Mwanzo 21:1-34, Mwanzo 22:1-24, Mwanzo 23:1-20 NEN

Mwanzo 21:1-34

Kuzaliwa Kwa Isaki

21:1 Mwa 17:20; 1Sam 2:21; Mwa 8:1; 17:6; 18:14; 4:23; Ebr 11:11Wakati huu Bwana akamrehemu Sara kama alivyokuwa amesema, naye Bwana akamtendea Sara kile alichokuwa ameahidi. 21:2 Mwa 17:19; 30:6; 18:10; Gal 4:22; Ebr 11:11Sara akapata mimba, akamzalia Abrahamu mwana katika uzee wake, majira yale ya Mungu aliomwahidi. 21:3 Mwa 16:11; Yos 24:3Abrahamu akamwita Isaki yule mwana ambaye Sara alimzalia. 21:4 Mwa 17:10-12; Mdo 7:8Isaki alipokuwa na umri wa siku nane, Abrahamu akamtahiri, kama Mungu alivyomwamuru. 21:5 Mwa 12:4; Ebr 6:15Abrahamu alikuwa na miaka 100 wakati Isaki mwanawe alipozaliwa.

21:6 Mwa 17:17; Ay 8:21; Za 126:2; Isa 12:6; 35:2; 44:23; 52:9; 54:1Sara akasema, “Mungu ameniletea kicheko, kila mmoja atakayesikia jambo hili atacheka pamoja nami.” 21:7 Mwa 17:17Akaongeza kusema, “Nani angemwambia Abrahamu kuwa Sara angenyonyesha watoto? Tena nimemzalia mwana katika uzee wake.”

Hagari Na Ishmaeli Wafukuzwa

21:8 1Sam 1:23Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya. Siku hiyo Isaki alipoachishwa kunyonya, Abrahamu alifanya sherehe kubwa. 21:9 Mwa 16:15; 39:14; Gal 4:29Lakini Sara aliona kuwa mwana ambaye Hagari, Mmisri, aliyemzalia Abrahamu alikuwa anadhihaki, 21:10 Mwa 39:17; 25:6; Gal 4:30Sara akamwambia Abrahamu, “Mwondoe mwanamke huyo mtumwa pamoja na mwanawe, kwa kuwa mwana wa mwanamke mtumwa kamwe hatarithi pamoja na mwanangu Isaki.”

21:11 Mwa 17:18Jambo hili lilimhuzunisha sana Abrahamu kwa sababu lilimhusu mwanawe. 21:12 Mt 1:2; Rum 9:7; Ebr 11:18Lakini Mungu akamwambia, “Usihuzunike hivyo kwa sababu ya kijana na mtumishi wako wa kike. Sikiliza lolote Sara analokuambia, kwa sababu uzao wako utahesabiwa kupitia kwake Isaki. 21:13 Mwa 13:16Nitamfanya huyu mwana wa mtumishi wako wa kike kuwa taifa pia, kwa sababu naye ni uzao wako.”

21:14 Mwa 16:1; 22:19; 26:33; 28:10; 46:1-5; Yos 15:28; 19:2; Amu 20:1; 1Sam 3:20; 1Nya 4:28; Neh 11:27Kesho yake asubuhi na mapema, Abrahamu akachukua chakula na kiriba cha maji, akampa Hagari. Akaviweka mabegani mwa Hagari, akamwondoa pamoja na kijana. Hagari akashika njia, akatangatanga katika jangwa la Beer-Sheba.

Maji yalipokwisha kwenye kiriba, akamwacha kijana chini ya mojawapo ya vichaka. 21:16 Yer 6:26; Amo 8:10; Zek 12:10Kisha akajiendea zake akaketi karibu, umbali wa kutupa mshale, akawaza, “Siwezi kumwangalia kijana akifa.” Ikawa alipokuwa ameketi pale karibu, akaanza kulia kwa huzuni.

21:17 Kut 3:7; Hes 20:16; Za 6:8; Kum 26:7; Mwa 16:7; 22:11, 15; 15:1; 17:20Mungu akamsikia kijana akilia, malaika wa Mungu akamwita Hagari kutoka mbinguni na kumwambia, “Kuna nini Hagari? Usiogope, Mungu amesikia kijana analia akiwa amelala pale. Mwinue kijana na umshike mkono, kwa maana nitamfanya kuwa taifa kubwa.”

