enyi Waisraeli!

Sikieni, ee nyumba ya mfalme!

Hukumu hii ni dhidi yenu:

Mmekuwa mtego huko Mispa,

wavu uliotandwa juu ya Tabori.

5:2 Hos 4:2; 9:15Waasi wamezidisha sana mauaji.

Mimi nitawatiisha wote.

5:3 Eze 23:7; Za 90:8; Hos 1:2; 6:10; Amo 5:12Ninajua yote kuhusu Efraimu,

Israeli hukufichika kwangu.

Efraimu, sasa umegeukia ukahaba,

Israeli amenajisika.

5:4 Hos 4:6, 11; 7:10; Yer 4:22“Matendo yao hayawaachii

kurudi kwa Mungu wao.

Roho ya ukahaba imo ndani ya mioyo yao,

hawamkubali Bwana.

5:5 Isa 3:9; Yer 2:19; Hos 7:10Kiburi cha Israeli kinashuhudia dhidi yao;

Waisraeli, hata Efraimu,

wanajikwaa katika dhambi zao;

pia Yuda atajikwaa pamoja nao.

5:6 Mik 6:6-7; Mit 1:28; Mal 1:10; Eze 8:6; Isa 1:26Wakati wanapokwenda na makundi yao

ya kondoo na ngʼombe

kumtafuta Bwana,

hawatampata;

yeye amejiondoa kutoka kwao.

5:7 Isa 1:14; 24:16; Hos 2:4, 11-12; 6:7; Eze 12:28Wao si waaminifu kwa Bwana;

wamezaa watoto haramu.

Sasa sikukuu zao za Mwandamo wa Mwezi

zitawaangamiza wao

pamoja na mashamba yao.

5:8 Amu 19:12; Hos 4:15; 10:9; Isa 10:29; Yos 7:2; Hes 10:2; Yer 4:21“Pigeni tarumbeta huko Gibea,

baragumu huko Rama.

Paza kilio cha vita huko Beth-Aveni,5:8 Beth-Aveni maana yake Nyumba ya Ubatili (au Uovu), jina lingine la Betheli kwa dhihaka.

ongoza, ee Benyamini.

5:9 Isa 37:3; Hos 9:11-17; Isa 46:10; 7:16; Zek 1:6Efraimu ataachwa ukiwa

katika siku ya kuadhibiwa.

Miongoni mwa makabila ya Israeli

ninatangaza lile ambalo halina budi kutukia.

5:10 Kum 19:14; Eze 7:8Viongozi wa Yuda ni kama wale

wanaosogeza mawe ya mpaka.

Nitamwaga ghadhabu yangu juu yao

kama mafuriko ya maji.

5:11 Hos 9:16; Mik 6:16Efraimu ameonewa,

amekanyagwa katika hukumu

kwa kuwa amekusudia kufuatia sanamu.

5:12 Ay 13:28; Isa 51:8; Ay 18:16Mimi ni kama nondo kwa Efraimu,

na kama uozo kwa watu wa Yuda.

5:13 Hes 12:1; Eze 23:5; Mao 5:6; Hos 2:7; Yer 30:12; Isa 7:16; 3:7“Wakati Efraimu alipoona ugonjwa wake,

naye Yuda vidonda vyake,

ndipo Efraimu alipogeukia Ashuru,

na kuomba msaada kwa mfalme mkuu.

Lakini hawezi kukuponya,

wala hawezi kukuponya vidonda vyako.

5:14 Ay 10:16; Yer 4:7; Kum 32:39; Mik 5:8; Amo 3:4Kwa maana nitakuwa kama simba kwa Efraimu,

kama simba mkubwa kwa Yuda.

Nitawararua vipande vipande na kuondoka;

nitawachukua mbali,

na hakuna wa kuwaokoa.

5:15 Hes 21:7; Za 24:6; 50:15; Yer 2:27; Eze 20:43; Isa 18:4; 64:9Kisha nitarudi mahali pangu

mpaka watakapokubali kosa lao.

Nao watautafuta uso wangu;

katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.”

Read More of Hosea 5