Mwanzo 45:1-28, Mwanzo 46:1-34, Mwanzo 47:1-12 NEN

Mwanzo 45:1-28

Yosefu Anajitambulisha

45:1 2Sam 13:9Hapo Yosefu hakuweza kujizuia zaidi mbele ya wote waliokuwa wamesimama karibu naye, akapaza sauti, akasema, “Mwondoeni kila mtu mbele yangu!” Kwa hiyo hapakuwepo mtu yeyote pamoja na Yosefu alipojitambulisha kwa ndugu zake. 45:2 Mdo 7:13Naye akalia kwa sauti kubwa kiasi kwamba Wamisri walimsikia, hata watu wa nyumbani mwa Farao wakapata hizo habari.

45:3 Mwa 43:7Yosefu akawaambia ndugu zake, “Mimi ni Yosefu! Je, baba yangu angali hai bado?” Lakini ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwa sababu walipatwa na hofu kuu mbele yake.

45:4 Mwa 37:28Ndipo Yosefu akawaambia ndugu zake, “Sogeeni karibu nami.” Waliposogea, akasema, “Mimi ni ndugu yenu Yosefu, yule ambaye mlimuuza Misri! 45:5 Mwa 50:20; Za 105:17Sasa, msihuzunike wala msijichukie wenyewe kwa kuniuza huku, kwa sababu ilikuwa ni ili kuokoa maisha ya watu ndiyo sababu Mungu alinituma niwatangulie ninyi. Kwa miaka miwili sasa imekuwepo njaa katika nchi, pia kwa miaka mitano ijayo hapatakuwepo kulima wala kuvuna. Lakini Mungu alinitanguliza mbele yenu ili kuhifadhi mabaki kwa ajili yenu katika nchi, na kuokoa maisha yenu kwa wokovu mkuu.

45:8 Amu 17:10; Mwa 41:41“Kwa hiyo basi, si ninyi mlionileta huku, bali ni Mungu. Alinifanya kuwa baba kwa Farao, bwana wa watu wa nyumbani mwake wote, na mtawala wa Misri yote. Sasa rudini haraka kwa baba yangu na mwambieni, ‘Hili ndilo mwanao Yosefu asemalo: Mungu amenifanya mimi kuwa bwana wa Misri yote. Shuka uje kwangu, wala usikawie. 45:10 Mwa 47:1Nawe utaishi katika nchi ya Gosheni na kuwa karibu nami, wewe, watoto wako na wajukuu wako, makundi yako ya kondoo, mbuzi na ngʼombe, pamoja na vyote ulivyo navyo. Nitawatunza huko, kwa sababu bado iko miaka mingine mitano inayokuja ya njaa. La sivyo, wewe na nyumba yako na wote ulio nao mtakuwa fukara.’

“Mnaweza kujionea wenyewe, hata ndugu yangu Benyamini, kwamba hakika ni mimi ninayezungumza nanyi. 45:13 Mdo 7:14Mwambieni baba yangu juu ya heshima yote niliyopewa huku Misri, na kuhusu kila kitu mlichokiona. Mleteni baba yangu huku haraka.”

45:14 Mwa 29:13Ndipo akamkumbatia Benyamini ndugu yake na kulia, naye Benyamini akamkumbatia akilia. 45:15 Lk 15:20Pia akawabusu ndugu zake wote, huku akilia. Baada ya hayo ndugu zake wakazungumza naye.

45:16 Mwa 41:37Habari zilipofika kwenye jumba la Farao kwamba ndugu zake Yosefu wamefika, Farao na maafisa wake wote wakafurahi. 45:17 Mwa 42:5Farao akamwambia Yosefu, “Waambie ndugu zako, ‘Fanyeni hivi: Pakieni wanyama wenu mrudi mpaka nchi ya Kanaani, 45:18 Mwa 46:34; 47:6, 11, 27mkamlete baba yenu na jamaa zenu kwangu. Nitawapa sehemu nzuri sana ya nchi ya Misri nanyi mtafurahia unono wa nchi.’

45:19 Mwa 46:5“Mnaagizwa pia kuwaambia, ‘Fanyeni hivi: Chukueni magari ya kukokotwa kutoka Misri, kwa ajili ya watoto wenu na wake zenu, mkamchukue baba yenu mje. Msijali kamwe kuhusu mali zenu, kwa sababu mema yote ya Misri yatakuwa yenu.’ ”

Hivyo wana wa Israeli wakafanya hivyo. Yosefu akawapa magari ya kukokotwa, kama Farao alivyoagiza, pia akawapa mahitaji kwa ajili ya safari yao. Kila mmoja mavazi mapya, lakini Benyamini akampa shekeli 30045:22 Shekeli 300 za fedha ni sawa na kilo 3.4. za fedha, na jozi tano za nguo. Hivi ndivyo vitu alivyotuma kwa baba yake: punda kumi waliochukua vitu vizuri vya Misri, punda wake kumi waliobeba nafaka, mikate na mahitaji mengine ya safari. Akaagana na ndugu zake walipokuwa wakiondoka, akawaambia, “Msigombane njiani!”

