Mwanzo 25:1-34, Mwanzo 26:1-35 NEN

Mwanzo 25:1-34

Kifo Cha Abrahamu

Abrahamu alioa mke mwingine, ambaye jina lake aliitwa Ketura. 25:2 Yer 25:25; Mwa 36:35; 37:28, 36; Kut 2:15; Hes 22:4; 25:6; Amu 6:1-3; 8:22-24; 9:17; Za 83:9; Isa 9:4; 10:26; Hab 3:7; Ay 2:11Huyu alimzalia Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. Yokshani alikuwa baba wa Sheba na Dedani, wazao wa Dedani walikuwa Waashuri, Waletushi na Waleumi. 25:4 Isa 60:6Wana wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa. Hawa wote walikuwa uzao wa Ketura.

25:5 Mwa 24:36Abrahamu akamwachia Isaki kila kitu alichokuwa nacho. 25:6 Mwa 22:24; 21:10; Amu 6:3, 33; 1Fal 4:30; Eze 25:4Lakini Abrahamu alipokuwa bado hai, akawapa watoto wa masuria wake zawadi, kisha akawaondoa waende kuishi pande za mashariki mbali na mwanawe Isaki.

25:7 Mwa 12:4; 35:28; 47:9, 28; 50:22; Ay 42:16Kwa jumla, Abrahamu aliishi miaka 175. 25:8 Mwa 35:29; 49:29; Hes 20:24; 31:2; Kum 31:14; 32:50; 34:5Ndipo Abrahamu akapumua pumzi ya mwisho na akafa akiwa mwenye umri mzuri, mzee aliyeshiba siku, naye akakusanywa pamoja na watu wake. 25:9 Mwa 35:29; 47:30; 49:31; 23:9; 13:18; 50:13Watoto wake Isaki na Ishmaeli wakamzika katika pango la Makpela karibu na Mamre, katika shamba lililokuwa la Efroni mwana wa Sohari Mhiti, 25:10 Mwa 10:15Shamba ambalo Abrahamu alilinunua kwa Wahiti. Hapo ndipo Abrahamu alipozikwa pamoja na mkewe Sara. 25:11 Mwa 12:2; 16:14Baada ya kifo cha Abrahamu, Mungu akambariki mwanawe Isaki, ambaye baadaye aliishi karibu na Beer-Lahai-Roi.

Wana Wa Ishmaeli

25:12 Mwa 2:4; 17:20; 21:18Hivi ndivyo vizazi vya Ishmaeli mtoto wa Abrahamu, ambaye mjakazi wake Sara, Hagari Mmisri, alimzalia Abrahamu.

25:13 Mwa 28:9; 36:3; Za 120:5; Isa 21:16; 42:11; 60:7; Yer 2:10; 49:28; Eze 27:21Haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, yaliyoorodheshwa kulingana na jinsi walivyozaliwa: Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli ni Nebayothi, akafuatia Kedari, Adbeeli, Mibsamu, 25:14 Yos 15:25; Oba 1:1; Isa 21:11Mishma, Duma, Masa, 25:15 Ay 6:19; Isa 21:14; Yer 25:23; 1Nya 5:19Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi na Kedema. 25:16 Mwa 17:20; 13:16; Za 83:9Hawa walikuwa wana wa Ishmaeli na haya ni majina ya viongozi wa makabila kumi na mawili kulingana na makao yao na kambi zao. Kwa jumla Ishmaeli aliishi miaka 137. Akapumua pumzi ya mwisho, akafa, naye akakusanywa pamoja na watu wake. 25:18 Mwa 17:20; 21:18; 16:7, 12Wazao wa Ishmaeli waliishi kuanzia nchi ya Havila hadi Shuri, karibu na mpaka wa Misri, unapoelekea Ashuru. Hao waliishi kwa uhasama na ndugu zao wote.

Yakobo Na Esau

Hivi ndivyo vizazi vya Isaki mwana wa Abrahamu.

Abrahamu akamzaa Isaki, 25:20 Mwa 26:34; 48:7; 35:28; 24:67; 22:22; 28:2-6; 30:20; 31:18; 33:18; 46:15; 24:29; Kum 26:5Isaki alikuwa na umri wa miaka arobaini alipomwoa Rebeka binti Bethueli Mwaramu kutoka Padan-Aramu, nduguye Labani Mwaramu.

25:21 Mwa 30:17, 22; 11:30; Ezr 8:23; 1Sam 1:17, 23; 1Nya 5:20; 2Nya 33:13; Za 127:3Isaki akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, kwa sababu alikuwa tasa. Bwana akajibu maombi yake na Rebeka mkewe akapata mimba. 25:22 Kut 18:15; 28:30; 33:7; Law 24:12; Hes 9:6-8; 27:5; Kum 17:9; 2Fal 3:11; 22:13; Isa 30:2; Yer 21:2; 37:7; Eze 14:7; 2Watoto wakashindana tumboni mwake, akasema, “Kwa nini haya yanatokea kwangu?” Kwa hiyo akaenda kumuuliza Bwana.

