Mwanzo 29:1-35, Mwanzo 30:1-43 NEN

Mwanzo 29:1-35

Yakobo Awasili Padan-Aramu

29:1 Mwa 25:6Kisha Yakobo akaendelea na safari yake na akafika kwenye nchi za mataifa ya mashariki. Huko akaona kisima katika shamba, pamoja na makundi matatu ya kondoo yamelala karibu na kisima hicho kwa sababu walikuwa wanakunywa maji kutoka kwenye kisimani hicho. Jiwe lililokuwa mdomoni mwa kisima lilikuwa kubwa. Wakati kondoo wanapokuwa wamekusanyika hapo, wachungaji huvingirisha jiwe hilo kutoka kwenye mdomo wa kisima na kunywesha kondoo. Kisha hulirudisha jiwe mahali pake juu ya mdomo wa kisima.

29:4 Mwa 42:7; Amu 19:17Yakobo aliwauliza wachungaji, “Ndugu zangu, ninyi mmetoka wapi?”

Wakamjibu, “Tumetoka Harani.”

Aliwaambia, “Je, mnamjua Labani, mjukuu wa Nahori?”

Wakamjibu, “Ndiyo, tunamfahamu.”

29:6 Mwa 30:22-27; Kut 2:16Kisha Yakobo akawauliza, “Je, yeye ni mzima?”

Wakasema, “Ndiyo, ni mzima, na hapa yuaja Raheli binti yake akiwa na kondoo.”

Akasema, “Tazama, jua bado liko juu, si wakati wa kukusanya mifugo. Nywesheni kondoo na mwarudishe malishoni.”

Walijibu, “Haiwezekani, mpaka kondoo wote wakusanyike na jiwe liwe limevingirishwa kutoka mdomo wa kisima. Ndipo tutanywesha kondoo.”

Alipokuwa akizungumza nao, Raheli akaja pamoja na kondoo wa baba yake, kwa maana alikuwa mchunga kondoo. Yakobo alipomwona Raheli binti Labani, ndugu wa mama yake, pamoja na kondoo wa Labani, alikwenda na kulivingirisha jiwe kutoka mdomoni mwa kisima na kuwanywesha kondoo wa mjomba wake. 29:11 Mwa 33:4Kisha Yakobo akambusu Raheli na akaanza kulia kwa sauti. 29:12 Mwa 24:28; Lk 15:20Yakobo alikuwa amemwambia Raheli kuwa yeye alikuwa jamaa ya baba yake, na kwamba ni mwana wa Rebeka. Basi Raheli alikimbia na kumweleza baba yake.

29:13 Mwa 24:29; Lk 15:20Mara Labani aliposikia habari kuhusu Yakobo, mwana wa ndugu yake, aliharakisha kwenda kumlaki. Akamkumbatia na kumbusu, halafu akamleta nyumbani kwake, kisha Yakobo akamwambia mambo yote. 29:14 Amu 9:2; Isa 58:7Ndipo Labani akamwambia, “Wewe ni nyama yangu na damu yangu mwenyewe.”

Yakobo Awaoa Lea Na Raheli

Baada ya Yakobo kukaa kwa Labani mwezi mzima, Labani akamwambia, “Kwa vile wewe ni jamaa yangu, ndiyo sababu unifanyie kazi bila ujira? Niambie ujira wako utakuwa nini.”

29:16 Mwa 30:9; Rut 4:2, 11Labani alikuwa na binti wawili, binti mkubwa aliitwa Lea na binti mdogo aliitwa Raheli. Lea alikuwa na macho dhaifu, lakini Raheli alikuwa na umbo la kupendeza na mzuri wa sura. 29:18 Mwa 24:67; Hos 12:12Yakobo akampenda Raheli, akamwambia Labani, “Nitakutumikia kwa miaka saba kwa ajili ya kumpata Raheli binti yako mdogo.”

Labani akasema, “Ni bora zaidi nikupe Raheli kuliko kumpa mtu mwingine yeyote. Kaa pamoja na mimi hapa.” Kwa hiyo Yakobo akatumika miaka saba ili kumpata Raheli, lakini ilionekana kwake kama siku chache tu kwa sababu ya upendo wake kwa Raheli.

