Ezra 8:15-36, Ezra 9:1-15 NEN

Ezra 8:15-36

Kurudi Yerusalemu

8:15 Ezr 2:40; 7:7; Mdo 16:13; 20:28; Za 137:1; Mit 27:23; Ebr 13:17; Ezr 7:7; Hes 8:1Niliwakusanya kwenye mto utiririkao kuelekea Ahava, nasi tukapiga kambi pale siku tatu. Wakati nilipokagua kati ya watu na makuhani, sikuwapata Walawi. Basi niliwaita Eliezeri, Arieli, Shemaya, Elnathani, Yaribu, Elnathani, Nathani, Zekaria na Meshulamu waliokuwa viongozi na Yoyaribu na Elnathani waliokuwa wasomi, 8:17 Ezr 2:43nikawatuma kwa Ido kiongozi huko Kasifia. Niliwaambia watakayomwambia Ido na ndugu zake, watumishi wa Hekalu8:17 Yaani Wanethini (pia 8:20). huko Kasifia, ili waweze kutuletea wahudumu kwa ajili ya nyumba ya Mungu wetu. 8:18 Ezr 5:5Kwa sababu mkono wa neema wa Mungu wetu ulikuwa juu yetu, walituletea Sherebia, mtu mwenye uwezo kutoka wazao wa Mahli mwana wa Lawi, mwana wa Israeli, na wana wa Sherebia pamoja na ndugu zao wanaume kumi na wanane. Naye Hashabia, pamoja na Yeshaya kutoka wazao wa Merari na ndugu zake na wapwa wake wanaume ishirini. 8:20 1Nya 9:2; Ezr 2:43Vilevile walileta watumishi wa Hekalu 220, kikundi ambacho Daudi na maafisa walikuwa wamekiweka kusaidia Walawi. Wote walikuwa wameorodheshwa kwa majina.

8:21 2Nya 9:2; Ezr 2:438:21 2Nya 20:3; Za 27:11; Law 16:29; Za 5:8; 2Nya 20:3; Law 16:29; Isa 58:3-5Kando ya Mto Ahava, hapo nilitangaza kufunga, ili tujinyenyekeshe mbele za Mungu wetu na kumwomba kwa ajili ya kutujalia safari ya amani sisi na watoto wetu, pamoja na mali zetu zote. 8:22 Neh 2:9; Yer 41:16; Kum 31:17; 2Nya 15:2; 1Kor 9:15; 1Nya 28:9; Ezr 7:6-9; Za 33:18-19; Isa 3:10; Rum 8:28; 1Pet 3:12; Za 34:16; 2Nya 15:2Niliona aibu kumwomba mfalme askari na wapanda farasi wa kutulinda njiani kutokana na adui zetu, kwa sababu tulikwisha kumwambia mfalme, “Mkono wa neema wa Mungu wetu uko juu ya kila mmoja anayemtafuta, lakini hasira yake kubwa ni dhidi ya wote wamwachao.” 8:23 2Nya 33:13; Kum 4:29; Mdo 14:23; 1Nya 5:20; Isa 19:22; Yer 29:12-13Kwa hiyo tulifunga na kumwomba Mungu wetu kuhusu jambo hili, naye akajibu maombi yetu.

Kisha niliwatenga viongozi wa makuhani kumi na wawili, pamoja na Sherebia, Hashabia na ndugu zao kumi, 8:25 Ezr 7:15-16nami nikawapimia fedha, dhahabu na vifaa ambavyo mfalme, washauri wake, maafisa wake na Israeli wote waliokuwepo walikuwa wamevitoa sadaka kwa ajili ya nyumba ya Mungu wetu. Niliwapimia talanta 6508:26 Talanta 650 za fedha ni sawa na tani 25. za fedha, vifaa vingine vya fedha vya uzito wa talanta mia moja,8:26 Talanta 100 za fedha ni sawa na tani 3.75. talanta mia moja za dhahabu, mabakuli ishirini ya dhahabu ya thamani ya darkoni elfu moja,8:27 Darkoni 1,000 ni sawa na kilo 8.5. na vyombo viwili vya shaba iliyosuguliwa, ya thamani kama dhahabu.

