Mwanzo 4:17-26, Mwanzo 5:1-32, Mwanzo 6:1-22 NEN

Mwanzo 4:17-26

4:17 Za 55:9; 49:11Kaini akakutana kimwili na mkewe, naye akapata mimba na akamzaa Enoki. Wakati huo Kaini alikuwa anajenga mji, akauita Enoki jina la mtoto wake. Enoki akamzaa Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli, Mehuyaeli akamzaa Methushaeli, na Methushaeli akamzaa Lameki.

4:19 Mwa 2:9; 29:28; Kum 21:15; Rut 4:11; 1Sam 1:2Lameki alioa wanawake wawili, mmoja aliitwa Ada, na mwingine Sila. Ada akamzaa Yabali ambaye ni baba wa wale walioishi katika mahema na kufuga wanyama. 4:21 Mwa 31:27; Kut 15:20; 1Sam 16:16; 1Nya 25:3; Za 33:2; 43:4; 150:4; Isa 16:11; Dan 3:5; Ay 21:12; 30:31Kaka yake aliitwa Yubali, aliyekuwa baba wa wote wapigao zeze na filimbi. 4:22 Kut 35:35; 1Sam 13:19; 2Fal 24:14Pia Sila alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Tubali-Kaini ambaye alifua vifaa vya aina mbalimbali vya shaba na chuma. Naama alikuwa dada wa Tubali-Kaini.

4:23 Mwa 9:6-9; Kut 20:13; 21:12; 23:7; Law 19:18; 24:17; Kum 27:24Lameki akawaambia wake zake,

“Ada na Sila nisikilizeni mimi;

wake wa Lameki sikieni maneno yangu.

Nimemuua mtu kwa kunijeruhi,

kijana mdogo kwa kuniumiza.

4:24 Kum 32:35; 2Fal 9:7; Za 18:47; Isa 35:4; Yer 51:56; Mt 18:22; Nah 1:2Kama Kaini atalipizwa kisasi mara saba,

basi Lameki itakuwa mara sabini na saba.”

4:25 Mwa 5:3; 1Nya 1:1Adamu akakutana kimwili na mke wake tena, akamzaa mwana, akamwita Sethi, akisema, “Mungu amenijalia mwana mwingine badala ya Abeli, kwa kuwa Kaini alimuua.” 4:26 Mwa 5:3; 12:8; 13:4; 21:33; 22:9; 26:25; 33:20; Lk 3:38; Kut 17:15; Sef 3:9; 1Fal 18:24; Za 116:17; Yoe 2:32; Mdo 2:21Naye Sethi akamzaa mwana, akamwita Enoshi.

Wakati huo watu wakaanza kuliitia jina la Bwana.

Read More of Mwanzo 4

Mwanzo 5:1-32

Kutoka Adamu Hadi Noa

(1 Nyakati 1:1-4)

5:1 Mwa 1:27; 2:4; 1Nya 1:1; Kol 3:10; Efe 4:24Hii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu.

Wakati Mungu alipomuumba Adamu, alimfanya kwa sura ya Mungu. 5:2 Mwa 1:27-28; Mt 19:4; Mk 10:6; Gal 3:28Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa, akawaita “mwanadamu.”

5:3 Mwa 1:26; 4:25; 1Kor 15:49; Lk 3:38Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, alikuwa na mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita Sethi. Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka 800, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 5:5 Mwa 2:17; 3:19; Ebr 9:27Adamu aliishi jumla ya miaka 930, ndipo akafa.

5:6 Mwa 4:26; Lk 3:38Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi. Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka 807, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Sethi aliishi jumla ya miaka 912, ndipo akafa.

5:9 1Nya 1:2; Lk 3:37Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani. Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815, naye alikuwa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Enoshi aliishi jumla ya miaka 905, ndipo akafa.

5:12 1Nya 1:2; Lk 3:37Kenani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Kenani aliishi jumla ya miaka 910, ndipo akafa.

Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi. Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Mahalaleli aliishi jumla ya miaka 895, ndipo akafa.

5:18 1Nya 1:3; Lk 3:37; Yud 14Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, akamzaa Enoki. Baada ya kumzaa Enoki, Yaredi aliishi miaka 800, naye akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Yaredi aliishi jumla ya miaka 962, ndipo akafa.

5:21 1Nya 1:3; Lk 3:37Enoki alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. 5:22 Mwa 6:9; 17:1; 24:40; 48:15; 2Fal 20:3; Za 116:9; Mal 2:6; Mik 6:8Baada ya kumzaa Methusela, Enoki alitembea na Mungu miaka 300, na akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Enoki aliishi jumla ya miaka 365. 5:24 2Fal 2:1, 11; Za 49:15; 73:24; 89:48; Ebr 11:5Enoki akatembea na Mungu, kisha akatoweka, kwa sababu Mungu alimchukua.

5:25 1Nya 1:3; Lk 3:36Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, akamzaa Lameki. Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Methusela aliishi jumla ya miaka 969, ndipo akafa.

Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana. 5:29 1Nya 1:3; Lk 3:36; Mwa 3:17; Rum 8:20Akamwita jina lake Noa, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na Bwana.” Baada ya Noa kuzaliwa, Lameki aliishi miaka 595, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. Lameki aliishi jumla ya miaka 777, ndipo akafa.

5:32 Mwa 7:6, 11; 8:13; 6:10; 9:18; 10:1; Lk 3:36; 1Nya 1:4; Isa 65:20Baada ya Noa kuishi miaka 500, aliwazaa Shemu, Hamu na Yafethi.

