Ezekieli 28:1-26, Ezekieli 29:1-21 NEN

Ezekieli 28:1-26

Unabii Dhidi Ya Mfalme Wa Tiro

Neno la Bwana likanijia kusema: 28:2 Isa 14:13; Mwa 3:4-5; 2The 2:4; Kum 8:14; Mit 16:18; Sef 2:15; Za 9:20“Mwanadamu, mwambie mfalme wa Tiro, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Kwa sababu moyo wako umejivuna

na umesema, “Mimi ni mungu;

nami ninaketi katika kiti cha enzi cha mungu

katika moyo wa bahari.”

Lakini wewe ni mwanadamu, wala si mungu,

ingawa unafikiri kuwa una hekima kama mungu.

28:3 Dan 1:20; 2:20-23, 28; Zek 9:2; Eze 14:14Je, wewe una hekima kuliko Danieli?

Je, hakuna siri iliyofichika kwako?

28:4 Zek 9:3; Isa 10:13Kwa hekima yako na ufahamu wako,

umejipatia utajiri,

nawe umejikusanyia dhahabu

na fedha katika hazina zako.

28:5 Ay 31:25; Hos 13:6; Kum 8:12-14; Isa 23:8; Yer 9:23; 9:23; Eze 27:33Kwa werevu wako mwingi katika biashara,

umeongeza utajiri wako

na kwa sababu ya utajiri wako

moyo wako umekuwa na kiburi.

“ ‘Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Kwa sababu unafikiri una hekima,

mwenye hekima kama mungu,

28:7 Eze 32:12; 30:11; 31:12; Yer 9:23; Eze 7:24mimi nitawaleta wageni dhidi yako,

taifa katili kuliko yote;

watafuta panga zao dhidi ya uzuri wa hekima yako,

na kuchafua fahari yako inayongʼaa.

28:8 Za 55:23; Eze 32:30; 27:27; 26:12; Ufu 18:7Watakushusha chini shimoni,

nawe utakufa kifo cha kikatili

katika moyo wa bahari.

28:9 Isa 31:3; Eze 16:49Je, wakati huo utasema, “Mimi ni mungu,”

mbele ya wale wanaokuua?

Utakuwa mwanadamu tu, wala si mungu,

mikononi mwa hao wanaokuua.

28:10 1Sam 14:6; Yer 9:26; Eze 32:18-19Utakufa kifo cha wasiotahiriwa

kwa mkono wa wageni.

Kwa kuwa mimi nimenena, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

Neno la Bwana likanijia kusema: 28:12 Eze 19:1; 27:2-4“Mwanadamu, mfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, nawe umwambie: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Ulikuwa kipeo cha ukamilifu,

ukiwa umejaa hekima

na mkamilifu katika uzuri.

28:13 Mwa 2:8; Eze 31:8-9; 27:16; Ufu 17:4; Isa 14:11; Ufu 21:20Ulikuwa ndani ya Edeni,

bustani ya Mungu;

kila kito cha thamani kilikupamba:

akiki nyekundu, yakuti manjano na zumaridi,

krisolitho, shohamu na yaspi,

yakuti samawi, almasi na zabarajadi.

Kuwekwa kwa hayo mapambo na kushikizwa kwake

kulifanywa kwa dhahabu;

siku ile ulipoumbwa yaliandaliwa tayari.

28:14 Kut 30:26; 40:9; 25:17-20Ulitiwa mafuta kuwa kerubi mlinzi,

kwa kuwa hivyo ndivyo nilivyokuweka wakfu.

Ulikuwa kwenye mlima mtakatifu wa Mungu;

ulitembea katikati ya vito vya moto.

Ulikuwa mnyofu katika njia zako

tangu siku ile ya kuumbwa kwako,

hadi uovu ulipoonekana ndani yako.

28:16 Mwa 6:11; Hab 2:17; Mwa 3:24Kutokana na biashara yako iliyoenea,

ulijazwa na dhuluma,

nawe ukatenda dhambi.

Hivyo nilikuondoa kwa aibu kutoka mlima wa Mungu,

nami nikakufukuza, ee kerubi mlinzi,

kutoka katikati ya vito vya moto.

28:17 Isa 10:12; Eze 16:49; 31:10; 19:12Moyo wako ukawa na kiburi

kwa ajili ya uzuri wako,

nawe ukaiharibu hekima yako

kwa sababu ya fahari yako.

