Ezekieli 32:1-32, Ezekieli 33:1-32 NEN

Ezekieli 32:1-32

Maombolezo Kwa Ajili Ya Farao

32:1 Eze 31:1; 33:21Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kumi na mbili, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Bwana likanijia, kusema: 32:2 2Sam 1:17; 2Nya 35:25; 2Fal 24:1; Nah 2:11-13; Ay 41:31; Eze 29:3; Ay 3:8; Eze 34:18; 2Sam 3:33“Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Farao mfalme wa Misri na umwambie:

“ ‘Wewe ni kama simba miongoni mwa mataifa,

wewe ni kama joka kubwa baharini,

unayevuruga maji kwa miguu yako

na kuchafua vijito.

32:3 Eze 12:13; Hab 1:15“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Nikiwa pamoja na wingi mkubwa wa watu

nitautupa wavu wangu juu yako,

nao watakukokota katika wavu wangu.

32:4 Isa 18:6; 1Sam 17:44-46; Eze 39:4-5; 31:12-13Nitakutupa nchi kavu

na kukuvurumisha uwanjani.

Nitawafanya ndege wote wa angani watue juu yako

na wanyama wote wa nchi

watajishibisha nyama yako.

32:5 Eze 31:12Nitatawanya nyama yako juu ya milima

na kujaza mabonde kwa mabaki yako.

32:6 Isa 34:3; Eze 29:5Nitailowanisha nchi kwa damu yako inayotiririka

njia yote hadi milimani,

nayo mabonde yatajazwa na nyama yako.

32:7 Yoe 3:15; Mt 24:29; Ufu 6:12; Isa 34:4; Eze 30:3; Yoe 2:2Nitakapokuzimisha, nitafunika mbingu

na kuzitia nyota zake giza;

nitalifunika jua kwa wingu,

nao mwezi hautatoa nuru yake.

32:8 Za 102:26; Ay 9:7; Yer 4:23; Yoe 2:10Mianga yote itoayo nuru angani

nitaitia giza juu yako;

nitaleta giza juu ya nchi yako,

asema Bwana Mwenyezi.

Nitaifadhaisha mioyo ya mataifa mengi

nitakapokuangamiza miongoni mwa mataifa,

nikikuleta uhamishoni miongoni mwa nchi

ambazo haujapata kuzijua.

32:10 Yer 46:10; Eze 26:16; Ufu 18:9-10; Isa 30:32; Eze 27:35; 30:9Nitayafanya mataifa mengi wakustaajabie,

wafalme wao watatetemeka

kwa hofu kwa ajili yako

nitakapotikisa upanga wangu mbele yao.

Siku ya anguko lako

kila mmoja wao atatetemeka

kila dakika kwa ajili ya maisha yake.

32:11 Isa 19:4; Yer 46:26; Eze 21:19; 46:13; 29:19“ ‘Kwa kuwa hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Upanga wa mfalme wa Babeli

utakuja dhidi yako.

32:12 Eze 28:7; 31:11-12Nitafanya makundi yako ya wajeuri kuanguka

kwa panga za watu mashujaa,

taifa katili kuliko mataifa yote.

Watakivunjavunja kiburi cha Misri,

nayo makundi yake yote

ya wajeuri yatashindwa.

32:13 Eze 29:8-11Nitaangamiza mifugo yake yote

wanaojilisha kando ya maji mengi,

hayatavurugwa tena kwa mguu wa mwanadamu

wala kwato za mnyama

hazitayachafua tena.

Kisha nitafanya maji yake yatulie

na kufanya vijito vyake

vitiririke kama mafuta,

asema Bwana Mwenyezi.

32:15 Kut 7:5; Za 107:33-34; Kut 14:4; 18Nitakapoifanya Misri kuwa ukiwa

na kuiondolea nchi kila kitu

kilichomo ndani yake,

nitakapowapiga wote waishio humo,

ndipo watakapojua kuwa

Mimi ndimi Bwana.’

32:16 Mwa 50:10; 2Sam 1:17; Eze 26:17; 19:1“Hili ndilo ombolezo watakalomwimbia. Binti za mataifa wataliimba, kwa kuwa Misri na makundi yake yote ya wajeuri wataliimba, asema Bwana Mwenyezi.”

Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi, neno la Bwana likanijia kusema: 32:18 Yer 1:10; Mik 1:8; Eze 26:20; 31:14-16; 32:1“Mwanadamu, omboleza kwa ajili ya makundi ya wajeuri wa Misri na uwatupe kuzimu yeye na binti za mataifa yenye nguvu, waende huko pamoja nao washukao shimoni. 32:19 Eze 28:10; 31:18Je, ninyi mnamzidi nani kwa uzuri? Shukeni chini! Nanyi mkalazwe pamoja na hao wasiotahiriwa! 32:20 Za 28:3; Eze 31:17-18Wataanguka miongoni mwa wale waliouawa kwa upanga. Upanga umefutwa, mwache aburutwe mbali pamoja na hao wajeuri wake wote. 32:21 Isa 14:9; Eze 28:10Kutoka kuzimu viongozi hodari watanena kuhusu Misri pamoja na wale walioungana nao, ‘Wameshuka chini, nao wamelala kimya pamoja na hao wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.’

32:22 Eze 32:24, 26, 29, 30“Ashuru yuko huko pamoja na jeshi lake lote, amezungukwa na makaburi ya watu wake wote waliouawa, wale wote walioanguka kwa upanga. 32:23 Isa 14:15; Nah 1:14Makaburi yao yako kwenye kina cha chini cha shimo na jeshi lake limelala kulizunguka kaburi lake. Wote waliokuwa wameeneza hofu kuu katika nchi ya walio hai wameuawa, wameanguka kwa upanga.

32:24 Mwa 10:22; Yer 49:37; Ay 28:13; Eze 26:20“Elamu yuko huko, pamoja na makundi yake yote ya wajeuri wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote wameuawa, wameanguka kwa upanga. Wote waliokuwa wameeneza hofu katika nchi ya walio hai walishuka kuzimu bila kutahiriwa. Wanaichukua aibu yao pamoja na wale washukao shimoni. 32:25 Eze 28:10; 28:10Kitanda kimetandikwa kwa ajili yake miongoni mwa waliouawa, pamoja na makundi yake yote ya wajeuri wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote ni watu wasiotahiriwa, wameuawa kwa upanga. Kwa sababu vitisho vyao vilienea katika nchi ya walio hai, wameichukua aibu yao pamoja na wale washukao shimoni, nao wamewekwa miongoni mwa waliouawa.

32:26 Mwa 10:2; Eze 27:13“Mesheki na Tubali wako humo, pamoja na makundi yao ya wajeuri wakiwa wameyazunguka makaburi yao. Wote hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga kwa sababu walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai. Je, hawakulala na mashujaa wengine wasiotahiriwa waliouawa, ambao wameshuka kaburini wakiwa na silaha zao za vita, ambao panga zao ziliwekwa chini ya vichwa vyao na uovu wao juu ya mifupa yao? Adhabu kwa ajili ya dhambi zao ilikuwa juu ya mifupa yao, ingawa vitisho vya mashujaa hawa vilikuwa vimeenea hadi kwenye nchi ya walio hai.

“Wewe pia, ee Farao, utavunjwa nawe utalala miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.

32:29 Za 137:7; Eze 25:12-14; 35:15; Yer 49:7; Isa 34:5-15“Edomu yuko humo, wafalme wake wote na wakuu wake wote, ambao ijapokuwa wana nguvu, wamelazwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga. Wamelala pamoja na wasiotahiriwa, pamoja na wale washukao shimoni.

32:30 Isa 14:31; Yer 25:26; Mwa 10:15; Eze 38:6; Yer 25:22; Eze 28:10; 28:8“Wakuu wote wa kaskazini na Wasidoni wote wako huko, wameshuka chini pamoja na waliouawa kwa aibu ijapokuwa kuna vitisho vilivyosababishwa na nguvu zao. Wamelala bila kutahiriwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga na kuchukua aibu yao pamoja na wale washukao chini shimoni.

32:31 Eze 14:22; 31:16“Farao, yeye pamoja na jeshi lake lote, atakapowaona atafarijiwa kwa ajili ya makundi yake yote ya wajeuri, wale waliouawa kwa upanga, asema Bwana Mwenyezi. 32:32 Yer 44:30; Ay 3:14Ingawa nilimfanya Farao aeneze vitisho vyake katika nchi ya walio hai, Farao pamoja na makundi yake yote ya wajeuri watalazwa miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga, asema Bwana Mwenyezi.”

