Mwanzo 17:1-27, Mwanzo 18:1-33 NEN

Mwanzo 17:1-27

Agano La Tohara

17:1 Mwa 5:22; 12:4-7; 20:5; 28:3; 35:11; 43:14; 48:3; 49:25; Kut 6:3; 18:13; Rut 1:20; Ay 5:17; 6:4, 14; 22:21; 33:19; 36:16; Isa 13:6; Yoe 1:15; Mik 6:9; 1Fal 3:6; 9:4; Za 15:2; 18:23; 78:72; 101:2Abramu alipokuwa na miaka tisini na tisa, Bwana akamtokea akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi;17:1 Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote). enenda mbele zangu na uishi kwa unyofu. 17:2 Mwa 12:2; 15:18; 22:16-18Nami nitafanya Agano langu kati yangu na wewe, nami nitakuzidisha sana sana.”

17:3 Mwa 18:2; 19:1; 33:3; Kut 18:7; Hes 14:5; Yos 5:14; 7:6; Amu 13:20; Eze 1:28; 3:23Abramu akaanguka kifudifudi, naye Mungu akamwambia, 17:4 Mwa 15:18; 12:2; 25:23“Kwa upande wangu, hili ndilo Agano langu na wewe: Wewe utakuwa baba wa mataifa mengi. 17:5 Mwa 32:28; 35:10; 37:3, 13; 43:6; 46:2; 1Fal 18:31; 2Fal 17:34; 1Nya 1:34; Neh 9:7; Isa 48:1; Yn 1:42; Rum 4:17Jina lako hutaitwa tena Abramu, bali jina lako litakuwa Abrahamu,17:5 Abrahamu maana yake Baba wa watu wengi. kwa maana nimekufanya wewe baba wa mataifa mengi. 17:6 Mwa 1:28; 18:10; 21:1; 22:17; 26:22; 28:3; 35:11; 36:31; 41:52; 47:27; 48:4; 49:22; Law 26:9; Mt 1:6; Kum 7:13; Isa 51:2Nitakufanya uwe na uzao mwingi sana, kwako yatatoka mataifa nao wafalme watatoka kwako. 17:7 Mwa 6:18; 9:16; 18:15; Kut 6:7; 20:2; 29:45-46; Law 11:44-45; 18:2; 22:33; 25:38; 26:9, 12, 15; Hes 15:41; Kum 4:20; 7:6, 21; 29:13; 2Sam 7:24; Ebr 13:20; Yer 14:9; Ufu 21:7; Rum 9:8; Gal 3:16Nitalithibitisha Agano langu kama Agano la milele kati yangu na wewe na wazao wako baada yako na vizazi vijavyo niwe Mungu wako na Mungu wa wazao wako. 17:8 Mwa 10:19; 12:7; 15:7; 23:4; 28:4; 35:27; 37:1; Kut 6:4; Yer 31:1; 1Nya 29:15Nchi yote ya Kanaani, unakoishi sasa kama mgeni, nitakupa kuwa milki yako milele, na uzao wako, nami nitakuwa Mungu wao.”

17:9 Mwa 18:19; 22:18; Kut 19:5; Kum 5:2Ndipo Mungu akamwambia Abrahamu, “Kwa upande wako, lazima ushike Agano langu, wewe na wazao wako kwa ajili ya vizazi vijavyo. 17:10 Mwa 21:4; Law 12:3; Yos 5:2-7; Rum 4:11; Yn 7:22; Mdo 7:8Hili ni Agano langu na wewe pamoja na wazao wako baada yako, Agano mtakalolishika: Kila mwanaume miongoni mwenu atatahiriwa. 17:11 Kut 12:48; Kum 10:16; Mwa 9:12; Rum 4:11Mtafanyiwa tohara na hii itakuwa ni alama ya Agano kati yangu na ninyi. 17:12 Mwa 9:12; 21:4; Law 12:3; Yos 5:2; Lk 1:59; 2:21Kwa vizazi vijavyo, kila mwanaume miongoni mwenu mwenye siku nane ni lazima atahiriwe, pamoja na watakaozaliwa nyumbani mwako au walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, wale ambao sio watoto wako. 17:13 Kut 12:44-48; Mwa 9:16Awe amezaliwa nyumbani mwako au amenunuliwa kwa fedha yako, ni lazima watahiriwe. Agano langu katika mwili wako litakuwa ni Agano la milele. 17:14 Kut 4:24-26; 12:15, 19; 30:33; Eze 44:7; Yos 5:2-8; Law 7:20, 25; 17:4; 18:29; 19:8; 20:17; Hes 9:13; 15:30; 19:13; Kum 17:12; Ay 38:15; Za 37:28Kila mwanaume asiyetahiriwa, ambaye hajapata tohara ya mwilini, atatengwa na watu wake, amelivunja Agano langu.”

