Waebrania 12:14-29 NEN

Waebrania 12:14-29

Onyo Dhidi Ya Kuikataa Neema Ya Mungu

12:14 Rum 14:19; 6:22; Mt 5:8Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu, ambao bila kuwa nao hakuna mtu atakayemwona Bwana. 12:15 Gal 5:4; Ebr 3:12; 4:1; Kum 29:18Angalieni sana mtu yeyote asiikose neema ya Mungu na kwamba shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo. 12:16 1Kor 6:18Angalieni miongoni mwenu asiwepo mwasherati au mtu asiyemcha Mungu kama Esau, ambaye kwa ajili ya mlo mmoja aliuza haki ya uzaliwa wake wa kwanza. 12:17 Mwa 27:30-40Baadaye kama mnavyofahamu, alipotaka kurithi ile baraka, alikataliwa, maana hakupata nafasi ya kutubu, ingawa aliitafuta kwa machozi.

12:18 Kut 19:12-22; 20:18; Kum 4:11Hamjaufikia mlima ule uwezao kuguswa na ambao unawaka moto; wala kwenye giza, utusitusi na dhoruba; 12:19 Kut 20:18; Kum 4:12; Kut 20:19; Kum 5:5, 25; 18:16kwenye mlio wa tarumbeta, au kwenye sauti isemayo maneno ya kutisha kiasi ambacho wale walioisikia waliomba wasiambiwe neno jingine zaidi, 12:20 Kut 19:12, 13kwa sababu hawangeweza kustahimili neno lile lililoamriwa: “Hata kama mnyama atagusa mlima huu, atapigwa mawe.” 12:21 Kum 9:19Waliyoyaona yalikuwa ya kutisha kiasi kwamba Mose alisema, “Ninatetemeka kwa hofu.”

12:22 Isa 24:23; 60:14; Ufu 14:1; Gal 4:26; Ebr 11:10; 13:14; Mit 16:16Lakini ninyi mmekuja Mlima Sayuni, Yerusalemu ya mbinguni, mji wa Mungu aliye hai. Mmekuja penye kusanyiko kubwa la malaika maelfu kwa maelfu wasiohesabika wanaoshangilia, kwenye kanisa la wazaliwa wa kwanza wa Mungu, ambao majina yao yameandikwa mbinguni. Mmekuja kwa Mungu, mhukumu wa watu wote, kwenye roho za wenye haki waliokamilishwa, 12:24 Gal 3:20; Ebr 9:19; 10:22; 1Pet 1:2; Mwa 4:10; Ebr 11:4kwa Yesu mpatanishi wa agano jipya, na kwa damu iliyonyunyizwa, ile inenayo mambo mema kuliko damu ya Abeli.

12:25 Ebr 3:12; 1:1; 8:5; 11:7; 2:2, 3; 10:29; Kum 18:19Angalieni, msije mkamkataa yeye anenaye. Ikiwa wao hawakuepuka adhabu walipomkataa yeye aliyewaonya hapa duniani, sisi je, tutaokokaje tusipomsikiliza yeye anayetuonya kutoka mbinguni? 12:26 Kut 19:18; Hag 2:6Wakati ule sauti yake ilitetemesha dunia, lakini sasa ameahidi, “Kwa mara moja tena nitatetemesha si nchi tu bali na mbingu pia.”

12:27 Isa 34:4; 54:10; 1Kor 7:31; Ebr 1:11; 2Pet 3:10; 1Yn 2:17Maneno haya “kwa mara moja tena” yanaonyesha kuondoshwa kwa vile vitu vinavyoweza kutetemeshwa, yaani vile vitu vilivyoumbwa, kwa kusudi vile tu visivyoweza kutetemeshwa vibaki.

12:28 Za 15:5; Dan 2:44; Mal 2:5; 4:2; Ebr 13:15Kwa hiyo, kwa kuwa tunapokea ufalme ambao hauwezi kutetemeshwa, basi na tuwe na shukrani, na hivyo tumwabudu Mungu kwa namna inayompendeza, kwa unyenyekevu na uchaji, 12:29 Kut 24:17; Kum 4:24; 9:3; Za 97:3; Isa 33:14; 1The 1:7kwa kuwa “Mungu wetu ni moto ulao.”

Read More of Waebrania 12