Ezekieli 47:1-23, Ezekieli 48:1-35 NEN

Ezekieli 47:1-23

Mto Kutoka Hekaluni

47:1 Za 46:4; Ufu 22:1; Yoe 3:18; Isa 55:1Yule mtu akanirudisha mpaka kwenye ingilio la Hekalu, nami nikaona maji yakitoka chini ya kizingiti cha Hekalu yakitiririkia upande wa mashariki (kwa maana upande wa mbele wa Hekalu ulielekea mashariki). Maji yalikuwa yakitoka chini upande wa kusini wa Hekalu, kusini mwa madhabahu. 47:2 Eze 40:35Ndipo akanitoa nje kupitia lango la kaskazini na kunizungusha mpaka kwenye lango la nje linaloelekea mashariki, nayo maji yalikuwa yakitiririka kutoka upande wa kusini.

47:3 Eze 40:3; Ufu 11:1Mtu yule alipokwenda upande wa mashariki akiwa na kamba ya kupimia mkononi mwake, akapima dhiraa 1,00047:3 Dhiraa 1,000 ni sawa na mita 450. kisha akanipitisha kwenye hayo maji ambayo yalifika kwenye vifundo vya miguu. Akapima dhiraa 1,000 nyingine na kunipitisha kwenye hayo maji ambayo yalifika magotini. Akapima dhiraa nyingine 1,000 na kunipitisha kwenye hayo maji ambayo yalifika kiunoni. 47:5 Isa 11:9; Hab 2:14; Mwa 2:10Akapima tena dhiraa 1,000 nyingine, lakini wakati huu yalikuwa mto ambao sikuweza kuvuka, kwa kuwa maji yalikuwa na kina kirefu ambacho ni cha kuogelea, mto ambao hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kuvuka. 47:6 Ufu 22:2; Isa 41:19Akaniuliza, “Je, mwanadamu, unaona hili?”

Kisha akanirudisha mpaka kwenye ukingo wa huo mto. 47:7 Eze 47:12; Ufu 22:2; Za 1:3; 92:12Nilipofika pale, nikaona idadi kubwa ya miti kila upande wa ule mto.

47:8 Ufu 17:15; Yos 3:16; Isa 41:18; Kum 3:17Akaniambia, “Haya maji yanatiririka kuelekea nchi ya mashariki na kushuka mpaka Araba,47:8 Araba hapa ina maana ya Bonde la Yordani. ambapo huingia Baharini. Yanapomwagikia kwenye hiyo Bahari,47:8 Bahari hapa ina maana ya Bahari ya Chumvi. maji yaliyoko humo huponywa na kuwa safi. 47:9 Isa 12:3; Yn 4:14; 1Kor 15:45; Yn 7:37-38Popote mto huu uendapo kila kiumbe hai kinachoyaparamia hayo maji kitaishi, nako kutakuwa na samaki wengi mno, mara maji haya yafikapo huko. Maji hayo yatakuwa hai na kila kitu kitakachoishi kule mto uendako. 47:10 Isa 19:8; Mt 4:19; Yos 15:62; Eze 26:5; Mt 13:47; Hes 34:6Wavuvi watasimama kando ya bahari, kuanzia En-Gedi hadi En-Eglaimu huko patakuwa mahali pa kutandaza nyavu za kuvulia samaki. Samaki watakuwa wa aina nyingi, kama samaki wa Bahari Kuu47:10 Bahari Kuu hapa ina maana ya Bahari ya Mediterania. 47:11 Kum 29:23Lakini madimbwi yake na mabwawa yake hayatakuwa na maji yanayofaa kunywa, bali yatabakia kuwa maji ya chumvi. 47:12 Mwa 2:9; Ufu 22:2; Yer 17:8; Ay 18:6; Eze 36:8Miti ya matunda ya kila aina itaota kwenye kingo zote mbili za mto huu. Majani yake hayatanyauka wala haitaacha kuwa na matunda katika matawi yake. Kila mwezi kutakuwa na matunda, kwa sababu maji yatokayo patakatifu yanaitiririkia. Matunda yake yatakuwa chakula na majani yake yatakuwa dawa.”

