Mwanzo 7:1-24, Mwanzo 8:1-22, Mwanzo 9:1-17 NEN

Mwanzo 7:1-24

7:1 Mwa 6:18; 9:6; Mt 24:38; Ebr 11:7; Lk 17:26-27; 1Pet 3:20; 2Pet 2:5; Eze 14:14Ndipo Bwana akamwambia Noa, “Ingia katika safina wewe na jamaa yako yote, kwa sababu katika kizazi hiki nimeona ya kuwa wewe ni mwenye haki. 7:2 Mwa 8:20; Law 10:10; 11:1-47; Kum 14:3-20; Eze 44:23; Hag 2:12; Mdo 10:14-15Uchukue wanyama saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike, na wanyama wawili wawili wa kila aina walio najisi wa kiume na wa kike. 7:3 Mwa 6:20Pia uchukue ndege saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike, ili kuhifadhi aina zao mbalimbali katika dunia yote. 7:4 Mwa 2:8; 6:7, 13; 1Fal 13:34; Yer 28:16; Hes 13:25; 1Sam 17:16; 1Fal 19:8; Kut 24:18; 32:1; 34:28; Kum 9:9, 11, 18, 25; 10:10; Ay 37:6; Mt 4:2Siku saba kuanzia sasa nitaleta mvua juu ya nchi kwa siku arobaini usiku na mchana, nami nitafutilia mbali kutoka uso wa nchi kila kiumbe hai nilichokiumba.”

7:5 Mwa 6:22Noa akafanya yote kama Bwana alivyomwamuru.

7:6 Mwa 5:32Noa alikuwa na miaka 600 gharika ilipokuja juu ya dunia. 7:7 Mwa 6:18Noa na mkewe na wanawe na wake zao wakaingia katika safina ili waepuke ile gharika. Jozi ya wanyama walio safi na walio najisi, ndege na viumbe vitambaavyo, 7:9 Mwa 6:22wa kiume na wa kike, walikuja kwa Noa wakaingia katika safina kama Mungu alivyomwamuru Noa. Baada ya siku saba, maji ya gharika yakaja juu ya dunia.

7:11 Mwa 5:32; 8:2, 4, 14; Ay 28:11; Za 36:6; 42:7; 78:23; Mit 8:24; Isa 24:18; 51:10; Eze 26:19; 2; 2Fal 7:2; Mal 3:10Katika siku ya kumi na saba ya mwezi wa pili mwaka wa 600 wa kuishi kwake Noa, siku hiyo ndipo chemchemi zote hata zilizo chini sana ya ardhi zilibubujika kwa nguvu, na malango ya mafuriko ya mbinguni yakafunguliwa. 7:12 1Sam 12:17; Ay 28:26Mvua ikanyesha juu ya nchi siku arobaini usiku na mchana.

7:13 Mwa 8:16; 6:18; 1Pet 3:20; 2Pet 2:5Siku hiyo Noa, na mkewe, na wanawe Shemu, Hamu na Yafethi pamoja na wake zao wakaingia katika ile safina. 7:14 Mwa 1:11Nao walikuwa pamoja na kila mnyama wa mwituni kufuatana na aina yake, wanyama wote wafugwao kufuatana na aina zao, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi kwa aina yake, na kila ndege kufuatana na aina yake, naam kila kiumbe chenye mabawa. 7:15 Mwa 6:19Viumbe vyote vyenye pumzi ya uhai ndani yake vikaja kwa Noa viwili viwili, vikaingia katika safina. 7:16 Mwa 6:22Wanyama walioingia katika safina walikuwa wa kiume na wa kike, wa kila kiumbe chenye uhai kama Mungu alivyomwamuru Noa, ndipo Bwana akamfungia ndani.

Kwa siku arobaini mafuriko yaliendelea kujaa duniani na maji yalivyozidi kuongezeka, yaliinua safina juu sana kutoka kwenye uso wa nchi. Maji yakajaa na kuongezeka sana juu ya nchi, na safina ikaelea juu ya uso wa maji. 7:19 Za 104:6Maji yakazidi kujaa juu ya nchi, yakaifunika milima yote mirefu chini ya mbingu yote. 7:20 Mwa 8:4-5; 2Pet 3:6Maji yakaendelea kujaa yakaifunika milima kwa kina cha zaidi ya dhiraa kumi na tano.7:20 Dhiraa 15 ni sawa na mita 7. 7:21 Mwa 6:7, 13; 2Pet 3:6Kila kiumbe hai kitambaacho juu ya nchi kikaangamia: Ndege, wanyama wa kufugwa, wanyama pori, viumbe vyote juu ya nchi na wanadamu wote. 7:22 Mwa 1:30Kila kiumbe juu ya nchi kavu chenye pumzi ya uhai kikafa. 7:23 Ay 14:19; 21:18; 22:11, 16; Lk 17:27; Za 90:5; Isa 28:2; Mt 24:39; Ebr 11:7; 1Pet 3:20; 2Pet 2:5Kila kitu chenye uhai juu ya uso wa nchi kilifutiliwa mbali, watu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege warukao angani wakafutiliwa mbali toka duniani. Waliobaki ni Noa peke yake na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina.

