Ezekieli 26:1-21, Ezekieli 27:1-36 NEN

Ezekieli 26:1-21

Unabii Dhidi Ya Tiro

26:1 Eze 24:1; 29:1; 30:20Mwaka wa kumi na moja, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Bwana likanijia kusema: 26:2 Yos 19:29; 2Sam 5:11; Eze 25:3; Yoe 3:4-6“Mwanadamu, kwa sababu Tiro amesema kuhusu Yerusalemu, ‘Aha! Lango la kwenda kwa mataifa limevunjika, nayo milango yake iko wazi mbele yangu, sasa kwa kuwa amekuwa magofu nitastawi.’ 26:3 Isa 5:30; Yer 50:42; 51:42Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi niko kinyume na wewe, ee Tiro, nami nitaleta mataifa mengi dhidi yako, kama bahari inayovurumisha mawimbi yake. 26:4 Isa 23:1, 11; Amo 1:10Watavunja kuta za Tiro na kuibomoa minara yake, nitakwangua udongo wake na kuufanya mwamba mtupu. 26:5 Eze 27:32; Hes 14:3; Eze 29:19; Mt 4:19-21; Eze 47:10; Zek 9:2-4Itakuwa huko katikati ya bahari patakuwa mahali pa kutandaza nyavu za kuvulia samaki, kwa maana nimenena, asema Bwana Mwenyezi. Atakuwa nyara kwa mataifa, 26:6 Eze 25:5nayo makao yake huko bara yataangamizwa kwa upanga. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana.

26:7 Yer 27:6; Ezr 7:12; Dan 2:37; Nah 2:3-4; Eze 23:24“Kwa maana hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kutoka kaskazini nitamleta dhidi ya Tiro Mfalme Nebukadneza wa Babeli, mfalme wa wafalme, akiwa na farasi na magari ya vita, wapanda farasi na jeshi kubwa. 26:8 Yer 6:6; 33:4; Eze 21:22; 2Sam 20:15Atayaharibu makao yako huko bara kwa upanga, ataweka jeshi kukuzingira, atakuzingira mpaka kwenye kuta za ngome zako na kuinua ngao zake dhidi yako. 26:9 Eze 21:22Ataelekeza mapigo ya vyombo vyake vya kubomolea dhidi ya kuta zako na kubomoa minara yako kwa silaha zake. 26:10 Yer 4:13; 46:9; Eze 23:24Farasi zake zitakuwa nyingi sana kiasi kwamba utafunikwa na mavumbi watakayotimua. Kuta zako zitatikisika kwa mshindo wa farasi wa vita, magari makubwa na magari ya vita wakati aingiapo malango yako kama watu waingiao mji ambao kuta zake zimebomolewa kote.

26:11 Isa 5:28; Yer 43:13; Isa 26:5“Kwato za farasi zake zitakanyaga barabara zako zote, atawaua watu wako kwa upanga na nguzo zako zilizo imara zitaanguka chini. 26:12 Yer 4:7; Hab 1:8; Isa 23:8; Eze 27:3-27Watateka utajiri wako na kuchukua nyara bidhaa zako, watazivunja kuta zako na kuzibomoa nyumba zako nzuri, watatupa baharini mawe yako, mbao zako na kifusi chako. 26:13 Yer 7:34; Za 137:2; Isa 14:11; Ay 30:31; Ufu 18:22; Hos 2:11Nitakomesha kelele za nyimbo zako, na uimbaji wako wa kinubi kamwe hautasikika tena. 26:14 Ay 12:14; Mal 1:4Nitakufanya mwamba mtupu, nawe utakuwa mahali pa kutandazia nyavu za kuvulia samaki. Kamwe hutajengwa tena, kwa maana Mimi Bwana nimenena, asema Bwana Mwenyezi.

