Waebrania 10:19-39 NEN

Waebrania 10:19-39

Wito Wa Kuvumilia

10:19 Efe 3:12; Law 16:2; Efe 2:18; Ebr 9:8, 12, 25Kwa hiyo, ndugu zangu, kwa kuwa tunao ujasiri wa kupaingia Patakatifu pa Patakatifu kwa damu ya Yesu, 10:20 Ebr 9:8; 6:19; 9:3kwa njia mpya iliyo hai tuliyofunguliwa kwa ajili yetu kupitia kwenye lile pazia, yaani, mwili wake, 10:21 Ebr 2:17; 3:6basi kwa kuwa tunaye Kuhani Mkuu juu ya nyumba ya Mungu, 10:22 Ebr 10:1; 7:19; 3:12; Yak 1:6; 1Yn 3:21; Eze 36:25; 2Kor 7:1; 1Pet 1:2; Mdo 22:16sisi na tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu kwa imani timilifu, mioyo yetu ikiwa imenyunyizwa damu ya Kristo na kuwa safi kutokana na dhamiri mbaya nayo miili yetu ikiwa imeoshwa kwa maji safi. 10:23 Ebr 3:6; 3; 1; 1Kor 1:9Tushike kwa uthabiti lile tumaini la ukiri wetu bila kuyumbayumba, kwa maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu. 10:24 Tit 2:14Tuangaliane na kuhimizana sisi kwa sisi katika upendo na katika kutenda mema. 10:25 Mdo 2:42; Ebr 3:13; 1Kor 3:13Wala tusiache kukutana pamoja, kama wengine walivyo na desturi, bali tuhimizane sisi kwa sisi kadiri tuonavyo Siku ile inakaribia.

10:26 Kut 21:14; Hes 15:30; Ebr 5:2; 6:4-8; 2Pet 2:20; 1Tim 2:4Kama tukiendelea kutenda dhambi kwa makusudi baada ya kupokea ufahamu wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi. 10:27 Isa 26:11; 2The 1:7; Ebr 9:27; 12:29Lakini kinachobaki ni kungoja kwa hofu hukumu ya moto uwakao, utakaowaangamiza adui za Mungu. 10:28 Kum 17:6, 7; Mt 18:16; Ebr 2:2; Yn 8:17Yeyote aliyeikataa sheria ya Mose alikufa pasipo huruma kwa ushahidi wa watu wawili au watatu. 10:29 Ebr 2:3; 12:25; 1Kor 11:29; Mt 12:32; Efe 4:30; Mt 4:3; Ufu 1:5; Ebr 6:6; Mt 26:28Je, mnadhani ni adhabu kali kiasi gani anayostahili kupewa mtu aliyemkanyaga Mwana wa Mungu chini ya nyayo zake, yeye aliyeifanya damu ya Agano iliyomtakasa kuwa kitu najisi na kumtendea maovu Roho wa neema? 10:30 Kum 32:35; Rum 12:19; Kum 32:36; Za 135:14Kwa kuwa tunamjua yeye aliyesema, “Ni juu yangu kulipiza kisasi; nitalipiza.” Tena asema, “Bwana atawahukumu watu wake.” 10:31 2Kor 5:11; Isa 19:16; Mt 16:16Ni jambo la kutisha kuanguka mikononi mwa Mungu aliye hai.

10:32 Ebr 6:4; Flp 1:9, 30; Gal 3:4; 2Yn 8; Kol 2:1Kumbukeni siku zile za kwanza, ambazo mkiisha kutiwa nuru mlistahimili mashindano makali ya maumivu. Wakati mwingine mlitukanwa na kuteswa hadharani; wakati mwingine mlikuwa radhi kuungana na wale waliofanyiwa hivyo. 10:34 Ebr 13:3; 11:16; 1Pet 1:4, 5Mliwahurumia wale waliokuwa kifungoni, mkikubali kwa furaha kunyangʼanywa mali zenu kwa maana mlijua kwamba mnayo mali iliyo bora zaidi idumuyo.

10:35 Efe 3:12; Mt 5:12; 10:32Kwa hiyo msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kubwa mno. 10:36 Rum 5:3; Ebr 5:11; 12:1; Yak 1:3, 4, 12; 2Pet 1:6; Ebr 6:15; 9:15Inawapasa kuvumilia ili mkiisha kufanya mapenzi ya Mungu mpate kile alichoahidi. 10:37 Mt 11:3; Ufu 22:20; Lk 18:8; 2Pet 3:9; Hab 2:3, 4Kwa kuwa bado kitambo kidogo tu,

“Yeye ajaye atakuja wala hatakawia.

10:38 Rum 1:17; Gal 3:11; Hab 2:3, 4Lakini mwenye haki wangu

ataishi kwa imani.

Naye kama akisitasita,

sina furaha naye.”

10:39 2Pet 2:20, 21; Mdo 16:30, 31; 1The 5:9; 2The 2:14Lakini sisi hatumo miongoni mwa hao wanaositasita na kuangamia, bali tuko miongoni mwa hao wenye imani na hivyo tunaokolewa.

Read More of Waebrania 10