Mwanzo 11:10-32, Mwanzo 12:1-20, Mwanzo 13:1-18 NEN

Mwanzo 11:10-32

Shemu Hadi Abramu

(1 Nyakati 1:24-27)

11:10 Mwa 2:4; Lk 3:36Hivi ndivyo vizazi vya Shemu.

Miaka miwili baada ya gharika, Shemu alipokuwa na miaka 100, akamzaa Arfaksadi. Baada ya kumzaa Arfaksadi, Shemu aliishi miaka 500, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

11:12 Lk 3:35Wakati Arfaksadi alipokuwa na miaka thelathini na mitano, akamzaa Shela. Baada ya Arfaksadi kumzaa Shela, aliishi miaka 403, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

Shela alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Eberi. Shela baada ya kumzaa Eberi, aliishi miaka 403, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

Eberi alipokuwa na miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi. Baada ya Eberi kumzaa Pelegi, aliishi miaka 430, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

Pelegi alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Reu. Baada ya Pelegi kumzaa Reu, aliishi miaka 209, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

11:20 Lk 3:35Reu alipokuwa na miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi. Baada ya Reu kumzaa Serugi, aliishi miaka 207, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

11:22 Lk 3:34Serugi alipokuwa na miaka thelathini, akamzaa Nahori. Baada ya Serugi kumzaa Nahori, aliishi miaka 200, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

11:24 Lk 3:34Nahori alipokuwa na miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera. Baada ya Nahori kumzaa Tera, aliishi miaka 119, akazaa watoto wengine wa kiume na wa kike.

11:26 Lk 3:34; Yos 24:2; 2Fal 19:12; Isa 37:12; Eze 27:23Tera alipokuwa na miaka sabini, akamzaa Abramu, Nahori na Harani.

Wazao Wa Tera

11:27 Mwa 2:4; 31:53; 12:4; 13:1-5, 8, 12; 14:12; 19:1; Lk 17:28; 2Pet 2:5-7Hawa ndio wazao wa Tera.

Tera aliwazaa Abramu, Nahori na Harani. Harani akamzaa Loti. 11:28 Mwa 15:7; Neh 9:7; Ay 1:17; 16:11; Eze 23:23; Mdo 7:4Tera alipokuwa bado hai, Harani akafa huko Uru ya Wakaldayo, nchi alimozaliwa. 11:29 Mwa 22:20-23; 24:10-24; 29:5; 12:5; 16:1; 17:15Abramu na Nahori walioa. Mke wa Abramu aliitwa Sarai, na mke wa Nahori aliitwa Milka; Milka na Iska walikuwa watoto wa Harani. 11:30 Mwa 16:1; 18:11; 25:21; 29:31; 30:1, 22; Amu 13:2; 1Sam 1:5; Za 113:9Sarai alikuwa tasa, hakuwa na watoto.

11:31 Mwa 38:11; 10:19; 12:4; 27:43; 28:5-10; 29:4; Law 18:15; 20:21; Rut 1:6, 22; 2:20; 4:15; 1Sam 4:19; 1Nya 2:4; Mik 7:6; Eze 22:11; 27:23; Mdo 7:4; 2Fal 19:12Tera akamchukua Abramu mwanawe, Loti mwana wa Harani mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka kwa pamoja katika Uru ya Wakaldayo kwenda nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakaishi huko.

11:32 Yos 24:2Tera alikufa huko Harani akiwa na miaka 205.

Read More of Mwanzo 11

Mwanzo 12:1-20

Wito Wa Abramu

Bwana akawa amemwambia Abramu, “Ondoka kutoka nchi yako, uache jamii yako na nyumba ya baba yako, uende hadi nchi nitakayokuonyesha.

12:2 Mwa 13:16; 15:5; 17:2-4; 18:18; 22:17; 24:1, 35; 25:11; 26:3, 4; 28:3, 4, 14; 24:1, 35; 25:11; 32:12; 35:11; 41:49; 47:27; 48:16-19; 22:18; Kut 1:7; 5:5; 32:13; 20:24; Kum 1:10; 10:22; 13:17; 26:5; Yos 11:4; 24:3; 2Sam 17:11; 1Fal 3:8; 4:20; 1Nya 27:23; 2Nya 1:9; Neh 9:23; Za 107:38; 67:6; 115:12; Isa 6:13; 10:22; 48:19; 51:2; 54:3; 60:22; 19:24; Yer 4:2; 33:22; Mik 4:7; Hes 22:12; 23:8, 20; 24:9; Isa 44:3; 61:9; 65:23; Mal 3:12; Hag 2:19; Zek 8:13“Mimi nitakufanya taifa kubwa

na nitakubariki,

Nitalikuza jina lako,

nawe utakuwa baraka.

12:3 Mwa 27:29; 15:5; 18:18; 22:18; 26:4; 28:4, 14; Kut 23:22; Hes 24:9; Kum 30:7; 9:5; Za 72:17; Isa 19:25; Mdo 3:25; Gal 3:8Nitawabariki wale wanaokubariki,

na yeyote akulaaniye nitamlaani;

na kupitia kwako mataifa yote duniani

yatabarikiwa.”