17:15 Mwa 11:29Pia Bwana akamwambia Abrahamu, “Kwa upande wa Sarai mkeo, hutamwita tena Sarai bali jina lake litakuwa Sara. 17:16 Mwa 18:10; 24:60; Isa 29:22; Gal 4:31Nitambariki na hakika nitakupatia mwana kwake. Nitambariki na kwamba atakuwa mama wa mataifa, wafalme wa mataifa watatoka kwake.”

17:17 Mwa 12:4; 18:11-13; 21:6, 7; 24:1, 36; Yer 20:15; Lk 1:18; Rum 4:19; Gal 4:23; Ebr 11:11Abrahamu akaanguka kifudifudi, akacheka na kusema moyoni mwake, “Je, mtu wa miaka mia moja aweza kuzaa mwana? Je, Sara atazaa mtoto katika umri wa miaka tisini?” 17:18 Mwa 16:15; 21:11Abrahamu akamwambia Mungu, “Laiti Ishmaeli naye angeshiriki baraka yako!”

17:19 Mwa 9:16; 16:11; 18:14; 21:2; 26:3; 50:24; Kut 13:11; Kum 1:8; Gal 3:16; 1Sam 1:20; Mt 1:21; Lk 1:13, 31Ndipo Mungu akasema, “Ndiyo, lakini mkeo Sara atakuzalia wewe mwana, nawe utamwita jina lake Isaki.17:19 Isaki maana yake Kucheka. Nitalithibitisha Agano langu naye kama Agano la milele kwa ajili yake na wazao wake baada yake. 17:20 Mwa 13:16; 16:10; 25:12-18; 48:19Kwa upande wa Ishmaeli, nimekusikia: hakika nitambariki, nitamfanya awe na uzao mwingi na nitaongeza sana idadi yake. Atakuwa baba wa watawala kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kubwa. 17:21 Kut 34:10; Mwa 18:10-14; 21:2Lakini Agano langu nitalithibitisha kwa Isaki, ambaye Sara atakuzalia mwaka ujao majira kama haya.” 17:22 Mwa 18:33; 35:13; Hes 12:9Wakati alipomaliza kuzungumza na Abrahamu, Mungu akapanda juu akaondoka kwa Abrahamu.

17:23 Mwa 12:5Siku ile ile, Abrahamu akamchukua Ishmaeli mwanawe na wote waliozaliwa nyumbani mwake pamoja na walionunuliwa kwa fedha zake, kila mwanaume wa nyumbani mwake, akawatahiri, kama Mungu alivyomwagiza. 17:24 Mwa 12:4; Rum 4:11Abrahamu alikuwa na umri wa miaka tisini na tisa alipotahiriwa, 17:25 Mwa 16:16naye Ishmaeli mwanawe alitahiriwa akiwa na umri wa miaka kumi na mitatu. Abrahamu na Ishmaeli mwanawe walitahiriwa siku ile ile, 17:27 Mwa 14:14Kila mwanaume nyumbani mwa Abrahamu, pamoja na wote waliozaliwa nyumbani mwake au aliyenunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni, alitahiriwa pamoja naye.

Read More of Mwanzo 17

Mwanzo 18:1-33

Wageni Watatu

18:1 Mwa 12:7; 13:18; 14:13; 19:1; 23:10, 18; 34:20-24; Rut 4:1; Ebr 11:9; Za 69:12Bwana akamtokea Abrahamu karibu na mialoni ya Mamre wakati alipokuwa ameketi kwenye ingilio la hema lake wakati wa adhuhuri. 18:2 Mwa 17:2-3; 19:1, 10; 24:63; 32:24; 43:28; Yos 5:13; Ebr 13:2; Amu 13:6-11; Hos 12:2-4Abrahamu akainua macho akaona watu watatu wamesimama karibu naye. Alipowaona, aliharakisha kutoka kwenye ingilio la hema lake kuwalaki na kuwasujudia hadi nchi.

