Ezekieli 30:1-26, Ezekieli 31:1-18 NEN

Ezekieli 30:1-26

Maombolezo Kwa Ajili Ya Misri

Neno la Bwana likanijia kusema: 30:2 Isa 13:6; Yak 5:1“Mwanadamu, toa unabii na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Ombolezeni ninyi na mseme,

“Ole wa siku ile!”

30:3 Oba 1:15; Yoe 2:11; Eze 32:7; 34:12; 7:7; Yoe 1:15Kwa kuwa siku ile imekaribia,

siku ya Bwana imekaribia,

siku ya mawingu,

siku ya maangamizi kwa mataifa.

30:4 Eze 29:19; Yer 50:15; 25:19; Dan 11:43; Mwa 10:6; Eze 29:10Upanga utakuja dhidi ya Misri,

nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia.

Mauaji yatakapoangukia Misri,

utajiri wake utachukuliwa

na misingi yake itabomolewa.

30:5 Eze 27:10; Yer 25:20; 2Nya 9:14; Nah 3:9Kushi30:5 Kushi ndiyo Ethiopia. na Putu, Ludi na Arabia yote, Libya30:5 Libya ndiyo Kubu. na watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri.

30:6 Eze 29:10“ ‘Hili ndilo Bwana asemalo:

“ ‘Wale walioungana na Misri wataanguka

na kiburi cha nguvu zake kitashindwa.

Kutoka Migdoli hadi Aswani,

watauawa ndani yake kwa upanga,

asema Bwana Mwenyezi.

30:7 Eze 29:12“ ‘Hizo nchi zitakua ukiwa

miongoni mwa nchi zilizo ukiwa,

nayo miji yao itakuwa magofu

miongoni mwa miji iliyo magofu.

30:8 Yer 49:27; Eze 39:6; Nah 1:6; Eze 29:9Ndipo watakapojua kwamba mimi ndimi Bwana,

nitakapoiwasha Misri moto

na wote wamsaidiao watapondwa.

30:9 Kum 31:6; Mt 10:28; Eze 24:3; 44:630:9 Mwa 10:6; Isa 18:1-2; 23:5; Eze 32:9-10; Sef 2:12“ ‘Siku hiyo wajumbe watatoka kwangu kwa merikebu, ili kuwatia hofu Ethiopia, wakiwa katika hali yao ya kuridhika. Maumivu makali yatawapata siku ya maangamizi ya Misri, kwa kuwa hakika itakuja.

30:10 Yer 39:1; Eze 29:19“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Nitakomesha makundi ya wajeuri ya Misri

kwa mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli.

30:11 Eze 28:7; 29:19Yeye na jeshi lake, taifa lililo katili kuliko mataifa yote,

litaletwa ili kuangamiza nchi.

Watafuta panga zao dhidi ya Misri

na kuijaza nchi kwa waliouawa.

30:12 Isa 19:6; Yer 46:8; Eze 29:9; 19:7Nitakausha vijito vya Naili

na nitaiuza nchi kwa watu waovu,

kwa mkono wa wageni,

nitaifanya nchi ukiwa na kila kitu

kilichomo ndani yake.

Mimi Bwana nimenena haya.

30:13 Yer 43:12; Isa 19:13; Eze 6:6; Zek 10:11“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Nitaangamiza sanamu

na kukomesha vinyago katika Memfisi30:13 Kiebrania ni Nofu.

Hapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri,

nami nitaeneza hofu katika nchi nzima.

30:14 Eze 29:14; Hes 13:22; Za 78:12; Yer 46:25Nitaifanya Pathrosi30:14 Pathrosi ni Misri ya Juu. kuwa ukiwa

na kuitia moto Soani,

nami nitaipiga kwa adhabu Thebesi30:14 Thebesi kwa Kiebrania ni No (au No-Amoni), mji katika Misri.

Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu,30:15 Kiebrania ni Sini.

ngome ya Misri,

nami nitakatilia mbali

makundi ya wajeuri wa Thebesi.

30:16 Yos 7:15; Isa 19:13Nitaitia moto nchi ya Misri;

Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu.