Kwa hiyo nikakutupa chini;

nimekufanya kioja mbele ya wafalme.

28:18 Oba 1:18; Mal 4:3; Zek 9:2-4Kwa dhambi zako nyingi na biashara yako ya dhuluma,

umenajisi mahali pako patakatifu.

Kwa hiyo nilifanya moto utoke ndani yako,

nao ukakuteketeza,

nami nikakufanya majivu juu ya nchi,

machoni pa wote waliokuwa wakitazama.

28:19 Yer 51:64; Eze 26:21; Law 26:21Mataifa yote yaliyokujua

yanakustajabia;

umefikia mwisho wa kutisha

na hutakuwepo tena milele.’ ”

Unabii Dhidi Ya Sidoni

Neno la Bwana likanijia kusema: 28:21 Eze 6:2; 13:17; Yer 25:2; Mwa 10:15“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Sidoni, ukatabiri dhidi yake, 28:22 Kut 14:4; Za 9:16; Eze 30:19; 39:13; Law 10:3nawe useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Mimi ni kinyume chako, ee Sidoni,

nami nitapata utukufu ndani yako.

Nao watajua kwamba Mimi ndimi Bwana,

nitakapotekeleza hukumu zangu

na kuonyesha utakatifu wangu ndani yake.

28:23 Eze 5:17; 38:22Nitapeleka tauni ndani yake

na kufanya damu itiririke katika barabara zake.

Waliochinjwa wataanguka ndani yake,

kwa upanga dhidi yake kila upande.

Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana.

28:24 Hes 33:55; Yos 23:13; Isa 5:6; Eze 2:6“ ‘Nyumba ya Israeli hawatakuwa tena na majirani wenye nia ya kuwadhuru wanaoumiza kama michongoma na miiba mikali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana Mwenyezi.

28:25 Za 106:47; Yer 32:37; Isa 11:12; Eze 20:41; Yer 12:15; 12:15; 23:8; Eze 11:17“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitakapoikusanya nyumba ya Israeli kutoka mataifa ambako wametawanyika, nitajionyesha kuwa mtakatifu miongoni mwao machoni pa mataifa. Ndipo watakapoishi katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu Yakobo. 28:26 Law 25:18; Yer 23:6; Hos 2:15; Amo 9:14-15; 1Fal 4:25; Yer 17:25; Kum 20:6; Eze 38:8; 39:26-27; Isa 65:21Wataishi humo kwa salama na watajenga nyumba na kupanda mashamba ya mizabibu, wataishi kwa salama nitakapowaadhibu majirani zao wote ambao waliwafanyia uovu. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana, Mungu wao.’ ”

Read More of Ezekieli 28

Ezekieli 29:1-21

Unabii Dhidi Ya Misri

Katika mwaka wa kumi, mwezi wa kumi, siku ya kumi na mbili, neno la Bwana likanijia kusema: 29:2 Yer 25:19; Isa 19:1-17; Yer 46:2; Eze 25:2; 30:1-26; 31:1-18“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Farao mfalme wa Misri na utabiri dhidi yake na dhidi ya Misri yote. 29:3 Yer 44:30; Za 68:30; Isa 27:1; Eze 32:2; Yer 46:8Nena, nawe useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Mimi ni kinyume nawe, Farao, mfalme wa Misri,

joka kubwa ulalaye katikati ya vijito vyako.

Unasema, “Mto Naili ni wangu mwenyewe;

niliufanya kwa ajili yangu mwenyewe.”

29:4 2Fal 19:28; Ay 41:2; Eze 38:4Lakini nitatia ndoana katika mataya yako

nami nitawafanya samaki wa vijito vyako

washikamane na magamba yako.

Nitakutoa katikati ya vijito vyako,

pamoja na samaki wote

walioshikamana na magamba yako.

29:5 Yer 7:33; 34:20; 8:2; Eze 31:13; 32:4-6; 39:4Nitakutupa jangwani,

wewe pamoja na samaki wote wa vijito vyako.

Utaanguka uwanjani,

nawe hutakusanywa au kuchukuliwa.

Nitakutoa uwe chakula

kwa wanyama wa nchi

na ndege wa angani.

29:6 2Fal 18:21; Isa 36:6Ndipo wale wote waishio Misri watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.

