Mwanzo 9:18-29, Mwanzo 10:1-32, Mwanzo 11:1-9 NEN

Mwanzo 9:18-29

Wana Wa Noa

9:18 Mwa 5:32; 10:6, 15; Lk 3:36Wana wa Noa waliotoka ndani ya safina ni: Shemu, Hamu na Yafethi. (Hamu ndiye alikuwa baba wa Kanaani.) 9:19 Mwa 5:32; 1:22; 10:32; 11:4-9Hawa ndio waliokuwa wana watatu wa Noa, kutokana nao watu walienea katika dunia.

Noa akawa mkulima, akawa mtu wa kwanza kupanda mizabibu. 9:21 Mwa 19:35Alipokunywa huo mvinyo wake akalewa na akalala uchi kwenye hema lake. 9:22 Hab 2:15Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake na kuwaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje. Lakini Shemu na Yafethi wakachukua nguo wakaitanda mabegani mwao wote wawili, kisha wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zilielekea upande mwingine ili wasiuone uchi wa baba yao.

Noa alipolevuka kutoka kwenye mvinyo wake na kujua lile ambalo mwanawe mdogo kuliko wote alilokuwa amemtendea, 9:25 Mwa 27:12, 29-40; 25:23; 37:10; 49:8; Kut 20:5; Za 79:8; Isa 14:21; Yer 31:29; 32:18; Hes 24:18; Yos 9:23akasema,

“Alaaniwe Kanaani!

Atakuwa mtumwa wa chini sana

kuliko watumwa wote kwa ndugu zake.”

9:26 Mwa 14:20; Kut 18:10; Za 7:17; 1Fal 9:21Pia akasema,

“Abarikiwe Bwana, Mungu wa Shemu!

Kanaani na awe mtumwa wa Shemu.

9:27 Mwa 10:2-5; Efe 2:13-14; 3:6Mungu na apanue mipaka ya Yafethi;

Yafethi na aishi katika mahema ya Shemu,

na Kanaani na awe mtumwa wake.”

Baada ya gharika Noa aliishi miaka 350. 9:29 Mwa 2:17Noa alikuwa na jumla ya miaka 950, ndipo akafa.

Read More of Mwanzo 9

Mwanzo 10:1-32

Mataifa Yaliyotokana Na Noa

(1 Nyakati 1:5-23)

10:1 Mwa 2:4; 5:32; 1Nya 1:4Hawa ndio wazao wa Noa: Shemu, Hamu na Yafethi, ambao walizaa wana baada ya gharika.

Wazao Wa Yafethi

10:2 Eze 38:6; 39:1, 6; 27:13-19; 33:26; Ufu 20:8; Isa 66:19Wana wa Yafethi walikuwa:

Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.

10:3 Yer 51:27; Eze 27:13-14; 38:6Wana wa Gomeri walikuwa:

Ashkenazi, Rifathi na Togarma.

10:4 Eze 27:7, 10, 12, 25; 38:13; Za 48:7; 72:10; Isa 2:16; 23:1-6, 12; 66:19; Yer 2:10; 10:9; Yon 1:3; Hes 24:24; Dan 11:30Wana wa Yavani walikuwa:

Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. (Kutokana na hawa mataifa ya Pwani yalienea katika nchi zao, kwa koo zao katika mataifa yao, kila moja kwa lugha yake.)

Wazao Wa Hamu

10:6 2Fal 19:9; Nah 3:9; 2Nya 12:3; 16:8; Isa 11:11; 18:1; 20:3; 43:3; Yer 46:9; Eze 27:10; 30:4-9; 38:5; Mwa 9:18; Sef 2:12; 3:10Wana wa Hamu walikuwa:

Kushi, Misraimu,10:6 Yaani Misri. Putu na Kanaani.

10:7 Isa 21:13; 43:3; 60:6; Mwa 2:11; 25:3; Eze 38:13; 27:15, 20, 22; 1Fal 10:1; 2Nya 9:1; Ay 1:15; 6:19; 16:11; Za 72:10; Yer 25:23-24; 6:20; 49:8; Yoe 3:8; 1Nya 1:32Wana wa Kushi walikuwa:

Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.

Wana wa Raama walikuwa:

Sheba na Dedani.

10:8 Mik 5:6Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa duniani. 10:9 2Nya 14:9; 16:8; Isa 18:2; Mwa 25:27; 27:3Alikuwa mwindaji hodari mbele za Bwana. Ndiyo sababu watu husema, “Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda mbele za Bwana.” 10:10 Mwa 11:2, 9; 14:1; 2Nya 36:17; Isa 10:9; 13:1; Yer 21:2; 25:12; 50:1; Ezr 4:9; Amo 6:2; Zek 5:11Vituo vyake vya kwanza katika ufalme wake vilikuwa Babeli, Ereki, Akadi na Kalne katika Shinari. 10:11 Za 83:8; Isa 37:37; Mik 5:6; Sef 2:13; 2Fal 19:36; Yon 1:2; 3:2-3Kutoka nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehoboth-iri, Kala, na Reseni, iliyo kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa.

Misraimu alikuwa baba wa:

Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, 10:14 Mwa 21:32-34; 26:1, 8; Yos 13:2; Amu 3:3; Isa 14:31; Yer 47:1-4; Amo 9:7; Kum 2:23; 1Nya 1:12Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori.

