Mwanzo 34:1-31, Mwanzo 35:1-29 NEN

Mwanzo 34:1-31

Dina Na Washekemu

34:1 Mwa 30:21Basi Dina, binti wa Yakobo aliyezaliwa na Lea, akatoka nje kuwatembelea wanawake wa nchi ile. 34:2 Mwa 33:19Ikawa Shekemu mwana wa Hamori Mhivi, mtawala wa eneo lile alipomwona, akamchukua na kumnajisi. Moyo wake ukavutwa sana kwa Dina binti Yakobo, akampenda huyu msichana na akazungumza naye kwa kumbembeleza. 34:4 Mwa 21:21Shekemu akamwambia baba yake Hamori, “Nipatie msichana huyu awe mke wangu.”

34:5 Mwa 34:2-3Yakobo aliposikia kwamba binti yake Dina amenajisiwa, wanawe walikuwa mashambani wakichunga mifugo yake, kwa hiyo akalinyamazia jambo hilo mpaka waliporudi nyumbani.

34:6 Amu 14:2-5Kisha Hamori baba yake Shekemu akaenda kuzungumza na Yakobo. 34:7 Kum 22:21; Amu 20:6Basi wana wa Yakobo walikuwa wamerudi kutoka mashambani mara tu waliposikia kilichotokea. Walikuwa wamejawa na huzuni na ghadhabu, kwa sababu Shekemu alikuwa amefanya jambo la aibu katika Israeli kwa kukutana kimwili na binti wa Yakobo, kitu ambacho hakingepasa kufanyika.

34:8 Mwa 21:21Lakini Hamori akawaambia, “Moyo wa mwanangu Shekemu umeelekea kwa binti yenu. Tafadhali mpeni awe mke wake. 34:9 Kum 7:3Oaneni na sisi, tupeni binti zenu, nanyi mchukue binti zetu. 34:10 Mwa 47:6, 27; 13:9Mwaweza kuishi katikati yetu, nchi ni wazi kwenu. Ishini ndani yake, fanyeni biashara humu na mjipatie mali.”

34:11 Mwa 32:5Kisha Shekemu akamwambia baba yake Dina pamoja na ndugu zake, “Na nipate kibali machoni penu, nami nitawapa chochote mtakachosema. 34:12 Kum 22:29; 1Sam 18:25Niambieni kiasi cha mahari na zawadi nitakayoileta, hata iwe kubwa kiasi gani, nami nitawalipa chochote mtakachodai. Nipeni tu huyu msichana awe mke wangu.”

34:13 Mwa 27:36Kwa sababu ndugu yao Dina alikuwa amenajisiwa, wana wa Yakobo wakajibu kwa udanganyifu walipozungumza na Shekemu pamoja na baba yake Hamori. 34:14 Mwa 17:14; Isa 31:4Wakawaambia, “Hatuwezi kufanya jambo kama hili, hatuwezi kumtoa dada yetu kwa mtu ambaye hakutahiriwa. Hiyo itakuwa aibu kwetu. 34:15 1Sam 11:2; Kut 12:48Tutakuruhusu kwa sharti moja tu, kwamba mtakuwa kama sisi kwa kuwatahiri wanaume wenu wote. 34:16 Mwa 33:19Kisha tutawapa binti zetu na sisi tutawachukua binti zenu. Tutaishi kwenu na tutakuwa watu wamoja nanyi. Lakini mkikataa kutahiriwa, tutamchukua ndugu yetu na kuondoka.”

Pendekezo lao likawa jema kwa Hamori na Shekemu mwanawe. Kijana mdogo, ambaye alikuwa ameheshimiwa kati ya wote walioishi nyumbani mwa baba yake, hakupoteza muda kufanya waliyoyasema, kwa sababu alikuwa amependezwa sana na binti Yakobo. 34:20 Mwa 18:1Kwa hiyo Hamori na Shekemu mwanawe walikwenda kwenye lango la mji kuzungumza na wenzao wa mjini. 34:21 Mwa 33:19Wakasema, “Hawa watu ni marafiki kwetu, tuwaruhusu waishi katika nchi yetu na kufanya biashara ndani yake, nchi ina nafasi tele kwa ajili yao. Tunaweza kuoa binti zao. Nao wanaweza kuoa binti zetu. 34:22 Mwa 34:15Lakini watu hao watakuwa tayari kukubali kuishi nasi kama watu wamoja nao kwa sharti kwamba wanaume wetu watahiriwe, kama wao. 34:23 Mwa 34:28Je, si mifugo yao, mali zao na wanyama wao wengine wote watakuwa wetu? Basi na tuwape kibali, nao wataishi miongoni mwetu.”

