Ezekieli 43:1-27, Ezekieli 44:1-31 NEN

Ezekieli 43:1-27

Utukufu Warudi Hekaluni

43:1 Eze 10:19; 1Nya 9:18; Eze 8:16; 42:15Kisha yule mtu akanileta kwenye lango linaloelekea upande wa mashariki, 43:2 Za 18:4; Ufu 1:15; 21:11; Isa 6:3nami nikaona utukufu wa Mungu wa Israeli ukija kutoka upande wa mashariki. Sauti yake ilikuwa kama ya ngurumo ya maji yaendayo kasi, nayo nchi ikangʼaa kwa utukufu wake. 43:3 Eze 1:4; 3:21; Yer 1:10Maono niliyoyaona yalikuwa kama maono yale niliyokuwa nimeyaona wakati Mungu alipokuja kuangamiza mji na kama maono niliyokuwa nimeyaona kando ya Mto wa Kebari, nami nikaanguka kifudifudi. 43:4 Eze 1:28; 10:19; 44:2Utukufu wa Bwana ukaingia hekaluni kwa kupitia lango linaloelekea upande wa mashariki. 43:5 Eze 3:12; 11:24; Kut 16:7; Isa 6:4Kisha Roho akanichukua na kunileta katika ule ua wa ndani, nao utukufu wa Bwana ulilijaza Hekalu.

43:6 Eze 40:3Wakati yule mtu akiwa amesimama kando yangu, nilisikia mtu mmoja akisema nami kutoka ndani ya Hekalu. 43:7 Eze 20:29-39; Law 26:30; Kut 25:8; Yer 16:18; 16:18; 3:17; Eze 37:23Akasema, “Mwanadamu, hapa ni mahali pa kiti changu cha enzi na mahali pa kuweka nyayo za miguu yangu. Hapa ndipo nitakapoishi miongoni mwa Waisraeli milele. Kamwe nyumba ya Israeli hawatalinajisi tena Jina langu takatifu, yaani, wao wala wafalme wao, kwa ukahaba wao na kwa sanamu zao zisizokuwa na uhai za wafalme wao katika mahali pao pa juu pa kuabudia miungu. 43:8 2Fal 16:14Walipoweka kizingiti chao karibu na kizingiti changu na miimo yao ya milango karibu na miimo yangu, pakiwa na ukuta tu kati yangu na wao, walilinajisi Jina langu takatifu kwa matendo yao ya machukizo. Kwa sababu hiyo niliwaangamiza kwa hasira yangu. 43:9 Eze 37:26-28Basi sasa na waweke mbali nami ukahaba wao na sanamu za wafalme wao zisizo na uhai, nami nitakaa miongoni mwao milele.

43:10 Eze 16:61; 40:4“Mwanadamu, elezea hilo Hekalu kwa watu wa Israeli, ili wapate kuona aibu kwa ajili ya dhambi zao. Wao na wapime hicho kielelezo. 43:11 Eze 44:5-6; Mt 28:20Wakishaona aibu kwa ajili ya yale yote waliyotenda, wafahamishe kielelezo cha hilo Hekalu, yaani mpangilio wake, maingilio yake ya kutoka na kuingia, kielelezo chake chote, na masharti yake yote na sheria zake zote. Yaandike haya mbele yao ili wapate kuwa waaminifu kwa hicho kielelezo chake na kufuata masharti yake yote.

43:12 Eze 40:2; 42:20; Ufu 21:27; Eze 17:22“Hii ndiyo sheria ya Hekalu: Eneo lote linalozunguka Hekalu juu ya mlima litakuwa takatifu kuliko yote. Hii ndiyo sheria ya Hekalu.