Basi wakatoka Misri na kufika kwa baba yao Yakobo katika nchi ya Kanaani. Wakamwambia baba yao, “Yosefu angali hai! Ukweli ni kwamba yeye ndiye mtawala wa Misri yote.” Yakobo akapigwa na bumbuazi; hakuwasadiki. 45:27 Mwa 45:19Lakini walipokwisha kumweleza kila kitu ambacho Yosefu alikuwa amewaambia, na alipoona magari ya kukokotwa Yosefu aliyokuwa amempelekea ya kumchukua aende Misri, roho ya baba yao Yakobo ikahuishwa. Ndipo Israeli akasema, “Nimesadiki! Mwanangu Yosefu bado yu hai. Nitakwenda nikamwone kabla sijafa.”

Read More of Mwanzo 45

Mwanzo 46:1-34

Yakobo Aenda Misri

Hivyo Israeli akaondoka na vyote vilivyokuwa mali yake, naye alipofika Beer-Sheba, akamtolea dhabihu Mungu wa Isaki baba yake.

46:2 Mwa 15:1Mungu akanena na Israeli katika maono usiku na kusema, “Yakobo! Yakobo!”

Akajibu, “Mimi hapa.”

46:3 Mwa 12:2; 28:13Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa baba yako, usiogope kushuka Misri, kwa maana huko nitakufanya taifa kubwa. 46:4 Mwa 5:16Nitashuka Misri pamoja nawe, nami hakika nitakurudisha tena Kanaani. Mikono ya Yosefu mwenyewe ndiyo itakayofunga macho yako.”

46:5 Mwa 45:19Ndipo Yakobo akaondoka Beer-Sheba nao wana wa Israeli wakamchukua baba yao Yakobo na watoto wao na wake zao katika magari ya kukokotwa yale Farao aliyokuwa amempelekea kumsafirisha. 46:6 Kum 26:5; Mdo 7:15Wakachukua pia mifugo yao na mali walizokuwa wamezipata Kanaani, Yakobo na uzao wake wote wakashuka Misri. Akawachukua wanawe na binti zake, wajukuu wake wa kiume na wa kike, yaani uzao wake wote mpaka Misri.

Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli (Yakobo na wazao wake), waliokwenda Misri:

Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo.

Wana wa Reubeni ni:

Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi.

46:10 Kut 6:15Wana wa Simeoni ni:

Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli mwana wa mwanamke Mkanaani.

Wana wa Lawi ni:

Gershoni, Kohathi na Merari.

46:12 1Nya 2:5; Mt 1:3Wana wa Yuda ni:

Eri, Onani, Shela, Peresi na Zera (lakini Eri na Onani walifariki katika nchi ya Kanaani).

Wana wa Peresi ni:

Hesroni na Hamuli.

Wana wa Isakari ni:

Tola, Puva, Yashubu na Shimroni.

46:14 Mwa 30:20Wana wa Zabuloni ni:

Seredi, Eloni na Yaleeli.

46:15 Mwa 30:21Hawa ndio wana wa Lea aliomzalia Yakobo huko Padan-Aramu pamoja na binti yake Dina. Jumla ya wanawe na binti zake walikuwa thelathini na watatu.

46:16 Hes 26:15Wana wa Gadi ni:

Sefoni, Hagi, Shuni, Esboni, Eri, Arodi na Areli.

46:17 Mwa 30:13Wana wa Asheri ni:

Imna, Ishva, Ishvi na Beria.

Dada yao alikuwa Sera.

Wana wa Beria ni:

Heberi na Malkieli.

Hawa ndio watoto Zilpa aliomzalia Yakobo, ambao Labani alimpa binti yake Lea; jumla yao walikuwa kumi na sita.

Wana wa Raheli mke wa Yakobo ni:

Yosefu na Benyamini. 46:20 Mwa 41:51Huko Misri, Asenathi binti wa Potifera, aliyekuwa kuhani wa mji wa Oni,46:20 Yaani Heliopoli (Mji wa Jua). alimzalia Yosefu wana wawili, Manase na Efraimu.

46:21 1Nya 7:6-12Wana wa Benyamini ni:

Bela, Bekeri, Ashbeli, Gera, Naamani, Ehi, Roshi, Mupimu, Hupimu na Ardi.

Hawa ndio wana wa Raheli aliomzalia Yakobo; jumla yao ni kumi na wanne.

Mwana wa Dani ni:

Hushimu.

46:24 Mwa 30:8Wana wa Naftali ni:

Yaseeli, Guni, Yeseri na Shilemu.

