Ezekieli 7:1-27, Ezekieli 8:1-18, Ezekieli 9:1-11 NEN

Ezekieli 7:1-27

Mwisho Umewadia

Neno la Bwana likanijia kusema: 7:2 Amo 8:2-10; Ufu 20:8; Mao 4:18“Mwanadamu, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kwa nchi ya Israeli: Mwisho! Mwisho umekuja juu ya pembe nne za nchi. 7:3 Eze 18:30; Mwa 6:13Sasa mwisho umekuja juu yenu nami nitamwaga hasira yangu dhidi yenu. Nitawahukumu sawasawa na matendo yenu na kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za kuchukiza. 7:4 Yer 13:14; Eze 5:11; 23:49Sitawaonea huruma wala sitawarehemu, hakika nitalipiza kwa ajili ya matendo yenu na desturi zenu za machukizo miongoni mwenu. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.

7:5 2Fal 21:12“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Maafa! Maafa ambayo hayajasikiwa yanakuja. 7:6 Eze 39:8Mwisho umewadia! Mwisho umewadia! Umejiinua wenyewe dhidi yenu. Umewadia! 7:7 Sef 1:14; Mal 3:2; 1Pet 4:17; Ay 18:20; Isa 2:12; Amo 5:18-20; Eze 12:23Maangamizi yamekuja juu yenu, ninyi mnaoishi katika nchi. Wakati umewadia, siku imekaribia, kuna hofu kuu ya ghafula, wala si furaha, juu ya milima. 7:8 Hos 5:10; Nah 1:6; Eze 36:19; 14:19; 20:8, 21; 9:8; Isa 42:25Ninakaribia kumwaga ghadhabu yangu juu yenu na kumaliza hasira yangu dhidi yenu, nitawahukumu sawasawa na matendo yenu na kuwalipiza kwa ajili ya desturi zenu zote za machukizo. 7:9 Yer 21:9; Isa 9:13; Eze 5:11; 22:31; Za 39:10Sitawaonea huruma wala sitawarehemu; nitawalipiza sawasawa na matendo yenu na desturi zenu za machukizo miongoni mwenu. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana ambaye huwapiga kwa mapigo.

7:10 Za 89:32; Isa 10:5“Siku imefika! Imewadia! Maangamizi yamezuka ghafula, fimbo imechanua majivuno yamechipua! 7:11 Yer 16:6; Sef 1:18; Isa 58:4; Za 55:9Jeuri imeinuka kuwa fimbo ya kuadhibu uovu, hakuna hata mmoja wa hao watu atakayeachwa, hata mmoja wa kundi lile, hakuna utajiri, hakuna chenye thamani. 7:12 Isa 5:13-14; Eze 30:3; Isa 24:2Wakati umewadia, siku imefika. Mnunuzi na asifurahi wala muuzaji asihuzunike, kwa maana ghadhabu iko juu ya kundi lote. 7:13 Law 25:24-25Muuzaji hatajipatia tena ardhi aliyoiuza wakati wote wawili wangali hai, kwa kuwa maono kuhusu kundi lote hayatatanguka. Kwa sababu ya dhambi zao, hakuna hata mmoja atakayeokoa maisha yake. 7:14 Ay 39:24; Yer 25:38Wajapopiga tarumbeta na kuweka kila kitu tayari, hakuna hata mmoja atakayekwenda vitani, kwa maana ghadhabu yangu iko juu ya kundi lote.