10:15 Mwa 9:18; 5:20; 23:3; 25:10; 26:34; 27:46; 49:32; Yos 1:4; 11:8; Amu 10:6; Isa 23:2-4; Yer 25:22; 27:3; 47:4; Eze 16:3; 28:21; 32:30; Yoe 3:4; Zek 9:2; Kut 4:22; Hes 1:20; 3:2; 13:29; 18:15; 33:4; 1Sam 26:6Kanaani alikuwa baba wa:

Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi, 10:16 Amu 19:10; 1Nya 11:4; Ezr 9:1; Kut 3:8; 2Nya 8:7; Hes 13:29; 21:13; 32:39; Yos 2:10; Kum 1:4; 7:1; Yos 2:10; Mwa 15:18-21Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, 10:17 Mwa 34:2; 36:2; Kut 3:8; Kum 7:1; Amu 3:3Wahivi, Waariki, Wasini, 10:18 Eze 27:8; 1Nya 18:3; Mwa 12:6; 13:17; 50:11; Kut 13:11; Hes 13:29; 14:25; 21:3; 33:40; Kum 7:1; Amu 1:1Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.

Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika, 10:19 Mwa 11:31; 12:1; 13:12; 14:2; 17:8; 24:3; 26:34; 37:1; 27:46; 28:1-8; 31:18; 35:6; 49:13; Law 25:38; Yos 19:28; Amu 1:18, 31; 18:28; 6:4; 16:1, 21; 2Nya 24:6; 14:13; Kum 2:23; 29:23; Yos 10:41; 11:22; 15:47; 1Sam 6:17; Yer 25:20; 47:1; Amo 1:6; Sef 2:4na mipaka ya Kanaani ilienea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.

Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

Wazao Wa Shemu

10:21 Hes 24:24Shemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.

10:22 Mwa 14:1; Isa 11:11; 21:2; Yer 25:25; 49:34; Eze 27:23; 32:24; Dan 8:2; Lk 3:36; Hes 24:22-24; Amu 3:10; 1Fal 11:25; 19:15; 20:34; 22:31; 2Fal 5:1; 8:7Wana wa Shemu walikuwa:

Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.

10:23 Mwa 22:21; Ay 1:1; Yer 25:20; Mao 4:21Wana wa Aramu walikuwa:

Usi, Huli, Getheri na Mesheki.

10:24 Lk 3:35Arfaksadi alikuwa baba wa Shela,

naye Shela akamzaa Eberi.

Eberi akapata wana wawili:

Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake ndipo dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.

Yoktani alikuwa baba wa:

Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, 10:27 Eze 27:19Hadoramu, Uzali, Dikla, 10:28 1Fal 10:1; Ay 6:11; Za 72:10, 15; Isa 60:6; Eze 27:22Obali, Abimaeli, Sheba, 10:29 1Fal 9:28; 1Nya 29:4; Ay 22:24; 28:16; Za 45:9; Isa 13:12; 10:32; Mwa 9:19Ofiri, Havila na Yobabu. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.

Nchi waliyoishi ilienea toka Mesha kuelekea Sefari kwenye nchi ya vilima iliyoko mashariki.

Hao ndio wana wa Shemu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.

Hizi ndizo koo za wana wa Noa, kufuatana na vizazi vyao, katika mataifa yao. Kutokana na hawa mataifa yalienea duniani kote baada ya gharika.

Read More of Mwanzo 10

Mwanzo 11:1-9

Mnara Wa Babeli

Wakati huo dunia yote ilikuwa na lugha moja na msemo mmoja. 11:2 Mwa 10:10Watu walipoelekea upande wa mashariki, wakafika kwenye tambarare katika nchi ya Shinari11:2 Shinari ndio Babeli. nao wakaishi huko.

11:3 Kut 1:14; 5:7; Yer 43:9; Isa 9:10; Amo 5:11; Mwa 14:10Wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tufyatue matofali na tuyachome vizuri kwa moto.” Walitumia matofali badala ya mawe, na lami kwa ajili ya kushikamanishia hayo matofali. 11:4 Kum 1:28; 6:10; 9:1; Ay 20:6; Yer 51:53; 31:10; 40:15; Mwa 6:4; 9:19; Kum 30:3; 4:27; 1Fal 22:17; Es 3:8; Za 44:11; Eze 6:8; Yoe 3:2Ndipo wakasema, “Njooni, tujijengee mji wenye mnara ambao utafika hadi mbinguni, ili tujipatie jina tusije tukatawanyika usoni pa dunia yote.”

11:5 Mwa 18:21; Kut 3:6-8; 19:11, 18-20; Za 18:9; 144:5Lakini Bwana akashuka ili auone mji na mnara ambao wanadamu waliokuwa wanaujenga. Bwana akasema, “Ikiwa kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lolote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao. 11:7 Mwa 1:26; 42:23; Kum 28:49; Isa 28:11; 33:19; Yer 5:15; 1Kor 2:11Njooni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao.”

11:8 Mwa 9:19; Kum 32:8; Lk 1:51Hivyo Bwana akawatawanya kutoka mahali pale kwenda katika dunia yote, nao wakaacha kuujenga huo mji. 11:9 Mwa 10:10; Za 55:9; Mdo 2:5-11; Isa 2:10, 21; 13:14; 24:1Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo Bwana alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo Bwana akawatawanya katika uso wa dunia yote.

Read More of Mwanzo 11