7:24 Mwa 8:3; Ay 12:15Maji yakaifunika dunia kwa siku 150.

Read More of Mwanzo 7

Mwanzo 8:1-22

Mwisho Wa Gharika

8:1 Mwa 9:15; 19:29; 21:1; 30:22; Kut 2:23-24; Ay 12:15; 14:13; Rut 4:13; Nah 1:4; 1Sam 1:11, 19; 2Fal 20:3; 1Nya 16:15; Neh 1:8; 5:19; 13:11-31; Hes 10:9; Za 66:6; 105:42; 106:4; Lk 1:54, 72; Kut 14:21; Yos 2:10; 3:16; Isa 11:15; 44:27Mungu akamkumbuka Noa na wanyama wote wa porini na wa kufugwa waliokuwa naye ndani ya safina, akatuma upepo ukavuma katika dunia, nayo maji yakaondoka. 8:2 Mwa 7:4, 11Zile chemchemi zilizo chini sana ya ardhi pamoja na malango ya mafuriko ya mbinguni yakawa yamefungwa nayo mvua ikawa imekoma kunyesha kutoka angani. 8:3 Mwa 7:24Maji yakaendelea kupungua taratibu katika nchi. Kunako mwisho wa siku ya 150, maji yalikuwa yamepungua, 8:4 Mwa 7:11, 20; 2Fal 19:37; Yer 51:27katika siku ya kumi na saba ya mwezi wa saba, safina ikatua katika milima ya Ararati. Maji yakaendelea kupungua hadi mwezi wa kumi, na siku ya kwanza ya mwezi wa kumi, vilele vya milima vikaonekana.

Baada ya siku arobaini Noa akafungua dirisha alilokuwa amelifanya katika safina 8:7 Amu 11:15; Kum 14:14; 1Fal 17:4-6; Ay 38:41; Za 147:9; Mit 30:17; Isa 34:11; Lk 12:24na akamtoa kunguru, akawa akiruka kwenda na kurudi mpaka maji yalipokwisha kukauka juu ya nchi. 8:8 Ay 30:31; Za 55:6; 74:19; Wim 2:12-14; Isa 38:14; 59:11; 60:8; Yer 48:28; Eze 7:16; Nah 2:7; Hos 7:11; 11:11; Mt 3:16; 10:16; Yn 1:32Kisha akamtoa hua ili aone kama maji yameondoka juu ya uso wa ardhi. Lakini hua hakupata mahali pa kutua kwa kuwa maji yalienea juu ya uso wa dunia yote, kwa hiyo akarudi kwa Noa ndani ya safina. Noa akanyoosha mkono akamchukua yule hua akamrudisha ndani ya safina. Noa akangojea siku saba zaidi kisha akamtoa tena hua kutoka safina. Wakati hua aliporejea kwa Noa jioni, alikuwa amechukua katika mdomo wake jani bichi la mzeituni, lililochumwa wakati ule ule! Ndipo Noa akajua ya kuwa maji yameondoka juu ya uso wa dunia. Akangojea siku saba zaidi na akamtuma tena hua, lakini wakati huu hua hakurudi tena kwa Noa.

8:13 Mwa 5:32Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza ya mwaka 601, wa kuishi kwake Noa, maji yalikuwa yamekauka duniani. Kisha Noa akafungua mlango wa safina akaona ya kuwa uso wa ardhi ulikuwa umekauka. 8:14 Mwa 7:11Katika siku ya ishirini na saba ya mwezi wa pili dunia ilikuwa imekauka kabisa.

Ndipo Mungu akamwambia Noa, 8:16 Mwa 7:13“Toka ndani ya safina, wewe na mkeo na wanao na wake zao. 8:17 Mwa 1:22Utoe nje kila aina ya kiumbe hai aliye pamoja nawe: Ndege, wanyama na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi, ili wakazae, na kuongezeka na kuijaza tena dunia.”

8:18 1Pet 3:20; 2Pet 2:5Kwa hiyo Noa akatoka nje pamoja na mkewe, wanawe na wake zao. Wanyama wote na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi na ndege wote, kila kitu kiendacho juu ya nchi, aina moja baada ya nyingine vikatoka katika safina, kila aina ya kiumbe, kimoja baada ya kingine.

Noa Atoa Dhabihu

8:20 Mwa 12:7-8; 13:18; 22:9; 26:25; 33:20; 35:7; 7:8; 22:2-13; Kut 17:15; 24:4; 10:25; 20:24; 40:29; Ay 42:8; Law 1:3; 4:29; 6:8-13; Hes 6:11; Amu 6:26; 11:31; 1Sam 20:29Kisha Noa akamjengea Bwana madhabahu, akachukua baadhi ya wale wanyama na ndege wote walio safi, akatoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. 8:21 Kut 29:18, 25; Law 1:9, 13; 2:9; 4:31; Hes 15:3, 7; 2Kor 2:15; Mwa 3:17; 6:5; 9:11-15; Yer 17:9; Za 51:5; Mt 15:19; Rum 1:21; Yer 44:11; Isa 54:9Bwana akasikia harufu nzuri ya kupendeza, naye akasema moyoni mwake, “Kamwe sitailaani tena ardhi kwa sababu ya mwanadamu, hata ingawa kila mwelekeo wa moyo wake ni mbaya tangu ujana. Kamwe sitaangamiza tena viumbe hai vyote kama nilivyofanya.