7:15 Kum 32:25; Yer 14:18; Mao 1:20; Eze 5:12; 33:27“Nje ni upanga, ndani ni tauni na njaa, wale walioko shambani watakufa kwa upanga, nao wale waliomo mjini njaa na tauni vitawala. 7:16 Mwa 8:8; Isa 59:11; 10:20; Ezr 9:15; Yer 9:19; 41:16; 42:17Wale wote watakaopona na kutoroka watakuwa milimani, wakiomboleza kama hua wa mabondeni, kila mmoja kwa sababu ya dhambi zake. 7:17 2Fal 19:26; Isa 13:7; Dan 6:5; Yer 43:7; Eze 21:7; 22:14Kila mkono utalegea na kila goti litakuwa dhaifu kama maji. 7:18 Isa 15:2-3; Amo 8:10; Za 55:5; Yer 6:26; 4:8; 49:3; 48:37Watavaa nguo ya gunia na kufunikwa na hofu. Nyuso zao zitafunikwa na aibu na nywele za vichwa vyao zitanyolewa. 7:19 Isa 42:25; Sef 1:18; Hos 4:5; Eze 3:20; Mit 11:4; Yoe 1:15; Eze 13:5; 14:3Watatupa fedha yao barabarani, nayo dhahabu yao itakuwa najisi. Fedha yao na dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku hiyo ya ghadhabu ya Bwana. Hawatashibisha njaa yao au kujaza matumbo yao kwa hiyo fedha wala dhahabu, kwa sababu imewaponza wajikwae dhambini. 7:20 Eze 5:11; 16:17; Yer 7:30; 10:3; Isa 2:20Walijivunia vito vyao vizuri na kuvitumia kufanya sanamu za machukizo na vinyago vya upotovu. Kwa hiyo nitavifanya vitu hivyo kuwa najisi kwao. 7:21 2Fal 24:13; Hes 14:3Nitavitia vyote mikononi mwa wageni kuwa nyara na kuwa vitu vilivyotekwa mikononi mwa watu waovu wa dunia, nao watavinajisi. 7:22 Yer 2:27; 19:13; Eze 39:23-24; Za 74:7-8Nitageuza uso wangu mbali nao, nao waovu wa dunia watapanajisi mahali pangu pa thamani, wanyangʼanyi watapaingia na kupanajisi.

7:23 2Fal 21:16; Isa 1:15; Za 10:8; Eze 11:6; 22:9; Mwa 6:11“Andaa minyororo, kwa sababu nchi imejaa umwagaji wa damu na mji umejaa udhalimu. 7:24 Mao 2:7; Eze 24:21; 28:7; 2Nya 7:20Nitaleta taifa ovu kuliko yote ili kumiliki nyumba zao, nitakomesha kiburi cha wenye nguvu na mahali pao patakatifu patatiwa unajisi. 7:25 Yer 6:14; 8:11; Eze 13:10-16Hofu ya ghafula itakapokuja, watatafuta amani, lakini haitakuwepo. 7:26 Kum 29:21; 31:17; Yer 4:20; 18:18; Amo 8:11; Mik 3:6; Mal 2:7-9; Isa 47:11; 3:11; Eze 18:20; Za 109:19Maafa juu ya maafa yatakuja, tetesi ya mabaya juu ya tetesi ya mabaya. Watajitahidi kupata maono kutoka kwa nabii, mafundisho ya sheria toka kwa kuhani yatapotea, vivyo hivyo shauri kutoka kwa wazee. Mfalme ataomboleza, mwana wa mfalme atavikwa kukata tamaa, nayo mikono ya watu wa nchi itatetemeka. Nitawashughulikia sawasawa na matendo yao na kwa kanuni zao wenyewe nitawahukumu. Ndipo watajua kwamba Mimi ndimi Bwana.”

Read More of Ezekieli 7

Ezekieli 8:1-18

Ibada Ya Sanamu Hekaluni

8:1 2Fal 6:32; Eze 14:1; 33:31; 40:1; 24:1Katika siku ya tano ya mwezi wa sita mwaka wa sita, baada ya kupelekwa uhamishoni nilipokuwa nimeketi katika nyumba yangu na wazee wa Yuda walikuwa wameketi mbele yangu, mkono wa Bwana Mwenyezi ulikuja juu yangu. 8:2 Eze 1:4, 26-27; Dan 7:9Nikatazama, nikaona umbo mfano wa mwanadamu. Kutokana na kile kilichoonekana kuwa kiuno chake kuelekea chini alifanana na moto. Kuanzia kwenye kiuno kuelekea juu sura yake kama chuma kingʼaavyo kikiwa ndani ya moto. 8:3 Eze 3:12; 11:1; Kut 20:5; Kum 32:16; Yer 7:30; Kut 24:10; Eze 2:9Akanyoosha kitu kilichoonekana kama mkono, akaniinua kwa kushika nywele za kichwa changu. Roho akaniinua juu kati ya nchi na mbingu nikiwa katika maono ya Mungu akanichukua mpaka Yerusalemu, kwenye ingilio la lango la upande wa kaskazini ya ukumbi wa ndani, mahali iliposimama ile sanamu ichocheayo wivu. 8:4 Kut 24:16; Eze 1:28; 3:22Hapo mbele yangu palikuwa na utukufu wa Mungu wa Israeli, kama utukufu ule niliouona katika maono kule ua wa ndani.