29:21 Amu 15:1Ndipo Yakobo akamwambia Labani, “Nipe mke wangu. Muda wangu umekamilika, nami nataka nikutane naye kimwili.”

29:22 Amu 14:10; Yn 2:1-2Basi Labani akaalika watu wote wa mahali pale na akafanya karamu.

Lakini ilipofika jioni, akamchukua Lea binti yake akampa Yakobo, naye Yakobo akakutana naye kimwili. Naye Labani akamtoa Zilpa, mtumishi wake wa kike, kuwa mtumishi wa Lea, binti yake.

29:25 Mwa 12:18; 27:36Kesho yake asubuhi, Yakobo akagundua kuwa amepewa Lea! Basi Yakobo akamwambia Labani, “Ni jambo gani hili ulilonitendea? Nilikutumikia kwa ajili ya Raheli, sivyo? Kwa nini umenidanganya?”

29:26 1Sam 14:49; 2Sam 6:23Labani akajibu, “Si desturi yetu kumwoza binti mdogo kabla ya kumwoza binti mkubwa. Maliza juma la arusi ya binti huyu, kisha pia nitakupa huyu binti mdogo, kwa kutumika miaka mingine saba.”

Naye Yakobo akafanya hivyo. Akamaliza juma na Lea, kisha Labani akampa Raheli binti yake kuwa mke wake. 29:29 1Nya 5:1; Mwa 16:1Labani akamtoa Bilha mtumishi wake wa kike kwa Raheli ili kuwa mtumishi wake. Pia Yakobo akakutana na Raheli kimwili, naye akampenda Raheli zaidi kuliko Lea. Yakobo akamtumikia Labani kwa miaka mingine saba.

Wana Wa Yakobo

29:31 Kum 21:15-17; Za 127:3Bwana alipoona kwamba Lea hapendwi, akampa watoto, lakini Raheli alikuwa tasa. 29:32 Mwa 30:23; Hes 1:5Lea akapata mimba akazaa mwana. Akamwita Reubeni,29:32 Reubeni maana yake Ona mwana, yaani Yehova ameangalia taabu yangu. kwa maana alisema, “Ni kwa sababu Bwana ameona huzuni yangu. Hakika mume wangu sasa atanipenda.”

29:33 Kut 6:15; 1Nya 4:24Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Kwa sababu Bwana alisikia kwamba sipendwi, amenipa tena huyu mwana.” Kwa hiyo akamwita Simeoni.29:33 Simeoni maana yake Anasikia, yaani sasa ataungana nami kama Raheli.

Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Sasa afadhali mume wangu ataambatana na mimi, kwa sababu nimemzalia wana watatu.” Kwa hiyo akamwita Lawi.29:34 Lawi maana yake Nimeunganishwa, yaani na mume wangu.

29:35 Mwa 49:8; Mt 1:2-3Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana, akasema, “Wakati huu nitamsifu Bwana.” Kwa hiyo akamwita Yuda.29:35 Yuda maana yake Sifa, yaani Nitamsifu Yehova. Kisha akaacha kuzaa watoto.

Read More of Mwanzo 29

Mwanzo 30:1-43

Raheli alipoona hamzalii Yakobo watoto, akamwonea ndugu yake wivu. Hivyo akamwambia Yakobo, “Nipe watoto, la sivyo nitakufa!”

30:2 2Fal 5:7; Mwa 16:2Yakobo akamkasirikia, akamwambia, “Je, mimi ni badala ya Mungu, ambaye amekuzuia usizae watoto?”

30:3 Mwa 16:2Ndipo Raheli akamwambia, “Hapa yupo Bilha, mtumishi wangu wa kike. Kutana naye kimwili ili aweze kunizalia watoto na kwa kupitia yeye mimi pia niweze kuwa na uzao.”