8:28 Kum 33:8; Law 21:6; 22:2-3; 2Nya 24:14; Hes 4:4; Isa 52:11; 1Nya 23:28Niliwaambia, “Ninyi pamoja na vyombo hivi ni wakfu kwa Bwana. Fedha na dhahabu ni sadaka ya hiari kwa Bwana, Mungu wa baba zenu. 8:29 1Nya 26:20-26; Lk 12:38-39Vilindeni kwa uangalifu mpaka mtakapovipima ndani ya vyumba vya nyumba ya Bwana katika Yerusalemu mbele ya makuhani, viongozi na Walawi pamoja na wakuu wa jamaa za Israeli.” Ndipo makuhani na Walawi wakapokea fedha, dhahabu na vyombo vilivyowekwa wakfu ambavyo vilipimwa na kupelekwa katika nyumba ya Mungu wetu mjini Yerusalemu.

8:31 Ay 5:19-24; Isa 41:10-14; Ezr 7:6-7, 28Tulianza safari kutoka Mto Ahava kwenda Yerusalemu kwenye siku ya kumi na mbili ya mwezi wa kwanza. Mkono wa Mungu wetu ulikuwa juu yetu, naye njiani alitulinda dhidi ya adui na wanyangʼanyi. 8:32 Mwa 40:13; Neh 2:11; Isa 56:6; 14:1Kwa hiyo tuliwasili Yerusalemu ambapo tulipumzika kwa siku tatu.

8:33 Neh 3:3, 21-24Katika siku ya nne, ndani ya nyumba ya Mungu wetu, tulipima fedha, dhahabu na vyombo vilivyowekwa wakfu, tukakabidhi mikononi mwa kuhani Meremothi mwana wa Uria. Eleazari mwana wa Finehasi alikuwa pamoja naye, pia walikuwako Walawi wawili, Yozabadi mwana wa Yeshua na Noadia mwana wa Binui. Kila kitu kilihesabiwa kwa idadi na kupimwa kwa uzito, nao uzito wote uliandikwa wakati ule.

8:35 Law 1:3; 2Nya 29:21, 24; 30:24; Ezr 6:17Kisha mateka waliokuwa wamerudi kutoka utumwani wakatoa sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa Mungu wa Israeli: mafahali kumi na wawili kwa ajili ya Israeli wote, kondoo dume tisini na sita, wana-kondoo sabini na saba na mbuzi dume kumi na wawili kuwa sadaka ya dhambi. Hii yote ilikuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto kwa Bwana. 8:36 Ezr 7:21-24; Zek 8:1-23; Es 9:3Pia walikabidhi manaibu wa mfalme na watawala wa Ngʼambo ya Mto Frati maagizo ya mfalme, ambao baadaye walitoa msaada kwa watu na kwa nyumba ya Mungu.

Read More of Ezra 8

Ezra 9:1-15

Maombi Ya Ezra Kuhusu Kuoa Wake Wa Kigeni

9:1 Neh 9:2; Mwa 19:38; Kum 20:17; Amu 3:5; Kum 12:30Baada ya mambo haya kutendeka, viongozi walinijia na kusema, “Watu wa Israeli, wakiwemo makuhani na Walawi, hawakujitenga na majirani zao katika kufanya machukizo, kama yale ya Wakanaani, Wahiti, Waperizi, Wayebusi, Waamoni, Wamoabu, Wamisri na Waamori. 9:2 Law 27:30; Ezr 10:2; 2Kor 6:14; Kut 22:31; Kum 7:3Wamewaoa baadhi ya binti zao kuwa wake zao na wake za wana wao, nao wamechanganya taifa takatifu na watu waliowazunguka. Nao viongozi na maafisa wamekuwa mstari wa mbele katika njia hii potovu.”

9:3 Isa 15:2; Za 143:4Niliposikia jambo hili nilirarua koti langu na joho langu, nikazingʼoa nywele za kichwa changu na ndevu zangu na kuketi nikishangaa. 9:4 Za 119:120; Isa 66:2-59:4 Ezr 10:3; Kut 29:39Kisha kila mmoja aliyetetemeshwa na maneno ya Mungu wa Israeli alikusanyika kunizunguka kwa sababu ya upotovu huu wa hao watu waliorudi kutoka utumwani. Nami niliketi pale nikishangaa mpaka wakati wa dhabihu ya jioni.

