Ezra 7:11-28, Ezra 8:1-14 NEN

Ezra 7:11-28

Barua Ya Ezra Kutoka Kwa Mfalme Artashasta

Hii ni nakala ya barua ambayo Mfalme Artashasta alikuwa amempa Ezra aliyekuwa kuhani na mwalimu, mtu aliyeelimika katika mambo yahusuyo maagizo na amri za Bwana kwa Israeli.

7:12 Eze 26:7; Dan 2:37; Ezr 4:10Artashasta, mfalme wa wafalme,

Kwa Ezra kuhani, mwalimu wa Sheria ya Mungu wa mbinguni:

Salamu.

Sasa naamuru kwamba mtu yeyote Mwisraeli katika ufalme wangu, pamoja na makuhani na Walawi, ambaye anataka kwenda Yerusalemu pamoja nawe aweza kwenda. 7:14 Es 1:14Unatumwa na mfalme na washauri wake saba kuchunguza kuhusu Yuda na Yerusalemu kulingana na Sheria ya Mungu wako, iliyoko mkononi mwako. 7:15 Kum 12:5; 1Nya 29:6; 2Nya 6:2; Za 135:21Zaidi ya hayo, uchukue pamoja nawe fedha na dhahabu ambazo mfalme na washauri wake wamempa Mungu wa Israeli kwa hiari, Mungu ambaye maskani yake yako Yerusalemu, 7:16 Kut 3:22; Ezr 8:25; Zek 6:10; 1Nya 29:6pia fedha na dhahabu zote unazoweza kupata kutoka jimbo la Babeli, pamoja na sadaka za hiari watakazotoa watu na makuhani kwa ajili ya Hekalu la Mungu wao katika Yerusalemu. 7:17 2Fal 3:5; Hes 15:5-12; Kum 12:5-11Hakikisha kwamba fedha hizi zimetumika kununua mafahali, kondoo dume na wana-kondoo pamoja na sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji, uvitoe dhabihu juu ya madhabahu ya Hekalu la Mungu wenu katika Yerusalemu.

Kisha wewe na Wayahudi ndugu zako mnaweza kufanya lolote linaloonekana jema sana kwa fedha na dhahabu zilizosalia, kulingana na mapenzi ya Mungu wenu. 7:19 Ezr 5:14; Yer 27:22Uvitoe kwa Mungu wa Yerusalemu vyombo vyote ulivyokabidhiwa kwa ajili ya ibada katika Hekalu la Mungu wako. 7:20 Ezr 6:4; 1Kor 4:1-2Kitu kingine chochote kinachohitajika kwa ajili ya Hekalu la Mungu wenu ambacho unatakiwa kukitoa, waweza kukitoa kutoka hazina ya mfalme.

7:21 Ezr 4:16-20; 5:3-6Mimi, Mfalme Artashasta, sasa naagiza watunza hazina wote wa Ngʼambo ya Mto Frati kutoa kwa bidii chochote kwa Ezra kuhani na mwalimu wa Sheria ya Mungu wa mbinguni atakachohitaji kwenu, talanta 1007:22 Talanta 100 za fedha ni sawa na kilo 3,400. za fedha, ngano kori 100,7:22 Kori 100 za ngano ni sawa na kilo 10,000. divai bathi 100,7:22 Bathi 100 za divai ni sawa na lita 2,000. mafuta ya zeituni bathi 100, na chumvi kiasi chochote. 7:23 Ezr 6:10; Isa 60:12; Yer 12:14; Za 68:29; 1Tim 2:1-2Chochote ambacho Mungu wa mbinguni ameagiza, kifanyike kwa ukamilifu kwa ajili ya Hekalu la Mungu wa mbinguni. Kwa nini pawepo ghadhabu dhidi ya utawala wa mfalme na wanawe? 7:24 Ezr 4:13; 8:36Pia ninyi fahamuni kuwa hamna mamlaka ya kuwatoza kodi, ushuru au ada makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, watumishi wa Hekalu au wafanyakazi wengine kwenye nyumba ya Mungu.

