Ezekieli 20:45-49, Ezekieli 21:1-32, Ezekieli 22:1-22 NEN

Ezekieli 20:45-49

Unabii Dhidi Ya Kusini

Neno la Bwana likanijia kusema: 20:46 Eze 21:2; Amo 7:16; Isa 30:6; Yer 13:17-19“Mwanadamu, uelekeze uso wako upande wa kusini, hubiri juu ya upande wa kusini na utoe unabii juu ya msitu wa Negebu. 20:47 Yer 21:14; Isa 13:8; Eze 21:4; 2Fal 19:23; Isa 9:18-19; Eze 19:14Waambie watu wa Negebu: ‘Sikieni neno la Bwana. Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ninakaribia kukutia moto, nao utateketeza miti yako yote, mibichi na iliyokauka. Miali ya moto haitaweza kuzimwa na kila uso kutoka kusini mpaka kaskazini utakaushwa kwa moto huo. 20:48 Yer 7:20; Eze 21:5, 32; 23:25Kila mmoja ataona kuwa mimi Bwana ndiye niliyeuwasha huo moto, nao hautazimwa.’ ”

20:49 Amu 14:12; Yn 16:24-25; Eze 4:14; Za 78:2; Eze 12:9; Mt 13:13Ndipo niliposema, “Aa, Bwana Mwenyezi! Wao hunisema, ‘Huyu si huzungumza mafumbo tu?’ ”

Read More of Ezekieli 20

Ezekieli 21:1-32

Babeli, Upanga Wa Mungu Wa Hukumu

21:1 Eze 20:1Neno la Bwana likanijia kusema: 21:2 Yer 11:12; Eze 20:46; Amo 7:16; Eze 9:6; 13:17“Mwanadamu, uelekeze uso wako juu ya Yerusalemu na uhubiri dhidi ya mahali patakatifu. Tabiri dhidi ya nchi ya Israeli 21:3 Yer 21:13; 47:6-7; Ay 9:22; Isa 27:1; Eze 14:21uiambie: ‘Hili ndilo Bwana asemalo: Mimi niko kinyume nawe. Nitautoa upanga wangu kwenye ala yake na kumkatilia mbali mwenye haki na mwovu. 21:4 Eze 20:47; Law 26:25; Yer 25:27Kwa sababu nitamkatilia mbali mwenye haki na mwovu, upanga wangu utakuwa wazi dhidi ya kila mmoja kuanzia kusini mpaka kaskazini. 21:5 Eze 20:47-48; Isa 45:23; 34:5Ndipo watu wote watajua ya kuwa Mimi Bwana nimeutoa upanga wangu kwenye ala yake, nao hautarudi humo tena.’

21:6 Isa 22:4; Yer 30:6; Eze 9:4“Kwa hiyo lia kwa uchungu, mwanadamu! Lia kwa uchungu mbele yao kwa moyo uliopondeka na kwa huzuni nyingi. 21:7 Yer 47:3; Eze 7:17; Ay 23:2; Yos 7:5; Eze 22:14; Za 6:2; Ay 11:16Nao watakapokuuliza, ‘Kwa nini unalia kwa uchungu?’ Utasema hivi, ‘Kwa sababu ya habari zinazokuja. Kila moyo utayeyuka na kila mkono utalegea, kila roho itazimia na kila goti litalegea kama maji.’ Habari hizo zinakuja! Hakika zitatokea, asema Bwana Mwenyezi.”

Neno la Bwana likanijia, kusema: 21:9 Kum 32:41“Mwanadamu, tabiri na useme, ‘Hili ndilo Bwana asemalo:

“ ‘Upanga, upanga,

ulionolewa na kusuguliwa:

21:10 Za 105:5-6; Isa 34:5-6; Kum 32:41umenolewa kwa ajili ya mauaji,

umesuguliwa ili ungʼae

kama umeme wa radi!

“ ‘Je, tuifurahie fimbo ya utawala ya mwanangu Yuda? Upanga unaidharau kila fimbo ya namna hiyo.