Bwana akamjibu,

“Mataifa mawili yamo tumboni mwako,

na mataifa hayo mawili

kutoka ndani yako watatenganishwa.

Mmoja atakuwa na nguvu zaidi kuliko mwingine,

na yule mkubwa atamtumikia yule mdogo.”

Wakati wake wa kujifungua ulipotimia, walikuwepo mapacha wa kiume tumboni mwake. Wa kwanza kuzaliwa alikuwa mwekundu, mwili wake wote ulikuwa kama mtu aliyevaa vazi lenye nywele; wakamwita jina lake Esau.25:25 Esau maana yake Mwenye nywele nyingi. Baadaye, ndugu yake akatoka, mkono wake ukiwa umemshika Esau kisigino; akaitwa jina lake Yakobo.25:26 Yakobo maana yake Ashikaye kisigino, au Atwaaye mahali pa mwingine, au Mdanganyaji, au Mwenye hila, au Mlaghai, au Mjanja. Isaki alikuwa mwenye miaka sitini Rebeka alipowazaa.

Watoto wakakua, naye Esau akakuwa mwindaji hodari, mtu wa mbugani, wakati Yakobo alikuwa mtu mtulivu, mwenye kukaa nyumbani. Isaki, ambaye alikuwa anapendelea zaidi nyama za porini, alimpenda Esau, bali Rebeka alimpenda Yakobo.

Siku moja Yakobo alipika mchuzi wa dengu, Esau akarudi kutoka porini akiwa na njaa kali. Esau akamwambia Yakobo, “Haraka, nipe huo mchuzi mwekundu! Nina njaa kali sana!” (Hii ndiyo sababu pia aliitwa Edomu.)25:30 Edomu maana yake Mwekundu.

Yakobo akamjibu, “Niuzie kwanza haki yako ya mzaliwa wa kwanza.”

Esau akasema, “Tazama, mimi niko karibu ya kufa, itanifaa nini haki ya mzaliwa wa kwanza?”

Yakobo akamwambia, “Niapie kwanza.” Hivyo Esau akamwapia, akamuuzia Yakobo haki yake ya kuzaliwa.

Ndipo Yakobo akampa Esau mkate na ule mchuzi wa dengu. Akala na kunywa, kisha akainuka akaenda zake.

Kwa hiyo Esau alidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.

Read More of Mwanzo 25

Mwanzo 26:1-35

Isaki Na Abimeleki

26:1 Mwa 12:10; 20:1Basi njaa kubwa ikawa katika nchi hiyo, kuliko ile njaa iliyotangulia iliyotokea wakati wa Abrahamu. Isaki akamwendea Abimeleki mfalme wa Wafilisti huko Gerari. 26:2 Mwa 12:1, 7; 46:3Bwana akamtokea Isaki, akamwambia, “Usiende Misri, bali ukae katika nchi nitakayokuambia. 26:3 Kut 3:12; Mwa 12:2, 7Kaa katika nchi hii kwa kitambo, mimi nitakuwa pamoja na wewe na nitakubariki. Kwa maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote na nitatimiza kiapo nilichomwapia Abrahamu baba yako. 26:4 Mwa 26:24; 48:4; 12:2Nitafanya wazao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa nchi hizi zote na kutokana na uzao wako mataifa yote yatabarikiwa, 26:5 Mwa 18:19; Za 119:80, 112; Eze 18:21kwa sababu Abrahamu alinitii mimi akatunza kanuni zangu na maagizo yangu, amri zangu pamoja na sheria zangu.” 26:6 Mwa 20:1Hivyo Isaki akaishi huko Gerari.

26:7 Mwa 12:13Watu wa mahali pale walipomuuliza habari za mke wake, akasema, “Huyu ni dada yangu,” kwa sababu aliogopa kusema, “Huyu ni mke wangu.” Alifikiri, “Watu wa mahali pale wataweza kumuua kwa sababu ya Rebeka, kwa kuwa alikuwa mzuri wa sura.”

Wakati Isaki alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki mfalme wa Wafilisti akachungulia dirishani, akaona jinsi Isaki alivyomkumbatia Rebeka mke wake. Abimeleki akamwita Isaki akamwambia, “Hakika huyu ni mke wako! Mbona uliniambia, ‘Huyu ni dada yangu?’ ”

Isaki akamjibu, “Kwa sababu nilifikiri ningeweza kuuawa kwa sababu yake.”

26:10 Mwa 12:8Ndipo Abimeleki akamjibu, “Ni nini hiki ulichotufanyia? Ingewezekana mtu yeyote akawa amekutana kimwili na mke wako, nawe ungeleta hatia juu yetu.”

