Wagalatia 3:10-25 NEN

Wagalatia 3:10-25

Sheria Na Laana

3:10 Kum 27:26; Yer 11:3Kwa maana wote wanaotumainia matendo ya sheria wako chini ya laana, kwa kuwa imeandikwa, “Alaaniwe kila mtu asiyeshikilia kutii mambo yote yaliyoandikwa katika Kitabu cha Sheria.” 3:11 Gal 2:16; Hab 2:4; Rum 1:17; Ebr 10:38Basi ni dhahiri kwamba hakuna mtu anayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa kushikilia sheria, kwa maana, “Mwenye haki ataishi kwa imani.” 3:12 Rum 4:4, 5; Law 18:5; Neh 9:29; Eze 20:11Lakini sheria haitegemei imani. Kinyume chake, “Mtu atendaye matendo hayo ataishi kwa hayo.” 3:13 Rum 8:3; 2Kor 5:21; 4:5; Kum 21:23Kristo alitukomboa kutoka laana ya sheria kwa kufanyika laana kwa ajili yetu, kwa maana imeandikwa, “Amelaaniwa yeye aangikwaye juu ya mti.” 3:14 Rum 4:9, 16; Isa 32:15; 44:3; Yer 31:33; 32:40; Eze 11:19Alitukomboa ili kwamba baraka aliyopewa Abrahamu ipate kuwafikia watu wa Mataifa kwa njia ya Kristo Yesu, ili kwa imani tupate kupokea ile ahadi ya Roho.

Sheria Na Ahadi

3:15 Ebr 9:17; Rum 7:1Ndugu zangu, nataka nitoe mfano kutoka maisha ya kila siku. Kama vile hakuna mtu awezaye kutangua au kuongeza kitu katika agano la mtu ambalo limekwisha kuthibitishwa, vivyo hivyo kwa hali kama hii. 3:16 Mwa 17:19; Za 132:11; Mik 7:20; Lk 1:55; Rum 4:13, 16Ahadi zilinenwa kwa Abrahamu na kwa mzao wake. Maandiko hayasemi “kwa wazao,” likimaanisha watu wengi, bali “kwa mzao wako,” yaani mtu mmoja, ndiye Kristo. 3:17 Mwa 15:13, 14; Kut 12:40; Mdo 7:6Ninachotaka kusema ni kwamba, sheria, ambayo ilitolewa miaka 430 baadaye, haitangui Agano lililothibitishwa na Mungu ili kuibatilisha ahadi ile. 3:18 Rum 4:14Kwa maana kama urithi hupatikana kwa sheria, basi hautegemei tena ahadi, lakini Mungu kwa neema yake alimpa Abrahamu urithi kwa njia ya ahadi.

Kusudi La Sheria

3:19 Rum 5:20; 3:16; Kum 33:2; Mdo 7:53; Kut 20:19Kwa nini basi iwepo sheria? Sheria iliwekwa kwa sababu ya makosa mpaka atakapokuja yule Mzao wa Abrahamu, ambaye alitajwa katika ile ahadi. Sheria iliamriwa na malaika kwa mkono wa mpatanishi. 3:20 1Tim 2:5; Ebr 8:6; 9:15; 12:24Basi mpatanishi huhusisha zaidi ya upande mmoja, lakini Mungu ni mmoja.

3:21 Gal 2:17; Rum 7:12; Gal 2:21Je basi, sheria inapingana na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa maana kama sheria iliyotolewa ingeweza kuwapa watu uzima, basi haki ingepatikana kwa njia ya sheria. 3:22 Rum 3:9-19; 11:32Lakini Maandiko yamefanya vitu vyote vifungwe chini ya nguvu ya dhambi, ili yale yaliyoahidiwa kwa njia ya imani katika Yesu Kristo yapate kupewa wale wanaoamini.

3:23 Rum 11:32; Gal 3:25Kabla imani hii haijaja tulikuwa tumewekwa chini ya sheria, tumefungwa mpaka ile imani ifunuliwe. 3:24 Gal 3:19; Rum 10:4; 4:15; Gal 2:16Hivyo, sheria ilikuwa kiongozi kutufikisha kwa Kristo, ili tupate kuhesabiwa haki kwa imani. 3:25 Rum 7:4; 10:4Lakini sasa kwa kuwa ile imani imekuja, hatusimamiwi tena na sheria.

Read More of Wagalatia 3