8:5 Za 78:58-60; Yer 4:1; 32:34Kisha akaniambia, “Mwanadamu, tazama kuelekea kaskazini.” Hivyo nikatazama na kwenye ingilio upande wa kaskazini wa lango la madhabahu, nikaona sanamu hii ya wivu.

8:6 Eze 5:11; Kum 31:16; Hos 5:6Ndipo akaniambia, “Mwanadamu, je, unaona yale wanayofanya, haya mambo ya machukizo kabisa nyumba ya Israeli wanayotenda hapa, ambayo yatanifanya niende mbali na mahali pangu patakatifu? Lakini utaona vitu ambavyo vinachukiza zaidi hata kuliko hivi.”

Kisha akanileta mpaka ingilio la ukumbi. Nikatazama, nami nikaona tundu ukutani. Akaniambia, “Mwanadamu, sasa toboa kwenye ukuta huu.” Ndipo nikatoboa ule ukuta, nikaona hapo pana mlango.

Naye akaniambia, “Ingia ndani, ukaone maovu na machukizo wanayofanya humu.” 8:10 Kum 4:15-18; Yer 16:18; Amu 17:4-5; Eze 23:14; Yer 44:4; Kut 20:4Hivyo nikaingia ndani na kutazama, nikaona kuta zote zimechorwa kila aina ya vitu vitambaavyo na ya wanyama wachukizao wa kila aina na sanamu zote za nyumba ya Israeli. 8:11 Hes 16:17; Yer 26:24; Law 10:1; Hes 16:17-35; Kut 3:16; Eze 11:1-2Mbele yao walisimama wazee sabini wa nyumba ya Israeli, naye Yaazania mwana wa Shafani alikuwa amesimama miongoni mwao. Kila mmoja alikuwa na chetezo mkononi na moshi wa harufu nzuri ya uvumba ulikuwa unapanda juu.

8:12 2Fal 21:16; Za 10:11; Ay 22:13; Isa 29:15; Eze 9:9Akaniambia, “Mwanadamu, umeona wanayoyafanya wazee wa nyumba ya Israeli gizani, kila mmoja kwenye sehemu yake mwenyewe ya kufanyia ibada za sanamu yake? Wao husema, ‘Bwana hatuoni, Bwana ameiacha nchi.’ ” Akasema tena, “Bado utaona machukizo wanayofanya ambayo ni makubwa kuliko haya.”

8:14 Eze 11:12Ndipo akanileta mpaka ingilio la lango la kaskazini la nyumba ya Bwana, nami nikaona wanawake wameketi hapo, wakimwombolezea Tamuzi. Akaniambia, “Unaliona hili, mwanadamu? Utaona vitu ambavyo ni machukizo kuliko hili.”

8:16 Yoe 2:17; Kum 4:19; Ay 31:28; Mwa 1:16; Yer 2:27; Eze 40:6; 9:6Ndipo akanileta mpaka kwenye ukumbi wa ndani wa nyumba ya Bwana, nako huko katika ingilio la Hekalu, kati ya baraza na madhabahu, walikuwepo wanaume wapatao ishirini na watano. Wakiwa wamelipa kisogo Hekalu la Bwana na kuelekeza nyuso zao upande wa mashariki, wakilisujudia jua huko mashariki.

8:17 Mwa 6:11; Ezr 9:6; Hes 11:33; 1Fal 14:9; Eze 16:2; 16:26Akaniambia, “Je, umeona hili mwanadamu? Je, ni jambo dogo sana kwa nyumba ya Yuda kufanya machukizo wanayoyafanya hapa? Je, ni lazima pia waijaze nchi dhuluma na kuendelea siku zote kunikasirisha? Watazame wanavyonibania pua kana kwamba ninanuka! 8:18 Yer 13:14; 44:6; Eze 24:14; Isa 1:15; Mik 3:4; Mit 1:28; 1Sam 8:18; Isa 58:4; Eze 9:10Kwa hiyo nitashughulika nao kwa hasira, sitawaonea huruma wala kuwaachilia. Wajapopiga makelele masikioni mwangu, sitawasikiliza.”