26:11 1Sam 24:6; 26:9; Za 105:15Hivyo Abimeleki akatoa amri kwa watu wote, akisema, “Yeyote atakayemnyanyasa mtu huyu au mkewe hakika atauawa.”

26:12 Mt 13:8; Mwa 26:3Isaki akapanda mazao katika nchi hiyo, kwa mwaka huo huo, akavuna mara mia, kwa sababu Bwana alimbariki. 26:13 Mwa 13:2; Kum 8:18Isaki akawa tajiri, mali zake zikaendelea kuongezeka mpaka akawa tajiri sana. 26:14 Mwa 12:16; 24:36Akawa na mifugo ya kondoo na ngʼombe, na watumishi wengi sana, kiasi kwamba Wafilisti wakamwonea wivu. 26:15 Mwa 21:30; 21:25Kwa hiyo visima vyote vilivyochimbwa na watumishi wakati wa Abrahamu baba yake, Wafilisti wakavifukia, wakavijaza udongo.

Ndipo Abimeleki akamwambia Isaki, “Ondoka kwetu, kwa maana umetuzidi nguvu sana.”

Basi Isaki akatoka huko akajenga kambi katika Bonde la Gerari, akaishi huko. Ndipo Isaki akavichimbua tena vile visima vya maji ambavyo vilichimbwa siku zile za Abrahamu baba yake, ambavyo Wafilisti walivifukia baada ya kufa Abrahamu, akavipa majina yale yale ambayo baba yake alikuwa amevipa.

Watumishi wa Isaki wakachimba katika lile bonde wakagundua huko kisima chenye maji safi. Lakini wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaki wakisema, “Maji haya ni yetu!” Ndipo akakiita kile kisima Eseki,26:20 Eseki maana yake ni Ugomvi. kwa sababu waligombana naye. Kisha wakachimba kisima kingine, lakini hata hicho pia wakakigombania, akakiita Sitna.26:21 Sitna maana yake Upinzani. 26:22 Kut 18:19; Mwa 17:6Akaondoka huko, akachimba kisima kingine, wala hakuna yeyote aliyekigombania. Akakiita Rehobothi,26:22 Rehobothi maana yake ni Mungu ametufanyia nafasi. akisema, “Sasa Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutastawi katika nchi.”

Kutoka pale akaenda Beer-Sheba. 26:24 Mwa 24:12; 17:7Usiku ule Bwana akamtokea, akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa Abrahamu baba yako. Usiogope, kwa maana mimi niko pamoja nawe, nitakubariki na kuongeza idadi ya wazao wako kwa ajili ya Abrahamu mtumishi wangu.”

Isaki akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana. Akapiga hema lake huko, nao watumishi wake wakachimba kisima.

26:26 Mwa 21:22Wakati huo, Abimeleki alikuwa amemjia kutoka Gerari, akifuatana na Ahuzathi mshauri wake, pamoja na Fikoli jemadari wa majeshi yake. Isaki akawauliza, “Mbona mmekuja kwangu na ninyi mlinichukia na kunifukuza?”

26:28 Mwa 21:22Wakamjibu, “Tuliona wazi kuwa Bwana alikuwa pamoja nawe, kwa hiyo tukasema, ‘Inabidi kuwe na kiapo cha mapatano kati yetu, kati yetu na wewe. Na tufanye mkataba pamoja nawe 26:29 Mwa 31:29, 52; 24:31kwamba hutatudhuru, kama jinsi nasi hatukuwanyanyasa bali tuliwatendea mema wakati wote na kuwaondoa kwetu kwa amani. Tena sasa umebarikiwa na Bwana.’ ”

26:30 Mwa 31:54; Kut 18:12Basi Isaki akawaandalia karamu, nao wakala na kunywa. 26:31 Mwa 21:23, 27Kesho yake asubuhi na mapema, wakaapizana wao kwa wao. Kisha Isaki akawaruhusu waende zao, wakamwacha Isaki kwa amani.

26:32 Mwa 21:30Siku hiyo watumishi wa Isaki wakaja wakampa habari kuhusu kisima walichokuwa wamekichimba, wakamwambia, “Tumepata maji!” 26:33 Mwa 21:14Naye akakiita Shiba,26:33 Shiba kwa Kiebrania maana yake ni Saba. mpaka leo mji huo unaitwa Beer-Sheba.26:33 Beer-Sheba maana yake ni Kisima cha wale saba, yaani wale kondoo saba ambao Abrahamu aliwatoa kama ushahidi kati yake na Abimeleki.

26:34 Mwa 36:2Esau alipokuwa na umri wa miaka arobaini, akamwoa Yudithi binti Beeri Mhiti, kisha akamwoa Basemathi binti Eloni Mhiti. 26:35 Mwa 27:46; Ay 7:16Hawa walikuwa chanzo cha huzuni ya Isaki na Rebeka.

Read More of Mwanzo 26