Read More of Ezekieli 32

Ezekieli 33:1-32

Wajibu Wa Ezekieli Kuwa Mlinzi Kwa Watu Wake

Neno la Bwana likanijia kusema: 33:2 Law 26:25; Yer 12:12; Isa 14:16; 21:6-9; Yer 51:12“Mwanadamu, sema na watu wako uwaambie, ‘Nitakapoleta upanga dhidi ya nchi, nao watu wa nchi wakamchagua mmoja wa watu wao na kumfanya awe mlinzi wao, 33:3 Hes 10:7; Hos 5:8; Kut 20:18naye auonapo upanga unakuja dhidi ya nchi na kupiga tarumbeta kuonya watu, 33:4 2Nya 25:16; Mdo 18:6; Eze 18:13; Law 20:9; Yer 6:17kama mtu yeyote asikiapo sauti ya tarumbeta hakukubali kuonywa, basi upanga ujapo na kuutoa uhai wake, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe. 33:5 Law 20:9; Kut 9:21Kwa kuwa alisikia sauti ya tarumbeta lakini hakukubali maonyo, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe. Kama angekubali maonyo, angelijiokoa mwenyewe. 33:6 Isa 56:10-11; Eze 3:18Lakini kama mlinzi akiona upanga unakuja na asipige tarumbeta kuonya watu na upanga ukija na kutoa uhai wa mmoja wao, yule mtu ataondolewa kwa sababu ya dhambi yake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwa mlinzi huyo.’

33:7 Isa 52:8; Yer 26:5“Mwanadamu, nimekufanya wewe kuwa mlinzi kwa ajili ya nyumba ya Israeli, kwa hiyo sikia neno nisemalo na uwape maonyo kutoka kwangu. 33:8 Eze 33:14; Isa 3:11; Eze 18:14Nimwambiapo mtu mwovu, ‘Ewe mtu mwovu, hakika utakufa,’ nawe hukusema neno la kumwonya ili atoke katika njia zake, yule mtu mwovu atakufa kwa ajili ya dhambi yake, mimi nitaitaka damu yake mkononi mwako. 33:9 Eze 3:17-19; Mdo 13:46; Lk 12:4; Za 7:12Lakini kama utamwonya huyo mtu mwovu aache njia zake mbaya naye hafanyi hivyo, atakufa kwa ajili ya dhambi yake, lakini utakuwa umejiokoa mwenyewe.

33:10 Law 26:16; Eze 24:23; 4:17“Mwanadamu, sema na nyumba ya Israeli uwaambie, ‘Hili ndilo mnalosema: “Makosa yetu na dhambi zetu zimetulemea, nasi tunadhoofika kwa sababu ya hayo. Tutawezaje basi kuishi?” ’ 33:11 2Sam 14:14; Mao 3:33; 2Pet 3:9; Yoe 2:12; 1Tim 2:4; 2Nya 30:9; Yer 3:12; Isa 19:22; Yer 44:7-8Waambie, ‘Hakika kama mimi niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, sifurahii kifo cha watu waovu, bali kwamba wageuke kutoka njia zao mbaya wapate kuishi. Geukeni! Geukeni kutoka njia zenu mbaya! Kwa nini mkafe, ee nyumba ya Israeli?’

33:12 2Nya 7:14; Eze 18:21; 3:20“Kwa hiyo, mwanadamu, waambie watu wako, ‘Haki ya mtu mwenye haki haitamwokoa wakati anapoacha kutii, wala uovu wa mtu mwovu hautamsababisha yeye kuanguka anapotubu na kuacha uovu. Mtu mwenye haki, kama akitenda dhambi, hataishi kwa sababu ya uadilifu wake wa awali.’ 33:13 Eze 18:23; Ebr 10:38; Lk 18:9; 2Pet 2:20-21Kama nikimwambia mtu mwenye haki kwamba hakika utaishi, lakini akategemea hiyo haki yake na kutenda uovu, hakuna tendo lolote la haki alilotenda litakalokumbukwa, atakufa kwa ajili ya uovu alioutenda. 33:14 Yer 22:3; Eze 18:27Nami kama nikimwambia mtu mwovu, ‘Hakika utakufa,’ kisha akageuka kutoka dhambi yake na kufanya lile lililo haki na sawa, 33:15 Kut 22:1-4; Law 6:2-5; Lk 19:8; Isa 55:7; Yer 18:7-8kama akirudisha kile alichochukua rehani kwa ajili ya deni, akarudisha alichoiba na kufuata amri zile ziletazo uzima, wala hafanyi uovu, hakika ataishi, hatakufa. 33:16 Isa 43:25; Eze 18:22-26; Yer 50:20Hakuna dhambi yoyote aliyoitenda itakayokumbukwa juu yake. Ametenda lile lililo haki na sawa, hakika ataishi.