Read More of Mwanzo 5

Mwanzo 6:1-22

Gharika Kuu

6:1 Mwa 1:28Watu walipoanza kuongezeka idadi katika uso wa dunia na watoto wa kike wakazaliwa kwao, 6:2 Ay 1:6; 2:1; Kum 21:11; Mwa 4:19wana wa Mungu wakawaona kuwa hao binti za wanadamu walikuwa wazuri wa sura, wakaoa yeyote miongoni mwao waliyemchagua. 6:3 Ay 10:9; 34:14; Gal 5:15-17; Isa 40:6; 57:16; 1Pet 3:20; Za 78:39; 103:14Ndipo Bwana akasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa, siku zake zitakuwa miaka 120.”

6:4 Hes 13:33; Mwa 11:4Wanefili walikuwako duniani siku hizo, na baadaye, hao wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu na kuzaa nao. Wanefili walikuwa mashujaa na watu waliojulikana wa zamani hizo.

6:5 Mwa 38:7; 8:21; Ay 34:26; Yer 1:16; 44:5; Eze 3:19; Za 14:1-3Bwana akaona jinsi uovu wa mwanadamu ulivyokuwa mkubwa duniani, na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu. 6:6 Kut 32:14; 1Sam 15:11, 35; 2Sam 24:16; 1Nya 21:15; Isa 63:10; Efe 4:30; Yer 18:7-10Bwana akasikitika kwamba alimuumba mwanadamu duniani, moyo wa Mungu ukajaa masikitiko. 6:7 Eze 33:28; Sef 1:2, 18; Mwa 7:4, 21; Kut 28:36; 29:20Kwa hiyo Bwana akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemuumba kutoka kwenye uso wa dunia, wanadamu na wanyama, pamoja na viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Kwa maana nasikitika kuwaumba.” 6:8 Eze 14:14; Mwa 19:19; 39:4; Kut 33:12-17; 34:9; Hes 11:15; Rut 2:2; Lk 1:30; Mdo 7:46Lakini Noa akapata kibali machoni pa Bwana.

6:9 Mwa 2:4; 5:22; 7:1; 17:1; Kum 18:13; 2Sam 22:24; Ay 1:1; 4:6; 9:21; 12:4; 31:6; Za 15:2; 18:23; 19:13; 37:37; Mit 2:7; Yer 15:1; Eze 14:14-20; Dan 10:11; Lk 1:6; Ebr 11:7; 2Pet 2:5Hivi ndivyo vizazi vya Noa.

Noa alikuwa mtu wa haki, na mkamilifu miongoni mwa watu wa wakati wake, tena alitembea na Mungu. 6:10 Lk 3:36; Mwa 5:32Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi.

6:11 Kum 31:29; Amu 2:19; Za 73:6; Eze 7:23; 8:17; 28:16; Mal 2:16Wakati huu dunia ilikuwa imejaa uharibifu na ukatili machoni pa Mungu. 6:12 Kut 32:7; Kum 4:16; 9:12, 24; Za 14:1-3Mungu akaona jinsi dunia ilivyoharibika, kwa maana watu wote duniani walikuwa wameharibu njia zao. 6:13 Kum 28:63; 2Fal 8:19; Ezr 9:14; Yer 44:11, 27; Mwa 7:4, 21-23; Ay 34:15; Isa 5:6; 24:1-3; Eze 7:2-3Kwa hiyo Mungu akamwambia Noa, “Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika mimi nitaangamiza watu pamoja na dunia. 6:14 Ebr 11:7; 1Pet 3:20; Kut 2:3Kwa hiyo jitengenezee safina kubwa kwa mbao za mvinje, tengeneza vyumba ndani yake na uipake lami ndani na nje. Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa 300,6:15 Dhiraa 300 ni sawa na mita 135. upana wake dhiraa hamsini6:15 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22:5. na kimo chake dhiraa thelathini.6:15 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13:5. Itengenezee paa na umalizie safina kwa kuacha nafasi ya dhiraa moja6:16 Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45. juu. Weka mlango ubavuni mwa safina, na uifanye ya ghorofa ya chini, ya kati na ya juu. 6:17 Za 29:10; 2Pet 2:5Nitaleta gharika ya maji juu ya nchi ili kuangamiza uhai wote chini ya mbingu, kila kiumbe chenye pumzi ya uhai ndani yake. Kila kitu juu ya nchi kitaangamia. 6:18 Mwa 7:1, 7; 9:9-16; 17:7; 19:12; Kut 6:4; 34:10; Za 25:10; 74:20; 106:45; Eze 16:60; Kum 29:13-15; Isa 55:3; Hag 2:5; Yer 32:40; 1Pet 3:20Lakini Mimi nitaweka Agano langu na wewe, nawe utaingia ndani ya Safina, wewe pamoja na mke wako, wanao na wake zao. 6:19 Mwa 7:15Utaingiza ndani ya Safina kila aina ya kiumbe hai wawili wawili, wa kiume na wa kike, ili kuwahifadhi hai pamoja na wewe. 6:20 Mwa 7:3, 15; 1:11Wawili wa kila aina ya ndege, wa kila aina ya mnyama na wa kila aina ya kitambaacho ardhini watakuja kwako ili wahifadhiwe hai. Utachukua kila aina ya chakula kitakacholiwa, na ukiweke akiba kama chakula kwa ajili yako na yao.”

6:22 Mwa 7:5; 9:16; Kut 7:6; 39:43; 40:16, 19, 21-32Noa akafanya kila kitu kama vile Mungu alivyomwamuru.

Read More of Mwanzo 6