21:19 Hes 22:31; Mwa 16:7Ndipo Mungu akamfumbua Hagari macho yake naye akaona kisima cha maji. Hivyo akaenda akajaza kiriba maji na kumpa kijana anywe.

21:20 Mwa 26:3, 24; 28:15; 39:2; Lk 1:66Mungu akawa pamoja na huyu kijana alipokuwa akiendelea kukua. Aliishi jangwani na akawa mpiga upinde. 21:21 Mwa 14:6; 24:4, 38; 28:2; 34:4-8; Amu 14:2Alipokuwa akiishi katika Jangwa la Parani, mama yake akampatia mke kutoka Misri.

Mapatano Katika Beer-Sheba

21:22 Mwa 20:2; 26:26-28; 28:15; 31:3-5, 42; 39:2-3; Za 46:7; 1Sam 3:19; 16:18; Isa 7:14; 8:8-10; 41:10; 43:5Wakati huo Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakamwambia Abrahamu, “Mungu yu pamoja nawe katika kila kitu unachofanya. 21:23 Mwa 25:33; 26:31; 31:53; Yos 2:12; 1Fal 2:8; 1Sam 24:21Sasa niapie hapa mbele za Mungu kwamba hutanitenda hila mimi, watoto wangu wala wazao wangu. Nitendee mimi na nchi ambayo unaishi kama mgeni wema ule ule ambao nimekutendea.”

Abrahamu akasema, “Ninaapa hivyo.”

21:25 Mwa 26:15-22Ndipo Abrahamu akalalamika kwa Abimeleki kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki walikuwa wamekinyangʼanya. Lakini Abimeleki akasema, “Sijui ni nani ambaye amefanya hili. Hukuniambia, leo tu ndipo ninasikia habari zake.”

21:27 Mwa 26:28-31; 31:44, 53Hivyo Abrahamu akaleta kondoo na ngʼombe, akampa Abimeleki, nao watu hawa wawili wakafanya mapatano. Abrahamu akatenga kondoo wa kike saba kutoka kwenye kundi, Abimeleki akamuuliza Abrahamu, “Ni nini maana ya hawa kondoo wa kike saba uliowatenga peke yao?”

21:30 Mwa 31:44-52; Isa 19:20; Yos 22:27-34; 24:27; Mal 2:14Abrahamu akamjibu, “Upokee hawa kondoo wa kike saba kutoka mkononi mwangu kama ushahidi kuwa nilichimba kisima hiki.”

Hivyo mahali pale pakaitwa Beer-Sheba, kwa sababu watu wawili waliapiana hapo.

21:32 Mwa 10:14; 26:33Baada ya mapatano kufanyika huko Beer-Sheba, Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakarudi katika nchi ya Wafilisti. 21:33 1Sam 22:6; 31:13; Mwa 4:26; Kut 15:18; Kum 32:40; 33:27; Ay 36:26; Za 10:16; 45:6; 90:2; 93:2; 102:24; 103:19; 146:10; Isa 40:28; Yer 10:10; Hab 1:12; 3:6; Ebr 13:8Abrahamu akapanda mti wa mkwaju huko Beer-Sheba, na hapo akaliitia jina la Bwana, Mungu wa milele. 21:34 Mwa 10:14Naye Abrahamu akakaa katika nchi ya Wafilisti kwa muda mrefu.

Read More of Mwanzo 21

Mwanzo 22:1-24

Kujua Uthabiti Wa Abrahamu

22:1 Kut 15:25; 16:4; 20:20; Kum 8:2, 16; 13:3; Amu 2:22; 3:1; 2Nya 32:31; Za 66:10; Ebr 11:17; Yak 1:12-13; Mwa 31:11; 46:2; 1Sam 3:4-8; Isa 6:8Baadaye Mungu akamjaribu Abrahamu. Akamwambia, “Abrahamu!”

Abrahamu akajibu, “Mimi hapa.”

22:2 Yn 3:16; Ebr 11:17; 1Yn 4:9; Mwa 8:20Kisha Mungu akamwambia, “Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, Isaki umpendaye, uende katika nchi ya Moria. Mtoe huko kama sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.”

