Mwanzo 2:18-25, Mwanzo 3:1-24, Mwanzo 4:1-16 NEN

Mwanzo 2:18-25

2:18 Mit 11:31; 1Kor 11:9; 1Tim 2:13Bwana Mungu akasema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.”

2:19 Za 8:7; Mwa 1:5, 20, 24Basi Bwana Mungu alikuwa amefanyiza kutoka ardhi wanyama wote wa porini na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lolote alilokiita kila kiumbe hai, likawa ndilo jina lake. 2:20 Mwa 3:20; 4:1Hivyo Adamu akawapa majina wanyama wote wa kufugwa, ndege wa angani, na wanyama wote wa porini.

Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa. 2:21 Mwa 15:12; 1Sam 26:12; Ay 33:15Hivyo Bwana Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake, akapafunika mahali pale kwa nyama. 2:22 1Kor 11:8-9, 12; 1Tim 2:12Kisha Bwana Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume.

2:23 Mwa 29:14; Efe 5:28-30; 1Kor 11:8Huyo mwanaume akasema,

“Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu

na nyama ya nyama yangu,

ataitwa ‘mwanamke,’2:23 Jina la Kiebrania la mwanamke linafanana na lile la mwanaume.

kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.”

2:24 Mal 2:15; Mt 19:5; Mk 10:7-8; Efe 5:31; 1Kor 6:16Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

2:25 Mwa 3:7, 10-11; Isa 47:3; Mao 1:8Adamu na mkewe wote wawili walikuwa uchi, wala hawakuona aibu.

Read More of Mwanzo 2

Mwanzo 3:1-24

Kuanguka Kwa Mwanadamu

3:1 Ay 1:7; 2:2; 2Kor 11:3; Ufu 12:9; 20:2; Mwa 2:17Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa porini ambao Bwana Mungu aliwafanya. Nyoka akamwambia mwanamke, “Ati kweli Mungu alisema, ‘Kamwe msile matunda ya mti wowote wa bustanini’?”

3:2 Mwa 2:16-17Mwanamke akamjibu nyoka, “Tunaweza kula matunda ya miti iliyoko bustanini, lakini Mungu alisema, ‘Kamwe msile tunda la mti ulio katikati ya bustani, wala kuugusa, la sivyo mtakufa.’ ”

3:4 Yn 8:44; 2Kor 11:3Lakini nyoka akamwambia mwanamke, “Hakika hamtakufa. 3:5 Mwa 1:26; 14:18-19; Za 7:8; Isa 14:14; Eze 28:2Kwa maana Mungu anajua ya kuwa wakati mtakapoyala, macho yenu yatafumbuliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.”

3:6 Yak 1:14-15; 1Yn 2:16; Hes 30:7-8; Yer 44:15, 19, 24; 2Kor 11:3; 1Tim 2:14Mwanamke alipoona ya kuwa tunda la mti huo lilikuwa zuri kwa chakula na la kupendeza macho, tena linatamanika kwa kujipatia hekima, basi akachuma katika matunda yake, akala, pia akampa mumewe, aliyekuwa pamoja naye, naye akala. 3:7 Mwa 2:25Ndipo macho yao wote wawili yakafumbuliwa, wakajiona kwamba walikuwa uchi; hivyo wakashona majani ya mtini, wakajifunika.

3:8 Law 26:12; Kum 23:14; Ay 13:16; 23:7; 34:22-23; Isa 29:15; Za 139:7-12; Yer 16:17; 23:24; 49:10; Ufu 6:15-16Ndipo yule mwanaume na mkewe, waliposikia sauti ya Bwana Mungu alipokuwa akitembea bustanini jioni, wakajificha kutoka mbele za Bwana Mungu katikati ya miti ya bustani. 3:9 Mwa 4:9; 16:8; 18:9; 1Fal 19:9-13Lakini Bwana Mungu akamwita Adamu, “Uko wapi?”

3:10 Kut 19:16; 20:18; Kum 5:5; Mwa 2:25; 1Sam 12:18Naye akajibu, “Nilikusikia katika bustani nikaogopa kwa sababu nilikuwa uchi, hivyo nikajificha.”

3:11 Mwa 2:17, 25Mungu akamuuliza, “Ni nani aliyekuambia ya kuwa ulikuwa uchi? Je, umekula matunda ya mti niliokuamuru usile?”