Thebesi itachukuliwa na tufani,

Memfisi itakuwa katika taabu daima.

30:17 Mwa 41:45Wanaume vijana wa Oni30:17 Yaani Heliopoli (Mji wa Jua). na wa Pi-Besethi30:17 Yaani Bubasti.

wataanguka kwa upanga

nayo hiyo miji itatekwa.

30:18 Law 26:13; Isa 9:4; Yer 2:16; 43:7Huko Tahpanhesi mchana utatiwa giza

nitakapovunja kongwa la Misri;

hapo kiburi cha nguvu zake kitakoma.

Atafunikwa na mawingu

na vijiji vyake vitatekwa.

30:19 Eze 28:22Kwa hiyo nitaipiga Misri kwa adhabu,

nao watajua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”

30:20 Eze 26:1; 29:17; 32:1Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa kwanza, siku ya saba, neno la Bwana likanijia kusema: 30:21 Yer 48:25; 44:30; 30:13; 46:11“Mwanadamu, nimevunja mkono wa Farao mfalme wa Misri. Haukufungwa ili upone au kuwekewa kipande cha ubao ili upate nguvu za kuweza kuchukua upanga. 30:22 Mwa 15:18; Yer 46:25; Za 37:17; Zek 11:17Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume na Farao mfalme wa Misri. Nitavunja mikono yake yote miwili, ule mkono ulio mzima pia na ule uliovunjika na kuufanya upanga uanguke toka mkononi mwake. 30:23 Eze 29:12Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi zote. 30:24 Zek 10:6-12; 12:5; Eze 21:14; Sef 2:12; Yer 51:52Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli na kuutia upanga wangu mkononi mwake, lakini nitavunja mikono ya Farao, naye atalia kwa huzuni mbele yake kama mtu aliyetiwa jeraha la kumfisha. 30:25 Kut 7:5; Za 9:16; 59:13; 1Nya 21:12; Isa 10:5; Eze 29:19Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli, lakini mikono ya Farao italegea. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana, nitakapoutia upanga wangu mkononi mwa mfalme wa Babeli, naye ataunyoosha dhidi ya Misri. 30:26 Eze 29:12Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi mbalimbali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana.”

Read More of Ezekieli 30

Ezekieli 31:1-18

Mwerezi Katika Lebanoni

31:1 Yer 52:5; Eze 32:17; 30:20Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa tatu, siku ya kwanza, neno la Bwana likanijia, kusema: 31:2 Eze 31:18“Mwanadamu, mwambie Farao mfalme wa Misri na makundi yake ya wajeuri:

“ ‘Je, ni nani awezaye kulinganishwa

na wewe katika fahari.

31:3 Nah 3:18; Isa 10:34; Eze 19:11; Sef 2:13; Yer 50:18; 2Fal 19:23; Hab 2:17; Zek 11:1Angalia Ashuru, wakati fulani ilikuwa mwerezi huko Lebanoni,

ukiwa na matawi mazuri ukitia msitu kivuli;

ulikuwa mrefu sana,

kilele chake kilipita majani ya miti yote.

31:4 Eze 17:7; Dan 4:10Maji mengi yaliustawisha,

chemchemi zenye maji mengi ziliufanya urefuke;

vijito vyake vilitiririka pale

ulipoota pande zote

na kupeleka mifereji yake

kwenye miti yote ya shambani.

31:5 Hes 24:6; Eze 17:5; Dan 4:11Hivyo ukarefuka

kupita miti yote ya shambani;

vitawi vyake viliongezeka

na matawi yake yakawa marefu,

yakitanda kwa sababu ya wingi wa maji.

31:6 Eze 17:23; Mt 13:32; Dan 4:12; Mwa 31:7-9Ndege wote wa angani

wakaweka viota kwenye vitawi vyake,

wanyama wote wa shambani

wakazaana chini ya matawi yake,

mataifa makubwa yote

yaliishi chini ya kivuli chake.