21:11 Yer 46:4“ ‘Upanga umewekwa tayari ili kusuguliwa,

ili upate kushikwa mkononi,

umenolewa na kusuguliwa,

umewekwa tayari kwa mkono wa muuaji.

21:12 Yer 31:19Piga kelele na uomboleze, ee mwanadamu,

kwa kuwa upanga u dhidi ya watu wangu;

u dhidi ya wakuu wote wa Israeli.

Wametolewa wauawe kwa upanga

pamoja na watu wangu.

Kwa hiyo pigapiga kifua chako.

21:13 Ay 9:23; 2Kor 8:2“ ‘Kwa maana upanga huu umejaribiwa na kuhakikishwa, itakuwaje basi fimbo ya ufalme ya Yuda inayoudharau kama haitakuwepo tena, bali itakuwa imeondolewa kabisa? asema Bwana Mwenyezi.’

21:14 Hes 24:10; Eze 6:11; 30:24; 8:12“Hivyo basi, mwanadamu, tabiri

na ukapige makofi.

Upanga wako na upige mara mbili,

naam, hata mara tatu.

Ni upanga wa kuchinja,

upanga wa mauaji makuu,

ukiwashambulia kutoka kila upande.

21:15 2Sam 17:10; Za 22:14Ili mioyo ipate kuyeyuka

na wanaouawa wawe wengi,

nimeweka upanga wa kuchinja

kwenye malango yao yote.

Lo! Umetengenezwa

umetemete kama umeme wa radi,

umeshikwa kwa ajili ya kuua.

21:16 Eze 14:17Ee upanga, kata upande wa kuume,

kisha upande wa kushoto,

mahali popote makali yako

yatakapoelekezwa.

21:17 Eze 22:13; 5:13; 14:17; 16:42Mimi nami nitapiga makofi,

nayo ghadhabu yangu itapungua.

Mimi Bwana nimesema.”

Neno la Bwana likanijia kusema: 21:19 Eze 14:21; 32:11; Yer 31:21“Mwanadamu, weka alama njia mbili ambazo upanga wa mfalme wa Babeli utapitia, njia hizo zikianzia katika nchi hiyo hiyo. Weka kibao pale ambapo njia zinagawanyika kuelekea mjini. 21:20 Yer 49:2; Amo 1:14; Kum 3:11Weka alama njia moja kwa ajili ya upanga upate kuja dhidi ya Raba ya Waamoni na nyingine upate kuja dhidi ya Yuda na Yerusalemu iliyozungushiwa ngome. 21:21 Mit 16:33; Hes 20:7; 23:23; Zek 10:2Kwa kuwa mfalme wa Babeli sasa amesimama katika njia panda, katika makutano ya njia mbili, akipiga ramli: anapiga kura kwa kutumia mishale, anataka shauri kwa sanamu zake, anachunguza maini ya wanyama. 21:22 2Fal 25:1; Eze 4:2; Yer 51:14; 4:16; 32:24; Eze 26:9Upande wake wa kuume inakuja kura ya Yerusalemu, ambapo ataweka vyombo vya kuvunjia boma, ili kuamrisha mauaji, kupiga ukelele wa vita, kuweka vyombo vya kuvunjia boma kwenye malango, kuweka jeshi kuzunguka na kufanya uzingiraji. 21:23 Hes 5:15; Eze 17:19Itakuwa kama kupiga ramli kwa uongo kwa wale watu ambao wameapa kumtii yeye. Lakini mfalme wa Babeli atawakumbusha juu ya uovu wao na kuwachukua mateka.

“Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: ‘Kwa sababu enyi watu mmekumbusha uovu wenu kwa kuasi waziwazi, mkidhihirisha dhambi zenu katika yale yote mfanyayo, kwa kuwa mmefanya jambo hili, mtachukuliwa mateka.