3:12 Mwa 2:22Adamu akasema, “Huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nami alinipa sehemu ya tunda kutoka kwenye huo mti, nami nikala.”

3:13 Rum 7:11; 2Kor 11:3; 1Tim 2:14Ndipo Bwana Mungu akamuuliza mwanamke, “Ni nini hili ambalo umelifanya?” Mwanamke akajibu, “Nyoka alinidanganya, nami nikala.”

3:14 Za 72:9; Mik 7:17; Kum 28:15-20; Isa 49:23; 65:25Hivyo Bwana Mungu akamwambia nyoka, “Kwa kuwa umefanya hili,

“Umelaaniwa kuliko wanyama wote

wa kufugwa na wa porini!

Utatambaa kwa tumbo lako

na kula mavumbi

siku zote za maisha yako.

3:15 Yn 8:44; 1Yn 3:8; Mdo 13:10; Mwa 16:11; Amu 13:5; Ebr 2:14; Isa 7:14; 8:3; 9:6; Mt 1:23; Lk 1:31; Gal 4:4; Ufu 12:17; Rum 16:20Nami nitaweka uadui

kati yako na huyo mwanamke,

na kati ya uzao wako na wake,

yeye atakuponda kichwa,

nawe utamuuma kisigino.”

3:16 Za 48:5-6; Isa 13:8; 21:3; 26:17; Yer 4:31; 6:24; Mik 4:9; 1Kor 11:3; Efe 5:22; 1Tim 2:15Kwa mwanamke akasema,

“Nitakuzidishia sana utungu wakati wa kuzaa kwako;

kwa utungu utazaa watoto.

Tamaa yako itakuwa kwa mumeo

naye atakutawala.”

3:17 Mwa 2:17; 5:29; 6:13; 8:21; 47:9; 29:32; 31:42; Hes 35:33; Za 66:11; 106:39; 127:2; Isa 24:5; Rum 8:20-22; Isa 54:9; Kut 3:7; Mhu 1:13; 2:23; Ay 5:7; 14:1; Yer 20:18Kwa Adamu akasema, “Kwa sababu umemsikiliza mke wako na ukala kutoka kwenye mti niliokuamuru, ‘Msile tunda lake,’

“Ardhi imelaaniwa kwa sababu yako,

kwa kazi ngumu utakula chakula kitokacho humo

siku zote za maisha yako.

3:18 Za 104:14; Ay 31:40; Isa 5:6; Ebr 6:8Itazaa miiba na mibaruti kwa ajili yako,

nawe utakula mimea ya shambani.

3:19 Mwa 2:7; 14:18; Kum 8:3, 9; 23:4; Rum 1:6; 2:14; 2The 3:10; Ay 7:21; Ebr 9:27; Za 146:4; 104:23; Rut 1:6; 2:14; 1Kor 15:47Kwa jasho la uso wako

utakula chakula chako

hadi utakaporudi ardhini,

kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo,

kwa kuwa wewe u mavumbi

na mavumbini wewe utarudi.”

3:20 Mwa 2:20; 2Kor 11:3; 1Tim 2:13Adamu akamwita mkewe Eva, kwa kuwa atakuwa mama wa wote walio hai.

Bwana Mungu akawatengenezea Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. 3:22 Mwa 2:9; 1:26; Ufu 2:7Kisha Bwana Mungu akasema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya. Sharti asiruhusiwe kunyoosha mkono wake na kuchuma pia kutoka mti wa uzima akala, naye akaishi milele.” 3:23 Mwa 2:7-8Hivyo Bwana Mungu akamfukuzia mbali kutoka Bustani ya Edeni, akalime ardhi ambamo alitolewa. 3:24 Kut 25:18-22; 1Sam 4:4; 2Sam 6:2; 22:11; 1Fal 6:27; 8:6; 2Fal 19:15; 2Nya 5:8; Za 18:10; 104:4; Isa 27:1; 37:16; Eze 10:1; Mwa 2:9; Ay 40:19Baada ya kumfukuzia mbali Adamu, Mungu akaweka makerubi mashariki ya Bustani ya Edeni, pamoja na upanga wa moto ukimulika huku na huko kulinda njia ya kuuendea mti wa uzima.