Akasema, “Kama nimepata kibali machoni penu, ee bwana wangu, usimpite mtumishi wako. 18:4 Mwa 19:2; 24:32; 43:24; Amu 19:21; 2Sam 11:8; Lk 7:44Acha yaletwe maji kidogo, kisha ninyi nyote mnawe miguu yenu na mpumzike chini ya mti huu. 18:5 Amu 13:15; 19:5Niruhusuni niwapatie chakula kidogo mle, ili mpate nguvu mwendelee na safari yenu, kwa kuwa mmekuja kwa mtumishi wenu.”

Nao wakamjibu, “Vema sana, fanya kama unavyosema.”

18:6 Mwa 19:3; 2Sam 13:8Hivyo Abrahamu akaharakisha akaingia hemani kwa Sara, akamwambia, “Chukua vipimo vitatu vya unga laini haraka, ukande na uoke mikate.”

18:7 1Sam 28:24; Lk 15:23Kisha Abrahamu akakimbia kwenda kwenye kundi, akachagua ndama mzuri, laini na akampa mtumishi, ambaye aliharakisha kumtayarisha. 18:8 Isa 7:15, 22; Amu 4:19; 5:25; 6:19Kisha akaleta jibini, maziwa na nyama ya yule ndama iliyoandaliwa, akaviweka mbele ya wageni. Walipokuwa wakila, alisimama karibu nao chini ya mti.

18:9 Mwa 3:9; 24:67; Ebr 11:9Wakamuuliza, “Yuko wapi Sara mkeo?”

Akasema, “Yuko huko, ndani ya hema.”

18:10 Mwa 17:6, 21; 21:2; 2Fal 4:16; Rum 6:6Kisha Bwana akasema, “Hakika nitakurudia tena majira kama haya mwakani na Sara mkeo atakuwa ana mwana.”

Sara alikuwa akiwasikiliza kwenye ingilio la hema, lililokuwa nyuma yake. 18:11 Mwa 11:30; 17:17; Lk 1:18; Rum 4:19; Ebr 11:11-12Abrahamu na Sara walikuwa wazee tena waliosogea miaka, naye Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. 18:12 Mwa 17:17; 21:6; 1Pet 3:6Hivyo Sara akacheka kimoyomoyo alipokuwa akiwaza, “Baada ya mimi kuwa mkongwe hivi na bwana wangu amezeeka, je, nitaweza kufurahia jambo hili?”

18:13 Mwa 17:17Ndipo Bwana akamwambia Abrahamu, “Kwa nini Sara amecheka na kusema, ‘Kweli nitazaa mtoto nami sasa ni mzee?’ 18:14 Ay 42:2; Isa 40:29; 50:2; 51:9; Gal 4:23; Yer 32:17; Mt 19:26; Rum 4:21; 9:9; Mwa 17:19Je, kuna jambo lolote gumu lisilowezekana kwa Bwana? Nitakurudia mwakani majira kama haya, naye Sara atakuwa na mwana.”

Sara akaogopa kwa kuwa alidanganya na kusema, “Mimi sikucheka.”

Lakini Bwana akasema, “Ndiyo, ulicheka!”

Abrahamu Aiombea Sodoma

Wakati watu hao waliposimama ili waondoke, walielekeza nyuso zao Sodoma, Abrahamu akawatoa kitambo kidogo ili awasindikize. 18:17 Amo 3:7; Mwa 19:24; Ay 1:16; Za 107:34Ndipo Bwana akasema, “Je, nimfiche Abrahamu jambo ninalokusudia kufanya? 18:18 Mwa 12:2; Gal 3:8Hakika Abrahamu atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, kupitia kwake mataifa yote ya dunia yatabarikiwa. 18:19 Mwa 16:11; 17:9; 22:12, 18; 26:5; Kum 4:9-10; 6:7; Isa 14:1; Efe 6:4; Yos 24:15; Yer 23:5; 2Sam 8:15; Za 17:2; 99:4Kwa maana nimemchagua yeye, ili awaongoze watoto wake na jamaa yake kufuata njia ya Bwana, kwa kuwa waadilifu na kutenda haki, ili Bwana atimize ahadi yake kwa Abrahamu.”