46:25 Mwa 30:8Hawa walikuwa wana wa Bilha aliomzalia Yakobo, ambaye Labani alikuwa amempa Raheli binti yake; jumla yao walikuwa saba.

46:26 Kut 1:5; Kum 10:22Wote waliokwenda Misri pamoja na Yakobo, waliokuwa wazao wake hasa pasipo kuhesabu wakwe zake, walikuwa watu sitini na sita. 46:27 Mdo 7:14Pamoja na wana wawili waliozaliwa na Yosefu huko Misri, jumla yote ya jamaa ya Yakobo, waliokwenda Misri, walikuwa sabini.

46:28 Mwa 45:10Basi Yakobo akamtanguliza Yuda aende kwa Yosefu ili amwelekeze njia ya Gosheni. Walipofika nchi ya Gosheni, 46:29 Mwa 29:11gari kubwa zuri la Yosefu liliandaliwa, naye akaenda Gosheni kumlaki baba yake Israeli. Mara Yosefu alipofika mbele yake, alimkumbatia baba yake, akalia kwa muda mrefu.

46:30 Mwa 44:28Israeli akamwambia Yosefu, “Sasa niko tayari kufa, kwa kuwa nimejionea mwenyewe kwamba bado uko hai.”

46:31 Mwa 45:10Ndipo Yosefu akawaambia ndugu zake na watu wa nyumbani mwa baba yake, “Nitapanda kwa Farao na kumwambia, ‘Ndugu zangu na watu wa nyumbani mwa baba yangu, waliokuwa wakiishi katika nchi ya Kanaani, wamekuja kwangu. 46:32 Mwa 42:20Watu hao ni wachunga mifugo, huchunga mifugo, wamekuja na makundi ya kondoo, mbuzi na ngʼombe pamoja na kila kitu walicho nacho.’ 46:33 Mwa 47:3Farao atakapowaita na kuwaulizeni, ‘Kazi yenu ni nini?’ 46:34 Mwa 43:32Mjibuni, ‘Watumwa wako wamekuwa wachunga mifugo tangu ujana wetu mpaka sasa, kama baba zetu walivyofanya.’ Ndipo mtakaporuhusiwa kukaa katika nchi ya Gosheni, kwa kuwa wachunga mifugo wote ni chukizo kwa Wamisri.”

Read More of Mwanzo 46

Mwanzo 47:1-12

Yakobo Ambariki Farao

47:1 Mwa 46:31Yosefu akaenda na kumwambia Farao, “Baba yangu na ndugu zangu wamekuja kutoka nchi ya Kanaani wakiwa na makundi yao ya kondoo, mbuzi na ngʼombe, pamoja na kila kitu walicho nacho, nao sasa wapo huko Gosheni.” Akachagua ndugu zake watano na kuwaonyesha kwa Farao.

47:3 Mwa 46:33Farao akawauliza hao ndugu zake, “Kazi yenu ni nini?”

Wakamjibu, “Watumishi wako ni wachunga mifugo, kama vile baba zetu walivyokuwa.” 47:4 Mwa 46:34Pia wakamwambia Farao, “Tumekuja kukaa huku kwa muda mfupi, kwa sababu njaa ni kali huko Kanaani, na mifugo ya watumishi wako haina malisho. Kwa hiyo sasa, tafadhali uruhusu watumishi wako wakae huko Gosheni.”

Farao akamwambia Yosefu, “Baba yako na ndugu zako wamekuja kwako, 47:6 Kut 18:21nayo nchi ya Misri ipo mbele yako, uwakalishe baba yako na ndugu zako katika sehemu iliyo bora kupita zote katika nchi. Na waishi Gosheni. Kama unamfahamu yeyote miongoni mwao mwenye uwezo maalum, waweke wawe wasimamizi wa mifugo yangu.”

47:7 2Sam 14:22Ndipo Yosefu akamleta Yakobo baba yake na kumtambulisha mbele ya Farao. Baada ya Yakobo kumbariki Farao, Farao akamuuliza, “Je una umri gani?”

47:9 Mwa 25:7Naye Yakobo akamwambia Farao, “Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni miaka 130. Miaka yangu imekuwa michache na ya taabu, wala haikufikia miaka ya kusafiri ya baba zangu.” 47:10 Mwa 47:7Kisha Yakobo akambariki Farao, naye akaondoka mbele ya uso wake.

47:11 Hes 33:3, 5Ndipo Yosefu akawakalisha baba yake na ndugu zake katika nchi ya Misri na kuwapa milki katika sehemu bora sana ya nchi, wilaya ya Ramesesi, kama Farao alivyoelekeza. 47:12 Mwa 45:11Pia Yosefu akampa baba yake, na ndugu zake na wote wa nyumbani mwa baba yake vyakula, kwa kulingana na hesabu ya watoto wao.

Read More of Mwanzo 47