Wagalatia 5:7-26 NEN

Wagalatia 5:7-26

5:7 1Kor 9:24; Gal 3:1Mlikuwa mkipiga mbio vizuri. Ni nani aliyewazuia msiitii kweli? 5:8 Rum 8:28; Gal 1:6Ushawishi wa namna hiyo haukutokana na yule anayewaita. 5:9 1Kor 5:6; 15:33“Chachu kidogo huchachua donge zima.” 5:10 2Kor 2:3; Flp 3:15; Gal 1:7Nina hakika katika Bwana kwamba hamtakuwa na msimamo mwingine. Mtu anayewachanganya anastahili adhabu, hata awe nani. 5:11 Gal 4:29; 6:12; Lk 2:34Lakini ndugu zangu, kama mimi bado ninahubiri kuhusu kutahiriwa, kwa nini bado ninateswa? Katika hiyo hali basi, kwazo la msalaba limeondolewa. 5:12 Gal 5:10; Yos 7:25; 1Kor 5:13; Gal 1:8, 9; Mdo 15:1, 2, 24Laiti hao wanaowavuruga wangejihasi wao wenyewe!

5:13 Gal 5:1, 24; 1Kor 8:9; 1Pet 2:16; 1Kor 9:19; 2Kor 4:5Ndugu zangu, ninyi mliitwa ili mwe huru, hivyo msitumie uhuru wenu kama fursa ya kufuata tamaa za mwili, bali tumikianeni ninyi kwa ninyi kwa upendo. 5:14 Law 19:18; Mt 5:43; Gal 6:2Kwa maana sheria yote hukamilika katika amri moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” Kama mkiumana na kutafunana, angalieni, msije mkaangamizana.

Maisha Ya Kiroho

5:16 Gal 5:18, 25; Rum 8:2, 4-6, 9; 14; 2Kor 5:17; Gal 5:14Kwa hiyo nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 5:17 Rum 8:5-8; 7:15-23Kwa maana mwili hutamani yale yaliyo kinyume na Roho, naye Roho hutamani yale yaliyo kinyume na mwili. Roho na mwili hupingana na kwa sababu hiyo hamwezi kufanya mnayotaka. 5:18 Rum 2:12; 6:14; Gal 5:16; 1Tim 1:9Lakini kama mkiongozwa na Roho, hamko chini ya sheria.

5:19 1Kor 6:18; 3:3; Efe 5:3; Kol 3:5; Yak 3:14, 15Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: Uasherati, uchafu, ufisadi, kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 5:21 Rum 13:13; Mt 15:19; 25:34; 1Kor 6:9husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama hayo, hawataurithi Ufalme wa Mungu.

5:22 Mt 7:16-20Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi. Katika mambo kama haya hakuna sheria. Wote walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili na shauku zake pamoja na tamaa zake. Kwa kuwa tunaishi kwa Roho, basi, tuenende kwa Roho. 5:26 Flp 2:3; Mt 18:15; Yak 2:19Tusijisifu bure, tukichokozana na kuoneana wivu.

Read More of Wagalatia 5