Hosea 10:1-15, Hosea 11:1-12 NEN

Hosea 10:1-15

10:1 Eze 15:2; 1Fal 14:23; Hos 4:7; 8:11; 12:11; 13:15Israeli alikuwa mzabibu uliostawi sana,

alijizalia matunda mwenyewe.

Kadiri matunda yake yalivyoongezeka,

alijenga madhabahu zaidi;

kadiri nchi yake ilivyostawi,

alipamba mawe yake ya ibada.

10:2 1Fal 18:21; Hos 13:16; Mik 5:13Moyo wao ni mdanganyifu,

nao sasa lazima wachukue hatia yao.

Bwana atabomoa madhabahu zao

na kuharibu mawe yao ya ibada.

10:3 Mik 4:9Kisha watasema, “Hatuna mfalme

kwa sababu hatukumheshimu Bwana.

Lakini hata kama tungelikuwa na mfalme,

angeweza kutufanyia nini?”

10:4 Hos 4:2; Eze 17:19; Amo 5:7; 6:12; Hos 4:2; Eze 17:19; Amo 5:7; 6:12Wanaweka ahadi nyingi,

huapa viapo vya uongo

wanapofanya mapatano;

kwa hiyo mashtaka huchipuka

kama magugu ya sumu

katika shamba lililolimwa.

10:5 Hos 5:8; 8:5-6; 2Fal 23:5; Sef 1:4; Amu 18:17-18; 1Fal 12:28; Kut 32:4; Isa 44:17-20Watu wanaoishi Samaria huogopa

kwa ajili ya sanamu ya ndama ya Beth-Aveni.10:5 Beth-Aveni maana yake Nyumba ya Ubatili (au Uovu), jina lingine la Betheli kwa dhihaka.

Watu wake wataiombolezea,

vivyo hivyo kuhani wake wa kuabudu sanamu,

wale waliokuwa wamefurahia fahari yake,

kwa sababu itaondolewa kutoka kwao

kwenda uhamishoni.

10:6 2Fal 16:7; Hos 4:7; 5:13; 11:5; Isa 30:3; Amu 3:15; Yer 48:13Itachukuliwa kwenda Ashuru

kama ushuru kwa mfalme mkuu.

Efraimu atafedheheshwa;

Israeli ataaibika kwa ajili ya sanamu zake za mti.

10:7 Hos 13:11; 10:15Samaria na mfalme wake wataelea

kama kijiti juu ya uso wa maji.

10:8 1Fal 12:28-30; Hos 9:6; Kum 9:21; Ufu 6:16; Isa 32:13; Amo 3:14-15; 7:9; Ay 30:6; Eze 6:6; Lk 23:30Mahali pa kuabudia sanamu pa uovu10:8 Yaani Aveni kwa Kiebrania, kumaanisha Beth-Aveni, jina lingine la Betheli kwa dhihaka. pataharibiwa:

ndiyo dhambi ya Israeli.

Miiba na mibaruti itaota

na kufunika madhabahu zao.

Kisha wataiambia milima, “Tufunikeni!”

na vilima, “Tuangukieni!”

10:9 Hos 5:8; Ay 7:11“Tangu siku za Gibea, mmetenda dhambi, ee Israeli,

huko ndiko mlikobaki.

Je, vita havikuwapata

watenda mabaya huko Gibea?

10:10 Eze 5:13; Hos 4:9; Amo 8:14Wakati nitakapopenda, nitawaadhibu;

mataifa yatakusanywa dhidi yao

ili kuwaweka katika vifungo

kwa ajili ya dhambi zao mbili.

10:11 Yer 15:12; 31:18Efraimu ni mtamba wa ngʼombe aliyefundishwa

ambaye hupenda kupura,

hivyo nitamfunga nira

juu ya shingo yake nzuri.

Nitamwendesha Efraimu,

Yuda lazima alime,

naye Yakobo lazima avunjavunje

mabonge ya udongo.

10:12 Mit 11:18; Yak 3:18; Hos 12:6; Isa 19:22; 45:8; Mhu 11:1; Yer 4:3Jipandieni wenyewe haki,

vuneni matunda ya upendo usio na kikomo,

vunjeni ardhi yenu isiyolimwa;

kwa kuwa ni wakati wa kumtafuta Bwana,

mpaka atakapokuja

na kuwanyeshea juu yenu haki.