Read More of Ezekieli 8

Ezekieli 9:1-11

Waabudu Sanamu Wauawa

Kisha nikamsikia akiita kwa sauti kubwa akisema, “Walete wasimamizi wa mji hapa, kila mmoja akiwa na silaha mkononi mwake.” 9:2 Dan 10:5; 12:6; Ufu 15:6; Eze 10:2; Law 16:4Nami nikaona watu sita wakija toka upande wa lango la juu, linalotazama kaskazini kila mmoja na silaha za kuangamiza mkononi mwake. Pamoja nao alikuwepo mtu aliyekuwa amevaa mavazi ya kitani safi, naye alikuwa na vifaa vya mwandishi akiwa amevishikilia upande mmoja. Wakaingia ndani ya Hekalu wakasimama pembeni mwa madhabahu ya shaba.

9:3 1Sam 4:21; Eze 10:4; 11:22Basi utukufu wa Mungu wa Israeli ukaondoka hapo juu ya makerubi, ulikokuwa umekaa, ukaenda kwenye kizingiti cha Hekalu. Ndipo Bwana akamwita yule mtu aliyevaa kitani safi aliyekuwa na vifaa vya mwandishi akiwa amevishikilia upande wake mmoja, 9:4 Mwa 4:15; 2Kor 1:22; Yer 7:29; Amo 6:6; Za 119:53; Kut 12:7; Yer 25:29akamwambia, “Pita katika mji wote wa Yerusalemu ukaweke alama juu ya vipaji vya nyuso za wale watu wanaohuzunika na kuomboleza kwa sababu ya machukizo yote yanayotendeka katika mji huu.”

9:5 Yer 13:14; Eze 5:11; Kut 32:27; Isa 13:18Nikiwa ninasikia, akawaambia wale wengine, “Mfuateni anapopita katika mji wote mkiua, pasipo huruma wala masikitiko. 9:6 Eze 8:11-16; Yer 25:29; 1Pet 4:17; Yer 7:32; Mwa 4:15; Kut 12:7Waueni wazee, vijana wa kiume na wa kike, wanawake na watoto, lakini msimguse mtu yeyote mwenye alama. Anzieni katika mahali pangu patakatifu.” Kwa hiyo wakaanza na wale wazee waliokuwa mbele ya Hekalu.

9:7 Eze 6:7Ndipo akawaambia, “Linajisini Hekalu na mkazijaze kumbi zake maiti za wale waliouawa. Nendeni!” Kwa hiyo wakaenda wakaanza kuua watu mjini kote. 9:8 Yos 7:6; Hes 14:5; Amo 7:1-6; Eze 11:3; 7:8Wakati walikuwa wakiwaua watu, nami nilikuwa nimeachwa peke yangu, nikaanguka kifudifudi, nikapiga kelele nikisema, “Ee Bwana Mwenyezi! Je, utaangamiza mabaki yote ya Israeli, katika kumwagwa huku kwa ghadhabu yako juu ya Yerusalemu?”

9:9 Za 58:2; Hab 1:4; Ay 22:13; Eze 14:23; Isa 29:15; Eze 22:13Bwana akanijibu, “Dhambi ya nyumba ya Israeli na Yuda imekuwa kubwa mno kupita kiasi, nchi imejaa umwagaji damu na mjini kumejaa udhalimu. Kwani wamesema, ‘Bwana ameiacha nchi, Bwana hauoni.’ 9:10 Yer 13:14; Eze 22:29; Isa 22:5; Eze 23:49; 8:18; Isa 22:5Kwa hiyo sitawahurumia wala kuwaachilia lakini nitaleta juu ya vichwa vyao, yale waliyoyatenda.”

Ndipo mtu yule aliyekuwa amevaa nguo ya kitani safi na vifaa vya mwandishi akiwa amevishikilia upande wake mmoja, akarudi na kutoa taarifa akisema, “Nimefanya kama ulivyoniagiza.”

Read More of Ezekieli 9