Wagalatia 4:21-31, Wagalatia 5:1-6 NEN

Wagalatia 4:21-31

Mfano Wa Hagari Na Sara

4:21 Rum 2:12Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria, je, hamjui sheria inavyosema? Kwa maana imeandikwa kwamba Abrahamu alikuwa na wana wawili, mmoja wa mwanamke mtumwa na wa pili wa mwanamke huru. 4:23 Gal 4:28, 29; Rum 9:7, 8; Mwa 17:16-21; 18:10-14; 4:24Lakini, mtoto wa mwanamke mtumwa alizaliwa kwa mapenzi ya mwili, na yule mwingine wa mwanamke huru alizaliwa kutokana na ahadi ya Mungu.

Mambo haya yanaweza kuchukuliwa kama mfano. Kwa maana hao wanawake wawili ni mfano wa maagano mawili: Agano la kwanza, ni lile lililofanyika katika Mlima Sinai, lizaalo watoto wa utumwa. Hili ndilo huyo Hagari. Basi Hagari anawakilisha Mlima Sinai ulioko Arabuni, na unafanana na Yerusalemu ya sasa ambayo iko utumwani pamoja na watoto wake. 4:26 Flp 2:3; Ebr 12:22; Isa 2:2; Ufu 3:12; 21:2, 10Lakini Yerusalemu wa juu ni huru, nayo ndiye mama yetu. 4:27 Isa 54:1Kwa maana imeandikwa:

“Furahi, ewe mwanamke tasa,

wewe usiyezaa;

paza sauti, na kuimba kwa furaha,

wewe usiyepatwa na utungu wa kuzaa;

kwa maana watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi

kuliko wa mwanamke mwenye mume.”

4:28 Mdo 3:25; Rum 9:8; Gal 3:29Basi, sisi ndugu zangu, ni kama Isaki, tu watoto wa ahadi. 4:29 Mwa 21:9; Gal 5:11; 6:12Lakini, kama vile ilivyokuwa siku zile yule aliyezaliwa kwa mwili alivyomchokoza yule aliyezaliwa kwa Roho, ndivyo ilivyo hata sasa. 4:30 Mwa 21:10Lakini Maandiko yasemaje? “Mwondoe mwanamke mtumwa pamoja na mwanawe, kwa sababu mwana wa mwanamke mtumwa kamwe hatarithi pamoja na mwana wa aliye huru.” 4:31 Rum 7:4; Gal 4:22Kwa hiyo ndugu zangu, sisi si watoto wa mwanamke mtumwa, bali wa yule aliye huru.

Read More of Wagalatia 4

Wagalatia 5:1-6

Uhuru Ndani Ya Kristo

5:1 Gal 5:13; 2:4; Yn 8:32; Rum 7:4; 1Kor 16:13; Mt 23:4Kristo alitupa uhuru, akataka tubaki huru. Hivyo simameni imara wala msikubali tena kulemewa na kongwa la utumwa.

5:2 Gal 5:3; Mdo 15:1Sikilizeni! Mimi, Paulo, nawaambieni kwamba kama mkikubali kutahiriwa, basi Kristo hatawafaidia chochote. 5:3 Rum 2:25; Gal 3:10; Yak 2:10Namshuhudia tena kila mtu anayekubali kutahiriwa kwamba inampasa kushika sheria yote. 5:4 Rum 3:28; Ebr 12:15; 2Pet 3:17Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria mmetengwa na Kristo, mko mbali na neema ya Mungu. 5:5 Rum 8:23, 24; 2Tim 4:8; 1Kor 7:19Kwa maana, kwa njia ya Roho kwa imani, tunangojea kwa shauku tumaini la haki. 5:6 Rum 16:3; 1Kor 7:19; 1The 1:3; Yak 2:22Kwa maana ndani ya Kristo Yesu, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kwa njia ya upendo.

Read More of Wagalatia 5