Madhabahu

43:13 Kut 20:24; 2Nya 4:1“Hivi ndivyo vipimo vya madhabahu kwa dhiraa ndefu, yaani, dhiraa moja na nyanda nne:43:13 Dhiraa 1 na nyanda 4 ni sawa na sentimita 53. Tako lake liwe na kina cha hiyo dhiraa moja na upana wa hiyo dhiraa moja, ikiwa na ukingo wa shibiri moja43:13 Shibiri 1 ni sawa na sentimita 22.5. kuizunguka pembeni. Hiki kitakuwa ndicho kimo cha madhabahu: Kimo cha msingi kuanzia usawa wa ardhi mpaka kwenye mfereji sehemu ya chini kimo chake ni dhiraa mbili na upana wake ni dhiraa moja na kuanzia kwenye ukingo mdogo hadi kwenye ukingo mpana kimo chake ni dhiraa nne na upana wake ni dhiraa moja. 43:15 Kut 27:2; Isa 29:2Pale pawashwapo moto madhabahuni kimo chake kitakuwa dhiraa nne, na pembe nne zinazoelekeza juu kutoka pale pawashwapo moto. 43:16 Ufu 21:16Pale pawashwapo moto pa madhabahu ni mraba, urefu wake ni dhiraa kumi na mbili43:16 Dhiraa 12 ni sawa na mita 5.4. na upana wa dhiraa kumi na mbili. 43:17 Kut 20:26; Eze 45:19; Kut 27:1Pia sehemu ya juu ni mraba, urefu wake dhiraa kumi na nne na upana wa dhiraa kumi na nne, ikiwa na ukingo wa nusu dhiraa na mfereji kuizunguka madhabahu. Ngazi za kupandia madhabahuni zitaelekea upande wa mashariki.”

43:18 Kut 40:29; Ebr 9:21-22Kisha akaniambia, “Mwanadamu, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Haya ndiyo yatakayokuwa masharti ya kutoa dhabihu za kuteketezwa na kunyunyiza damu juu ya madhabahu itakapokuwa imejengwa. 43:19 Law 4:3; Eze 45:18-19; 2Nya 8:17; Ezr 7:2; Hes 16:40; Eze 40:46Utatoa fahali mchanga kuwa sadaka ya dhambi kwa makuhani, ambao ni Walawi, wa jamaa ya Sadoki, ndio watakaonikaribia kuhudumu mbele zangu, asema Bwana Mwenyezi. 43:20 Law 16:19; 4:7Itakupasa kuchukua baadhi ya hiyo damu ya mnyama huyo na kuiweka juu ya hizo pembe nne za madhabahu na juu ya ncha zake nne za sehemu ya juu kuzunguka ukingo wote, ili kuitakasa madhabahu na kufanya upatanisho kwa ajili yake. 43:21 Kut 29:14; Ebr 13:11Itakupasa kumchukua huyo fahali mchanga kwa ajili ya sadaka ya dhambi na kumteketeza mahali palipoagizwa katika eneo la Hekalu nje ya mahali Patakatifu.

“Siku ya pili yake utamtoa beberu asiye na dosari kwa ajili ya sadaka ya dhambi, nayo madhabahu itatakaswa kama ilivyotakaswa kwa yule fahali. 43:23 Kut 29:1; Law 22:20Utakapokuwa umemaliza kazi ya kuitakasa, utamtoa fahali mchanga pamoja na kondoo dume toka kwenye kundi, wote wawe hawana dosari. 43:24 Mk 9:49-50Utawatoa mbele za Bwana, nao makuhani watanyunyizia chumvi juu yao na kuwatoa kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana.

“Kwa siku saba itakupasa kutoa beberu kila siku kwa ajili ya sadaka ya dhambi, pia itakupasa kutoa fahali mchanga na kondoo dume kutoka zizini, wote wawe hawana dosari. Kwa siku saba itawapasa kufanya upatanisho kwa ajili ya madhabahu na kuitakasa na hivyo ndivyo watakavyoiweka wakfu. 43:27 Kut 32:6; Law 17:5; Ay 42:8; Isa 60:7Mwishoni mwa hizi siku saba, kuanzia siku ya nane na kuendelea, itawapasa makuhani kutoa sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka za amani juu ya madhabahu. Kisha nitawakubali ninyi, asema Bwana Mwenyezi.”

Read More of Ezekieli 43

Ezekieli 44:1-31

Mkuu, Walawi, Makuhani

44:1 Eze 43:1Ndipo yule mtu akanirudisha mpaka kwenye lango la nje la mahali Patakatifu, lile linaloelekea upande wa mashariki, nalo lilikuwa limefungwa. 44:2 Eze 43:4-5Bwana akaniambia, “Lango hili litabaki limefungwa. Haliruhusiwi kufunguliwa, wala hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuingilia kwenye lango hili. Litabaki limefungwa kwa sababu Bwana, Mungu wa Israeli, ameingia kwa kupitia lango hili. 44:3 Zek 6:12; Kut 24:9-11; Eze 46:2-8Yeye aliye mkuu peke yake ndiye anayeweza kukaa penye njia ya hilo lango na kula chakula mbele za Bwana. Itampasa aingie kwa njia hiyo ya lango la ukumbini na kutokea njia iyo hiyo.”