21:25 Eze 35:5; Mwa 13:13; Eze 22:4“ ‘Ee mtawala kafiri na mwovu wa Israeli, ambaye siku yako imewadia, ambaye wakati wako wa adhabu umefikia kilele chake, 21:26 Isa 28:5; Yer 13:18; Isa 40:4; Mt 23:12; Za 75:7hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Vua kilemba, ondoa taji. Kwa kuwa mambo hayatakuwa kama yalivyokuwa. Aliye mnyonge atakwezwa na aliyekwezwa atashushwa. 21:27 Mwa 49:10; Za 2:6; Hag 2:21-22; Yer 23:5-6; Eze 37:24Mahame! Mahame! Nitaufanya mji kuwa mahame! Hautajengwa upya mpaka aje yule ambaye ndiye mwenye haki nao; yeye ndiye nitakayempa.’

21:28 Mwa 19:38; Sef 3:8; Yer 12:12“Nawe, mwanadamu, tabiri na useme, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kuhusu Waamoni na matukano yao.

“ ‘Upanga, upanga,

umefutwa kwa ajili ya kuua,

umesuguliwa ili kuangamiza

na unametameta kama umeme wa radi!

21:29 Eze 22:28; 35:5; Yer 27:9Wakati wakitoa maono ya uongo kwa ajili yako,

wanapobashiri uongo kwa ajili yako,

wanakuweka wewe kwenye shingo za watu wapotovu,

wale walio waovu,

wale ambao siku yao imewadia,

wakati wa adhabu yao ya mwisho.

21:30 Yer 47:6; Eze 16:3Urudishe upanga kwenye ala yake!

Katika mahali ulipoumbiwa,

katika nchi ya baba zako,

huko nitakuhukumu.

21:31 Za 79:6; Eze 22:20-21; Yer 51:20-23; Za 18:15; Isa 11:4; Eze 16:39Nitamwaga ghadhabu yangu juu yako

na kupuliza moto wa hasira yangu dhidi yako;

nitakutia mikononi mwa watu wakatili,

watu stadi katika kuangamiza.

21:32 Eze 20:47-48; 25:10; Mal 4:1Mtakuwa kuni za kuwashia moto,

damu yenu itamwagwa katika nchi yenu,

wala hamtakumbukwa tena;

kwa maana Mimi Bwana nimesema.’ ”

Read More of Ezekieli 21

Ezekieli 22:1-22

Dhambi Za Yerusalemu

22:1 Hab 2:12; Hos 4:2; Eze 16:2; 23:36; 24:6Neno la Bwana likanijia kusema: 22:2 Eze 24:6, 9; Hos 4:2; Nah 3:1; Hab 2:12; Eze 16:2; 23:36“Mwanadamu, je, wewe utauhukumu? Je, utauhukumu huu mji umwagao damu? Basi uujulishe juu ya matendo yake yote ya machukizo 22:3 Eze 23:45; 24:2; Mik 6:16uuambie: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ee mji ule ujileteao maangamizi wenyewe kwa kumwaga damu ndani yake na kujinajisi wenyewe kwa kutengeneza sanamu, 22:4 2Fal 21:16; Eze 5:14; 21:25; Za 44:13-14; Dan 9:16; Za 137:3umekuwa na hatia kwa sababu ya damu uliyomwaga na umetiwa unajisi kwa sanamu ulizotengeneza. Umejiletea mwisho wa siku zako na mwisho wa miaka yako umewadia. Kwa hiyo nitakufanya kitu cha kudharauliwa kwa mataifa na kitu cha mzaha kwa nchi zote. 22:5 Isa 22:2Wale walio karibu na wale walio mbali watakudhihaki, Ewe mji wenye sifa mbaya, uliyejaa ghasia.