33:17 Eze 33:20; 18:25-29“Lakini watu wako wanasema, ‘Njia ya Bwana si sawa.’ Lakini ni njia zao ambazo si sawa. 33:18 Eze 3:20; 18:26; Yer 18:10Kama mtu mwenye haki akigeuka kutoka uadilifu wake na kufanya uovu, atakufa kwa ajili ya huo uovu. 33:19 Eze 33:14-15Naye mtu mwovu kama akigeuka kutoka uovu wake na kufanya lile lililo haki na sawa, kwa kufanya hivyo ataishi. 33:20 Ay 34:11; Eze 33:17; 18:25-29Lakini, ee nyumba ya Israeli, unasema, ‘Njia ya Bwana si sawa.’ Lakini nitamhukumu kila mmoja wenu sawasawa na njia zake mwenyewe.”

Anguko La Yerusalemu Laelezewa

33:21 Eze 24:26; 2Fal 25:4, 10; Yer 52:4-7; Eze 32:1Mwaka wa kumi na mbili wa uhamisho wetu, mwezi wa kumi, siku ya tano, mtu aliyekuwa ametoroka kutoka Yerusalemu akanijia na kusema, “Mji wa Yerusalemu umeanguka!” 33:22 Eze 3:26-27; 24:27; Lk 1:64; Eze 29:21Basi jioni kabla mtu huyo hajaja, mkono wa Bwana, ulikuwa juu yangu, naye alifungua kinywa changu kabla ya mtu yule aliyenijia asubuhi hajafika. Basi kinywa changu kilifunguliwa na sikuweza tena kunyamaza.

Ndipo neno la Bwana likanijia kusema: 33:24 Eze 36:4; Isa 51:2; Lk 3:8; Mik 3:11; Mdo 7:5; Yer 40:7; Eze 11:15“Mwanadamu, watu wanaoishi katika magofu hayo katika nchi ya Israeli wanasema hivi, ‘Abrahamu alikuwa mtu mmoja tu, hata hivyo akaimiliki nchi. Lakini sisi ni wengi, hakika tumepewa nchi kuwa milki yetu.’ 33:25 Mwa 9:4; Kum 12:16; Yer 7:9-10; Eze 22:6, 27; Yer 7:21Kwa hiyo waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa kuwa mnakula nyama pamoja na damu na kuinulia sanamu zenu macho na kumwaga damu, je, mtaimiliki nchi? 33:26 Yer 41:7; Eze 22:11Mnategemea panga zenu, mnafanya mambo ya machukizo na kila mmoja wenu humtia unajisi mke wa jirani yake. Je, mtaimiliki nchi?’

33:27 1Sam 13:6; Isa 2:19; Amu 6:2; Yer 42:22; Eze 7:15; 14:21“Waambie hivi: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Hakika kama niishivyo, wale waliobaki katika magofu wataanguka kwa upanga, wale walio nje mashambani nitawatoa wararuliwe na wanyama pori, nao wale walio katika ngome na kwenye mapango watakufa kwa tauni. 33:28 Isa 41:15; Mwa 6:7; Yer 9:10Nitaifanya nchi kuwa ukiwa na utupu na kiburi cha nguvu zake zitafikia mwisho, nayo milima ya Israeli itakuwa ukiwa ili mtu yeyote asipite huko. 33:29 Law 26:34; Yer 18:16; 44:22; Eze 36:4; Mik 7:13Kisha watajua kuwa Mimi ndimi Bwana, nitakapokuwa nimeifanya nchi kuwa ukiwa na utupu kwa sababu ya mambo yote ya machukizo waliyotenda.’

33:30 Isa 29:13“Kwa habari yako wewe, mwanadamu, watu wako wanaongea habari zako wakiwa karibu na kuta na kwenye milango ya nyumba, wakiambiana kila mmoja na mwenzake, ‘Njooni msikie ujumbe ule utokao kwa Bwana.’ 33:31 Eze 8:1; Isa 33:15; Mt 13:22; Za 119:36; 78:36-37; Isa 29:13; Yer 3:10Watu wangu wanakujia, kama wafanyavyo, nao wanaketi mbele yako kama watu wangu na kusikiliza maneno yako, lakini hawayatendi. Kwa maana udanganyifu u katika midomo yao, lakini mioyo yao ina tamaa ya faida isiyo halali. 33:32 Mk 6:20; Yak 1:22Naam, mbele yao umekuwa tu kama yeye aimbaye nyimbo za mapenzi kwa sauti nzuri za kuvutia na kupiga vyombo kwa ustadi, kwa kuwa wanasikia maneno yako lakini hawayatendi.

Read More of Ezekieli 33