12:4 Mwa 11:27, 31; 16:3, 16; 17:17-24; 21:5Hivyo Abramu akaondoka kama Bwana alivyokuwa amemwambia; naye Loti akaondoka pamoja naye. Wakati Abramu alipoitwa aondoke Harani, alikuwa na miaka sabini na mitano. 12:5 Mwa 11:29, 31; 13:2-6; 31:18; 46:6; 14:14; 15:3; 17:23; 16:3; Mhu 2:7; Ebr 11:8Abramu akamchukua Sarai mkewe pamoja na Loti mwana wa ndugu yake, mali zote walizokuwa nazo pamoja na watu aliokuwa amewapata huko Harani, wakasafiri mpaka nchi ya Kanaani, wakafika huko.

12:6 Ebr 11:9; 1Fal 12:1; Mwa 10:18; 33:18; 17:12; 35:4; Yos 17:7; 20:7; 24:26; Amu 7:1; 9:6; 8:31; 21:19; Za 60:6; 108:7Abramu akasafiri katika nchi hiyo akafika huko Shekemu, mahali penye mti wa mwaloni ulioko More. Wakati huo Wakanaani walikuwa wanaishi katika nchi hiyo. 12:7 Mwa 8:20; 17:1, 8; 18:1; 26:2; 35:1; 13:4, 15-17; 15:18; 23:18; 24:7; 26:3-4; 28:13; 35:12; 48:4; 50:24; Kut 6:4-8; 6:3; 13:5, 11; 32:13; 33:1; Mdo 7:2, 5; Hes 10:29; 11:12; Kum 1:8; 2:31; 9:5; 11:9; 34:4; 30:5; Ebr 11:8; Rum 4:13; 2Fal 25:21; 1Nya 16:16; 2Nya 20:7; Za 109:9-11; Yer 25:5; Eze 47:14; Gal 3:16Bwana akamtokea Abramu, akamwambia, “Nitawapa uzao wako nchi hii.” Hivyo hapa akamjengea madhabahu Bwana aliyekuwa amemtokea.

12:8 Mwa 4:26; 8:20; 13:3; 28:11, 19; 26:25; 33:19; 35:1, 8, 15; Yos 7:2; 8:9; 12:9; Yer 49:3; 1Sam 7:16; 1Fal 12:29; Hos 12:4; Amo 3:14; 4:4; Ebr 11:9; Ezr 2:28; Neh 7:32Kutoka huko Abramu akasafiri kuelekea kwenye vilima mashariki ya Betheli, naye akapiga hema huko, Betheli ikiwa upande wa magharibi na Ai upande wa mashariki. Huko alimjengea Bwana madhabahu na akaliitia jina la Bwana. 12:9 Mwa 13:1-3; 20:1; 24:62; Hes 13:17; 33:40; Kum 34:3; Yos 10:40Kisha Abramu akasafiri kuelekea upande wa Negebu.

Abramu Katika Nchi Ya Misri

12:10 Mwa 41:27; 42:5; 43:1; 47:4, 13; 41:30, 54-56; 47:20; Rut 1:1; 1Sam 21:1; 2Fal 8:1; Za 105:16Basi kulikuwako na njaa katika nchi, naye Abramu akashuka kwenda Misri kukaa huko kwa muda, kwa maana njaa ilikuwa kali. 12:11 Mwa 11:29; 24:16; 26:7; 29:17; 39:6Alipokuwa karibu kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, “Ninajua ya kwamba wewe ni mwanamke mzuri wa sura. Wakati Wamisri watakapokuona, watasema, ‘Huyu ni mke wake.’ Ndipo wataniua, lakini wewe watakuacha hai. 12:13 Mwa 20:2; 26:7Sema wewe ni dada yangu, ili nitendewe mema kwa ajili yako, na maisha yangu yatahifadhiwa kwa sababu yako.”

Abramu alipoingia Misri, Wamisri wakamwona Sarai kuwa ni mwanamke mzuri sana wa sura. Maafisa wa Farao walipomwona, wakamsifia kwa Farao; ndipo Sarai akapelekwa kwa nyumba ya mfalme. 12:16 Mwa 24:35; 26:14; 30:43; 32:5; 34:23; 47:17; Ay 1:3; 31:25Kwa ajili ya Sarai, Farao akamtendea Abramu mema, naye Abramu akapata kondoo, ngʼombe, punda, ngamia na watumishi wa kiume na wa kike.

12:17 2Fal 15:5; Isa 53:4; Ay 30:11; 1Nya 16:21; Za 105:14Lakini Bwana akamwadhibu Farao na nyumba yake kwa maradhi ya kufisha kwa sababu ya kumchukua Sarai, mke wa Abramu. 12:18 Mwa 20:9; 26:10; 29:25; 31:26; 44:15; Isa 43:27; 51:2; Eze 16:3Ndipo Farao akamwita Abramu, akamuuliza, “Umenifanyia nini? Kwa nini hukuniambia ni mke wako? 12:19 Mwa 20:5; 26:9Kwa nini ulisema, ‘Yeye ni dada yangu,’ hata nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa basi, mke wako huyu hapa. Mchukue uende zako!” Kisha Farao akawapa watu wake amri kuhusu Abramu, wakamsindikiza pamoja na mke wake na kila alichokuwa nacho.

