Hosea 1:1-11, Hosea 2:1-23 NEN

Hosea 1:1-11

1:1 Mik 1:1; Isa 1:1; 2Fal 13:13; 14:12; 1Nya 3:12-13; Yer 1:2; 2Fal 14:21Neno la Bwana lililomjia Hosea mwana wa Beeri wakati wa utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda, na wakati wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi, mfalme wa Israeli.

Mke Wa Hosea Na Watoto

1:2 Amu 2:17; Yer 3:14; Hos 2:5; 3:1; Yer 3:1; Kum 31:16Wakati Bwana alipoanza kuzungumza kupitia Hosea, Bwana alimwambia, “Nenda ukajitwalie mwanamke wa uzinzi na watoto wa uzinzi, kwa sababu nchi ina hatia ya uzinzi wa kupindukia kwa kumwacha Bwana.” 1:3 Hos 1:6Kwa hiyo alimwoa Gomeri binti Diblaimu, naye akachukua mimba na kumzalia Hosea mwana.

1:4 1Sam 29:1; 1Fal 18:45; 2Fal 10:1-14; Hos 2:22Kisha Bwana akamwambia Hosea, “Mwite Yezreeli,1:4 Yezreeli maana yake Mungu hupanda. kwa kuwa kitambo kidogo nitaiadhibu nyumba ya Yehu kwa ajili ya mauaji ya kule Yezreeli, nami nitaukomesha ufalme wa Israeli. 1:5 Yos 15:56; 1Sam 29:1; 2Fal 15:29Katika siku ile nitavunja upinde wa Israeli katika Bonde la Yezreeli.”

1:6 Hos 2:4, 23; 1:6Gomeri akachukua tena mimba akamzaa binti. Kisha Bwana akamwambia Hosea, “Mwite Lo-Ruhama,1:6 Lo-Ruhama maana yake Sio mpenzi wangu. kwa maana sitaonyesha tena upendo kwa nyumba ya Israeli, kwamba nisije kabisa nikawasamehe. 1:7 Za 44:6; Zek 2:6Hata hivyo nitaonyesha upendo kwa nyumba ya Yuda, nami nitawaokoa si kwa upinde, upanga au vita, wala kwa farasi na wapanda farasi, bali kwa njia ya Bwana Mungu wao.”

Baada ya Gomeri kumwachisha Lo-Ruhama kunyonya, Gomeri alipata mwana mwingine. 1:9 Eze 11:19-20; 1Pet 2:10Kisha Bwana akasema, “Mwite Lo-Ami1:9 Lo-Ami maana yake Sio watu wangu. kwa maana ninyi si watu wangu, nami si Mungu wenu.

1:10 Mwa 22:17; Yer 33:22; Rum 9:26; Hos 2:23; Hes 23:10; Yos 3:10“Hata hivyo Waisraeli watakuwa kama mchanga kando ya bahari, ambao hauwezi kupimika wala kuhesabiwa. Mahali pale walipoambiwa, ‘Ninyi si watu wangu,’ wao wataitwa ‘wana wa Mungu aliye hai.’ 1:11 Isa 11:12-13; Yer 23:5-8; 30:9; Eze 37:15-28Watu wa Yuda na watu wa Israeli wataunganishwa tena, nao watamchagua kiongozi mmoja nao watakwea watoke katika nchi, kwa kuwa siku ya Yezreeli itakuwa kuu sana.

Read More of Hosea 1

Hosea 2:1-23

2:1 1Pet 2:10; Hos 2:5“Waambie ndugu zako, ‘Watu wangu,’ na pia waambie dada zako, ‘Wapendwa wangu.’

Israeli Aadhibiwa Na Kurudishwa

2:2 Isa 1:21; 50:1; Eze 16:25; 23:45; Hos 4:5“Mkemeeni mama yenu, mkemeeni,

kwa maana yeye si mke wangu,

nami si mume wake.

Aondoe sura ya uzinzi katika uso wake

na uzinzi kati ya matiti yake.

2:3 Eze 16:4, 37; 19:13; Isa 32:13-14Kama sivyo nitamvua nguo zake awe uchi

na kumwacha uchi kama siku ile aliyozaliwa.

Nitamfanya kama jangwa,

nitamgeuza awe nchi ya kiu,

nami nitamuua kwa kiu.

2:4 Eze 8:18; Hos 1:6; 5:7Sitaonyesha upendo wangu kwa watoto wake,

kwa sababu ni watoto wa uzinzi.

2:5 Yer 3:6; 44:17-18; Hos 1:2Mama yao amekosa uaminifu

na amewachukua mimba katika aibu.

Gomeri alisema, ‘Nitawaendea wapenzi wangu,

ambao hunipa chakula changu

na maji yangu,

sufu yangu na kitani yangu, mafuta yangu

na kinywaji changu.’

2:6 Ay 3:23; 19:8; Mao 3:9Kwa hiyo mimi Mungu nitaizuia njia yake

kwa vichaka vya miiba,

nitamjengea ukuta ili kwamba

asiweze kutoka.