Mipaka Mipya Ya Nchi

47:13 Hes 34:2-12; Yer 3:18; Mwa 48:5-16; 49:26Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “Hii ndiyo mipaka ambayo kwayo mtagawanya hiyo nchi kuwa urithi miongoni mwa hayo makabila kumi na mawili ya Israeli, pamoja na mafungu mawili ya Yosefu. 47:14 Kum 1:8; Mwa 12:7; Eze 36:12Mtagawa kwa usawa miongoni mwao. Kwa sababu niliapa kwa mkono ulioinuliwa kuwapa baba zenu, nchi hii itakuwa urithi wenu.

47:15 Eze 48:1; Hes 34:2-8“Huu ndio utakuwa mpaka wa hiyo nchi:

“Upande wa kaskazini utaanzia Bahari Kuu kwa njia ya Hethloni kupitia Lebo-Hamathi hadi maingilio ya Sedadi. 47:16 2Sam 8:8; Hes 13:21; Yer 49:23; Amo 6:2Berotha na Sibraimu (ambao uko kwenye mpaka kati ya Dameski na Hamathi), hadi kufikia Haser-Hatikoni, ambao uko katika mpaka wa Haurani. 47:17 Hes 34:9; Eze 48:1Hivyo mpaka utaendelea kuanzia Baharini hadi Hasar-Enoni, ukiambaa na mpaka wa kaskazini wa Dameski, pamoja na mpaka wa Hamathi upande wa kaskazini. Huu utakuwa ndio mpaka wa kaskazini.

47:18 Eze 27:18Upande wa mashariki mpaka utapita kati ya Haurani na Dameski, kuambaa Yordani na kati ya Gileadi na nchi ya Israeli, hadi bahari ya mashariki47:18 Bahari ya mashariki hapa ina maana ya Bahari ya Chumvi. na kufika Tamari. Huu utakuwa ndio mpaka wa mashariki.

47:19 Mwa 15:18; Kum 32:51; Isa 27:12; Eze 48:28Upande wa kusini utaanzia Tamari hadi kufikia maji ya Meriba-Kadeshi, kisha utaambaa na Kijito cha Misri hadi Bahari Kuu. Huu utakuwa ndio mpaka wa kusini.

47:20 Hes 13:21; 34:6; Eze 48:1Upande wa magharibi, Bahari Kuu itakuwa ndio mpaka hadi kwenye sehemu mkabala na Lebo-Hamathi. Huu utakuwa ndio mpaka wa magharibi.

47:21 Kum 24:19; Efe 2:19-22; Rum 10:12; Law 24:22; Mal 3:5; Efe 3:6; Isa 56:6-7“Mtagawanya nchi hii miongoni mwenu kufuatana na makabila ya Israeli. 47:22 Mdo 2:5; Efe 2:19-22; Rum 10:12; Efe 3:6; Ufu 7:9-10; Gal 3:28; Kol 3:11Mtaigawanya kuwa urithi kwa ajili yenu na kwa ajili ya wageni wanaoishi miongoni mwenu na ambao wana watoto. Wao watakuwa kwenu kama wenyeji wazawa wa Israeli, pamoja na ninyi watagawiwa urithi miongoni mwa makabila ya Israeli. 47:23 Kum 10:19Katika kabila lolote mgeni atakapoishi hapo ndipo mtakapompatia urithi wake,” asema Bwana Mwenyezi.

Read More of Ezekieli 47

Ezekieli 48:1-35

Mgawanyo Wa Nchi

48:1 Mwa 30:6; Hes 34:7-9; Eze 47:15-20“Haya ndiyo majina ya makabila na sehemu zao: Kwenye mpaka wa kaskazini, Dani atakuwa na sehemu moja, mpaka huo utafuata barabara ya Hethloni hadi Lebo-Hamathi, Hasar-Enani hata mpaka wa kaskazini wa Dameski karibu na Hamathi utakuwa sehemu ya huo mpaka wake kuanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi.

48:2 Yos 19:24-31“Asheri atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Dani kuanzia mashariki hadi upande wa magharibi.

48:3 Yos 19:32-39“Naftali atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Asheri kuanzia mashariki hadi magharibi.