44:4 Isa 6:4; Ufu 15:8; Eze 1:28; Dan 8:17; Eze 40:35; 10:4Kisha yule mtu akanileta kwa njia ya lango la kaskazini mpaka mbele ya Hekalu. Nikatazama nami nikauona utukufu wa Bwana ukilijaza Hekalu la Bwana, nami nikaanguka kifudifudi.

44:5 Eze 40:4; 43:10-11; 42:9Bwana akaniambia, “Mwanadamu, angalia kwa uangalifu, usikilize kwa bidii na uzingatie kila kitu ninachokuambia kuhusu masharti yote yanayohusu Hekalu la Bwana. Uwe mwangalifu kuhusu wale wanaoruhusiwa hekaluni na wale wasioruhusiwa kuingia mahali patakatifu. 44:6 Eze 3:19Iambie nyumba ya kuasi ya Israeli, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Matendo yenu ya machukizo yatosha, ee nyumba ya Israeli! 44:7 Law 26:4; Mwa 17:14; Kut 12:48; Mdo 21:28; Law 22:25Zaidi ya matendo yenu yote ya machukizo, mmewaleta wageni wasiotahiriwa mioyo na miili katika patakatifu pangu, mkilinajisi Hekalu langu, huku mkinitolea chakula, mafuta ya wanyama na damu, nanyi mmevunja Agano langu. 44:8 Law 22:2; Hes 18:7; 2Tim 4:1Badala ya kutimiza wajibu wenu kuhusiana na vitu vyangu vitakatifu, mmeweka watu wengine kuwa viongozi katika patakatifu pangu. 44:9 Yoe 3:17; Zek 14:21Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Hakuna mgeni asiyetahiriwa moyo na mwilini anayeruhusiwa kuingia patakatifu pangu, wala hata wageni wanaoishi miongoni mwa Waisraeli.

44:10 Neh 9:34; 2Fal 23:8; Za 95:10; Hes 18:23“ ‘Walawi walioniacha wakati Waisraeli walipopotoka wakatoka kwangu na kutangatanga kwa kufuata sanamu zao, watachukua adhabu ya dhambi zao. 44:11 2Nya 29:34; Hes 16:9; 1Nya 26:12-19; Hes 3:5-37Wanaweza wakatumika katika mahali patakatifu pangu, wakiwa na uangalizi wa malango ya Hekalu, nao watachinja sadaka za kuteketezwa na dhabihu kwa ajili ya watu na kusimama mbele ya watu ili kuwahudumia. 44:12 2Fal 16:10-16; Yer 14:10; Za 106:26; Yer 18:15Lakini kwa sababu waliwatumikia watu mbele ya sanamu zao na kuifanya nyumba ya Israeli ianguke kwenye dhambi, kwa hiyo nimeapa kwa mkono ulioinuliwa kwamba ni lazima wachukue matokeo ya dhambi yao, asema Bwana Mwenyezi. 44:13 Eze 16:6; Hes 18:3; Hos 5:1Hawaruhusiwi kukaribia ili kunitumikia kama makuhani wala kukaribia chochote changu kilicho kitakatifu au sadaka iliyo takatifu kupita zote, bali watachukua aibu ya matendo yao ya kuchukiza. 44:14 1Sam 2:36; 2Fal 23:9; 1Nya 23:28-32Lakini nitawaweka katika uangalizi wa Hekalu na kazi zote zile zinazotakiwa kufanyika ndani yake.

44:15 Yer 33:18; Zek 3:7; Kum 10:8; 2Sam 8:17; Eze 7:2; Kum 29:13; Eze 40:46“ ‘Lakini makuhani, ambao ni Walawi na wazao wa Sadoki, ambao walitimiza wajibu wao kwa uaminifu katika patakatifu pangu wakati Waisraeli walipopotoka, watakaribia ili kutumika mbele zangu. Itawapasa wasimame mbele zangu ili kutoa dhabihu za mafuta ya wanyama na damu, asema Bwana Mwenyezi. 44:16 Eze 41:22; 1Sam 2:35; Mal 2:7; Law 3:16-17; Hes 8:15; Law 17:5-6Wao peke yao ndio wenye ruhusa ya kuingia mahali patakatifu pangu. Wao peke yao ndio watakaokaribia meza yangu ili kuhudumu mbele zangu na kufanya utumishi wangu.