2:7 Hos 5:13; Yer 3:1; Eze 16:8; Isa 54:5Gomeri atawafuatia wapenzi wake lakini hatawapata;

atawatafuta lakini hatawapata.

Kisha atasema,

‘Nitarudi kwa mume wangu kama kwanza,

kwa maana nilikuwa na hali njema zaidi

kuliko sasa.’

2:8 Eze 16:15-19; Hes 18:12; Kum 8:18; Hos 8:4Gomeri hajakubali kuwa mimi ndiye

niliyempa nafaka, divai mpya na mafuta,

niliyemwongezea fedha na dhahabu waliyoitumia

kwa kumtumikia Baali.

2:9 Hos 8:7; 9:2“Kwa hiyo nitachukua nafaka yangu wakati itakapokomaa

na divai yangu mpya wakati itakapokuwa tayari.

Nitamnyangʼanya sufu yangu na kitani yangu

iliyokusudiwa kufunika uchi wake.

2:10 Eze 16:37; 23:10; Yer 13:26Basi sasa nitaufunua ufisadi wake

mbele ya wapenzi wake;

hakuna yeyote atakayemtoa

mikononi mwangu.

2:11 Isa 1:14; 24:8; Amo 5:21; 8:10; Yer 7:34; 16:9; Hos 9:5Nitakomesha furaha na macheko yake yote:

sikukuu zake za mwaka,

sikukuu za Miandamo ya Mwezi,

siku zake za Sabato,

sikukuu zake zote zilizoamriwa.

2:12 Isa 5:6; 7:23; Yer 8:13; Hos 5:7; 13:8Nitaiharibu mizabibu yake na mitini yake,

ambayo alisema yalikuwa malipo yake

kutoka kwa wapenzi wake;

nitaifanya kuwa kichaka,

nao wanyama pori wataila.

2:13 Yer 7:9; Hos 4:13; 8:14; 11:2; 13:6; Eze 16:17; 23:40; Isa 65:7Nitamwadhibu kwa ajili ya siku

alizowafukizia uvumba Mabaali;

alipojipamba kwa pete

na kwa vito vya thamani,

na kuwaendea wapenzi wake,

lakini mimi alinisahau,”

asema Bwana.

2:14 Eze 19:14“Kwa hiyo sasa nitamshawishi;

nitamwongoza hadi jangwani

na kuzungumza naye kwa upole.

2:15 Yos 7:24-26; Kut 15:1-18; Eze 16:22; 28:26; Hos 12:9; 1Kor 13:13Huko nitamrudishia mashamba yake ya mizabibu,

nami nitalifanya Bonde la Akori2:15 Akori maana yake ni Taabu.

mlango wa matumaini.

Huko ataimba kama alivyofanya katika siku za ujana wake,

kama siku zile alizotoka Misri.

2:16 Isa 54:5“Katika siku ile,” asema Bwana,

“utaniita mimi ‘Mume wangu’;

hutaniita tena mimi ‘Bwana wangu.’

2:17 Kut 23:13; Za 16:4; Yer 23:7; Zek 13:2Nitaondoa majina ya Mabaali kutoka midomoni mwake,

wala hataomba tena kwa majina yao.

2:18 Ay 5:22-23; Za 49:6; Zek 9:10; Eze 34:25; Yer 23:6Katika siku ile nitafanya Agano kwa ajili yao

na wanyama wa kondeni, na ndege wa angani,

na viumbe vile vitambaavyo ardhini.

Upinde, upanga na vita,

nitaondolea mbali katika nchi,

ili kwamba wote waweze kukaa salama.

2:19 Isa 1:27; 62:4; 54:8; 2Kor 11:2Nitakuposa uwe wangu milele;

nitakuposa kwa uadilifu na haki,

kwa upendo na huruma.

2:20 Yer 31:34; Hos 4:1; 6:6; 13:4; Eze 16:8Nitakuposa kwa uaminifu,

nawe utamkubali Bwana.

2:21 Zek 8:12; Mal 3:10-11; Isa 55:10“Katika siku ile nitajibu,”

asema Bwana,

“nitajibu kwa anga,

nazo anga zitajibu kwa nchi;

2:22 Yer 31:12; Yoe 2:19; Hos 14:7; Eze 36:29-30nayo nchi itajibu kwa nafaka,

divai mpya na mafuta,

navyo vitajibu kwa Yezreeli.

2:23 Yer 29:12; 31:27; Isa 19:25; Hos 1:10; Rum 9:25; Zek 13:9; 1Pet 2:10Nitampanda katika nchi kwa ajili yangu mwenyewe;

nami nitaonyesha pendo langu kwake

yule ambaye nilimwita, ‘Si mpenzi wangu.2:23 Kiebrania ni Lo-Ruhama.

Nitawaambia wale walioitwa, ‘Sio watu wangu,’2:23 Kiebrania ni Lo-Ami.

‘Ninyi ni watu wangu’;

nao watasema, ‘Wewe ndiwe Mungu wangu.’ ”

Read More of Hosea 2