Ezekieli 33:21-33, Ezekieli 34:1-31, Ezekieli 35:1-15 NEN

Ezekieli 33:21-33

Anguko La Yerusalemu Laelezewa

33:21 Eze 24:26; 2Fal 25:4, 10; Yer 52:4-7; Eze 32:1Mwaka wa kumi na mbili wa uhamisho wetu, mwezi wa kumi, siku ya tano, mtu aliyekuwa ametoroka kutoka Yerusalemu akanijia na kusema, “Mji wa Yerusalemu umeanguka!” 33:22 Eze 3:26-27; 24:27; Lk 1:64; Eze 29:21Basi jioni kabla mtu huyo hajaja, mkono wa Bwana, ulikuwa juu yangu, naye alifungua kinywa changu kabla ya mtu yule aliyenijia asubuhi hajafika. Basi kinywa changu kilifunguliwa na sikuweza tena kunyamaza.

Ndipo neno la Bwana likanijia kusema: 33:24 Eze 36:4; Isa 51:2; Lk 3:8; Mik 3:11; Mdo 7:5; Yer 40:7; Eze 11:15“Mwanadamu, watu wanaoishi katika magofu hayo katika nchi ya Israeli wanasema hivi, ‘Abrahamu alikuwa mtu mmoja tu, hata hivyo akaimiliki nchi. Lakini sisi ni wengi, hakika tumepewa nchi kuwa milki yetu.’ 33:25 Mwa 9:4; Kum 12:16; Yer 7:9-10; Eze 22:6, 27; Yer 7:21Kwa hiyo waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa kuwa mnakula nyama pamoja na damu na kuinulia sanamu zenu macho na kumwaga damu, je, mtaimiliki nchi? 33:26 Yer 41:7; Eze 22:11Mnategemea panga zenu, mnafanya mambo ya machukizo na kila mmoja wenu humtia unajisi mke wa jirani yake. Je, mtaimiliki nchi?’

33:27 1Sam 13:6; Isa 2:19; Amu 6:2; Yer 42:22; Eze 7:15; 14:21“Waambie hivi: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Hakika kama niishivyo, wale waliobaki katika magofu wataanguka kwa upanga, wale walio nje mashambani nitawatoa wararuliwe na wanyama pori, nao wale walio katika ngome na kwenye mapango watakufa kwa tauni. 33:28 Isa 41:15; Mwa 6:7; Yer 9:10Nitaifanya nchi kuwa ukiwa na utupu na kiburi cha nguvu zake zitafikia mwisho, nayo milima ya Israeli itakuwa ukiwa ili mtu yeyote asipite huko. 33:29 Law 26:34; Yer 18:16; 44:22; Eze 36:4; Mik 7:13Kisha watajua kuwa Mimi ndimi Bwana, nitakapokuwa nimeifanya nchi kuwa ukiwa na utupu kwa sababu ya mambo yote ya machukizo waliyotenda.’

33:30 Isa 29:13“Kwa habari yako wewe, mwanadamu, watu wako wanaongea habari zako wakiwa karibu na kuta na kwenye milango ya nyumba, wakiambiana kila mmoja na mwenzake, ‘Njooni msikie ujumbe ule utokao kwa Bwana.’ 33:31 Eze 8:1; Isa 33:15; Mt 13:22; Za 119:36; 78:36-37; Isa 29:13; Yer 3:10Watu wangu wanakujia, kama wafanyavyo, nao wanaketi mbele yako kama watu wangu na kusikiliza maneno yako, lakini hawayatendi. Kwa maana udanganyifu u katika midomo yao, lakini mioyo yao ina tamaa ya faida isiyo halali. 33:32 Mk 6:20; Yak 1:22Naam, mbele yao umekuwa tu kama yeye aimbaye nyimbo za mapenzi kwa sauti nzuri za kuvutia na kupiga vyombo kwa ustadi, kwa kuwa wanasikia maneno yako lakini hawayatendi.

33:33 1Sam 3:20; Yer 28:9; Eze 2:5“Wakati mambo haya yote yatakapotimia, kwa kuwa hakika yatatokea, ndipo watakapojua kwamba nabii amekuwepo miongoni mwao.”

