Mwanzo 1:1-31, Mwanzo 2:1-17 NEN

Mwanzo 1:1-31

Siku Sita Za Uumbaji Na Sabato

1:1 Za 89:11; 90:2; 96:5; 102:25; Mit 8:23; Isa 40:21; 42:5; 51:13; 41:4, 26; Yn 1:1-2; Mwa 2:3; 14:19; Neh 9:6; Ay 9:8; 37:18; Yer 10:12; 32:17; 51:15; 2Fal 19:15; Mdo 14:15; 7:24; Efe 3:9; Kol 1:16; Ebr 1:10; 3:4; 11:3; Ufu 4:11; 10:6Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia. 1:2 Isa 24:10; 27:10; 31:5; 32:14, 15; 34:11; 45:18; Yer 4:23; Mwa 8:2; Ay 7:12; 26:8; 33:4; 38:9; Za 36:6; 42:7; 104:6, 30; Mit 30:4Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametulia juu ya maji.

1:3 Za 33:6-9; 148:5; Ebr 11:3; 2Kor 4:6; 1Yn 5:7Mungu akasema, “Iwepo nuru,” nayo nuru ikawepo. 1:4 Za 18:28; 105:8; 104:31; 119:68; Yer 31:35; Kut 10:21-23; Ay 26:10; 8:19; Isa 42:16; 45:7Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza. 1:5 Mwa 2:19, 23; Za 74:16Mungu akaiita nuru “mchana,” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.

1:6 Isa 44:24; 2Pet 3:5; Za 24:2; 136:6Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji igawe maji na maji.” 1:7 Mwa 7:11; Ay 26:10; 38:8-16; Za 68:33; 148:4; Mit 8:28Kwa hiyo Mungu akafanya nafasi, akatenganisha maji yaliyo chini ya hiyo nafasi na maji yaliyo juu yake. Ikawa hivyo. 1:8 Ay 38:8-11; Za 33:7; 95:5; 104:6-9; Mit 8:29; Yer 5:22; 2Pet 3:5; Hag 2:6Mungu akaiita hiyo nafasi “anga.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili.

Mungu akasema, “Maji yaliyopo chini ya anga na yakusanyike mahali pamoja, pawepo na nchi kavu.” Ikawa hivyo. 1:10 Za 33:7; 90:2; 95:5; Ay 38:8Mungu akaiita nchi kavu “ardhi,” nalo lile kusanyiko la maji akaliita “bahari.” Mungu akaona kuwa ni vyema.

1:11 Za 65:9-13; 104:14; Mwa 2:9; Law 11:14, 19; 1Kor 15:38Kisha Mungu akasema, “Ardhi na itoe mimea: miche itoayo mbegu, miti juu ya nchi itoayo matunda yenye mbegu ndani yake, kila mmea kulingana na aina zake mbalimbali.” Ikawa hivyo. Ardhi ikachipua mimea: Mimea itoayo mbegu kulingana na aina zake, na miti itoayo matunda yenye mbegu kulingana na aina zake. Mungu akaona ya kuwa hili ni jema. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tatu.

1:14 Za 74:16; 136:7; 104:19; Yer 10:2; Mwa 8:22; Yer 31:35-36; 33:20, 25Mungu akasema, “Iwepo mianga kwenye nafasi ya anga ili itenganishe usiku na mchana, nayo iwe alama ya kutambulisha majira mbalimbali, siku na miaka, nayo iwe mianga kwenye nafasi ya anga ya kutia nuru juu ya dunia.” Ikawa hivyo. 1:16 Kum 17:3; Ay 38:33; 31:26; Yer 31:35; 43:13; Eze 8:16; Za 74:16; 104:19; 136:9; Yak 1:17; Kum 4:19Mungu akafanya mianga miwili mikubwa: mwanga mkubwa utawale mchana, na mwanga mdogo utawale usiku. Pia Mungu akafanya nyota. Mungu akaiweka katika nafasi ya anga iangaze dunia, 1:18 Yer 33:20itawale usiku na mchana, na ikatenganishe nuru na giza. Mungu akaona kuwa hili ni jema. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya nne.

1:20 Za 146:6; Mwa 2:19Mungu akasema, “Kuwepo na viumbe hai tele kwenye maji, nao ndege waruke juu ya dunia katika nafasi ya anga.” 1:21 Ay 3:8; 7:12; Za 74:13; 148:7; 104:25-26; Isa 27:1; Eze 32:2Kwa hiyo Mungu akaumba viumbe wakubwa wa baharini na kila kiumbe hai kiendacho majini kulingana na aina zake, na kila ndege mwenye mabawa kulingana na aina yake. Mungu akaona kuwa hili ni jema. 1:22 Mwa 8:17; 47:27; 9:17, 19; Law 26:9; Eze 36:11Mungu akavibariki, akasema, “Zaeni mwongezeke, mkayajaze maji ya bahari, nao ndege waongezeke katika dunia.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tano.

1:24 Mwa 2:19Mungu akasema, “Ardhi na itoe viumbe hai kulingana na aina zake: wanyama wa kufugwa, viumbe vitambaavyo ardhini na wanyama pori, kila mnyama kulingana na aina yake.” Ikawa hivyo. 1:25 Mwa 7:21-22; Yer 27:5Mungu akafanya wanyama pori kulingana na aina zake, wanyama wa kufugwa kulingana na aina zake, na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi kulingana na aina zake. Mungu akaona kuwa hili ni jema.

