Mwanzo 49:1-33, Mwanzo 50:1-26 NEN

Mwanzo 49:1-33

Yakobo Abariki Wanawe

49:1 Hes 24:14; Kum 31:29Ndipo Yakobo akawaita wanawe na kusema: “Kusanyikeni kunizunguka ili niweze kuwaambia lile litakalowatokea siku zijazo.

49:2 Yos 24:1; Za 34:11“Kusanyikeni na msikilize, enyi wana wa Yakobo,

msikilizeni baba yenu Israeli.

49:3 Mwa 29:32; Kum 21:17; Za 78:51“Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza,

nguvu zangu, tunda la kwanza la nguvu zangu,

umepita kwa heshima, umepita kwa uwezo.

Usiyezuiwa kama maji, basi hutakuwa mkuu tena,

kwa kuwa ulipanda kwenye kitanda cha baba yako,

kwenye kitanda changu na kukinajisi.

49:5 Mwa 29:33; Mit 4:17“Simeoni na Lawi ni wana ndugu:

panga zao ni silaha za jeuri.

49:6 Mit 1:15; Efe 5:11Mimi na nisiingie katika baraza lao,

nami nisiunganike katika kusanyiko lao,

kwa kuwa wamewaua watu katika hasira yao,

walikata mishipa ya miguu ya mafahali

kama walivyopenda.

49:7 Yos 19:1, 9; Mwa 29:35Hasira yao na ilaaniwe, kwa kuwa ni kali mno,

nayo ghadhabu yao ni ya ukatili!

Nitawatawanya katika Yakobo

Na kuwasambaza katika Israeli.

49:8 1Nya 5:2; Kum 28:48“Yuda, ndugu zako watakusifu;

mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako;

wana wa baba yako watakusujudia.

49:9 Hes 24:9; Ay 38:39Ee Yuda, wewe ni mwana simba;

unarudi toka mawindoni, mwanangu.

Kama simba hunyemelea na kulala chini,

kama simba jike: nani athubutuye kumwamsha?

49:10 Eze 21:27; Isa 42:1Fimbo ya ufalme haitaondoka kwa Yuda,

wala fimbo ya mtawala kati ya miguu yake,

hadi aje yeye ambaye milki ni yake,

ambaye utii wa mataifa ni wake.

Atamfunga punda wake katika mzabibu,

naye mwana-punda wake kwenye tawi lililo bora zaidi;

atafua mavazi yake katika divai,

majoho yake katika damu ya mizabibu.

Macho yake yatakuwa mekundu kwa divai,

meno yake yatakuwa meupe kwa maziwa.

49:13 Mwa 30:20; 10:19“Zabuloni ataishi pwani ya bahari

na kuwa bandari za kuegesha meli;

mpaka wake utapanuka kuelekea Sidoni.

“Isakari ni punda mwenye nguvu

ambaye amelala kati ya mizigo yake.

49:15 Yos 19:17-23; Eze 29:18Aonapo palivyo pazuri mahali pake pa kupumzika

na jinsi nchi yake inavyopendeza,

atainamisha bega lake kwenye mzigo

na kujitolea kwa ajili ya kazi ngumu.

“Dani atahukumu watu wake kwa haki

kama mmoja wa makabila ya Israeli.

49:17 Amu 18:27; Yer 8:17Dani atakuwa nyoka kando ya barabara,

nyoka mwenye sumu kando ya njia,

yule aumaye visigino vya farasi

ili yule ampandaye aanguke chali.

“Ee Bwana, nautafuta wokovu wako.

“Gadi atashambuliwa ghafula na kundi la washambuliaji,

lakini yeye atawageukia na kuwashinda kabisa.

49:20 Mwa 30:13; Isa 25:6; Ay 29:6“Chakula cha Asheri kitakuwa kinono,

naye atatoa chakula kitamu kimfaacho mfalme.

“Naftali ni kulungu jike aliyeachiwa huru

azaaye watoto wazuri.

49:22 Mwa 30:24; Eze 19:10“Yosefu ni mzabibu uzaao,

mzabibu uzaao ulio kando ya chemchemi,

ambao matawi yake hutanda ukutani.

