Wagalatia 2:11-21, Wagalatia 3:1-9 NEN

Wagalatia 2:11-21

Paulo Ampinga Petro Huko Antiokia

2:11 Mdo 11:19; 15:35Lakini Petro alipofika Antiokia, mimi nilimpinga ana kwa ana kwa sababu alikuwa amekosea kwa wazi. 2:12 Mdo 11:2-3Kabla baadhi ya watu waliotoka kwa Yakobo hawajafika, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa. Lakini hao watu walipofika alianza kujiondoa na kujitenga na watu wa Mataifa kwa sababu aliwaogopa wale wa kundi la tohara. 2:13 Mdo 4:36Pia Wayahudi wengine waliungana naye katika unafiki huu, hata Barnaba naye akapotoshwa na unafiki wao.

2:14 Mdo 10:28; 1Tim 5:20; Mdo 11:3Nilipoona kwamba hawatendi sawasawa na kweli ya Injili, nilimwambia Petro mbele ya wote, “Wewe ni Myahudi, nawe unaishi kama mtu wa Mataifa na wala si kama Myahudi. Imekuwaje basi, mnawalazimisha watu wa Mataifa kufuata desturi za Kiyahudi?

Wayahudi Na Watu Wa Mataifa Wanaokolewa Kwa Imani

2:15 Flp 3:4-5; 1Sam 15:18“Sisi wenyewe ni Wayahudi kwa kuzaliwa na si watu wenye dhambi kama watu wa Mataifa, 2:16 Mdo 13:39; Rum 9:30bado tunajua ya kwamba mtu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria bali kwa njia ya imani katika Yesu Kristo. Hivyo sisi pia, tumemwamini Kristo Yesu ili tupate kuhesabiwa haki kwa njia ya imani katika Kristo, wala si kwa matendo ya sheria, kwa sababu kwa kushika sheria hakuna hata mtu mmoja atakayehesabiwa haki.

2:17 Gal 3:21“Lakini tukitafuta kuhesabiwa haki katika Kristo, inakuwa dhahiri kwamba sisi ni wenye dhambi. Je, ina maana kwamba Kristo amekuwa mtumishi wa dhambi? La hasha! Lakini ikiwa mimi ninajenga tena kile ambacho nimekwisha kukibomoa, basi ninaonyesha kwamba mimi ni mkosaji. 2:19 Rum 7:4; 6:10-14; 2Kor 5:15Kwa maana mimi kwa njia ya sheria, nimeifia sheria ili nipate kuishi kwa ajili ya Mungu. 2:20 Rum 6:6; 1Pet 4:2; Mt 4:3; Rum 8:37; Gal 1:4Nimesulubiwa pamoja na Kristo, wala si mimi tena ninayeishi, bali Kristo ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi kwa imani ya Mwana wa Mungu, aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu. 2:21 Gal 3:21Siibatilishi neema ya Mungu, kwa maana kama haki ingeweza kupatikana kwa njia ya sheria, basi Kristo alikufa bure!”

Read More of Wagalatia 2

Wagalatia 3:1-9

Imani Au Kushika Sheria?

3:1 Gal 5:7; 1Kor 1:23Ninyi Wagalatia wajinga! Ni nani aliyewaroga? Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele yenu kwamba amesulubiwa. 3:2 Rum 10:17; Yn 20:22; Gal 3:5, 10; 2:16; Rum 10:17Nataka nijifunze neno moja kutoka kwenu: Je, mlipokea Roho wa Mungu kwa kushika sheria, au kwa kuyaamini yale mliyosikia? 3:3 Gal 4:9; Ebr 7:16; 9:10Je, ninyi ni wajinga kiasi hicho? Baada ya kuanza kwa Roho, je, sasa mwataka kumalizia katika mwili? 3:4 Ebr 10:35, 36; 2Yn 8Je, mlipata mateso kiasi hicho bure? Ni kama kweli yalikuwa bure! 3:5 1Kor 12:10; 2Kor 3:8Je, Mungu huwapa Roho wake na kufanya miujiza katikati yenu kwa sababu mnatii sheria, au kwa sababu mnaamini kile mlichosikia?

3:6 Mwa 15:6; Rum 4:3Kama vile “Abrahamu alimwamini Mungu na ikahesabiwa kwake kuwa haki.” 3:7 Yn 8:39; Rum 4:11, 12, 16Fahamuni basi kwamba wale walio na imani, hao ndio watoto wa Abrahamu. 3:8 Mwa 18:18; Mdo 3:25Maandiko yakitabiri kwamba Mungu angewahesabia haki watu wa Mataifa kwa imani, alitangulia kumtangazia Abrahamu Injili akisema kwamba, “Kwa kupitia kwako mataifa yote yatabarikiwa.” 3:9 Rum 4:16; Gal 3:7; Rum 4:18-22Kwa sababu hii, wale wote wanaoamini wanabarikiwa pamoja na Abrahamu, mtu wa imani.

Read More of Wagalatia 3