10:13 Ay 4:8; Gal 6:7-8; Za 33:16; Mit 22:8; Hos 7:3; 8:7; 11:12Lakini mmepanda uovu,

mkavuna ubaya,

mmekula tunda la udanganyifu.

Kwa sababu mmetegemea nguvu zenu wenyewe

na wingi wa mashujaa wenu,

10:14 Isa 13:16; 17:3; Mik 5:11; Hos 13:16; 2Fal 17:3mngurumo wa vita utainuka dhidi ya watu wako,

ili kwamba ngome zako zote zitaharibiwa:

kama Shalmani alivyoharibu Beth-Arbeli katika siku ile ya vita,

wakati mama pamoja na watoto wao

walipotupwa kwa nguvu ardhini.

10:15 Hos 10:7Ndivyo itakavyotokea kwako, ee Betheli,

kwa sababu uovu wako ni mkuu.

Siku ile itakapopambazuka,

mfalme wa Israeli ataharibiwa kabisa.

Read More of Hosea 10

Hosea 11:1-12

Upendo Wa Mungu Kwa Israeli

11:1 Kut 4:22; Mt 2:15; Yer 2:2; Eze 16:22; Hos 12:9; 13:4“Wakati Israeli alipokuwa mtoto, nilimpenda,

nilimwita mwanangu kutoka Misri.

11:2 Hos 2:13; 4:13; 2Fal 17:15; Isa 65:7; Yer 18:15Lakini kadiri nilivyomwita Israeli,

ndivyo walivyokwenda mbali nami.

Walitoa dhabihu kwa Mabaali

na kufukiza uvumba kwa vinyago.

11:3 Kum 1:31; 32:11; Kut 15:26; Yer 30:17Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea,

nikiwashika mikono;

lakini hawakutambua

kuwa ni mimi niliyewaponya.

11:4 Yer 31:2-3, 20; Law 26:13; Kut 16:32; Za 78:25Niliwaongoza kwa kamba za huruma ya kibinadamu,

kwa vifungo vya upendo;

niliondoa nira shingoni mwao

nami nikainama kuwalisha.

11:5 Yer 8:4-6; Hos 7:16; 10:6; Kut 13:17“Je, hawatarudi Misri,

nayo Ashuru haitawatawala

kwa sababu wamekataa kutubu?

11:6 Hos 13:16; Mao 2:9Panga zitametameta katika miji yao,

zitaharibu makomeo ya malango yao

na kukomesha mipango yao.

11:7 Yer 3:6-7; 8:5; Isa 26:10Watu wangu wamedhamiria kuniacha.

Hata kama wakimwita Yeye Aliye Juu Sana,

kwa vyovyote hatawainua.

11:8 Mwa 14:8; 19:25; Hos 6:4; Mao 3:32; Yer 7:29; Za 25:6; 1Fal 3:26“Efraimu, ninawezaje kukuacha?

Ee Israeli, ninawezaje kukutoa?

Nitawezaje kukutendea kama Adma?

Nitawezaje kukufanya kama Seboimu?

Moyo wangu umegeuka ndani yangu,

huruma zangu zote zimeamshwa.

11:9 Kum 13:17Sitatimiza hasira yangu kali,

wala sitageuka na kumharibu Efraimu.

Kwa kuwa mimi ndimi Mungu,

wala si mwanadamu,

Aliye Mtakatifu miongoni mwenu.

Sitakuja kwa ghadhabu.

11:10 Hos 3:5; 6:1-3; Isa 31:4; 42:13; Za 18:45Watamfuata Bwana;

atanguruma kama simba.

Wakati angurumapo,

watoto wake watakuja wakitetemeka

kutoka magharibi.

11:11 Isa 11:11; Mwa 8:8; Eze 28:26; 34:25-28Watakuja wakitetemeka

kama ndege wakitoka Misri,

kama hua wakitoka Ashuru.

Nitawakalisha katika nyumba zao,”

asema Bwana.

Dhambi Ya Israeli

11:12 Hos 4:2; 10:13; Kum 7:9Efraimu amenizunguka kwa uongo,

nyumba ya Israeli kwa udanganyifu.

Naye Yuda ni mkaidi dhidi ya Mungu,

hata kinyume cha yule mwaminifu Aliye Mtakatifu.

Read More of Hosea 11