Waebrania 4:14-16, Waebrania 5:1-10 NEN

Waebrania 4:14-16

Yesu Kristo Kuhani Mkuu Kuliko Wote

4:14 Ebr 2:17; 6:20; 8:1; 9:2; Mt 4:3; Ebr 3:1Kwa kuwa tunaye Kuhani Mkuu kuliko wote ambaye ameingia mbinguni, Yesu Mwana wa Mungu, basi na tushikamane sana kwa uthabiti na ule ukiri wa imani yetu. 4:15 Ebr 2:17, 18; 2Kor 5:21; Isa 53:3; Lk 22:28; 1Pet 2:22; 1Yn 3:5; Ebr 7:26Kwa kuwa hatuna Kuhani Mkuu asiyeweza kuchukuliana na sisi katika udhaifu wetu, lakini tunaye mmoja ambaye alijaribiwa kwa kila namna, kama vile sisi tujaribiwavyo: lakini yeye hakutenda dhambi. 4:16 Ebr 7:19; Efe 2:18; 3:12; Ebr 10:19Basi na tukikaribie kiti cha rehema kwa ujasiri, ili tupewe rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

Read More of Waebrania 4

Waebrania 5:1-10

5:1 Ebr 2:17; 8:3; 9:9-27Kwa maana kila kuhani mkuu anayechaguliwa miongoni mwa wanadamu anawekwa kuwawakilisha kwa mambo yanayomhusu Mungu, ili apate kutoa matoleo na dhabihu kwa ajili ya dhambi. 5:2 Ebr 2:18; 4:15; 7:28Kwa kuwa yeye mwenyewe ni dhaifu, aweza kuwachukulia kwa upole wale wasiojua na kupotoka. 5:3 Law 4:3; 9:7; 16:6; 15:16, 17; Ebr 7:27; 9:7Hii ndiyo sababu inampasa kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe na vivyo hivyo kwa ajili ya dhambi za watu. 5:4 Kut 28:1; Hes 14:40; 18:7; 2Nya 26:18; 1Nya 23:13; Yn 3:27Hakuna anayejitwalia heshima hii mwenyewe; ni lazima aitwe na Mungu, kama vile Aroni alivyoitwa. 5:5 Yn 8:54; Ebr 2:17; 1:5; 1:1; Za 2:7; Mdo 13:33Pia Kristo hakujitwalia utukufu yeye mwenyewe wa kuwa Kuhani Mkuu, bali Mungu alimwambia,

“Wewe ni Mwanangu;

leo mimi nimekuzaa.”

5:6 Ebr 5:10; 6:20; 7:2-22; 7:17, 21; Mwa 14:18; Za 110:4Pia mahali pengine asema,

“Wewe ni kuhani milele,

kwa mfano wa Melkizedeki.”

5:7 Lk 22:41-44; 23:46; Mt 27:46; Za 22:24; Mk 14:36Katika siku za maisha ya Yesu hapa duniani, alimtolea maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, yeye awezaye kumwokoa na mauti, naye Mungu akamsikia kwa sababu ya kutii kwake kwa unyenyekevu. 5:8 Ebr 1:2; 3:6; Flp 2:8Ingawa alikuwa Mwana, alijifunza utiifu kutokana na mateso aliyoyapata, 5:9 Ebr 2:10; 11:40; Isa 45:17; Yn 17:1, 5na akiisha kukamilishwa, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii. 5:10 Ebr 5:6; 6:20; 2:17Naye amewekwa na Mungu kuwa Kuhani Mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.

Read More of Waebrania 5