Ezekieli 17:1-24, Ezekieli 18:1-32 NEN

Ezekieli 17:1-24

Tai Wawili Na Mizabibu

17:1 Amu 14:12; Eze 20:49Neno la Bwana likanijia kusema: 17:2 Amu 14:12; Eze 20:49“Mwanadamu, tega kitendawili, ukawaambie nyumba ya Israeli fumbo. 17:3 Kum 28:49; Dan 7:4; Yer 22:23; 49:22; Hos 8:1Waambie hivi, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Tai mkubwa mwenye mabawa yenye nguvu, yaliyojaa manyoya marefu ya rangi mbalimbali, alikuja Lebanoni. Akatua kwenye kilele cha mwerezi, 17:4 Isa 10:33akakwanyua ncha yake na kuichukua mpaka nchi ya wafanyabiashara, akaipanda huko katika mji wa wachuuzi.

17:5 Kum 8:7-9; Isa 15:7; Eze 31:5; Isa 44:5“ ‘Akachukua baadhi ya mbegu za nchi yako na kuziweka katika udongo wenye rutuba. Akazipanda kama mti umeao kando ya maji mengi, 17:6 Isa 18:5; Ay 5:3nazo zikaota na kuwa mzabibu mfupi, unaoeneza matawi yake. Matawi yake yakamwelekea huyo tai, mizizi yake ikabaki chini ya huo mzabibu. Kwa hiyo ukawa mzabibu na kutoa matawi na vitawi vyenye majani mengi.

17:7 Eze 31:4“ ‘Lakini kulikuwa na tai mwingine mkubwa, mwenye mabawa yenye nguvu yaliyojaa manyoya. Tazama! Huu mzabibu ukatoa mizizi yake kumwelekea huyo tai kutoka mle kwenye shamba lile ulikopandwa na kutanda matawi yake kumwelekea kwa ajili ya kupata maji. 17:8 Ay 18:19; Mal 4:1Ulikuwa umepandwa katika udongo mzuri wenye maji mengi ili uweze kutoa matawi, kuzaa matunda na uweze kuwa mzabibu mzuri sana.’

17:9 Yer 42:10; Amo 2:9“Waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Je, utastawi? Je, hautangʼolewa na kuondolewa matunda yake, ili uweze kunyauka? Majani yake mapya yanayochipua yote yatanyauka. Hautahitaji mkono wenye nguvu au watu wengi kuungʼoa na mizizi yake. 17:10 Ay 1:19; Hos 12:1; Yud 12; Eze 15:4; Hos 13:15Hata kama utapandwa pengine, Je, utastawi? Je, hautanyauka kabisa wakati upepo wa mashariki utakapoupiga, yaani, hautanyauka kabisa katika udongo mzuri ambamo ulikuwa umestawi vizuri?’ ”

Ndipo neno la Bwana likanijia kusema: 17:12 Eze 12:9; 2Fal 24:15; Kum 21:10; 2Nya 36:10; Eze 24:19“Waambie nyumba hii ya kuasi, ‘Je, mnajua hii ina maana gani?’ Waambie: ‘Mfalme wa Babeli alikwenda Yerusalemu na kumchukua mfalme na watu maarufu, akarudi nao na kuwaleta mpaka Babeli. 17:13 2Nya 36:13; 2Fal 24:17; Kut 23:32; Isa 3:2Ndipo akamchukua mmoja wa jamaa ya mfalme na kufanya mapatano naye, akamfanya aape. Akawachukua pia viongozi wa nchi, 17:14 Eze 29:14ili kuudhoofisha ufalme huo, usiweze kuinuka tena, ila uweze kuendelea tu chini ya mapatano yake. 17:15 Yer 52:3; Kum 17:16; Isa 30:2; Za 56:7; Kum 17:16; Yer 34:3; Eze 29:16Lakini mfalme aliasi dhidi yake kwa kutuma wajumbe wake kwenda Misri ili kupatiwa farasi na jeshi kubwa. Je, atashinda? Je, atafanikiwa? Je, mtu afanyaye mambo kama hayo ataokoka? Je, atavunja mapatano na bado aokoke?