7:25 Kut 18:21-26; 16:18; Za 19:7; Kol 1:28; Kum 16:18; 2Nya 17:7; Mal 2:7; Mt 13:52Nawe Ezra, kufuatana na hekima ya Mungu wenu uliyo nayo, weka mahakimu na waamuzi wote wanaozifahamu sheria za Mungu wenu ili watoe haki kwa watu wote wa Ngʼambo ya Mto Frati. Nawe inakupasa umfundishe yeyote ambaye hazifahamu. 7:26 Eze 6:11Yeyote ambaye hataitii sheria ya Mungu wenu pia sheria ya mfalme, hakika lazima aadhibiwe kwa kuuawa, kuhamishwa, kunyangʼanywa mali au kufungwa gerezani.

7:27 Ezr 6:22; 1Nya 29:12; Neh 2:12; 2Kor 8:16; Flp 4:10; Mit 16:7Sifa ziwe kwa Bwana, Mungu wa baba zetu, Mungu ambaye kwa njia hii ameweka ndani ya moyo wa mfalme kuipa heshima nyumba ya Bwana iliyoko Yerusalemu, kwa namna hii 7:28 2Fal 25:28; Ezr 5:5; 9:9; Neh 1:117:28 Neh 8:7; Rum 8:28; Mit 3:6; Law 10:10-11; 2Nya 30:22ambaye ameniongezea kibali chake mbele ya mfalme, washauri wake na maafisa wote wa mfalme wenye uwezo. Kwa kuwa mkono wa Bwana Mungu wangu ulikuwa pamoja nami, nilijipa moyo nikakusanya watu walio viongozi kutoka Israeli wakwee pamoja nami.

Read More of Ezra 7

Ezra 8:1-14

Orodha Ya Viongozi Wa Jamaa Waliorudi Na Ezra

8:1 Ezr 7:7Hawa ndio viongozi wa jamaa pamoja na wale walioandikwa ambao walikuja pamoja nami kutoka Babeli wakati wa utawala wa Mfalme Artashasta:

8:2 1Nya 3:22wa wazao wa Finehasi, alikuwa Gershoni;

wa wazao wa Ithamari, alikuwa Danieli;

wa wazao wa Daudi, alikuwa Hatushi 8:3 1Nya 3:22; Ezr 2:3wa wazao wa Shekania;

wa wazao wa Paroshi, alikuwa Zekaria, na watu 150 walioandikishwa pamoja naye;

8:4 Ezr 2:6wa wazao wa Pahath-Moabu, alikuwa Eliehoenai mwana wa Zerahia na wanaume 200 pamoja naye;

wa wazao wa Zatu, alikuwa Shekania mwana wa Yahazieli na wanaume 300 pamoja naye;

8:6 Ezr 2:15; Neh 7:20wa wazao wa Adini, alikuwa Ebedi mwana wa Yonathani na wanaume 50 pamoja naye;

wa wazao wa Elamu, alikuwa Yeshaya mwana wa Athalia, na wanaume 70 pamoja naye;

wa wazao wa Shefatia, alikuwa Zebadia mwana wa Mikaeli na wanaume 80 pamoja naye;

wa wazao wa Yoabu, alikuwa Obadia mwana wa Yehieli na wanaume 218 pamoja naye;

wa wazao wa Bani, alikuwa Shelomithi mwana wa Yosifia na wanaume 160 pamoja naye;

wa wazao wa Bebai, alikuwa Zekaria mwana wa Bebai na wanaume 28 pamoja naye;

wa wazao wa Azgadi, alikuwa Yohanani mwana wa Hakatani na wanaume 110 pamoja naye;

8:13 Ezr 2:13wa wazao wa Adonikamu, hawa walikuwa wa mwisho ambao majina yao ni Elifeleti, Yeueli, Shemaya na wanaume 60 pamoja nao;

wa wazao wa Bigwai, walikuwa Uthai na Zakuri na wanaume 70 pamoja nao.

Read More of Ezra 8