Waebrania 5:11-14, Waebrania 6:1-12 NEN

Waebrania 5:11-14

Wito Wa Kukua Kiroho

5:11 Yn 16:12; 2Pet 3:16; Mt 13:15Tunayo mengi ya kusema kuhusu habari ya ukuhani huu, lakini ni vigumu kuyaeleza, kwa sababu ninyi ni wazito wa kuelewa. 5:12 Ebr 6:1; 1Kor 3:2; 1Pet 2:2Kwa hakika, ingawa mpaka wakati huu ingewapasa kuwa walimu, bado mnahitaji mtu wa kuwafundisha tena hatua za awali za kweli ya Neno la Mungu. Mnahitaji maziwa, wala si chakula kigumu! 5:13 1Kor 13:11; 14:20; Efe 4:14; 1Pet 2:2Kwa maana yeyote aishiye kwa kunywa maziwa bado yeye ni mtoto mchanga, hana ujuzi katika mafundisho kuhusu neno la haki. 5:14 1Kor 2:6; Isa 7:15; 1Kor 2:14, 15Lakini chakula kigumu ni kwa ajili ya watu wazima, ambao kwa kujizoeza wamejifunza kupambanua kati ya mema na mabaya.

Read More of Waebrania 5

Waebrania 6:1-12

Hatari Ya Kuanguka

6:1 Flp 3:12, 13, 14; Ebr 5:12; 9:14Kwa hiyo, tukiachana na mafundisho yale ya awali kuhusu Kristo na tukisonga mbele ili tufikie utimilifu, sio kuweka tena msingi wa mafundisho ya kuzitubia kazi zisizo na uhai na imani katika Mungu, 6:2 Yn 3:25; Mdo 6:6; 2:24; 17:18, 22mafundisho kuhusu aina za ubatizo, kuwekea watu mikono, ufufuo wa wafu, na hukumu ya milele. 6:3 Mdo 18:21; 1Kor 4:19Mungu akitujalia tutafanya hivyo.

6:4 Ebr 10:22; Efe 2:8; Gal 3:2; Mt 12:31, 32; 2Pet 2:20, 21; 1Yn 5:16; Yn 4:10; 6:32Kwa kuwa ni vigumu kwa wale ambao wakati fulani walishapata nuru, ambao walishaonja kipawa cha mbinguni, ambao wamekwisha kushiriki katika Roho Mtakatifu, 6:5 Ebr 2:5; 4:12; Za 34:8ambao wameonja uzuri wa Neno la Mungu na nguvu za wakati ujao, 6:6 2Pet 2:21; 1Yn 5:16; Mt 4:3; Ebr 10:29kisha wakianguka, kuwarejesha tena katika toba. Kwa kuwa wanamsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili na kumdhalilisha hadharani, nayo ikawa hasara kwao.

6:7 Za 65:10; Mwa 1:11, 12Ardhi ile ipokeayo mvua inyeshayo juu yake mara kwa mara hutoa mazao yanayowanufaisha wale ambao kwa ajili yao yalimwa, nayo nchi hiyo hupokea baraka kutoka kwa Mungu. 6:8 Mwa 3:17, 18; Isa 5:6; 27:4Lakini ardhi ikizaa miiba na mibaruti, haina thamani na iko hatarini ya kulaaniwa. Mwisho wake ni kuchomwa moto.

6:9 1Kor 10:14Ingawa tunasema hivi, ndugu zangu wapendwa, kwa upande wenu tuna hakika ya mambo mema zaidi, mambo yale yahusuyo wokovu. 6:10 Mt 10:40, 42; 1The 1:3Mungu si mdhalimu: yeye hataisahau kazi yenu na upendo ule mlioonyesha kwa ajili yake katika kuwahudumia watakatifu na hata sasa mnaendelea kuwahudumia. 6:11 Ebr 3:6, 14; Kol 2:2; Flp 1:6Nasi twataka kila mmoja wenu aonyeshe bidii iyo hiyo ili mpate kujua uhakika kamili wa lile tumaini mpaka mwisho, 6:12 Ebr 13:7; 10:36; 2The 1:4; Yak 1:3; Ufu 13:10; 14:12ili msije mkawa wavivu, bali mpate kuwaiga wale ambao kwa imani na saburi hurithi zile ahadi.

Read More of Waebrania 6