17:16 Yer 52:11; Eze 12:13; Yer 32:5; 2Fal 24:17“ ‘Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, atafia huko Babeli, katika nchi ya mfalme aliyemketisha katika kiti cha enzi, ambaye alidharau kiapo chake na kuvunja mapatano yake. 17:17 Yer 37:7; Eze 4:2; Isa 36:6; Mao 4:17; Eze 29:6-7Farao na jeshi lake kubwa, na wingi wake wa watu hawataweza kusaidia chochote katika vita, wakati watakapozungukwa na jeshi ili kukatilia mbali maisha ya watu wengi. 17:18 2Fal 10:15; 1Nya 29:24Alidharau kiapo kwa kuvunja Agano. Kwa sababu aliahidi kwa mkono wake mwenyewe na bado akafanya mambo haya yote, hataokoka.

17:19 Yer 7:9; Hos 10:4; Eze 16:59; 21:23“ ‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Hakika kama niishivyo, nitaleta juu ya kichwa chake kiapo changu, alichokidharau na Agano langu lile alilolivunja. 17:20 Yos 10:16-18; Mhu 9:12; Eze 12:13; 32:3; 20:36; 15:8; Yer 2:35Nitautandaza wavu wangu kwa ajili yake, naye atanaswa katika mtego wangu. Nitamleta mpaka Babeli na kutekeleza hukumu juu yake huko kwa kuwa hakuwa mwaminifu kwangu. 17:21 Eze 12:14; 2Fal 25:11; Law 26:33; Zek 2:5-6; 2Fal 25:5Askari wake wote wanaotoroka wataanguka kwa upanga, nao watakaonusurika watatawanyika katika pande zote za dunia. Ndipo utakapojua kuwa Mimi Bwana nimesema.

Hatimaye Israeli Kutukuzwa

17:22 Isa 2:2; 53:2; Yer 23:5; 2Fal 19:30; Isa 4:2; Eze 20:40; 40:2; 43:12“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi mwenyewe nitachukua chipukizi kutoka kwenye kilele cha juu sana cha mwerezi na kukipanda, nitavunja kitawi kichanga kutoka matawi yake ya juu kabisa na kukipanda juu ya mlima mrefu ulioinuka sana. 17:23 Dan 4:12; Mt 13:32; Mik 4:1; Yer 31:12; Isa 27:6; 2:2; Za 92:12; Hos 14:5-7Katika vilele vya mlima mrefu wa Israeli nitakipanda, kitatoa matawi na kuzaa matunda na kuwa mwerezi mzuri sana. Ndege wa kila aina wataweka viota vyao ndani yake, nao watapata makazi katika kivuli cha matawi yake. 17:24 Za 96:12; Isa 2:13; Eze 19:12; 21:26; 22:14; Amo 9:11; Za 52:5; Hes 17:8; Dan 5:21; 1Sam 2:7-8; Eze 37:13Miti yote ya kondeni itajua kuwa Mimi Bwana ninaishusha miti mirefu na kuikuza miti mifupi kuwa miti mirefu. Mimi naikausha miti mibichi na kuifanya miti mikavu istawi.

“ ‘Mimi Bwana nimesema, nami nitatenda.’ ”

Read More of Ezekieli 17

Ezekieli 18:1-32

Roho Itendayo Dhambi Itakufa

Neno la Bwana likanijia kusema: 18:2 Isa 3:15; Mao 5:7; Ay 21:19; Yer 31:29“Je, ninyi watu mna maana gani kutumia mithali hii inayohusu nchi ya Israeli:

“ ‘Baba wamekula zabibu zenye chachu,

nayo meno ya watoto yametiwa ganzi’?

18:3 Za 49:4“Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hamtatumia tena mithali hii katika Israeli. 18:4 Mwa 18:32; Rum 6:23; Ebr 12:9; 2Fal 14:6; Mit 13:21; Kut 17:14; Ay 21:20; Isa 42:5; Eze 33:8Kwa kuwa kila roho ni mali yangu, kama vile ilivyo roho ya baba, vivyo hivyo roho ya mtoto ni mali yangu. Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa.

“Mtu aweza kuwa ni mwenye haki

atendaye yaliyo haki na sawa.