“ ‘Umekuwa fimbo ya tete kwa nyumba ya Israeli. 29:7 Yer 17:5; Eze 17:15-17; 2Fal 18:21; Isa 36:6Walipokushika kwa mikono yao, ulivunjika na kuchana mabega yao; walipokuegemea, ulivunjika na migongo yao ikateguka.

29:8 Eze 14:17; 25:13; 32:11-13“ ‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitaleta upanga juu yako na kuua watu wako na wanyama wao. 29:9 Eze 30:7-8, 13-19; Mit 16:18; Yer 46:8Misri itakuwa ukiwa na isiyolimwa wala kukaliwa na watu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.

“ ‘Kwa sababu ulisema, “Mto Naili ni wangu; mimi niliufanya,” 29:10 Eze 30:6-12; Yer 21:13; Kut 3:22; Yer 46:19; Kut 14:2; Isa 18:1kwa hiyo mimi ni kinyume nawe na kinyume na vijito vyako, nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa magofu na ukiwa isiyolimwa wala kukaliwa na watu kuanzia Migdoli hadi Aswani, hata kufikia mpakani wa Ethiopia. 29:11 Eze 32:13Hakuna unyayo wa mtu au mnyama utakaopita ndani yake, wala hakuna yeyote atakayeishi humo kwa muda wa miaka arobaini. 29:12 Yer 46:19; Eze 30:7; 34:10Nitaifanya nchi ya Misri ukiwa, miongoni mwa nchi zilizo ukiwa, nayo miji yake itabaki ukiwa miaka arobaini miongoni mwa miji iliyo magofu. Nami nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi nyingine.

29:13 Isa 19:23; Yer 46:26“ ‘Lakini hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mwishoni mwa hiyo miaka arobaini, nitawakusanya Wamisri kutoka mataifa walikotawanywa. 29:14 Isa 11:11; Eze 30:14; 17:14; Isa 19:22; Yer 46:26Nitawarudisha hao Wamisri kutoka kwenye kutekwa kwao na kuwaweka katika Pathrosi,29:14 Pathrosi ni Misri ya Juu. nchi ya baba zao. Huko watakuwa na ufalme usiokuwa na nguvu. 29:15 Zek 10:11Utakuwa ufalme dhaifu kuliko zote na kamwe Misri haitajikweza tena juu ya mataifa mengine. Nitaufanya ufalme wake dhaifu sana kiasi kwamba kamwe hautatawala tena juu ya mataifa mengine. 29:16 2Nya 32:10; Isa 20:5; Hos 8:13; Isa 30:2; Mao 4:17; Hes 5:15Misri haitakuwa tena tumaini la watu wa Israeli bali itakuwa kumbukumbu ya dhambi yao kwa kuigeukia kuomba msaada. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana Mwenyezi.’ ”

29:17 Eze 30:20; 24:1; 40:1Katika mwaka wa ishirini na saba, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza, neno la Bwana likanijia, kusema: 29:18 Yer 27:6; Law 13:40; Ay 1:20; Yer 39:1“Mwanadamu, Nebukadneza mfalme wa Babeli aliongoza jeshi lake kufanya kazi ngumu dhidi ya Tiro; kila kichwa kilipata upaa na kila bega likachunika. Lakini yeye na jeshi lake hawakupata malipo yoyote kutokana na muda wote aliongoza hiyo vita dhidi ya Tiro. 29:19 Yer 43:10-13; Eze 32:11; Yer 27:6; Isa 19:4; Eze 26:5; 30:4, 10Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitaitia Misri mikononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, naye atachukua utajiri wa Misri. Atateka mateka na kuchukua nyara mali za Misri kama ujira kwa ajili ya jeshi lake. 29:20 Isa 45:1; Yer 25; 9; Isa 43:3; 10:6-7Nimempa mfalme wa Babeli nchi ya Misri kuwa ujira kwa juhudi zake kwa sababu yeye na jeshi lake walifanya kwa ajili yangu, asema Bwana Mwenyezi.

29:21 Lk 1:69; 1Sam 2:10; Za 132:17; Eze 33:22; 3:27; 24:27“Katika siku hiyo nitaifanya nyumba ya Israeli iwe na nguvu nami nitakifungua kinywa chako miongoni mwao. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana.”

Read More of Ezekieli 29