48:4 Yos 17:1-11“Manase atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Naftali kuanzia mashariki hadi magharibi.

48:5 Yos 16:5-9; 17:7-10, 17“Efraimu atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Manase kuanzia mashariki hadi magharibi.

48:6 Yos 13:15-21“Reubeni atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Efraimu kuanzia mashariki hadi magharibi.

48:7 Yos 15:1-63“Yuda atakuwa na sehemu moja, itapakana na nchi ya Reubeni kuanzia mashariki hadi magharibi.

48:8 Eze 45:1; 48:21“Kupakana na nchi ya Yuda kuanzia mashariki mpaka magharibi itakuwa ndiyo sehemu utakayoitoa ili kuwa toleo maalum. Itakuwa na upana wa dhiraa 25,00048:8 Dhiraa 25,000 ni sawa na kilomita 11.25. na urefu wake kuanzia mashariki mpaka magharibi utakuwa ule ule wa sehemu moja ya kabila, mahali patakatifu patakuwa katikati ya eneo hilo.

48:9 Eze 45:1“Hiyo sehemu maalum mtakayotoa kwa Bwana itakuwa na urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,00048:9 Dhiraa 10,000 ni sawa na kilomita 4.5. 48:10 Eze 45:1-4Hii itakuwa ni sehemu takatifu kwa ajili ya makuhani. Itakuwa na urefu wa dhiraa 25,000 upande wa kaskazini, upana wa dhiraa 10,000 upande wa magharibi, dhiraa 10,000 upande wa mashariki na urefu wa dhiraa 25,000 upande wa kusini. Katikati yake patakuwa mahali patakatifu pa Bwana. 48:11 2Sam 8:17; Law 8:35; Eze 14:11; 44:15; Yer 23:11; Neh 9:34Hii itakuwa kwa ajili ya makuhani waliowekwa wakfu, Wasadoki, waliokuwa waaminifu katika kunitumikia nao hawakupotoka kama Walawi walivyofanya wakati Waisraeli walipopotoka. Itakuwa toleo maalum kwao kutoka sehemu takatifu ya nchi, yaani, sehemu takatifu sana, inayopakana na nchi ya Walawi.

48:13 Eze 45:5“Kando ya nchi ya makuhani, Walawi watakuwa na mgawo wa urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000. Urefu wake utakuwa jumla dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000. 48:14 Law 25:34; 27:10, 28Hawataruhusiwa kuuza wala kuibadilisha hata mojawapo. Hii ndiyo sehemu nzuri ya nchi kuliko nyingine zote, hivyo haitakuwa mikononi mwa watu wengine, kwa sababu ni takatifu kwa Bwana.

48:15 Kum 20:5; Eze 42:20; 44:23; 45:6“Eneo linalobaki lenye upana wa dhiraa 5,00048:15 Dhiraa 5,000 ni sawa na kilomita 2.25. na urefu wa dhiraa 25,000, litakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya mji, kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na malisho. Mji utakuwa katikati yake 48:16 Ufu 21:16nao utakuwa na vipimo hivi: upande wa kaskazini dhiraa 4,500,48:16 Dhiraa 4,500 ni sawa na kilomita 2.025. upande wa kusini dhiraa 4,500, upande wa mashariki dhiraa 4,500 na upande wa magharibi dhiraa 4,500. Sehemu ya malisho kwa ajili ya mji itakuwa na eneo la dhiraa 25048:17 Dhiraa 250 ni sawa na sentimita 112.5. upande wa kaskazini, dhiraa 250 upande wa kusini, dhiraa 250 upande wa mashariki na dhiraa 250 upande wa magharibi. 48:18 Eze 21:16Eneo linalobaki, linalopakana na sehemu takatifu likiwa na urefu sawa nalo, litakuwa dhiraa 10,000 upande wa mashariki na dhiraa 10,000 upande wa magharibi. Mazao yake yatawapa watumishi wa mji chakula. 48:19 Eze 45:6; Ufu 7:5Watumishi wa mji wanaolima shamba hili watatoka katika makabila yote ya Israeli. 48:20 Hes 24:5; Isa 33:20; Ufu 21:16Eneo lote la hiyo sehemu litakuwa mraba, yaani, dhiraa 25,000 kila upande. Kama toleo maalum mtatenga sehemu takatifu, pamoja na milki ya mji.