44:17 Kut 39:27-28; Ufu 19:8“ ‘Watakapoingia kwenye malango ya ukumbi wa ndani, watavaa nguo za kitani safi, hawaruhusiwi kamwe kuvaa mavazi ya sufu wakati wanapokuwa wakihudumu kwenye malango ya ukumbi wa ndani wala ndani ya Hekalu. 44:18 Kut 28:39; Isa 3:20; Law 16:4; Kut 28:42Watavaa vilemba vya kitani safi vichwani mwao na nguo za ndani za kitani safi viunoni mwao. Hawatavaa chochote kitakachowafanya kutoa jasho. 44:19 Law 6:27; Eze 46:20; Kut 39:27-29; Law 6:10-11Watakapotoka ili kuingia katika ukumbi wa nje mahali watu walipo, watavua nguo walizokuwa wakihudumu nazo na wataziacha katika vyumba vitakatifu nao watavaa nguo nyingine, ili kwamba wasije wakaambukiza watu utakatifu kwa njia ya mavazi yao.

44:20 Law 21:5; Hes 6:5; Isa 28:7“ ‘Hawatanyoa nywele za vichwa vyao wala kuziacha ziwe ndefu, bali watazipunguza. 44:21 Law 10:9Kuhani yeyote asinywe mvinyo aingiapo katika ukumbi wa ndani. 44:22 Law 21:7Wasioe wanawake wajane wala walioachika, inawapasa kuoa wanawake bikira wenye heshima wa Israeli au wajane wa makuhani. 44:23 Eze 22:26; Hag 2:11-13; Mal 2:7; Mwa 7:2; Law 13:50; Yer 15:19Watawafundisha watu wangu tofauti kati ya vitu vitakatifu na vitu vya kawaida na kuwaonyesha jinsi ya kupambanua kati ya vitu najisi na vitu safi.

44:24 1Tim 4:5; 1Nya 23:4; 2Nya 19:8; Kum 17:8-9; 19:17“ ‘Katika magombano yoyote, makuhani watatumika kama mahakimu na kuamua hilo jambo kufuatana na sheria zangu. Watazishika sheria zangu na maagizo yangu katika sikukuu zangu zote zilizoamriwa, nao watatakasa Sabato zangu.

44:25 Law 21:1-4“ ‘Kuhani asijitie unajisi kwa kukaribia maiti, lakini, kama mtu aliyekufa alikuwa baba yake au mama yake, mwana au binti yake, ndugu yake au dada ambaye hajaolewa, basi aweza kujitia unajisi kwa hao. 44:26 Law 21:1-4; Hes 6:10Baada ya kujitakasa, atakaa hali hiyo kwa muda wa siku saba. 44:27 Hes 3:28; 6:11; Law 4:28Siku atakapoingia katika ukumbi wa ndani wa mahali patakatifu ili kuhudumu, atatoa sadaka ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe, asema Bwana Mwenyezi.

44:28 Kum 10:9; Yos 13:33; Hes 18:20; Kum 18:1-2“ ‘Mimi nitakuwa ndio urithi pekee walio nao makuhani katika Israeli. Msiwape wao milki, mimi nitakuwa milki yao. 44:29 Law 27:21; Hes 18:9, 14; Yos 13:14; Law 6:16Wao watakula sadaka za nafaka, sadaka za dhambi na sadaka za hatia na kila kitu kitakachotolewa kwa Bwana katika Israeli kitakuwa chao. 44:30 Hes 18:12-13; 2Nya 31:5; Hes 15:18-21; Neh 10:35-37; 2Nya 30:10Yote yaliyo bora ya malimbuko ya vitu vyote na matoleo yenu maalum vitakuwa vya makuhani. Inawapasa kuwapa malimbuko ya kwanza ya unga wenu ili kwamba baraka ipate kuwa katika nyumba zenu. 44:31 Kut 22:31; Law 22:8; 11:39-40Makuhani hawaruhusiwi kula chochote, ikiwa ni ndege au mnyama, aliyekutwa akiwa amekufa au aliyeraruliwa na wanyama pori.

Read More of Ezekieli 44