18:6 Eze 6:2; 22:9; Kum 4:19; Amo 5:26; Ebr 13:4; Eze 6:13; Law 15:24Hakula katika mahali pa ibada za miungu

kwenye milima

wala hakuziinulia macho sanamu

za nyumba ya Israeli.

Hakumtia unajisi mke wa jirani yake,

wala hakukutana kimwili na mwanamke

wakati wa siku zake za hedhi.

18:7 Yak 5:4; Kut 22:26; Kum 24:12; 24:12; 15:11; Lk 3:11; Kut 20:15; Ay 22:7Hamwonei mtu yeyote,

bali hurudisha kilichowekwa rehani kwake.

Hanyangʼanyi, bali huwapa wenye njaa chakula chake

na huwapa nguo walio uchi.

18:8 Zek 8:16; Kut 18:21; Kum 23:19-20; Yer 22:3; Kut 22:25; Law 25:35-37Hakopeshi kwa riba

wala hajipatii faida ya ziada.

Huuzuia mkono wake usifanye mabaya,

naye huhukumu kwa haki kati ya mtu na mtu.

18:9 Hab 2:4; Law 18:5; Amo 5:4; Law 19:37; Eze 11:12; 20:11Huzifuata amri zangu

na kuzishika sheria zangu kwa uaminifu.

Huyo mtu ni mwenye haki;

hakika ataishi,

asema Bwana Mwenyezi.

18:10 Kut 21:12; Eze 22:6“Aweza kuwa ana mwana jeuri, amwagaye damu au atendaye mojawapo ya mambo haya 18:11 Kut 22:22; Ay 24:9; Isa 54:9; 59:6-7; Hab 2:6; Kut 22:17; Eze 16:49(ingawa baba yake hakufanya mojawapo ya haya):

“Hula katika mahali pa ibada za miungu kwenye milima.

Humtia unajisi mke wa jirani yake.

18:12 Kut 22:22; 22:27; Ay 24:9; Amo 4:1; 2Fal 21:11Huwaonea maskini na wahitaji.

Hunyangʼanyana.

Harudishi kile kilichowekwa rehani kwake.

Huziinulia sanamu macho.

Hufanya mambo ya machukizo.

18:13 Kut 22:25; Law 20:9; Hos 12:14; Eze 33:4-5Hukopesha kwa riba na kutafuta faida ya ziada.

Je, mtu wa namna hii ataishi? Hapana, hataishi! Kwa sababu amefanya mambo haya yote ya machukizo, hakika atauawa na damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.

18:14 2Nya 34:21; Mit 23:24“Lakini yawezekana mwana huyo ana mwana aonaye dhambi hizi zote anazofanya baba yake, naye ingawa anaziona, yeye hafanyi mabaya kama haya:

18:15 Eze 22:9; Za 24:4“Hakula katika mahali pa ibada za miungu

kwenye milima,

wala hainulii macho sanamu

za nyumba ya Israeli.

Hakumtia unajisi

mke wa jirani yake.

18:16 Kut 22:27; Ay 22:7; Mit 22:9; Za 41:1; Eze 16:49; Isa 7:10Hakumwonea mtu yeyote

wala hakutaka rehani kwa ajili ya mkopo.

Hanyangʼanyi,

bali huwapa wenye njaa chakula chake

na huwapa nguo walio uchi.

18:17 Za 1:2Huuzuia mkono wake usitende dhambi,

hakopeshi kwa riba

wala hajipatii faida ya ziada.

Huzishika amri zangu

na kuzifuata sheria zangu.

Hatakufa kwa ajili ya dhambi za baba yake; hakika ataishi. 18:18 Eze 3:18Lakini baba yake atakufa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe, kwa sababu alitoza bei isiyo halali kwa nguvu, akamnyangʼanya ndugu yake na kufanya yaliyo mabaya miongoni mwa watu wake.