31:7 Ay 14:9Ulikuwa na fahari katika uzuri,

ukiwa na matawi yaliyotanda,

kwa kuwa mizizi yake ilikwenda chini

mpaka kwenye maji mengi.

31:8 Za 80:10; Mwa 2:8-9; 30:37Mierezi katika bustani ya Mungu

haikuweza kushindana nao,

wala misunobari haikuweza

kulingana na vitawi vyake,

wala miaramoni

haikulinganishwa na matawi yake,

wala hakukuwa na mti katika bustani ya Mungu

wa kulinganisha na uzuri wake.

31:9 Kut 9:16; Dan 4:22-24; Mwa 13:10; Eze 28:13Niliufanya kuwa mzuri

ukiwa na matawi mengi,

ulionewa wivu na miti yote ya Edeni

katika bustani ya Mungu.

31:10 Isa 2:11; 14:13-14; Ay 40:11-12; Mit 16:18; Dan 5:20; Eze 28:17“ ‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu ulikuwa mrefu sana, kilele chake kikiwa juu ya majani manene ya miti na kwa sababu ulikuwa na kiburi cha urefu wake, 31:11 Dan 5:20niliutia mikononi mwa mtawala wa mataifa, ili yeye aushughulikie sawasawa na uovu wake. Nikaukatilia mbali, 31:12 Eze 32:5; 28:7; 32:11-12; 35:8; Dan 4:12-14nayo mataifa mageni yaliyo makatili sana yaliukata huo mti na kuuacha. Matawi yake yalianguka juu ya milima na kwenye mabonde yote, vitawi vyake vikavunjika na kusambaa katika makorongo yote ya nchi. Mataifa yote ya duniani yakaondoka kutoka kwenye kivuli chake na kuuacha. 31:13 Isa 18:6; Eze 29:5; 32:431:13 Isa 18:6; Eze 29:5; 32:4Ndege wote wa angani wakakaa kwenye ule mti ulioanguka na wanyama pori wote wakakaa katikati ya vitawi vyake. 31:14 Za 82:7; Hes 14:11; Za 63:9; Eze 32:18; Za 49:14Kamwe hakutakuwa na miti mingine kando ya hayo maji itakayorefuka zaidi ya huo, vilele vyake vikiwa juu ya majani yote ya miti. Hakuna miti mingine, hata kama imekunywa maji vizuri namna gani, itakayofikia urefu huo. Yote mwisho wake ni kifo, na kuingia ardhini, kama vile ilivyo kwa wanadamu, pamoja na wale waendao shimoni.

31:15 2Sam 1:21“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika siku ile mwerezi uliposhushwa chini kaburini31:15 Yaani Kuzimu, Sheol kwa Kiebrania; pia mstari 16, 17. nilizifunika chemchemi zenye maji mengi kwa maombolezo: Nilivizuia vijito vyake na wingi wa maji yake nikauzuia. Kwa sababu yake niliivika Lebanoni huzuni, nayo miti yote ya shambani ikanyauka. 31:16 Yer 49:21; Eze 26:15; Isa 14:8; Eze 32:18, 31; Isa 14:15; Eze 14:22Niliyafanya mataifa yatetemeke kwa kishindo cha kuanguka kwake wakati nilipoushusha chini kaburini pamoja na wale washukao shimoni. Ndipo miti yote ya Edeni, miti iliyo bora kuliko yote na iliyo mizuri sana ya Lebanoni, miti yote ile iliyokunywa maji vizuri, ilifarijika hapa duniani. 31:17 Za 9:17Wale walioishi katika kivuli chake, wale walioungana naye miongoni mwa mataifa, nao pia walikuwa wamezikwa pamoja naye, wakiungana na wale waliouawa kwa upanga.

31:18 Yer 9:26; Eze 32:19-21; 28:10“ ‘Ni miti ipi ya Edeni inayoweza kulinganishwa nawe kwa fahari na utukufu? Hata hivyo, wewe pia, utashushwa chini pamoja na miti ya Edeni mpaka kuzimu, utalala miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.

“ ‘Huyu ni Farao pamoja na makundi yake yote ya wajeuri, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

Read More of Ezekieli 31