Mwanzo 32:1-32, Mwanzo 33:1-20 NEN

Mwanzo 32:1-32

Yakobo Ajiandaa Kukutana Na Esau

Yakobo pia akaondoka akaenda zake, nao malaika wa Mungu wakakutana naye. Yakobo alipowaona, akasema, “Hii ni kambi ya Mungu!” Kwa hiyo akapaita mahali pale Mahanaimu.32:2 Mahanaimu maana yake Kambi mbili.

32:3 Mwa 25:30Yakobo akatuma wajumbe kumtangulia kwa Esau ndugu yake huko Seiri, katika nchi ya Edomu. 32:4 Mwa 18:3Akawaagiza akisema: “Hili ndilo mtakalomwambia bwana wangu Esau: ‘Mtumishi wako Yakobo anasema, nimekuwa nikiishi pamoja na Labani na nimekuwako huko mpaka sasa. 32:5 Mwa 24:9; 34:11Ninao ngʼombe na punda, kondoo na mbuzi, watumishi wa kiume na wa kike. Sasa ninatuma ujumbe huu kwa bwana wangu, ili nipate kibali machoni pako.’ ”

32:6 Mwa 33:1Wajumbe waliporudi kwa Yakobo, wakamwambia, “Tulikwenda kuonana na ndugu yako Esau, naye sasa anakuja kukulaki akifuatana na wanaume 400.”

Kwa hofu kuu na huzuni, Yakobo akagawanya watu aliokuwa nao katika makundi mawili, pia akagawanya makundi ya kondoo na mbuzi, na vilevile ngʼombe na ngamia. Yakobo alifikiri, “Kama Esau akija na kushambulia kundi moja, kundi lililobaki litaweza likanusurika.”

32:9 Mwa 31:13Ndipo Yakobo akaomba, “Ee Mungu wa baba yangu Abrahamu, Mungu wa baba yangu Isaki, Ee Bwana, ambaye uliniambia, ‘Rudi katika nchi yako na jamaa yako, nami nitakufanya ustawi,’ 32:10 Mwa 24:27mimi sistahili fadhili na uaminifu wako wote ulionitendea mimi mtumishi wako. Nilikuwa na fimbo tu mkononi mwangu nilipovuka mto huu wa Yordani, lakini sasa ninayo makundi mawili. 32:11 Mwa 27:41Nakuomba, uniokoe na mkono wa ndugu yangu Esau, kwa maana ninaogopa kuwa atakuja kunishambulia, pia mama pamoja na watoto wao. 32:12 Hos 1:10Lakini umeshasema, ‘Hakika nitakufanya ustawi na kuufanya uzao wako kuwa mwingi kama mchanga wa baharini ambao hauwezi kuhesabika!’ ”

32:13 Mwa 43:11, 15, 25, 26; Mit 18:16Akalala pale usiku ule, miongoni mwa vitu alivyokuwa navyo, akachagua zawadi kwa ajili ya Esau ndugu yake: 32:14 Hes 7:88Mbuzi waume ishirini na mbuzi wake 200, kondoo dume ishirini na kondoo wake 200. 32:15 Mwa 13:2Ngamia wake thelathini pamoja na ndama zao, ngʼombe wake arobaini na mafahali kumi, punda wake ishirini na punda waume kumi. 32:16 Mwa 33:8Akaviweka chini ya uangalizi wa watumishi wake, kila kundi peke yake na kuwaambia, “Nitangulieni na kuacha nafasi kati ya makundi.”

Akamwagiza yule aliyetangulia kuwa, “Ndugu yangu Esau atakapokutana nawe na kukuuliza, ‘Wewe ni wa nani? Unakwenda wapi? Wanyama hawa wote mbele yako ni mali ya nani?’ 32:18 Mwa 18:3Ndipo utakaposema, ‘Ni mali ya mtumishi wako Yakobo. Ni zawadi ambazo zimetumwa kwa bwana wangu Esau, naye anakuja nyuma yetu.’ ”

Akamwagiza pia yule mtumishi wa kundi la pili, la tatu na yale mengine yote yaliyofuata akiwaambia, “Mtamwambia Esau maneno hayo hayo mtakapokutana naye. 32:20 1Sam 9:7Hakikisheni mmesema, ‘Mtumishi wako Yakobo anakuja nyuma yetu.’ ” Kwa kuwa alifikiri, “Nitaweza kumtuliza kwa zawadi hizi ninazotanguliza, hatimaye, nitakapomwona, huenda atanikubali.” Kwa hiyo zawadi za Yakobo zilitangulia mbele yake, lakini yeye mwenyewe alilala kambini usiku ule.

Yakobo Ashindana Mweleka Na Mungu

32:22 Kum 2:37; 3:16Usiku ule Yakobo akaamka akawachukua wake zake wawili, watumishi wake wawili wa kike na wanawe kumi na mmoja na akavuka kivuko cha Yaboki. Baada ya kuwavusha ngʼambo ya kijito, alivusha pia mali zake zote. Kwa hiyo Yakobo akaachwa peke yake na mtu mmoja akashikana naye mweleka mpaka mapambazuko. Yule mtu alipoona kuwa hawezi kumshinda, aligusa kiungio cha nyonga ya Yakobo kwa hiyo nyonga yake ikateguka wakati alipokuwa akishikana mweleka na yule mtu. 32:26 Hos 12:4Ndipo yule mtu akasema, “Niache niende, kwa kuwa ni mapambazuko.”

Lakini Yakobo akajibu, “Sitakuacha uende usiponibariki.”

