Waebrania 10:1-18 NEN

Waebrania 10:1-18

Dhabihu Ya Kristo Ni Mara Moja Tu

10:1 Kol 2:17; Ebr 8:5; 9:23; 9:11; 9:9; 9:14Sheria ni kivuli tu cha mambo mema yajayo, wala si uhalisi wa mambo yenyewe. Kwa sababu hii, haiwezekani kamwe kwa njia ya dhabihu zitolewazo mwaka hadi mwaka kuwakamilisha wale wanaokaribia ili kuabudu. 10:2 Ebr 9:9Kama dhabihu hizo zingeweza kuwakamilisha, hazingeendelea kutolewa tena. Kwa kuwa hao waabuduo wangekuwa wametakaswa mara moja tu, wala wasingejiona tena kuwa na dhambi. 10:3 Law 16:21; 16:34; Ebr 9:7Lakini zile dhabihu zilikuwa ukumbusho wa dhambi kila mwaka, 10:4 Mik 6:6, 7; Ebr 9:13; 9:11kwa sababu haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi.

10:5 Ebr 1:6; 2:14; 1Pet 2:24; Za 40:6; 50:8; Isa 1:11; Yer 6:20; Amo 5:21, 22Kwa hiyo, Kristo alipokuja duniani, alisema:

“Dhabihu na sadaka hukuzitaka,

bali mwili uliniandalia;

sadaka za kuteketezwa na za dhambi

hukupendezwa nazo.

10:7 Ezr 6:2; Yer 36:2; Za 40:6-8; Mt 26:39Ndipo niliposema, ‘Mimi hapa, nimekuja,

imeandikwa kunihusu katika kitabu:

Nimekuja kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu.’ ”

10:8 Ebr 10:5, 6; Mk 12:33Kwanza alisema, “Dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa na za dhambi hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo” (ingawa sheria iliagiza zitolewe). 10:9 Ebr 10:7Kisha akasema “Mimi hapa, nimekuja kuyafanya mapenzi yako.” Aondoa lile Agano la kwanza ili kuimarisha la pili. 10:10 Ebr 10:14; Efe 5:26; Ebr 2:14; 7:27; 1Pet 2:24Katika mapenzi hayo sisi tumetakaswa na kufanywa watakatifu kwa njia ya sadaka ya mwili wa Yesu Kristo alioutoa mara moja tu.

10:11 Ebr 5:1; 10:1, 4; Hes 28:3; Ebr 7:27Kila kuhani husimama siku kwa siku akifanya huduma yake ya ibada, na kutoa tena na tena dhabihu zile zile ambazo haziwezi kamwe kuondoa dhambi. 10:12 Ebr 5:1; Mk 16:19; Ebr 1:3; Kol 3:1Lakini huyu kuhani akiisha kutoa dhabihu moja kwa ajili ya dhambi kwa wakati wote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu. 10:13 Yos 10:24; Ebr 1:13; Za 110:1; Mdo 2:35; 1Kor 15:25Tangu wakati huo anangoja mpaka adui zake wawekwe chini ya miguu yake, 10:14 Ebr 10:1; Efe 5:26kwa sababu kwa dhabihu moja amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wote wanaotakaswa.

10:15 Ebr 3:7Pia Roho Mtakatifu anatushuhudia kuhusu jambo hili. Kwanza anasema:

10:16 Yer 31:33; Ebr 8:10“Hili ndilo Agano nitakalofanya nao

baada ya siku hizo, asema Bwana.

Nitaziweka sheria zangu mioyoni mwao,

na kuziandika katika nia zao.”

10:17 Yer 31:34; Ebr 8:12Kisha aongeza kusema:

“Dhambi zao na kutokutii kwao

sitakumbuka tena.”

Basi haya yakiisha kusamehewa, hakuna tena dhabihu yoyote inayotolewa kwa ajili ya dhambi.

Read More of Waebrania 10