26:15 Isa 41:5; Eze 27:35; Yer 49:21; Ay 24:12“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kwa Tiro: ‘Je, nchi za pwani hazitatetemeka kwa kishindo cha anguko lako, wakati majeruhi wanapolia kwa maumivu makali na wakati mauaji yanaendelea ndani yako? 26:16 Ay 8:22; Hos 11:10; Isa 3:26; Eze 32:10; Kut 26:36; Ay 2:8-13; Law 26:32Ndipo wakuu wote wa mataifa ya pwani watashuka kutoka kwenye viti vyao vya enzi na kuweka kando majoho yao na kuvua nguo zao zilizotariziwa. Wakiwa wamevikwa hofu kuu, wataketi chini ardhini, wakiwa wanatetemeka kila dakika na wakikustajabia. 26:17 Eze 19:1; Isa 14:12Ndipo wao watakuombolezea na kukuambia:

“ ‘Tazama jinsi ulivyoharibiwa,

ee mji uliokuwa na sifa,

wewe uliyekaliwa na mabaharia!

Ulikuwa na nguvu kwenye bahari,

wewe na watu wako;

wote walioishi huko,

uliwatia hofu kuu.

26:18 Isa 23:5; 41:5; Za 46:6; Yer 49:21; Eze 27:35Sasa nchi za pwani zinatetemeka

katika siku ya anguko lako;

visiwa vilivyomo baharini

vinaogopa kwa kuporomoka kwako.’

26:19 Isa 8:7-8; Mwa 7:11“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitakapokufanya uwe mji wa ukiwa, kama miji isiyokaliwa tena na watu, nitakapoleta vilindi vya bahari juu yako na maji yake makuu yatakapokufunika, 26:20 Amo 9:2; Yon 2:2-6; Ay 28:13; Isa 14:9-10; Eze 32:18; Ay 28:13; Hes 16:30ndipo nitakapokushusha chini pamoja na wale washukao shimoni, kwa watu wa kale, nami nitakufanya uishi katika pande za chini za nchi kama katika magofu ya kale, pamoja na wale washukao shimoni, nawe hutarudi au kurejea kwenye makao yako katika nchi ya walio hai. 26:21 Yer 20:4; Ufu 18:21; Za 37:36; Yer 51:64; Dan 11:19Nitakufikisha mwisho wa kutisha wala hutakuwepo tena. Watu watakutafuta, lakini kamwe hutaonekana tena, asema Bwana Mwenyezi.”

Read More of Ezekieli 26

Ezekieli 27:1-36

Maombolezo Kwa Ajili Ya Tiro

Neno la Bwana likanijia kusema: 27:2 Eze 19:1; 26:17; 28:12; 32:2“Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Tiro. 27:3 Hos 9:13; Isa 23:9; Eze 28:2; Za 83:16Umwambie Tiro, ulioko kwenye lango la bahari, ufanyao biashara na mataifa mengi ya pwani, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“ ‘Ee Tiro, wewe umesema,

“Mimi ni mkamilifu katika uzuri.”

27:4 Eze 28:12Mipaka yako ilikuwa katika moyo wa bahari,

wajenzi wako walikamilisha uzuri wako.

27:5 Kum 3:9; Isa 2:13Walizifanya mbao zako zote

kwa misunobari itokayo Seniri;27:5 Yaani Hermoni.

walichukua mierezi kutoka Lebanoni

kukutengenezea mlingoti.

27:6 Za 29:9; Zek 11:2; Mwa 10:4; Isa 23:12; Yer 22:20; Hes 21:33Walichukua mialoni toka Bashani

wakakutengenezea makasia yako;

kwa miti ya msanduku

kutoka pwani ya Kitimu

wakatengeneza sitaha27:6 Yaani sakafu ya merikebu au mashua. yako

na kuipamba kwa pembe za ndovu.

27:7 Kut 25:4; Yer 10:9; Isa 19:9; Mwa 10:4; Kut 26:36Kitani safi kilichotariziwa kutoka Misri kilikuwa tanga lako,

nacho kilikuwa bendera yako;

chandarua chako kilikuwa cha rangi ya buluu na ya zambarau

kutoka visiwa vya Elisha.