8:22 Yos 3:15; Za 67:6; 74:17; Yer 5:24; Zek 14:8; Mwa 1:14“Kwa muda dunia idumupo,

wakati wa kupanda na wa kuvuna,

wakati wa baridi na wa joto,

wakati wa kiangazi na wa masika,

usiku na mchana

kamwe havitakoma.”

Read More of Mwanzo 8

Mwanzo 9:1-17

Mungu Aweka Agano Na Noa

9:1 Mwa 1:22Ndipo Mungu akambariki Noa na wanawe, akiwaambia, “Zaeni mkaongezeke kwa idadi na mkaijaze tena dunia. 9:2 Mwa 1:26Wanyama wote wa duniani, ndege wote wa angani, kila kiumbe kitambaacho juu ya ardhi, na samaki wote wa baharini wamekabidhiwa mikononi mwenu, nao watawaogopa na kuwahofu. 9:3 Mwa 1:29; Kol 2:16; Mdo 10:15Kila kitu chenye uhai kiendacho kitakuwa chakula chenu. Kama vile nilivyowapa mimea mbalimbali, sasa nawapa kila kitu.

9:4 Law 3:17; 7:26; 17:10-14; 19:26; Kum 12:16, 23-25; 15:23; 1Sam 14:33; Eze 33:25; Mdo 15:20, 29“Lakini kamwe msile nyama ambayo bado ina damu ya uhai wake, kwa maana damu ni uhai. 9:5 Mwa 4:10; 42:22; 50:15; 1Fal 2:32; 2Nya 24:22; Za 9:12; Kut 21:28-32Hakika damu ya uhai wenu nitaidai. Nitaidai kutoka kwa kila mnyama. Kutoka kwa kila mwanadamu pia nitaidai kwa ajili ya uhai wa mtu mwenzake.

9:6 Mwa 1:26; 4:14; Amu 9:24; Mt 26:52“Yeyote amwagaye damu ya mwanadamu,

damu yake itamwagwa na mwanadamu,

kwa kuwa katika mfano wa Mungu,

Mungu alimuumba mwanadamu.

9:7 Mwa 1:22; 9:19Kuhusu ninyi, zaeni mwongezeke kwa wingi, mzidi katika dunia na kuijaza.”

Ndipo Mungu akamwambia Noa na wanawe pamoja naye: 9:9 Mwa 6:18“Sasa mimi ninaweka Agano langu nanyi, pamoja na uzao wenu baada yenu, pia na kila kiumbe hai kilichokuwa pamoja nanyi: Ndege, wanyama wa kufugwa na wanyama wote wa porini, wale wote waliotoka katika safina pamoja nanyi, kila kiumbe hai duniani. 9:11 Isa 24:5; 33:8; 54:9; Hos 6:7; Mwa 8:21Ninaweka Agano nanyi: Kamwe uhai hautafutwa tena kwa gharika, kamwe haitakuwepo tena gharika ya kuangamiza dunia.”

9:12 Mwa 17:11-12; Kut 12:14; Law 3:17; 6:18; 17:7; Hes 10:8Mungu akasema, “Hii ni ishara ya Agano ninalofanya kati yangu na ninyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, Agano kwa vizazi vyote vijavyo: 9:13 Eze 1:28; Ufu 4:3; 10:1Nimeweka upinde wangu wa mvua mawinguni, nao utakuwa ishara ya Agano nifanyalo kati yangu na dunia. Wakati wowote ninapotanda mawingu juu ya dunia na upinde wa mvua ukijitokeza mawinguni, 9:15 Mwa 8:1, 21; Kut 2:24; 6:5; 34:10; Law 26:42-45; Kum 7:9; Za 89:34; 103:18; 105:8; 106:45; Eze 16:60nitakumbuka Agano langu kati yangu na ninyi na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina. Kamwe maji hayatakuwa tena gharika ya kuangamiza uhai wote. 9:16 Mwa 17:7-13, 19; 2Sam 7:13; 23:5; Za 105:9-10; Isa 9:7; 54:10; 55:3; 59:21; 61:8; Yer 31:34; 32:40; 33:21; Eze 16:60; 37:26; Ebr 13:20Wakati wowote upinde wa mvua unapotokea mawinguni, nitauona na kukumbuka Agano la milele kati ya Mungu na viumbe vyote vilivyo hai vya kila aina duniani.”

Hivyo Mungu akamwambia Noa, “Hii ndiyo ishara ya Agano ambalo nimelifanya kati yangu na viumbe vyote vilivyo hai duniani.”

Read More of Mwanzo 9