22:3 Yos 8:10Abrahamu akaamka asubuhi na mapema siku iliyofuata, akamtayarisha punda wake. Akawachukua watumishi wake wawili pamoja na Isaki mwanawe. Baada ya kuchanja kuni za kutosha kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka kuelekea mahali Mungu alipokuwa amemwambia. Siku ya tatu Abrahamu akainua macho, akapaona mahali pale kwa mbali. 22:5 Kut 24:14Akawaambia watumishi wake, “Kaeni hapa pamoja na punda, wakati mimi na kijana tunakwenda kule. Tutakwenda kuabudu na kisha tutawarudia.”

22:6 Yn 19:17; Amu 19:29Abrahamu akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, akamtwika Isaki mwanawe, yeye mwenyewe akachukua moto na kisu. Walipokuwa wakienda pamoja, 22:7 Kut 29:38-42; Law 1:10; Ufu 13:8Isaki akanena akamwambia Abrahamu baba yake, “Baba yangu!”

Abrahamu akaitika, “Mimi hapa, mwanangu.”

Isaki akasema, “Moto na kuni zipo, Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?”

22:8 Yn 1:29Abrahamu akajibu, “Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa.” Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja.

22:9 Mwa 4:26; 8:20; Law 1:7; 1Fal 18:33; Ebr 11:17-19; Yak 2:21Walipofika mahali pale alipokuwa ameambiwa na Mungu, Abrahamu akajenga madhabahu hapo, akaziweka kuni juu yake. Akamfunga Isaki mwanawe na akamlaza kwenye madhabahu, juu ya zile kuni. 22:10 Mwa 18:19Kisha akanyoosha mkono wake na akachukua kisu ili amchinje mwanawe. 22:11 Mwa 16:7; 21:17; 46:2Lakini malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Abrahamu! Abrahamu!”

Akajibu, “Mimi hapa.”

22:12 Mwa 18:19; 42:18; Kut 18:21; 1Sam 15:22; Ay 1:1; 37:24; Mit 8:13; Yak 2:21-23; Yn 3:16; 1Yn 4:9Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.”

22:13 Mwa 8:20; Rum 8:32Abrahamu akainua macho yake, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake nyuma yake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. 22:14 Kut 17:15; Amu 6:24; Isa 30:29Abrahamu akapaita mahali pale Yehova-Yire.22:14 Yehova-Yire maana yake Bwana atatupa. Mpaka siku ya leo inasemekana, “Katika mlima wa Bwana itapatikana.”

22:15 Mwa 21:17Basi malaika wa Bwana akamwita Abrahamu kutoka mbinguni mara ya pili, 22:16 Kut 13:11; 32:13; 33:1; Isa 45:23; 62:8; Yer 22:5; 44:26; 49:13; 51:14; Amo 6:8; Ebr 6:13; Lk 1:73akasema, “Ninaapa kwa nafsi yangu, asema Bwana, kwamba kwa sababu umefanya jambo hili na hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee, 22:17 Mwa 12:2; 15:5; 26:24; 24:60; Ebr 6:14; Kut 32:13; Kum 7:7; 28:62; Hos 1:10; Rum 9:27; Ebr 11:12; Es 9:2hakika nitakubariki, na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga ulioko pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao, 22:18 Mwa 12:2-3; 17:2, 9; Mdo 3:25; Gal 3:8; Za 105:9na kupitia uzao wako mataifa yote duniani yatabarikiwa, kwa sababu umenitii.”

22:19 Mwa 21:14; 26:23; 28:10Ndipo Abrahamu akawarudia watumishi wake, wakaondoka wakaenda wote pamoja mpaka Beer-Sheba. Abrahamu akaishi huko Beer-Sheba.

Wana Wa Nahori

22:20 Mwa 11:29Baada ya muda, Abrahamu akaambiwa, “Milka pia amepata watoto, amemzalia ndugu yako Nahori wana: 22:21 Mwa 10:23; Ay 32:2; Yer 25:23Usi mzaliwa wake wa kwanza, Buzi nduguye, Kemueli (baba wa Aramu), 22:22 Mwa 24:15, 47; 25:20Kesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu na Bethueli.” 22:23 Mwa 24:15; 11:29Bethueli akamzaa Rebeka. Milka alimzalia Nahori nduguye Abrahamu hao wana wanane. 22:24 Mwa 25:6; 35:22; 36:12; Amu 8:31; 2Sam 3:7; 1Fal 2:22; 11:3; 1Nya 1:32; Wim 6:8Suria wake Nahori aliyeitwa Reuma pia alikuwa na wana: Teba, Gahamu, Tahashi na Maaka.