18:20 Isa 1:10; Yer 23:14; Eze 16:46; Mwa 13:13; 19:13Basi Bwana akasema, “Kilio dhidi ya Sodoma na Gomora ni kikubwa sana na dhambi yao inasikitisha sana, 18:21 Mwa 11:5kwamba nitashuka nione kama waliyoyatenda ni mabaya kiasi cha kilio kilichonifikia. Kama sivyo, nitajua.”

18:22 Mwa 19:1, 27Basi wale watu wakageuka wakaenda kuelekea Sodoma, lakini Abrahamu akabaki amesimama mbele za Bwana. 18:23 Kut 23:7; 2Pet 2:9; Law 4:3, 22, 27; Hes 16:22; Eze 18:4; Kum 27:25; 2Sam 24:17; Za 11:4-7; 94:21Ndipo Abrahamu akamsogelea akasema: “Je, utawaangamiza wenye haki na waovu? 18:24 Yer 5:1Je, ikiwa watakuwepo watu wenye haki hamsini katika mji huo, hivi kweli utauangamiza na wala hutauacha kwa ajili ya hao watu hamsini wenye haki waliomo ndani yake? 18:25 Mwa 20:4; 44:7; Kum 32:4; 1:16-17; Rum 3:6; Ay 8:3-7; 9:15; 34:10; 36:23; Isa 3:10-11; 5:20; Amo 5:15; Mal 2:17; 3:18; Amu 11:27; Za 7:11; 58:11; 75:7; 94:2; 119:137; Ebr 12:23; 2Nya 19:7; Ezr 9:15; Neh 9:33; Eze 18:25; Dan 4:37; 9:14Hilo na liwe mbali nawe, kufanya jambo kama hilo, kuwaua wenye haki pamoja na waovu, kuwatendea wenye haki sawasawa na waovu. Iwe mbali nawe! Je, Mwamuzi wa dunia yote hatafanya lililo sawa?”

Bwana akasema, “Kama nikipata watu hamsini wenye haki katika mji wa Sodoma, nitausamehe huo mji wote kwa ajili yao.”

18:27 Mwa 2:7; Ay 2:8Kisha Abrahamu akasema tena: “Sasa kwa kuwa nimekuwa na ujasiri wa kuzungumza na Bwana, ingawa mimi si kitu bali ni mavumbi na majivu; je, kama hesabu ya wenye haki imepungua watano katika hamsini, utauangamiza huo mji wote kwa ajili ya hao watano waliopungua?”

Bwana akamwambia, “Kama nikiwakuta huko watu arobaini na watano, sitauangamiza.”

Abrahamu akazungumza naye kwa mara nyingine, “Je, kama huko watapatikana watu arobaini tu?”

Akamjibu, “Kwa ajili ya hao arobaini, sitauangamiza.”

18:30 Mwa 44:18; Kut 32:22Ndipo akasema, “Bwana na asikasirike, lakini niruhusu nizungumze. Je, kama huko watakuwepo thelathini tu?”

Akajibu, “Sitapaangamiza ikiwa nitawakuta huko watu thelathini.”

Abrahamu akasema, “Sasa kwa kuwa nimekuwa na ujasiri sana kuzungumza na Bwana, je, kama wakipatikana huko watu ishirini tu?”

Bwana akajibu, “Kwa ajili ya hao ishirini, sitauangamiza.”

18:32 Amu 6:39; Yer 5:1Abrahamu akasema, “Bwana na asikasirike, lakini niruhusu nizungumze tena mara moja tu. Itakuwaje kama watapatikana huko watu kumi tu?”

Bwana akajibu, “Kwa ajili ya hao kumi, sitauangamiza.”

18:33 Kut 31:18; Mwa 17:22; 31:55Bwana alipomaliza kuzungumza na Abrahamu, akaondoka, naye Abrahamu akarudi nyumbani kwake.

Read More of Mwanzo 18