22:6 Isa 1:23; Eze 11:6; 18:10; 33:25“ ‘Ona jinsi kila mkuu wa Israeli aliyeko ndani yako anavyotumia nguvu zake kumwaga damu. 22:7 Kum 27:16; Mik 7:6; Kut 22:21-22; Kum 5:16; Kut 23:9Ndani yako wamewadharau baba na mama, ndani yako wamewatendea wageni udhalimu na kuwaonea yatima na wajane. 22:8 Kut 20:8; Law 19:30; Eze 23:38-39Mmedharau vitu vyangu vitakatifu na kuzinajisi Sabato zangu. 22:9 Law 19:16; Eze 18:11; Hos 4:10-14; Isa 59:3; Eze 23:29Ndani yako wako watu wasingiziaji, watu walio tayari kumwaga damu, ndani yako wako wale wanaokula vyakula vilivyotolewa mahali pa ibada za miungu kwenye milima, na kutenda matendo ya uasherati. 22:10 Law 12:2; 18:8; 1Kor 5:1Ndani yako wako wale wanaovunjia heshima vitanda vya baba zao, ndani yako wamo wale wanaowatendea wanawake jeuri wakiwa katika hedhi, wakati wakiwa si safi. 22:11 Mwa 11:31; Law 18:15; 18:9; 2Sam 13:14; Yer 5:8; Eze 18:9Ndani yako mtu hufanya mambo ya machukizo na mke wa jirani yake, mwingine kwa aibu kubwa hukutana kimwili na mke wa mwanawe, mwingine humtenda jeuri dada yake, binti wa baba yake hasa. 22:12 Kut 18:21; Amo 5:12; Law 19:13; Kum 16:19; Za 26:10; Isa 5:23; 17:10Ndani yako watu hupokea rushwa ili kumwaga damu, mnapokea riba na faida ya ziada na kupata faida isiyokuwa halali kutoka kwa jirani ili kupata faida kubwa kupita kiasi. Nawe umenisahau mimi, asema Bwana Mwenyezi.

22:13 Eze 21:17; Hes 24:10; Isa 33:15; Eze 6:11“ ‘Hakika nitapiga makofi kwa ajili ya faida isiyo halali uliyojipatia na kwa damu uliyoimwaga ndani yako. 22:14 Eze 17:24; 21:7; 24:14; 1Kor 10:22; Za 76:7; Yoe 2:11Je, ujasiri wako utadumu au mikono yako itakuwa na nguvu siku hiyo nitakapokushughulikia? Mimi Bwana nimesema na nitalifanya. 22:15 Kum 4:27; Zek 7:14; Eze 16:41; 23:27; Law 26:33Nitakutawanya miongoni mwa mataifa na kukutapanya katika nchi mbalimbali nami nitakomesha unajisi wako. 22:16 Za 9:16; Eze 6:7Ukiisha kunajisika mbele ya mataifa, utajua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”

Ndipo neno la Bwana likanijia kusema: 22:18 Za 119:119; Isa 1:22; Yer 6:28-30; Isa 48:10“Mwanadamu, nyumba ya Israeli imekuwa kwangu takataka ya chuma, wote kwangu wamekuwa shaba, bati, chuma na risasi iliyoachwa kalibuni. Wao ni taka ya madini ya fedha tu. 22:19 Za 119:119Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: ‘Kwa kuwa wote mmekuwa takataka ya chuma, nitawakusanya Yerusalemu. 22:20 Hos 8:10; Mal 3:2Kama vile watu wakusanyavyo fedha, shaba, chuma, risasi na bati kalibuni ili kuyeyusha kwa moto mkali, ndivyo nitakavyowakusanya katika hasira yangu na ghadhabu yangu kuwaweka ndani ya mji na kuwayeyusha. 22:21 Isa 40:7; Za 68:2; Eze 21:31Nitawakusanya na kupuliza juu yenu moto wa hasira yangu na ghadhabu yangu nanyi mtayeyushwa ndani ya huo mji. 22:22 Isa 1:25; 64:7; Eze 20:8; 7:8Kama fedha iyeyukavyo kalibuni, ndivyo mtakavyoyeyuka ndani ya huo mji, nanyi mtajua kuwa Mimi Bwana nimemwaga ghadhabu yangu juu yenu.’ ”

Read More of Ezekieli 22