Read More of Ezekieli 33

Ezekieli 34:1-31

Wachungaji Na Kondoo

Neno la Bwana likanijia kusema: 34:2 Mik 3:11; Yud 12; Yer 3:15; Isa 40:11; Za 78:70-72; Yn 21:15-17“Mwanadamu, tabiri juu ya wachungaji wa Israeli, tabiri na uwaambie: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ole wa wachungaji wa Israeli ambao hujitunza wenyewe tu! Je, haiwapasi wachungaji kutunza kundi la kondoo? 34:3 Amo 6:4; Zek 11:5; Eze 22:27; Isa 56:11Mnakula mafuta ya wanyama, mnavaa mavazi ya sufu na kuchinja kondoo walionona, lakini hamlitunzi kundi. 34:4 Law 25:43; Mik 3:3; 2Tim 2:24; Mdo 9:36; Isa 3:7; Zek 11:15-17Hamkuwatia nguvu walio dhaifu wala hamkuwaganga wenye maradhi wala kuwafunga waliojeruhiwa. Hamkuwarudisha waliotangatanga wala kuwatafuta wale waliopotea. Badala yake mmewatawala kwa ukali na kwa ukatili. 34:5 Hes 27:17; Isa 56:9; Mdo 20:29Hivyo walitawanyika kwa sababu hapakuwepo mchungaji, nao walipotawanyika, wakawa chakula cha wanyama wa mwitu wote. 34:6 Yer 50:6; Law 26:33; Za 95:10; Yer 10:21; 2Nya 18:16; Za 142:4; Hos 7:13; Mt 9:36; 18:12-13Kondoo wangu walitawanyika, wakatangatanga kwenye milima yote na kwenye kila kilima kirefu. Kondoo wangu walitawanyika juu ya uso wa dunia yote bila kuwa na yeyote wa kuwaulizia wala wa kuwatafuta.

“ ‘Kwa hiyo, ninyi wachungaji, lisikieni neno la Bwana: 34:8 2Nya 18:16; 1Pet 2:25; Yer 50:6; Za 95:10; Yer 10:21; Hos 7:13; Za 42:4; Mt 18:12-13Kwa hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, kwa sababu kondoo zangu wamekosa mchungaji na hivyo wametekwa nyara na kuwa chakula cha wanyama wote wa mwituni na kwa sababu wachungaji wangu, hawakuwatafuta kondoo zangu, bali wachungaji wamejitunza wenyewe, nao hawakuwalisha kondoo zangu, 34:9 Amu 2:14; Isa 59:6; Yud 12kwa hiyo enyi wachungaji, sikieni neno la Bwana: 34:10 Yer 21:13; Za 72:14; Yer 23:2; Zek 10:3; 1Sam 2:29-30Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume na wachungaji nami nitawadai kondoo zangu mikononi mwao. Nitawafukuza kutoka kwenye kuchunga kundi langu, ili wachungaji wasiendelee kujitunza wenyewe. Nitaokoa kondoo zangu kutoka kwenye vinywa vyao, nao kondoo hawatakuwa tena chakula chao.

34:11 Za 119:176“ ‘Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi mwenyewe nitawaulizia kondoo wangu na kuwatafuta. 34:12 Zek 10:3; Lk 19:10; Eze 30:3; 32:7; Mdo 2:19-21; Isa 40:11Kama vile mchungaji atafutavyo kundi lake lililotawanyika wakati akiwa pamoja nalo, hivyo ndivyo nitakavyowatafuta kondoo wangu. Nitawaokoa kutoka mahali pote walipokuwa wametawanyikia katika siku ya mawingu na giza nene. 34:13 Mwa 48:21; Yer 23:3, 8; 50:19; Kum 30:4; Eze 11:17Nitawatoa katika mataifa na kuwakusanya kutoka nchi mbalimbali, nami nitawaleta katika nchi yao wenyewe. Nitawalisha kwenye milima ya Israeli, katika mabonde na mahali pote panapokalika katika nchi. 34:14 Eze 20:40; 37:22; Za 23:2; 37:3; Isa 65:10; Amo 9:14; Eze 36:29-30Nitawachunga kwenye malisho mazuri na miinuko ya mlima wa Israeli patakuwa mahali pao pa malisho. Huko watajipumzisha kwa amani katika nchi ya malisho mazuri, nao watajilisha huko katika malisho tele katika milima ya Israeli. 34:15 Sef 3:13; Mik 5:4; Za 23:1-2; Yer 33:12Mimi mwenyewe nitawachunga kondoo zangu na kuwafanya wapumzike, asema Bwana Mwenyezi. 34:16 Isa 61:1-2; Mik 4:6; Sef 3:19; Yer 31:8; Lk 5:32; Mt 2:17; 15:24Nitawaulizia kondoo waliopotea na kuwaleta waliotangatanga. Nitawafunga waliojeruhiwa na kuwatia nguvu walio dhaifu lakini wale waliojikinai na wenye nguvu nitawaangamiza. Nitalichunga kundi kwa haki.