27:8 Mwa 10:18; 1Fal 9:23-27Watu kutoka Sidoni na Arvadi walikuwa wapiga makasia yako;

watu wako wenye ustadi, ee Tiro,

walikuwa ndio mabaharia wako.

27:9 Yos 13:5; 1Fal 5:18; Za 104:26Wazee wa Gebali27:9 Yaani Bubilo, mji wa zamani sana wa Ufoinike (kama kilomita 80 kaskazini mwa Beiruti). pamoja na mafundi stadi

walikuwa mafundi wako melini.

Meli zote za baharini na mabaharia wao

walikuja kwako ili kubadilishana bidhaa zako.

27:10 Dan 8:20; Mwa 10:6; Nah 3:9; Yer 46:9; Eze 38:5; 2Nya 36:20; Isa 66:19; Wim 4:4“ ‘Watu wa Uajemi, Ludi na Putu

walikuwa askari katika jeshi lako.

Walitundika ngao zao na chapeo zao kwenye kuta zako,

wakileta fahari yako.

27:11 Eze 27:27Watu wa Arvadi na wa Heleki

walikuwa juu ya kuta zako pande zote;

watu wa Gamadi

walikuwa kwenye minara yako.

Walitundika ngao zao kuzizunguka kuta zako;

wakaukamilisha uzuri wako.

27:12 Mwa 10:4; 2Nya 20:36“ ‘Tarshishi walifanya biashara nawe kwa sababu ya utajiri wako mkubwa wa bidhaa, walibadilisha fedha, chuma, bati na risasi kwa mali zako.

27:13 Isa 66:19; Ufu 18:13; Yoe 3:6; Mwa 10:2; Eze 32:26; 38:2“ ‘Uyunani, Tubali na Mesheki, walifanya biashara nawe, walibadilisha watumwa na vyombo vya shaba kwa bidhaa zako.

27:14 Mwa 10:3; Eze 38:6“ ‘Watu wa Beth-Togarma walibadilisha farasi wa mizigo, farasi wa vita na nyumbu kwa mali zako.

27:15 Mwa 10:7; Yer 25:22; 1Fal 10:22; Ufu 18:12“ ‘Watu wa Dedani27:15 Yaani Rhodes. walifanya biashara nawe, watu wengi wa nchi za pwani walikuwa wachuuzi wako, walikulipa kwa pembe za ndovu na mpingo.

27:16 Amu 10:6; Isa 7:1-8; Kut 28:18; 39:11; Eze 28:13; 16:10; Ay 28:18“ ‘Watu wa Aramu walifanya biashara nawe kwa ajili ya wingi wa kazi za mikono yako, wakibadilishana kwa almasi, vitambaa vya rangi ya zambarau, vitambaa vilivyotariziwa, kitani safi, matumbawe27:16 Yaani marijani, jiwe laini la pwani au baharini, kama mawe ya chokaa. na akiki nyekundu.

27:17 Amu 11:33; Mdo 12:20; Mwa 43:11“ ‘Yuda na Israeli walifanya biashara nawe, walibadilishana kwa ngano kutoka Minithi, mtama, asali, mafuta na zeri ya kuponyeshea.

27:18 Mwa 14:15; Eze 47:16-18“ ‘Dameski, kwa sababu ya wingi wa kazi za mikono yako na ukuu wa utajiri wa mali, walifanya biashara nawe wakibadilishana mvinyo kutoka Helboni na sufu kutoka Zahari.

27:19 Kut 30:24; Mwa 10:2, 27“ ‘Wadani na Wayunani kutoka Uzali, walikuletea mali za biashara, nao wakabadilishana nawe chuma kilichofuliwa, mdalasini na mchaichai.

27:20 Mwa 10:7“ ‘Dedani alifanya biashara nawe kwa matandiko ya farasi.

27:21 Mwa 25:13; Isa 60:7; 2Nya 9:14; Isa 21:17“ ‘Arabuni na wakuu wote wa Kedari walikuwa wanunuzi wako waliobadilishana bidhaa zako na wana-kondoo, kondoo dume na mbuzi.

