Waebrania 7:11-28 NEN

Waebrania 7:11-28

Yesu Mfano Wa Melkizedeki

7:11 Ebr 7:18-19; 8:7; 10:1; 7:17; 5:6; Gal 2:21Kama ukamilifu ungeweza kupatikana kwa njia ya ukuhani wa Walawi (kwa kuwa katika msingi huo, sheria ilitolewa kwa watu), kwa nini basi imekuwepo haja ya kuja kuhani mwingine: kuhani kwa mfano wa Melkizedeki, wala si kwa mfano wa Aroni? Kwa kuwa yanapotokea mabadiliko ya ukuhani, pia lazima yawepo mabadiliko ya sheria. 7:13 Ebr 7:11, 14Yeye ambaye mambo haya yanasemwa alikuwa wa kabila lingine, na hakuna mtu wa kabila hilo aliyewahi kuhudumu katika madhabahu. 7:14 Isa 11:1; Mt 1:3; 2:6; Lk 3:33; Ufu 5:5Kwa maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda, tena kuhusu kabila hilo Mose hakusema lolote kwa habari za makuhani. Tena hayo tuliyosema yako wazi zaidi kama akitokea kuhani mwingine kama Melkizedeki, yeye ambaye amefanyika kuhani si kwa misingi ya sheria kama ilivyokuwa kwa baba zake, bali kwa misingi ya uwezo wa uzima usioharibika. 7:17 Za 110:4; Ebr 7:21; 5:6, 10; 6:20Kwa maana imeshuhudiwa kwamba:

“Wewe ni kuhani milele,

kwa mfano wa Melkizedeki.”

7:18 Rum 8:3; Gal 4:9Kwa upande mmoja, ile amri ya mwanzo isiyofaa na dhaifu imebatilishwa 7:19 Ebr 7:11; 9:9; 10:1; Rum 3:20; 7:7, 8; Gal 3:21; Yak 4:8(kwa maana sheria haikufanya kitu chochote kuwa kikamilifu). Kwa upande mwingine, tumeletewa tumaini lililo bora zaidi ambalo linatuleta karibu na Mungu.

Nalo tumaini hilo halikutolewa pasipo kiapo! Wengine walikuwa makuhani pasipo kiapo chochote, 7:21 Za 110:4; Hes 23:19; 1Sam 15:29; Mal 3:6; Rum 1:29; Ebr 5:6lakini Yesu alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alimwambia:

Bwana ameapa

naye hatabadilisha mawazo yake:

‘Wewe ni kuhani milele.’ ”

7:22 Ebr 8:6; 9:15; 12:24; Lk 22:20Kwa ajili ya kiapo hiki, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.

Basi pamekuwepo na makuhani wengi wa aina hiyo, kwa kuwa kifo kiliwazuia kuendelea na huduma yao ya ukuhani. 7:24 Ebr 7:28Lakini kwa sababu Yesu anaishi milele, anao ukuhani wa kudumu. 7:25 Rum 11:14; 8:34; Ebr 7:19; 1Tim 2:5; 1Yn 2:1Kwa hiyo anaweza kuwaokoa kabisa wale wanaomjia Mungu kupitia kwake, kwa sababu yeye adumu daima kuomba kwa ajili yao.

7:26 Ebr 4:15; 8:1; Efe 1:20; 4:10; 2Kor 5:21Kwa kuwa ilitupasa tuwe na Kuhani Mkuu wa namna hii, yaani, aliye mtakatifu, asiye na lawama, asiye na dosari, aliyetengwa na wenye dhambi na kuinuliwa juu ya mbingu. 7:27 Ebr 5:1, 3; Rum 6:10; Ebr 9:12, 26, 28; 10:10; 1Pet 3:18; Efe 5:2Yeye hahitaji kutoa dhabihu siku kwa siku kwa ajili ya dhambi, kwanza kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi za watu kama wale makuhani wakuu wengine. Yeye alitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zao mara moja tu, alipojitoa mwenyewe. 7:28 Ebr 5:2; 1:2; 2:10Kwa kuwa sheria huwaweka makuhani wakuu watu ambao ni dhaifu; lakini lile neno la kiapo, lililokuja baada ya sheria, lilimweka Mwana, ambaye amefanywa kuwa mkamilifu milele.

Read More of Waebrania 7