34:17 Mt 25:32-33; Eze 20:37“ ‘Kwa habari yenu, enyi kundi langu, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitahukumu kati ya kondoo na kondoo, kati ya kondoo dume na mbuzi. 34:18 Mwa 30:15; Eze 32:2Je, haiwatoshi ninyi kujilisha kwenye malisho mazuri? Je, ni lazima ninyi kuyakanyaga pia malisho yenu yaliyobaki kwa miguu yenu? Je, haiwatoshi ninyi kunywa maji safi? Je, ni lazima kuyachafua maji mengine kwa miguu yenu? Je, ni lazima kundi langu wajilishe kwa yale mliyoyakanyaga na kunywa maji mliyoyachafua kwa miguu yenu?

34:20 Eze 34:17“ ‘Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenyezi awaambialo: Tazama, mimi mwenyewe nitahukumu kati ya kondoo wanono na waliokonda. 34:21 Kum 33:17Kwa sababu mmewapiga kikumbo na kuwapiga kwa pembe zenu kondoo wote walio dhaifu mpaka wakawafukuza, 34:22 Za 72:12-14; Yer 23:2-3; Eze 20:37-38nitaliokoa kundi langu na hawatatekwa nyara tena. Nitahukumu kati ya kondoo na kondoo. 34:23 Ebr 13:20; Isa 40:11; Eze 37:24; Isa 31:4; Mik 5:4Nitaweka juu yao mchungaji mmoja, mtumishi wangu Daudi, naye atawachunga, atawachunga na kuwa mchungaji wao. 34:24 Eze 36:28; Yer 33:14; 30:4; Yn 10:16; Kut 29:45; Za 89:49; Isa 53:4; Ufu 7:17Mimi Bwana nitakuwa Mungu wao, naye mtumishi wangu Daudi atakuwa mkuu miongoni mwao. Mimi Bwana nimenena.

34:25 Law 26:6; 25:18; Hos 2:18; Yer 23:6; Isa 11:6-9; Hes 25:12; Eze 16:62“ ‘Nitafanya nao Agano la amani na kuwaondoa wanyama wa mwitu kutoka nchi yao ili kondoo wangu waweze kupumzika nyikani na msituni kwa salama. 34:26 Mwa 12:2; Za 68:9; Yoe 2:23; Kum 28:12; 11:13-15Nitawabariki wao pamoja na maeneo yanayozunguka kilima changu. Nitawanyeshea mvua kwa majira yake, kutakuwepo mvua za baraka. 34:27 Yer 2:20; Law 26:13; Yer 30:8; Eze 20:42; Yer 25:14; Za 72:16; Ay 14:9Miti ya shambani itatoa matunda yake na ardhi itatoa mazao yake, watu watakaa salama katika nchi yao. Watajua kuwa Mimi ndimi Bwana, nitakapovunja vifungo vya nira zao na kuwaokoa kutoka mikono ya wale waliowafanya watumwa. 34:28 Hos 11:11; Zek 14:11; Amo 9:15; Yer 30:10; 32:37; Eze 28:26; 39:26Hawatatekwa tena nyara na mataifa, wala wanyama pori hawatawala tena. Wataishi kwa salama, wala hakuna yeyote atakayewatia hofu. 34:29 Isa 4:2; Yoe 2:19; Eze 36:15, 29; Za 137:3Nitawapa nchi yenye sifa kutokana na mazao yake, hawatapatwa na njaa katika nchi tena wala hawatadharauliwa na mataifa. 34:30 Eze 14:11; 37:27; 2Tim 1:12Ndipo watakapojua kuwa Mimi, Bwana, Mungu wao, niko pamoja nao, na kwamba wao, nyumba ya Israeli, ni watu wangu, asema Bwana Mwenyezi. 34:31 Za 100:3; Yer 23:1; Za 28:9Ninyi ni kondoo wangu, kondoo wa malisho yangu, ninyi ni watu wangu, nami ni Mungu wenu, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