30:4 Mwa 16:3-4Hivyo Raheli akampa Yakobo Bilha awe mke wake. Yakobo akakutana naye kimwili, Bilha akapata mimba, naye akamzalia Yakobo mwana. 30:6 Za 35:24; 1Sam 1:20; Yos 19:40Ndipo Raheli akasema, “Mungu amenipa haki yangu, amesikiliza maombi yangu na kunipa mwana.” Kwa sababu hiyo akamwita Dani.30:6 Dani maana yake Anahukumu, yaani Mungu amenipa haki yangu.

Bilha mtumishi wa kike wa Raheli akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili. 30:8 Hos 12:3-4; Hes 1:42Ndipo Raheli akasema, “Nilikuwa na mashindano makubwa na ndugu yangu, nami nimeshinda.” Kwa hiyo akamwita Naftali.30:8 Naftali maana yake Nimeshindana nami nimeshinda.

30:9 Mwa 29:16Lea alipoona kuwa amekoma kuzaa watoto, alimchukua mtumishi wake wa kike Zilpa, naye akampa Yakobo awe mke wake. Mtumishi wa Lea yaani Zilpa, akamzalia Yakobo mwana. 30:11 Mwa 35:26; Kut 1:4Ndipo Lea akasema, “Hii ni bahati nzuri aje!” Kwa hiyo akamwita Gadi.

Mtumishi wa kike wa Lea akamzalia Yakobo mwana wa pili. 30:13 Lk 1:48Ndipo Lea aliposema, “Jinsi gani nilivyo na furaha! Wanawake wataniita furaha.” Kwa hiyo akamwita Asheri.30:13 Asheri maana yake Nimefurahi, yaani Mungu amenifurahisha.

30:14 Wim 7:13Wakati wa kuvuna ngano, Reubeni akaenda shambani akakuta tunguja, ambazo alizileta kwa Lea mama yake. Raheli akamwambia Lea, “Tafadhali nakuomba unipe baadhi ya tunguja za mwanao.”

30:15 Isa 7:13Lakini Lea akamwambia, “Haikukutosha kumtwaa mume wangu? Je, utachukua na tunguja za mwanangu pia?”

Raheli akasema, “Vema sana! Yakobo atakutana nawe kimwili leo usiku, kwa malipo ya tunguja za mwanao.”

Kwa hiyo Yakobo alipokuja kutoka shambani jioni ile, Lea akaenda kumlaki, akamwambia, “Lazima ukutane nami kimwili. Nimekukodisha kwa tunguja za mwanangu.” Kwa hiyo akakutana naye kimwili usiku ule.

30:17 Mwa 25:21Mungu akamsikiliza Lea, naye akapata mimba akamzalia Yakobo mwana wa tano. 30:18 Hes 1:8, 24Ndipo Lea akasema, “Mungu amenizawadia kwa kumpa mume wangu mtumishi wangu wa kike.” Kwa hiyo akamwita Isakari.30:18 Isakari maana yake Zawadi, yaani Mungu amenizawadia.

Lea akapata mimba tena akamzalia Yakobo mwana wa sita. 30:20 1Pet 3:7Ndipo Lea aliposema, “Mungu amenizawadia kwa zawadi ya thamani sana. Wakati huu mume wangu ataniheshimu kwa sababu nimemzalia wana sita.” Kwa hiyo akamwita Zabuloni.30:20 Zabuloni maana yake Heshima.

30:21 Mwa 34:1Baadaye akamzaa mtoto wa kike akamwita Dina.30:21 Dina maana yake Tetea haki, yaani Mungu amenitetea katika mashindano yangu.

30:22 Mwa 11:30Ndipo Mungu akamkumbuka Raheli, akasikia maombi yake na akafungua tumbo lake. 30:23 Isa 4:1; Lk 1:25Akapata mimba na akamzaa mwana na kusema, “Mungu ameniondolea aibu yangu.”

30:24 Mwa 35:17Akamwita Yosefu30:24 Yosefu maana yake Yeye na aongeze, yaani Mungu na aniongezee. na kusema, “Bwana na anipe mwana mwingine.”