9:5 Kut 9:29; 29:41Ndipo wakati wa kutoa dhabihu ya jioni nikainuka kutoka kujidhili kwangu nikiwa na koti na joho langu lililoraruka, nikapiga magoti mikono yangu ikiwa imeinuliwa kwa Bwana Mungu wangu. 9:6 Ufu 18:5; Dan 9:7; Isa 59:12Nami nikaomba:

“Ee Mungu wangu, natahayari na kuona aibu kukuinulia uso wangu Mungu wangu, kwa sababu dhambi zetu zimejikusanya hata kupita juu ya vichwa vyetu na hatia yetu imefika mbinguni. 9:7 2Nya 29:6; Eze 21:1-32; Kum 28:36-64; Za 106:6; 2Nya 19:2; Mwa 18:19Tokea siku za babu zetu mpaka sasa, hatia yetu imekuwa kubwa. Kwa sababu ya dhambi zetu, sisi na wafalme wetu na makuhani wetu tumekabiliwa na vita, utumwa, kutekwa na kudhiliwa katika mikono ya wafalme wa kigeni, kama ilivyo leo.

9:8 Isa 33:2; Za 13:3; Mhu 12:11; Mwa 45:7; Isa 22:23; Za 19:8“Lakini sasa, kwa muda mfupi, Bwana Mungu wetu amekuwa na neema kwa kutuachia mabaki na kutupa mahali imara katika mahali pake patakatifu, hivyo Mungu wetu atupa mwanga machoni petu na unafuu katika utumwa wetu. 9:9 Neh 9:36; Kut 1:14; 2Fal 25:28; Zek 1:16-17; Ezr 7:28Ingawa tu watumwa, Mungu wetu hajatuacha katika kufungwa kwetu. Ametuonyesha huruma mbele ya wafalme wa Uajemi: Ametujalia maisha mapya kwa kujenga upya nyumba ya Mungu wetu na kukarabati magofu yake, naye ametupa ukuta wa ulinzi katika Yuda na Yerusalemu.

9:10 Kum 11:8; Isa 1:19-20“Lakini sasa, Ee Mungu wetu, tunaweza kusema nini baada ya hili? Kwa maana tumedharau maagizo 9:11 Law 18:25-28; Kum 18:9; 1Fal 14:24uliyoyatoa kupitia watumishi wako manabii uliposema: ‘Nchi mnayoiingia kuimiliki ni nchi iliyochafuliwa na uovu wa watu wake. Kwa matendo yao ya machukizo wameijaza nchi kwa unajisi wao kutoka mwisho mmoja hadi mwingine. 9:12 Kut 34:15; Kum 7:39:12 Mit 13:22; Kut 23:32-33; Amu 2:2; 2Pet 2:20; 2Kor 6:14Kwa hiyo, msiwaoze binti zenu kwa wana wao wala binti zao kwa wana wenu. Msitafute mkataba wa urafiki nao kwa wakati wowote. Ndipo mtakapofanikiwa na kula mema ya nchi na kuwaachia watoto wenu nchi hiyo kama urithi wao wa milele.’

9:13 Ay 15:5; Za 103:10“Yale yaliyotupata ni matokeo ya matendo yetu mabaya, pia hatia yetu kubwa. Hata hivyo, wewe Mungu wetu, umetuadhibu kidogo kuliko dhambi zetu zilivyostahili na umetupa mabaki kama haya. 9:14 Kum 9:8-14; Neh 13:27; Yn 5:14Je, tutavunja maagizo yako tena na kuoana na watu ambao hufanya mambo ya machukizo? Je, hutakuwa na hasira ya kutosha juu yetu na kutuangamiza, bila kutuachia mabaki wala atakayenusurika? 9:15 Neh 9:33; Za 51:4; Rum 3:19; Isa 24:16; 1Fal 8:47; Dan 9:14; Za 130:3Ee Bwana, Mungu wa Israeli, wewe ni mwenye haki! Leo hii tumeachwa kama mabaki. Tupo hapa mbele zako na hatia yetu, ingawa katika hali hii hakuna hata mmoja wetu anayeweza kusimama mbele zako.”

Read More of Ezra 9