Read More of Ezekieli 34

Ezekieli 35:1-15

Unabii Dhidi Ya Edomu

Neno la Bwana likanijia kusema: 35:2 Mwa 14:6; Kum 2:5; Yer 49:7-8; Amo 1:11“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya mlima Seiri, utabiri dhidi yake 35:3 Yer 6:12; Eze 34:10; 25:12-14; Oba 1:10na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume nawe, ee mlima Seiri, nami nitanyoosha mkono wangu dhidi yako na kukufanya ukiwa na usiyekaliwa na watu wala kulimika. 35:4 Yer 49:10; 44:2Nitaifanya miji yako kuwa magofu nawe utakuwa ukiwa. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.

35:5 Za 137:7; Eze 21:29; Za 63:10; Oba 1:13“ ‘Kwa sababu ulificha moyoni uadui wa siku nyingi nawe ukawatoa Waisraeli wauawe kwa upanga wakati wa maafa yao, wakati adhabu yake ilipofikia kilele chake, 35:6 Isa 63:2-6; 34:3kwa hiyo hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, nitakutia katika umwagaji damu nao utakufuatia. Kwa kuwa hakuchukia kumwaga damu, kumwaga damu kutakufuatia. 35:7 Yer 46:19; 49:17Nitaufanya Mlima Seiri ukiwa na usiokaliwa na watu wala kulimika na kuukatilia mbali na wote wanaokuja na wanaokwenda. 35:8 Eze 31:12Nitaijaza milima yenu kwa watu wake waliouawa, wale waliouawa kwa upanga wataanguka juu ya vilima vyako na katika mabonde yako na katika makorongo yako yote. 35:9 Isa 34:5-6; Yer 49:13-17; Oba 1:10Nitakufanya ukiwa milele, watu hawataishi katika miji yako. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.

35:10 Za 83:12; Eze 36:2-5“ ‘Kwa sababu umesema, “Mataifa haya mawili na nchi hizi zitakuwa zetu nasi tutazimiliki,” ingawa hata mimi Bwana nilikuwa huko, 35:11 Eze 25:14; Oba 1:15; Mt 7:2; Isa 26:9; Za 9:16kwa hiyo hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, nitakutenda kwa kadiri ya hasira na wivu uliouonyesha katika chuki yako juu yao nami nitafanya nijulikane miongoni mwao wakati nitakapokuhukumu. 35:12 Yer 50:7; Za 9:16Ndipo utakapojua kuwa Mimi Bwana nimesikia mambo yote ya dharau uliyosema dhidi ya milima ya Israeli. Ulisema, “Wamefanyika ukiwa na kutiwa mikononi mwetu tuwararue.” 35:13 Dan 11:36; Yer 49:16Ulijigamba dhidi yangu na kusema maneno dhidi yangu bila kujizuia, nami nikayasikia. 35:14 Yer 51:48Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Wakati dunia yote inashangilia nitakufanya ukiwa. 35:15 Mit 17:5; Eze 36:5; Oba 1:12; Mao 4:4-21; Yer 50:11-13; Isa 34:5-6; Eze 32:29Kwa sababu ulishangilia wakati urithi wa nyumba ya Israeli ulipofanyika ukiwa, hivyo ndivyo nitakavyokutendea. Utakuwa ukiwa, ee mlima Seiri, wewe na Edomu yote. Kisha ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”

Read More of Ezekieli 35