18:19 Kut 20:5; Kum 5:9; Yer 15:4; Zek 1:3-6“Lakini mnauliza, ‘Kwa nini mwana asiadhibiwe kwa uovu wa baba yake?’ Kwa vile mwana ametenda yaliyo haki na sawa na amekuwa mwangalifu kuzishika amri zangu zote, hakika ataishi. 18:20 Kum 24:16; Rum 2:9; Isa 3:10; Hes 15:31; 1Fal 8:32; 2Fal 14:6; Eze 7:27; Mt 16:27Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa. Mwana hataadhibiwa kwa ajili ya makosa ya baba yake, wala baba hataadhibiwa kwa ajili ya makosa ya mwanawe. Haki ya mtu mwenye haki itahesabiwa juu yake na uovu wa mtu mwovu utalipizwa juu yake.

18:21 Eze 13:22; 33:12-19; Yer 18:8; Mwa 26:5“Lakini mtu mwovu akiacha dhambi zake zote alizozitenda na kushika amri zangu zote na kufanya lililo haki na sawa, hakika ataishi, hatakufa. 18:22 Dan 4:27; Mik 7:19; Mit 18:20-24; Isa 43:25Hakuna kosa lolote alilotenda litakalokumbukwa juu yake. Kwa ajili ya mambo ya haki aliyoyatenda, ataishi. 18:23 Mao 3:33; 2Pet 3:9; 1Tim 2:4; Za 147:11; Ay 37:23; Eze 16:6; Mik 7:18Je, mimi ninafurahia kifo cha mtu mwovu? Asema Bwana Mwenyezi. Je, si mimi ninafurahi wanapogeuka kutoka njia zao mbaya na kuishi?

18:24 Ay 35:8; 2Pet 2:20-22; Ebr 10:38; Yer 34:6; Eze 15:8; 1Sam 15:11; 2Nya 24:17-20“Lakini kama mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda dhambi na kufanya mambo ya machukizo ambayo mtu mwovu hufanya, Je, ataishi? Hakuna hata mojawapo ya matendo ya haki aliyotenda litakalokumbukwa. Kwa sababu ya kukosa uaminifu kwake anayo hatia na kwa sababu ya dhambi alizozitenda, atakufa.

18:25 Sef 3:5; Mal 3:1-17; Mwa 18:25; Yer 2:29; Eze 33:17; Mal 2:17“Lakini mnasema, ‘Njia ya Bwana si ya haki.’ Sikia, ee nyumba ya Israeli: Njia yangu siyo iliyo ya haki? Je, si njia zenu ndizo ambazo si za haki? 18:26 Eze 18:24Kama mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda dhambi, atakufa kwa ajili ya dhambi yake, kwa sababu ya dhambi alizotenda, atakufa. 18:27 Isa 1:18; Eze 13:22Lakini mtu mwovu akigeuka kutoka maovu aliyoyatenda na kufanya yaliyo haki na sawa, ataokoa maisha yake. 18:28 Eze 18:14; Isa 55:7Kwa kuwa anayafikiria na kugeuka kutoka makosa yake yote aliyoyatenda na kuyaacha, hakika ataishi, hatakufa. Lakini nyumba ya Israeli inasema, ‘Njia za Bwana si haki.’ Je, njia zangu si za haki, ee nyumba ya Israeli? Je, si njia zenu ndizo ambazo si za haki?”

18:30 Yer 35:15; Eze 7:13; Mt 3:2; Hos 12:6; 1Pet 1:17; Isa 27“Kwa hiyo, ee nyumba ya Israeli, nitawahukumu, kila mmoja sawasawa na njia zake, asema Bwana Mwenyezi. Tubuni! Geukeni kutoka makosa yenu yote, ndipo dhambi haitakuwa anguko lenu. 18:31 Za 51:10; Isa 1:16-17; Eze 36:26; Efe 4:22; Amu 6:8; Yer 27:13; Eze 11:19Tupilieni mbali makosa yenu yote mliyoyatenda, nanyi mpate moyo mpya na roho mpya. Kwa nini mfe, ee nyumba ya Israeli? 18:32 2Nya 7:14; Ay 37:23; Eze 33:11; Ay 22:23; Isa 55:7; Mal 3:7; Eze 16:6Kwa maana sifurahii kifo cha mtu awaye yote afaye katika uovu, asema Bwana Mwenyezi. Tubuni basi, mkaishi!

Read More of Ezekieli 18