34:24 Mwa 18:1Wanaume wote waliotoka nje ya lango la mji walikubaliana na Hamori na Shekemu mwanawe na kila mwanaume katika mji ule akatahiriwa.

34:25 Mwa 49:5; 49:7Baada ya siku tatu, wakati wote wakiwa wangali katika maumivu, wana wawili wa Yakobo, yaani Simeoni na Lawi, ndugu zake Dina, wakachukua panga zao na kuvamia mji ambao haukutazamia vita, wakaua kila mwanaume. Wakawaua Hamori na Shekemu mwanawe kwa upanga kisha wakamchukua Dina kutoka nyumba ya Shekemu na kuondoka. Wana wa Yakobo walipita juu ya maiti katika kuteka nyara mji ule ambamo dada yao alikuwa amenajisiwa. Wakachukua kondoo na mbuzi, ngʼombe, punda na kila kitu kilichokuwa chao ndani ya mji ule na mashambani. Walichukua utajiri wao wote pamoja na wanawake na watoto wao, wakachukua nyara kila kitu ndani ya nyumba zao.

Kisha Yakobo akawaambia Simeoni na Lawi, “Mmeleta taabu kwangu kwa kunifanya ninuke kama uvundo kwa Wakanaani na Waperizi, watu waishio katika nchi hii. Sisi ni wachache, kama wakiunganisha nguvu zao dhidi yangu na kunishambulia, mimi na nyumba yangu tutaangamizwa.”

Lakini wakamjibu, “Je, ilikuwa vyema kumtendea dada yetu kama kahaba?”

Read More of Mwanzo 34

Mwanzo 35:1-29

Yakobo Arudi Betheli

35:1 Mwa 12:8Kisha Mungu akamwambia Yakobo, “Panda uende Betheli ukakae huko na ukamjengee Mungu madhabahu huko, Yeye aliyekutokea ulipokuwa unamkimbia Esau ndugu yako.”

35:2 Yos 24:15; Kut 19:10, 14Hivyo Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake pamoja na wote waliokuwa naye, “Iondoeni miungu ya kigeni ile iliyoko katikati yenu, jitakaseni na mkabadilishe nguo zenu. 35:3 Mwa 32:7; Amu 2:15Kisha njooni, twende Betheli, mahali nitakapomjengea Mungu madhabahu, aliyenijibu katika siku ya shida yangu, ambaye amekuwa pamoja nami popote nilipokwenda.” 35:4 Mwa 24:22Kwa hiyo wakampa Yakobo miungu yote ya kigeni waliyokuwa nayo, pamoja na pete zilizokuwa masikioni mwao. Yakobo akavizika chini ya mti wa mwaloni huko Shekemu. 35:5 Kut 15:16Kisha wakaondoka, na hofu ya Mungu ikawapata miji yote iliyowazunguka. Kwa hiyo hakuna aliyewafuatia wana wa Yakobo.

35:6 Mwa 28:19; 10:19Yakobo na watu wote waliokuwa pamoja naye wakafika Luzu (ndio Betheli), katika nchi ya Kanaani. 35:7 Mwa 8:20Huko akajenga madhabahu na akapaita mahali pale El-Betheli,35:7 El-Betheli maana yake Mungu wa Betheli. kwa sababu mahali pale ndipo Mungu alipojifunua kwake alipokuwa akimkimbia ndugu yake.