Read More of Mwanzo 3

Mwanzo 4:1-16

Kaini Na Abeli

4:1 Mwa 2:20; Ebr 11:4; 1Yn 3:12; Yud 11Adamu akakutana kimwili na mkewe Eva, naye akapata mimba, akamzaa Kaini. Eva akasema, “Kwa msaada wa Bwana nimemzaa mwanaume.” 4:2 Mt 23:35; Lk 11:51; Ebr 11:4; 12:24; Mwa 2:7Baadaye akamzaa Abeli ndugu yake.

Basi Abeli akawa mfugaji, na Kaini akawa mkulima. 4:3 Law 2:1-2; Isa 43:23; Yer 41:5; Hes 18:12Baada ya muda Kaini akaleta baadhi ya mazao ya shamba kama sadaka kwa Bwana. 4:4 Law 3:16; 2Nya 29:35; Kut 13:2, 12; Kum 15:19; Ebr 11:4Lakini Abeli akaleta fungu nono kutoka baadhi ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo yake. Bwana akamkubali Abeli pamoja na sadaka yake, lakini Mungu hakumkubali Kaini pamoja na sadaka yake. Kwa hiyo Kaini akakasirika sana, uso wake ukawa na huzuni.

Kisha Bwana akamwambia Kaini, “Kwa nini umekasirika? Kwa nini uso wako una huzuni? 4:7 Mwa 44:16; Hes 32:23; Isa 59:12; Ay 11:15; 22:27; Za 27:3; 46:2; Rum 6:16Ukifanya lililo sawa, je, hutakubalika? Lakini usipofanya lililo sawa, dhambi inakuvizia mlangoni mwako, inakutamani wewe, lakini inakupasa uishinde.”

4:8 Mt 23:35; Lk 11:51; 1Yn 3:12; Yud 11Basi Kaini akamwambia ndugu yake Abeli, “Twende shambani.” Walipokuwa shambani, Kaini akamshambulia Abeli ndugu yake, akamuua.

4:9 Mwa 3:9; Yn 8:44Kisha Bwana akamuuliza Kaini, “Ndugu yako Abeli yuko wapi?”

Akamjibu, “Sijui, je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”

4:10 Mwa 9:5; 37:20, 26; Kut 21:12; Hes 35:33; Kum 21:7-9; 2Sam 4:11; Ay 16:18; 24:2; 31:38; Za 9:12; 106:38; Ebr 12:24; Ufu 6:9-10Bwana akasema, “Umefanya nini? Sikiliza! Damu ya ndugu yako inanililia mimi kutoka ardhini. 4:11 Kum 11:28; 2Fal 2:24Sasa umelaaniwa na umehamishwa kutoka ardhi, ambayo imefungua kinywa chake na kupokea damu ya ndugu yako kutoka mkononi mwako. 4:12 Kum 28:15-24; Za 37:25; 59:15; 109:10Utakapoilima ardhi, haitakupa tena mazao yake. Utakuwa mtu wa kutangatanga duniani asiye na utulivu.”

Kaini akamwambia Bwana, “Adhabu yangu ni zaidi ya niwezavyo kustahimili. 4:14 2Fal 17:18; Za 51:11; 139:7-12; Yer 7:15; 52:3; Kum 28:64-67; Mwa 9:6; Kut 21:12-14; Law 24:17; Hes 35:19-21, 27; 1Fal 2:32; 2Fal 11:16Leo unanifukuza kutoka nchi, nami nitafichwa mbali na uwepo wako. Nitakuwa mtu wa kutangatanga asiyetulia duniani na yeyote anionaye ataniua.”

4:15 Eze 9:4, 6; Kut 21:20; Law 26:21; Za 79:12Lakini Bwana akamwambia, “La sivyo, ikiwa mtu yeyote atamuua Kaini atalipizwa kisasi mara saba zaidi.” Kisha Bwana akamwekea Kaini alama ili mtu yeyote ambaye angemwona asimuue. 4:16 Yud 11; Mwa 2:8Kwa hiyo Kaini akaondoka mbele za Bwana akaenda kuishi katika nchi ya Nodi, iliyoko mashariki ya Edeni.

Read More of Mwanzo 4