27:22 1Fal 10:1-2; Isa 60:8; Mwa 43:11; Za 72:10; Ufu 18:12“ ‘Wafanyabiashara wa Sheba na wa Raama walifanya biashara nawe, wakabadilishana bidhaa zako na aina zote za vikolezi, vito vya thamani na dhahabu.

27:23 Mwa 11:26; 2Fal 19:12; Isa 37:12; Mwa 10:22; Hes 24:24“ ‘Harani, Kane na Edeni na wafanyabiashara wa Sheba, Ashuru na Kilmadi walifanya biashara nawe. Kwenye soko lako, walifanya biashara nawe kwa mavazi mazuri, vitambaa vya buluu, nguo za kutariziwa na mazulia ya rangi mbalimbali yenye kamba zilizosokotwa na kuwekwa mafundo imara.

27:25 Mwa 10:4; Isa 2:16; Ufu 18:3“ ‘Merikebu za Tarshishi ndizo

zinazokusafirishia bidhaa zako.

Umejazwa shehena kubwa

katika moyo wa bahari.

27:26 Mwa 41:6; Za 48:7; Yer 18:7Wapiga makasia wako wanakupeleka

mpaka kwenye maji makavu.

Lakini upepo wa mashariki umekuvunja vipande vipande

katika moyo wa bahari.

27:27 Mit 11:4; Eze 28:8Utajiri wako, bidhaa zako na mali zako,

mabaharia wako, manahodha wako,

mafundi wako wa meli,

wafanyabiashara wako na askari wako wote,

na kila mmoja aliyeko melini

atazama kwenye moyo wa bahari

siku ile ya kuvunjika kwa meli yako.

27:28 Yer 49:21; Eze 26:15Nchi za pwani zitatetemeka

wakati mabaharia wako watakapopiga kelele.

27:29 Ufu 18:17Wote wapigao makasia

wataacha meli zao,

mabaharia wote na wanamaji wote

watasimama pwani.

27:30 Yos 7:6; Yer 6:26; Ufu 18:17-19; Mao 2:10Watapaza sauti zao

na kulia sana kwa ajili yako;

watajitupia mavumbi juu ya vichwa vyao

na kujivingirisha kwenye majivu.

27:31 Isa 16:9; Ay 3:20; Es 4:1; Law 13:40; Ay 1:20; Isa 3:17; Yer 48:37; Isa 22:12; Mao 2:10; Eze 7:16Watanyoa nywele zao kwa ajili yako,

nao watavaa nguo za magunia.

Watakulilia kwa uchungu wa moyo

na kwa maombolezo makuu.

27:32 Eze 19:1; 26:17; Isa 23:1-6Watakapokuwa wanalia na kuomboleza juu yako,

watafanya maombolezo kukuhusu wakisema:

“Ni nani aliyepata kuangamizwa kama Tiro,

katika moyo wa bahari?”

27:33 Eze 28:4-5Wakati bidhaa zako zilipotoka baharini,

ulitosheleza mataifa mengi;

kwa wingi wa utajiri wako na bidhaa zako

ulitajirisha wafalme wa dunia.

27:34 Za 9:4Sasa umevunjavunjwa na bahari,

katika vilindi vya maji,

bidhaa zako na kundi lako lote

vimezama pamoja nawe.

27:35 Eze 26:15; Law 26:32; Ay 18:20; Eze 32:10Wote waishio katika nchi za pwani

wanakustaajabia;

wafalme wao wanatetemeka kwa hofu kuu,

nazo nyuso zao zimekunjamana kwa woga.

27:36 Yer 18:16; Sef 2:15; Eze 26:21; Za 37:10; Yer 19:8; 49:17; 50:13Wafanyabiashara miongoni mwa mataifa wanakucheka;

umefikia mwisho wa kutisha

nawe hutakuwepo tena.’ ”

Read More of Ezekieli 27