35:8 Mwa 24:59; 12:8Wakati huu Debora, mlezi wa Rebeka, akafa na akazikwa chini ya mti wa mwaloni ulioko chini ya Betheli. Kwa hiyo pakaitwa Alon-Bakuthi.35:8 Alon-Bakuthi maana yake Mwaloni wa Kilio.

35:9 Mwa 28:13; 32:29Baada ya Yakobo kurudi kutoka Padan-Aramu, Mungu alimtokea tena na kumbariki. 35:10 Mwa 17:5Mungu akamwambia, “Jina lako ni Yakobo, lakini hutaitwa tena Yakobo, jina lako utakuwa Israeli.” Kwa hiyo akamwita Israeli.

35:11 Mwa 17:1; 17:6Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi,35:11 Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote). ukazae na kuongezeka. Taifa na jamii ya mataifa itatoka kwako, nao wafalme watatoka viunoni mwako. 35:12 Mwa 28:13; 12:7Nchi niliyowapa Abrahamu na Isaki nakupa wewe pia, nami nitawapa wazao wako baada yako.” 35:13 Mwa 17:22Kisha Mungu akapanda juu kutoka kwake mahali pale alipozungumza naye.

35:14 Mwa 28:18; Kut 29:40Yakobo akasimamisha nguzo ya jiwe mahali pale Mungu alipozungumza naye, akamimina sadaka ya kinywaji juu yake, pia akamimina mafuta juu yake. 35:15 Mwa 12:8Yakobo akapaita mahali pale Mungu alipozungumza naye Betheli.35:15 Betheli maana yake Nyumba ya Mungu.

Vifo Vya Raheli Na Isaki

35:16 Mwa 48:7Kisha wakaondoka Betheli. Walipokuwa umbali fulani kabla ya kufika Efrathi, Raheli akaanza kusikia uchungu na alipata shida kuu. 35:17 Kut 1:15; Mwa 30:24Alipokuwa katika shida hii katika kujifungua, mkunga akamwambia, “Usiogope, kwa sababu umempata mwana mwingine.” 35:18 1Sam 4:21Hapo alipopumua pumzi yake ya mwisho, kwa maana alikuwa akifa, akamwita mwanawe Benoni.35:18 Benoni maana yake Mwana wa huzuni yangu. Lakini babaye akamwita Benyamini.35:18 Benyamini maana yake Mwana wa mkono wangu wa kuume.

35:19 Mwa 48:7Kwa hiyo Raheli akafa, akazikwa kando ya njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu). 35:20 1Sam 10:2; 6:18Juu ya kaburi lake, Yakobo akasimamisha nguzo, ambayo mpaka leo inatambulisha kaburi la Raheli.

Israeli akaendelea tena na safari yake na kupiga hema mbele mnara wa Ederi. Wakati Israeli alipokuwa akiishi katika nchi ile, Reubeni mwanawe alikutana kimwili na suria wa baba yake aitwaye Bilha, naye Israeli akasikia jambo hili.

Yakobo alikuwa na wana kumi na wawili:

Wana wa Lea walikuwa:

Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo,

Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari na Zabuloni.

35:24 Mwa 30:24; 35:18Wana wa Raheli walikuwa:

Yosefu na Benyamini.

35:25 Mwa 30:24Wana waliozaliwa na Bilha mtumishi wa kike wa Raheli walikuwa:

Dani na Naftali.

35:26 Mwa 37:2Wana waliozaliwa na Zilpa mtumishi wa kike wa Lea walikuwa:

Gadi na Asheri.

Hawa walikuwa wana wa Yakobo, waliozaliwa kwake akiwa Padan-Aramu.

35:27 Mwa 13:18; Amu 1:10Yakobo akarudi nyumbani kwa baba yake Isaki huko Mamre, karibu na Kiriath-Arba (yaani Hebroni), ambapo walikuwa wameishi Abrahamu na Isaki. 35:28 Mwa 25:7Isaki aliishi miaka 180. 35:29 Mwa 15:15; 25:8-9Kisha Isaki akapumua pumzi yake ya mwisho akafa, akakusanywa pamoja na watu wake akiwa mzee wa miaka mingi. Nao wanawe Esau na Yakobo wakamzika.

Read More of Mwanzo 35