Makundi Ya Yakobo Yaongezeka

30:25 Mwa 24:54Baada ya Raheli kumzaa Yosefu, Yakobo akamwambia Labani, “Nipe ruhusa nirudi katika nchi yangu. Nipe wake zangu na watoto, ambao nimetumika kuwapata, nami niende zangu. Unajua ni kazi kiasi gani ambayo nimekufanyia.”

30:27 Mwa 26:24Lakini Labani akamwambia, “Ikiwa nimepata kibali machoni pako, tafadhali ukae. Nimegundua kwa njia ya uaguzi kwamba Bwana amenibariki kwa sababu yako.” 30:28 Mwa 29:15Akaongeza kumwambia, “Taja ujira wako nami nitakulipa.”

Yakobo akamwambia, “Unajua jinsi ambavyo nimekutumikia na jinsi ambavyo wanyama wako walivyolishwa vizuri chini ya uangalizi wangu. Kidogo ulichokuwa nacho kabla sijaja kimeongezeka sana, naye Bwana amekubariki popote nilipokuwa. Lakini sasa, ni lini nitashughulikia mambo ya nyumba yangu mwenyewe?”

Labani akamuuliza, “Nikupe nini?”

Yakobo akamjibu, “Usinipe chochote lakini kama utanifanyia jambo hili moja, nitaendelea kuchunga na kuyaangalia makundi yako. 30:32 Mwa 31:8, 12Niruhusu nipite katika makundi yako yote leo niondoe humo kila kondoo mwenye mabakabaka au madoadoa, kila mwana-kondoo mweusi na kila mbuzi mwenye madoadoa au mabakabaka. Hawa watakuwa ujira wangu. Uadilifu wangu utanishuhudia siku zijazo, kila utakapochunguza ujira ambao umenilipa mimi. Mbuzi yeyote wangu ambaye hana mabakabaka wala madoadoa, au mwana-kondoo ambaye si mweusi, atahesabika ameibwa.”

Labani akasema, “Ninakubali na iwe kama ulivyosema.” Siku ile ile Yakobo akawaondoa beberu wote waliokuwa na mistari au madoadoa na mbuzi wake wote waliokuwa na mistari au madoadoa (wote waliokuwa na alama nyeupe juu yao) na wana-kondoo weusi wote, akawaweka chini ya uangalizi wa wanawe. Kisha Labani akamwacha Yakobo kwa mwendo wa safari ya siku tatu kati yake na Yakobo, wakati Yakobo akiendelea kuchunga lile kundi la Labani lililobaki.

30:37 Yer 1:11Hata hivyo, Yakobo, akachukua fito mbichi zilizokatwa wakati huo huo za miti ya mlubna, mlozi na mwaramoni akazibambua ili mistari myeupe ionekane katika fito hizo. 30:38 Kut 2:16Kisha akaweka fito alizozibambua kwenye mabirika yote ya kunyweshea mifugo, ili ziwe mbele ya makundi walipokuja kunywa maji. Wanyama walipokuja kunywa maji, hali wakiwa wanahitaji mbegu, wakapandwa hizo fito zikiwa mbele yao. Wanyama waliopata mimba mbele ya hizo fito walizaa wanyama wenye mistari, madoadoa na mabakabaka. Yakobo akawatenga wadogo wa kundi peke yao, lakini akazielekeza nyuso za hao waliobaki kwenye wale wenye mistari na weusi waliokuwa mali ya Labani. Hivyo akatenga makundi yake mwenyewe, na wala hakuwachanganya na wanyama wa Labani. Kila mara wanyama wenye nguvu walipohitaji mbegu, Yakobo aliweka zile fito kwenye mabirika mbele ya hao wanyama, ili wapandwe karibu na hizo fito, lakini ikiwa wanyama walikuwa wadhaifu hakuziweka hizo fito. Hivyo wanyama wadhaifu wakawa wa Labani, na wanyama wenye nguvu wakawa wa Yakobo. 30:43 Mwa 12:16Kwa njia hii Yakobo akastawi sana, tena akawa na makundi makubwa, watumishi wa kike na wa kiume na ngamia na punda.

Read More of Mwanzo 30