Kwa uchungu wapiga mshale walimshambulia,

wakampiga mshale kwa ukatili.

49:24 Za 18:34; Isa 1:24Lakini upinde wake ulibaki imara,

mikono yake ikatiwa nguvu,

na mkono wa Mwenye Nguvu wa Yakobo,

kwa sababu ya Mchungaji, Mwamba wa Israeli,

49:25 Kut 18:4; Mwa 27:28kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia,

kwa sababu ya Mwenyezi,49:25 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania. yeye anayekubariki

kwa baraka za mbinguni juu,

baraka za kilindi kilichoko chini,

baraka za matitini na za tumbo la uzazi.

Baraka za baba yako ni kubwa

kuliko baraka za milima ya kale,

nyingi kuliko vilima vya kale.

Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yosefu,

juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake.

49:27 Amu 20:12-13; Ebr 1:8; Hes 31:11“Benyamini ni mbwa mwitu mlafi mwenye njaa kuu;

asubuhi hurarua mawindo yake,

jioni hugawa nyara.”

Haya yote ndiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, na hivi ndivyo baba yao alivyowaambia alipowabariki, akimpa kila mmoja baraka inayomfaa.

Kifo Cha Yakobo

49:29 Mwa 25:8; 2Sam 2:32Ndipo alipowapa maelekezo haya: “Mimi niko karibu kukusanywa kwa watu wangu. Mnizike pamoja na baba zangu kwenye pango katika shamba la Efroni, Mhiti, pango lililoko katika shamba la Makpela, karibu na Mamre huko Kanaani, ambalo Abrahamu alinunua kwa ajili ya mahali pa kuzikia kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba. 49:31 Mwa 25:9; 23:19Huko ndiko Abrahamu na Sara mkewe walikozikwa, huko akazikwa Isaki na Rebeka mkewe, na huko nilimzika Lea. Shamba hilo na pango lililoko ndani yake lilinunuliwa kutoka kwa Wahiti.”

49:33 Mwa 25:8; Mdo 7:15Baada ya Yakobo kumaliza kutoa maelekezo hayo kwa wanawe, akarudisha miguu yake kitandani, akapumua pumzi ya mwisho, na akakusanywa kwa watu wake.

Read More of Mwanzo 49

Mwanzo 50:1-26

Basi Yosefu akamwangukia baba yake, akalilia juu yake na akambusu. 50:2 Mwa 50:26; 2Nya 16:14Ndipo Yosefu akawaagiza matabibu waliokuwa wakimhudumia, wamtie baba yake Israeli dawa ili asioze. Hivyo matabibu wakamtia dawa asioze, 50:3 Kum 1:3; Mwa 30:27wakatumia siku arobaini, kwa maana ndio muda uliotakiwa wa kutia dawa ili asioze. Nao Wamisri wakamwombolezea Yakobo kwa siku sabini.

50:4 Mwa 27:41Siku za kumwombolezea zilipokwisha, Yosefu akawaambia washauri wa Farao, “Kama nimepata kibali machoni penu semeni na Farao kwa ajili yangu. Mwambieni, 50:5 Mwa 24:37; 2Sam 18:18‘Baba yangu aliniapisha na kuniambia, “Mimi niko karibu kufa; unizike katika kaburi lile nililochimba kwa ajili yangu mwenyewe katika nchi ya Kanaani.” Sasa nakuomba uniruhusu niende kumzika baba yangu, nami nitarudi.’ ”

Farao akasema, “Panda, uende kumzika baba yako, kama alivyokuapiza kufanya.”

50:7 Mwa 45:16Hivyo Yosefu akapanda kwenda kumzika baba yake. Maafisa wote wa Farao wakaenda pamoja naye, watu mashuhuri wa baraza lake na watu mashuhuri wote wa Misri. Hawa ni mbali na watu wote wa nyumbani kwa Yosefu, na ndugu zake, na wale wote wa nyumbani mwa baba yake. Ni watoto wao, makundi yao ya kondoo, mbuzi na ngʼombe tu waliobakia katika nchi ya Gosheni. 50:9 Mwa 41:43Magari makubwa na wapanda farasi pia walipanda pamoja naye. Likawa kundi kubwa sana.