Yule mtu akamuuliza, “Jina lako nani?”

Akajibu, “Yakobo.”

32:28 Mwa 17:5Ndipo yule mtu akasema, “Jina lako halitakuwa tena Yakobo, bali Israeli,32:28 Israeli maana yake Yeye ashindanaye na Mungu. kwa sababu umeshindana na Mungu na watu pia, nawe umeshinda.”

Yakobo akasema, “Tafadhali niambie jina lako.”

Lakini akajibu, “Kwa nini kuniuliza Jina langu?” Ndipo akambariki huko.

32:30 Mwa 16:13Kwa hiyo Yakobo akapaita mahali pale Penieli,32:30 Penieli maana yake Uso wa Mungu, ambalo ni sawa na Penueli kwa Kiebrania. akasema, “Ni kwa sababu nimemwona Mungu uso kwa uso na bado maisha yangu yameokoka.”

32:31 Amu 8:9Jua lilikuwa linachomoza Yakobo alipoondoka Penueli, naye alikuwa akichechemea kwa sababu ya nyonga yake. Kwa hiyo mpaka leo Waisraeli hawali mshipa ulioungana na kiungio cha nyonga, kwa sababu kiungio cha nyonga ya Yakobo kiliteguliwa karibu na mshipa huo.

Read More of Mwanzo 32

Mwanzo 33:1-20

Yakobo Akutana Na Esau

33:1 Mwa 32:6Yakobo akainua macho akamwona Esau akija na watu wake 400, kwa hiyo akawagawanya watoto kati ya Lea, Raheli na wale watumishi wake wawili wa kike. Akawaweka wale watumishi wa kike na watoto wao mbele, Lea na watoto wake wakafuata, Raheli na Yosefu wakaja nyuma. 33:3 Mwa 42:6Yeye mwenyewe akatangulia mbele na kusujudu mara saba alipomkaribia ndugu yake.

Lakini Esau akamkimbilia Yakobo kumlaki na kumkumbatia, akamwangukia shingoni na kumbusu. Nao wakalia. 33:5 Za 127:3; Isa 8:18Esau akainua macho akawaona wale wanawake na watoto. Akauliza, “Hawa uliofuatana nao ni nani?”

Yakobo akamjibu, “Ni watoto ambao Mungu amempa mtumishi wako kwa neema.”

Kisha wale watumishi wa kike na watoto wao wakakaribia na kusujudu. Kisha Lea na watoto wake wakaja na kusujudu. Mwisho wa wote wakaja Yosefu na Raheli, nao pia wakasujudu.

33:8 Mwa 24:9; 32:14-16Esau akauliza, “Una maana gani kuhusu makundi hayo yote niliyokutana nayo?”

Akasema, “Ni ili kupata kibali machoni pako, bwana wangu.”

33:9 Mwa 13:6Lakini Esau akamwambia, “Ndugu yangu, tayari nina wingi wa mali. Ulivyo navyo viwe vyako mwenyewe.”

33:10 Mwa 16:13Yakobo akasema, “La hasha! Tafadhali, kama nimepata kibali machoni pako, upokee zawadi hii kutoka kwangu. Kwa maana kuuona uso wako, ni kama kuuona uso wa Mungu, kwa kuwa umenipokea kwa takabali kubwa. 33:11 1Sam 25:27Tafadhali ukubali zawadi iliyoletwa kwako, kwa kuwa Mungu amenineemesha na ninavyo vyote ninavyohitaji.” Kwa sababu Yakobo alisisitiza, Esau akapokea.

Ndipo Esau akasema, “Na tuendelee na safari, nitakuwa pamoja nawe.”

33:13 Isa 40:11Lakini Yakobo akamwambia, “Bwana wangu unajua kwamba watoto ni wachanga na kwamba ni lazima nitunze hawa kondoo wake na ngʼombe wanaonyonyesha. Wakipelekwa kwa haraka hata kama ni kwa siku moja tu, wanyama wote watakufa. 33:14 Kut 12:38Hivyo bwana wangu umtangulie mtumishi wako, wakati mimi nikija polepole kwa mwendo wa makundi yaliyo mbele yangu na mwendo wa watoto, mpaka nifike kwa bwana wangu huko Seiri.”

33:15 Mwa 32:5Esau akamwambia, “Basi na niwaache baadhi ya watu wangu pamoja nawe.”

Yakobo akauliza, “Lakini kwa nini ufanye hivyo, niache tu nipate kibali machoni pa bwana wangu.”

33:16 Mwa 14:6Hivyo siku hiyo Esau akashika njia akarudi Seiri. 33:17 Amu 8:5, 6, 8, 14-16Pamoja na hayo, Yakobo akaenda Sukothi,33:17 Sukothi maana yake Vibanda. mahali alipojijengea makazi kwa ajili yake na mabanda kwa ajili ya mifugo yake. Hii ndiyo sababu sehemu ile inaitwa Sukothi.

33:18 Mwa 12:6Baada ya Yakobo kutoka Padan-Aramu, alifika salama katika mji wa Shekemu huko Kanaani na kuweka kambi yake karibu na mji. 33:19 Yos 24:32; Yn 4:5Akanunua kiwanja kutoka kwa wana wa Hamori, baba wa Shekemu, kwa bei ya vipande mia vya fedha, ambapo alipiga hema lake. Pale akajenga madhabahu na kupaita El-Elohe-Israeli.33:20 El-Elohe-Israeli maana yake Mungu, Mungu wa Israeli au Mwenye Nguvu ni Mungu wa Israeli.

Read More of Mwanzo 33