1:26 Mwa 5:3; 9:6; 9:2; Za 8:5-8; 8:8; 82:6; 89:6; Yak 3:9; 1Kor 11:7; 2Kor 4:4; Kol 1:15; 3:10; Mdo 17:28-29Ndipo Mungu akasema, “Tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale juu ya samaki wa baharini na ndege wa angani, juu ya mifugo, juu ya dunia yote, na juu ya viumbe wote watambaao juu ya nchi.”

1:27 Mwa 2:7; 5:1, 2; Za 103:14; 119:73; Mt 19:4; Mk 10:6; Gal 3:28; Kum 4:32Kwa hiyo Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake mwenyewe,

kwa mfano wa Mungu alimuumba;

mwanaume na mwanamke aliwaumba.

1:28 Mwa 6:1; 17:6; 33:5; Yos 24:3; Mdo 17:26; Za 8:6-8; 115:16; 113:9; 127:3, 5Mungu akawabariki na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.”

1:29 Mwa 9:3; 1Tim 4:3; Kum 12:15; Za 104:14Kisha Mungu akasema, “Nimewapa kila mche utoao mbegu juu ya uso wa dunia yote, na kila mti wenye matunda yenye mbegu ndani yake. Vitakuwa chakula chenu. 1:30 Mwa 2:7; 7:22; Ay 38:41; Za 78:25; 104:14, 27; 111:5; 136:25; 145:15Nao wanyama wote wa dunia, ndege wote wa angani, na viumbe vyote viendavyo juu ya ardhi: yaani kila kiumbe chenye pumzi ya uhai, ninawapa kila mche wa kijani kuwa chakula.” Ikawa hivyo.

1:31 Za 104:24; 136:5; Mhu 3:19; Yer 10:12; 1Tim 4:4Mungu akaona vyote alivyoumba, na tazama, ilikuwa vizuri sana. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya sita.

Read More of Mwanzo 1

Mwanzo 2:1-17

2:1 Kum 4:19; 17:3; 2Fal 17:16; 21:3; Za 104:2; Isa 44:24; 45:12; 48:13; 51:13Kwa hiyo mbingu na dunia zikakamilika, pamoja na vyote vilivyomo.

2:2 Kum 5:14; Ebr 4:4; Kut 20:11; 31:17; 34:21; Yn 5:17Katika siku ya saba Mungu alikuwa amekamilisha kazi aliyokuwa akiifanya, hivyo siku ya saba akapumzika kutoka kazi zake zote. 2:3 Kut 16:23; 20:10; 23:12; 31:15; 35:2; Law 23:3; Ebr 4:11; Neh 9:14; Mwa 1:1; Za 95:11; Isa 58:13; Yer 17:22Mungu akaibariki siku ya saba akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya.

Adamu Na Eva

2:4 Mwa 5:1; 6:9; 1:1; 10:1; 11:10; 27:25; Ay 38:8-11Haya ndiyo maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa.

Bwana Mungu alipoziumba mbingu na dunia, 2:5 Mwa 1:11; Ay 38:28; Za 65:9-10; Yer 10:13hapakuwepo na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwepo na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwa Bwana Mungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwepo mtu wa kuilima ardhi, lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi: 2:7 Isa 29:16; 43:1, 21; 44:2; Mwa 1:27; 3:19; 18:27; 5:23; 4:2; Ay 4:19; 10:9; 17:16; 34:15; Za 103:14; 90:3; Mhu 3:20; 12:7Bwana Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi2:7 Neno la Kiebrania la mavumbi ya ardhi ndilo kiini cha jina Adamu. ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai.

2:8 Mwa 3:23-24; 4:16; 13:10; Isa 51:3; Eze 28:13; 36:35; 31:9, 16; Yoe 2:3Basi Bwana Mungu alikuwa ameotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, huko akamweka huyo mtu aliyemuumba. 2:9 Eze 31:8; 47:12; Mit 3:18; 11:30; Ufu 2:7; Mwa 3:22, 24Bwana Mungu akafanya aina zote za miti ziote kutoka ardhini, miti yenye kupendeza macho na mizuri kwa chakula. Katikati ya bustani ulikuwepo mti wa uzima na mti wa kujua mema na mabaya.

2:10 Hes 24:6; Eze 47:5; Za 46:4Mto wa kunyeshea bustani ulitiririka toka Edeni, kuanzia hapa ukagawanyika kuwa mito minne. 2:11 Mwa 10:7; 25:18Mto wa kwanza uliitwa Pishoni, nao huzunguka nchi yote ya Havila ambako kuna dhahabu. 2:12 Hes 11:7(Dhahabu ya nchi hiyo ni nzuri, bedola na vito shohamu pia hupatikana huko.) Jina la mto wa pili ni Gihoni, ambao huzunguka nchi yote ya Kushi. 2:14 Mwa 15:18; 41:1; 31:21; Dan 10:4; Kut 23:31; Hes 22:5; Ufu 9:14; 1Fal 4:21; 2Sam 8:3; Kum 11:24; 2Fal 23:29; 24:7; 1Nya 5:9; 18:3; 2Nya 35:20; Yer 13:4; 42:6; 51:63Jina la mto wa tatu ni Tigrisi, unaopita mashariki ya Ashuru. Mto wa nne ni Frati.

Bwana Mungu akamchukua huyo mtu, akamweka kwenye Bustani ya Edeni ailime na kuitunza. 2:16 Mwa 3:1-2Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akamwambia, “Uko huru kula matunda ya mti wowote katika bustani, 2:17 Mwa 3:11, 17; 9:29; Yer 42:16; Kum 30:15, 19; Eze 3:18; Rum 5:13; 6:23lakini kamwe usile matunda ya mti wa kujua mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.”

Read More of Mwanzo 2