Read More of Mwanzo 22

Mwanzo 23:1-20

Kifo Cha Sara

Sara aliishi akawa na umri wa miaka mia na ishirini na saba. 23:2 Yos 14:15; 15:13; 20:7; 21:11; Mwa 13:18; 24:67Sara akafa huko Kiriath-Arba (yaani Hebroni) katika nchi ya Kanaani, Abrahamu akamwombolezea na kumlilia Sara.

23:3 Mwa 10:15Ndipo Abrahamu akainuka kutoka pale penye maiti ya mke wake. Akazungumza na Wahiti, akasema, 23:4 Mwa 17:8; 19:9; 49:30; Kut 2:22; Law 25:23; Za 39:12; 105:12; 119:19; Ebr 11:9-13; Mdo 7:16“Mimi ni mpitaji na mgeni miongoni mwenu. Niuzieni sehemu ya ardhi yenu ili niweze kumzika maiti wangu.”

Wahiti wakamjibu Abrahamu, 23:6 Mwa 14:14-16; 24:35; 25:9“Bwana, tusikilize. Wewe ni mtawala mkuu sana miongoni mwetu. Zika maiti wako katika kaburi unalolipenda kati ya makaburi yetu. Hakuna mtu wa kwetu atakayekuzuia kaburi lake ili kuzika maiti wako.”

Abrahamu akainuka na akasujudu mbele ya wenyeji wa nchi, yaani Wahiti. Akawaambia, “Kama mnaniruhusu kumzika maiti wangu, basi nisikilizeni mkamsihi Efroni mwana wa Sohari kwa niaba yangu 23:9 Mwa 25:9; 47:30; 49:30; 50:13ili aniuzie pango la Makpela, lililo mali yake, nalo liko mwisho wa shamba lake. Mwambieni aniuzie kwa bei kamili atakayosema ili liwe mahali pangu pa kuzikia miongoni mwenu.”

23:10 Kum 22:15; 25:7; Yos 20:4; Rut 4:11; 2Sam 15:2; 2Fal 15:35; Za 127:5; Mit 31:23; Yer 26:10; 6:10Efroni Mhiti alikuwa ameketi miongoni mwa watu wake, akamjibu Abrahamu mbele ya Wahiti wote waliokuwepo katika lango la mji. 23:11 2Sam 24:23“La hasha, bwana wangu, nisikilize, nakupa shamba, pia nakupa pango lililomo ndani yake. Nakupa mbele ya watu wangu. Uzike maiti wako.”

Abrahamu akasujudu tena, mbele ya wenyeji wa nchi, akamwambia Efroni wale watu wakiwa wanasikia, “Tafadhali nisikilize. Nitakulipa fedha za hilo shamba. Kubali kuzipokea ili niweze kumzika maiti wangu.”

Efroni akamjibu Abrahamu, 23:15 Eze 45:12“Nisikilize, bwana wangu, thamani ya ardhi hiyo ni shekeli 400 za fedha,23:15 Shekeli 400 za fedha ni sawa na kilo 4.5. lakini hiyo ni nini kati yako na mimi? Mzike maiti wako.”

23:16 2Sam 14:26; 24:24; Yer 32:9; Zek 11:12Abrahamu akakubali masharti ya Efroni, akampimia ile fedha aliyotaja masikioni mwa Wahiti: Shekeli 400 za fedha kulingana na viwango vya uzito vilivyokuwa vikitumika wakati huo na wafanyabiashara.

23:17 Mwa 13:18Hivyo shamba la Efroni huko Makpela karibu na Mamre, yaani shamba pamoja na pango lililokuwamo, nayo miti yote iliyokuwamo ndani ya mipaka ya shamba hilo, vilikabidhiwa, 23:18 Mwa 18:1, 7kwa Abrahamu kuwa mali yake mbele ya Wahiti wote waliokuwa wamekuja kwenye lango la mji. 23:19 Mwa 13:18; Yos 14:13; 1Nya 29:27; 23:20; Yer 32:10; Mwa 10:15; 35:29; 49:30, 31; 50:5Baada ya hayo Abrahamu akamzika Sara mkewe kwenye pango ndani ya shamba la Makpela karibu na Mamre (huko Hebroni) katika nchi ya Kanaani. Hivyo Wahiti wakamkabidhi Abrahamu shamba pamoja na pango lililokuwa humo kuwa mahali pa kuzikia.

Read More of Mwanzo 23