50:10 Hes 15:20; 1Sam 31:13Walipofika kwenye sakafu ya kupuria nafaka ya Atadi, karibu na Yordani, wakalia kwa sauti na kwa uchungu; Yosefu akapumzika huko kwa siku saba kumwombolezea baba yake. 50:11 Mwa 10:18; 37:34Wakanaani walioishi huko walipoona maombolezo yaliyofanyika katika sakafu ile ya kupuria ya Atadi, wakasema, “Wamisri wanafanya maombolezo makubwa.” Kwa hiyo mahali pale karibu na Yordani pakaitwa Abel-Mizraimu.50:11 Abel-Mizraimu maana yake Maombolezo ya Wamisri.

Hivyo wana wa Yakobo wakafanya kama baba yao alivyowaagiza: 50:13 Mwa 23:20Wakamchukua mpaka nchi ya Kanaani, wakamzika kwenye pango katika shamba la Makpela, karibu na Mamre, ambalo Abrahamu alilinunua kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba liwe mahali pa kuzikia. Baada ya Yosefu kumzika baba yake, akarudi Misri pamoja na ndugu zake na wale wote waliokuwa wamekwenda naye kumzika baba yake.

Yosefu Awaondolea Ndugu Zake Mashaka

50:15 Mwa 37:28Ndugu zake Yosefu walipoona kwamba baba yao amekufa, wakasema, “Itakuwaje kama Yosefu ataweka kinyongo dhidi yetu na kutulipa mabaya yote tuliyomtendea?” Kwa hiyo wakampelekea Yosefu ujumbe, wakasema, “Kabla baba yako hajafa aliacha maagizo haya: 50:17 Mt 6:14; Mwa 29:11‘Hili ndilo mtakalomwambia Yosefu: Ninakuomba uwasamehe ndugu zako dhambi na mabaya kwa vile walivyokutenda vibaya.’ Sasa tafadhali samehe dhambi za watumishi wa Mungu wa baba yako.” Ujumbe huu ulipomfikia, Yosefu akalia.

50:18 Mwa 37:7Ndipo ndugu zake wakaja na kujitupa chini mbele yake. Wakasema, “Sisi ni watumwa wako.”

50:19 Rum 12:19; Ebr 10:30Lakini Yosefu akawaambia, “Msiogope. Je, mimi ni badala ya Mungu? 50:20 Rum 8:28; Mwa 45:5Mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema, ili litimie hili linalofanyika sasa, kuokoa maisha ya watu wengi. 50:21 Mwa 45:11; Efe 4:32Hivyo basi, msiogope. Mimi nitawatunza ninyi nyote pamoja na watoto wenu.” Akawahakikishia na kusema nao kwa wema.

Kifo Cha Yosefu

50:22 Mwa 25:7; Yos 24:29Yosefu akakaa katika nchi ya Misri, yeye pamoja na jamaa yote ya baba yake. Akaishi miaka 110, naye akaona kizazi cha tatu cha watoto wa Efraimu. Pia akaona watoto wa Makiri mwana wa Manase, wakawekwa magotini mwa Yosefu walipozaliwa.

50:24 Rut 1:6; Za 35:2; Mwa 12:7Ndipo Yosefu akawaambia ndugu zake, “Mimi ninakaribia kufa. Lakini kwa hakika Mungu atawasaidia na kuwachukueni kutoka nchi hii na kuwapeleka katika nchi aliyomwahidi kwa kiapo Abrahamu, Isaki na Yakobo.” Naye Yosefu akawaapisha wana wa Israeli na kuwaambia, “Hakika Mungu atawasaidia, nanyi ni lazima mhakikishe mmepandisha mifupa yangu kutoka mahali hapa.”

Kwa hiyo Yosefu akafa akiwa na umri wa miaka 110. Baada ya kumtia dawa ili asioze, akawekwa kwenye jeneza huko Misri.

Read More of Mwanzo 50