Read More of Mwanzo 12

Mwanzo 13:1-18

Abramu Na Loti Watengana

13:1 Mwa 45:25; 12:9; 11:27Hivyo Abramu akakwea kutoka Misri kwenda Negebu, yeye na mkewe na kila kitu alichokuwa nacho, pia Loti akaenda pamoja naye. 13:2 Mwa 12:5; 26:13; 32:15; Mit 10:22; Ay 1:3; 42:12Wakati huo Abramu alikuwa tajiri sana wa mifugo, fedha na dhahabu.

13:3 Mwa 12:8-9Kutoka Negebu, akapita mahali hadi mahali, hadi akafika Betheli, mahali hapo ambapo mwanzoni alipiga hema lake kati ya Betheli na Ai 13:4 Mwa 12:7; 4:26hapo ambapo alikuwa amejenga madhabahu ya kwanza. Huko Abramu akaliitia jina la Bwana.

13:5 Mwa 11:27Basi Loti, ambaye alikuwa anafuatana na Abramu, alikuwa pia na makundi ya mbuzi, kondoo, ngʼombe na mahema. 13:6 Mwa 12:5; 33:9; 36:7Lakini nchi haikuwatosha kukaa pamoja kwa ajili ya wingi wa mali zao. 13:7 Mwa 26:20-21; 10:18; 15:20; 12:6; 34:30; Hes 20:3; Kut 3:8; Amu 1:4Ukazuka ugomvi kati ya wachunga mifugo wa Abramu na wale wa Loti. Wakati huo, Wakanaani na Waperizi ndio waliokuwa wenyeji wa nchi hiyo.

13:8 Mwa 11:27; 19:9; Mit 15:18; 20:3; Kut 2:14; Hes 16:13; Za 133:1Hivyo Abramu akamwambia Loti, “Pasiwe na ugomvi wowote kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wako, kwa kuwa sisi ni ndugu. 13:9 Mwa 20:15; 34:10; 47:6; Yer 40:4Je, nchi yote haiko mbele yako? Tutengane. Kama ukielekea kushoto, nitakwenda kulia; kama ukielekea kulia, mimi nitakwenda kushoto.”

13:10 1Fal 7:47; 2Nya 4:17; Hes 13:29; 33:48; Mwa 19:22; 2:8-10; 46:7; 14:2, 8Loti akatazama akaona lile bonde lote la Yordani kuwa lilikuwa na maji tele, kama bustani ya Bwana, kama nchi ya Misri, kuelekea Soari. (Hii ilikuwa kabla Bwana hajaharibu Sodoma na Gomora.) Hivyo Loti akajichagulia bonde lote la Yordani, akaelekea upande wa mashariki. Watu hao wawili wakatengana: 13:12 Mwa 10:19; 11:27; 19:17-29; 14:12Abramu akaishi katika nchi ya Kanaani, wakati Loti aliishi miongoni mwa miji ya lile bonde na kupiga mahema yake karibu na Sodoma. 13:13 Mwa 18:20; 19:4; 19:5; 20:6; 39:9; Isa 1:10; 3:9; Hes 32:23; 1Sam 12:23; 2Sam 12:13; Za 51:4; Eze 16:49-50; 2Pet 2:8Basi watu wa Sodoma walikuwa waovu, wakifanya sana dhambi dhidi ya Bwana.

13:14 Mwa 28:14; 32:12; 48:16; Kum 3:27; 13:17; Isa 54:3Baada ya Loti kuondoka Bwana akamwambia Abramu, “Ukiwa hapo ulipo, inua macho yako utazame kaskazini na kusini, mashariki na magharibi. 13:15 Mwa 12:7; Gal 3:16Nchi yote unayoiona nitakupa wewe na uzao wako hata milele. 13:16 Mwa 12:2; 16:10; 17:20; 21:13-18; 25:16; Hes 23:10Nitaufanya uzao wako uwe mwingi kama mavumbi ya nchi, hivyo kama kuna yeyote awezaye kuhesabu mavumbi, basi uzao wako utahesabika. 13:17 Mwa 12:7; 15:7; Hes 13:17-25Ondoka, tembea katika marefu na mapana ya nchi, kwa maana ninakupa wewe.”

13:18 Mwa 8:20; 14:13; 18:1; 23:2, 17, 19; 25:9; 49:30; 50:13; 35:27; Hes 13:22; Yos 10:3, 36; Amu 1:10; 1Sam 30:31; 2Sam 2:1-11; 1Nya 11:1Basi Abramu akaondoa mahema yake, akaenda kuishi karibu na mialoni ya Mamre huko Hebroni, huko akamjengea Bwana madhabahu.

Read More of Mwanzo 13