48:21 Eze 45:7; Yos 18:1; Yn 12:32; Rum 15:9-12“Eneo linalobaki pande zote za eneo linalofanya sehemu takatifu na milki ya mji litakuwa mali ya mkuu atawalaye. Eneo hili litaenea upande wa mashariki kuanzia kwenye dhiraa 25,000 za sehemu takatifu hadi mpaka wa mashariki na kuelekea upande wa magharibi kuanzia kwenye dhiraa 25,000 hadi mpaka wa magharibi. Maeneo yote haya mawili yanayoenda sambamba na urefu wa sehemu za makabila yatakuwa ya mkuu anayetawala, na sehemu ile takatifu pamoja na mahali patakatifu pa Hekalu itakuwa katikati yake. Kwa hiyo milki ya Walawi na milki ya mji vitakuwa katikati ya eneo lile ambalo ni mali ya mkuu anayetawala. Eneo la mkuu anayetawala litakuwa kati ya mpaka wa Yuda na mpaka wa Benyamini.

48:23 Yos 18:11-28“Kuhusu makabila yaliyobaki: Benyamini atakuwa na sehemu moja, itakayoanzia upande wa mashariki hadi upande wa magharibi.

48:24 Mwa 29:33; Yos 19:1-9“Simeoni atakuwa na sehemu moja, itakayopakana na nchi ya Benyamini kuanzia mashariki hadi magharibi.

48:25 Yos 19:17-23“Isakari atakuwa na sehemu moja, itakayopakana na nchi ya Simeoni kuanzia mashariki hadi magharibi.

48:26 Yos 13:24-28“Zabuloni atakuwa na sehemu moja, itakayopakana na nchi ya Isakari kuanzia mashariki hadi magharibi.

48:27 Yos 13:24-28“Gadi atakuwa na sehemu moja, itakayopakana na nchi ya Zabuloni kuanzia mashariki hadi magharibi.

48:28 Mwa 14:7; Hes 34:6, 15; Mwa 15:18; Isa 27:12; Eze 47:19“Mpaka wa kusini wa Gadi utapita kusini kuanzia Tamari hadi maji ya Meriba-Kadeshi, kisha kupitia upande wa Kijito cha Misri hadi Bahari Kuu.48:28 Bahari Kuu hapa ina maana ya Bahari ya Mediterania.

48:29 Eze 47:14, 21, 22; 45:1“Hii ndiyo nchi mtakayogawanya kuwa urithi kwa makabila ya Israeli, nazo zitakuwa sehemu zao,” asema Bwana Mwenyezi.

Malango Ya Mji

“Haya yatakuwa ndiyo malango ya mji ya kutokea: Kuanzia upande wa kaskazini, ambayo urefu wake ni dhiraa 4,500, utakuwa na malango matatu, 48:31 Ufu 21:12; Isa 60:18malango hayo ya mji yatapewa majina ya makabila ya Israeli. Malango hayo matatu ya upande wa kaskazini moja litakuwa lango la Reubeni, lango la Yuda na lango la Lawi.

“Upande wa mashariki, wenye urefu wa dhiraa 4,500, utakuwa na malango matatu: lango la Yosefu, lango la Benyamini na lango la Dani.

“Upande wa kusini, wenye urefu wa dhiraa 4,500, utakuwa na malango matatu: lango la Simeoni, lango la Isakari na lango la Zabuloni.

48:34 2Nya 4:4; Ufu 21:12-13“Upande wa magharibi, wenye urefu wa dhiraa 4,500, utakuwa na malango matatu: lango la Gadi, lango la Asheri na lango la Naftali.

48:35 Za 72:8; Ufu 21:3; Zek 2:10; Amu 6:24; Isa 12:6; 24:23; Yer 31:17“Urefu wote kuzunguka utakuwa dhiraa 18,000.48:35 Dhiraa 18,000 ni sawa na kilomita 8.1.

“Nalo jina la mji huo kuanzia wakati huo na kuendelea litakuwa:

Bwana yupo hapa.”

Read More of Ezekieli 48