Ezekieli 13:1-23, Ezekieli 14:1-23, Ezekieli 15:1-8 NEN

Ezekieli 13:1-23

Manabii Wa Uongo Walaumiwa

Neno la Bwana likanijia kusema: 13:2 Yer 23:16; 37:19; 14:14; Isa 9:15; Yer 28:15; Eze 22:28“Mwanadamu, tabiri dhidi ya manabii wa Israeli wanaotabiri sasa. Waambie hao ambao hutabiri kutokana na mawazo yao wenyewe: ‘Sikia neno la Bwana! 13:3 Mao 2:14; Hos 9:7; Yer 23:25-32Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ole wao manabii wapumbavu wafuatao roho yao wenyewe na wala hawajaona chochote! 13:4 Mik 3:5; Wim 2:15; 2Kor 11:13Manabii wako, ee Israeli, ni kama mbweha katikati ya magofu. 13:5 Isa 58:12; Eze 22:30; 7:19; 30:3Hamjakwea kwenda kuziba mahali palipobomoka katika ukuta ili kuukarabati kwa ajili ya nyumba ya Israeli, ili kwamba isimame imara kwenye vita katika siku ya Bwana. 13:6 Yer 28:15; 29:9; 23:16; 14:14; Eze 12:24-25; 22:28Maono yao ni ya uongo na ubashiri wao ni wa udanganyifu. Wao husema, “Bwana amesema,” wakati Bwana hakuwatuma, bado wakitarajia maneno yao kutimizwa. 13:7 Yer 30:10Je, hamjaona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu hapo msemapo, “Bwana asema,” lakini Mimi sijasema?

13:8 Yer 21:13“ ‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu ya uongo wa maneno yenu na kwa madanganyo ya maono yenu, Mimi ni kinyume na ninyi, asema Bwana Mwenyezi. 13:9 Kum 32:32; Yer 17:13; Kut 6:2; Ebr 12:23; Yer 20:3-6; Eze 20:38Mkono wangu utakuwa dhidi ya manabii ambao huona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu. Hawatakuwa katika baraza la watu wangu au kuandikwa katika kumbukumbu ya nyumba ya Israeli wala hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana Mwenyezi.

13:10 2Tim 3:13; Yer 50:6; 23:13; Eze 7:25; 22:28; Yer 4:10“ ‘Kwa sababu ni kweli wanapotosha watu wangu, wakisema, “Amani,” wakati ambapo hakuna amani, pia kwa sababu, wakati ukuta dhaifu unapojengwa, wanaufunika kwa kupaka chokaa, 13:11 Eze 38:22; Za 11:6; Yos 10:11; Ay 38:23kwa hiyo waambie hao wanaoupaka chokaa isiyokorogwa vyema kwamba ukuta huo utaanguka. Mvua kubwa ya mafuriko itanyesha, nami nitaleta mvua ya mawe inyeshe kwa nguvu, nao upepo wa dhoruba utavuma juu yake. Wakati ukuta utakapoanguka, je, watu hawatawauliza, “Iko wapi chokaa mliyopaka ukuta?”

13:13 Yos 10:11; Ufu 11:19; Kut 9:25; Ay 38:23; Ufu 16:21; Isa 30:30“ ‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika ghadhabu yangu nitauachia upepo wa dhoruba, pia katika hasira yangu mvua ya mawe na mvua ya mafuriko itanyesha ikiwa na ghadhabu ya kuangamiza. 13:14 Mik 1:6; Yer 6:15; Eze 14:8; Isa 22:5Nitaubomoa ukuta mlioupaka chokaa na kuuangusha chini ili msingi wake uachwe wazi. Utakapoanguka, mtaangamizwa ndani yake, nanyi mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana. Hivyo ndivyo nitakavyoitimiza ghadhabu yangu dhidi ya huo ukuta na dhidi yao walioupaka chokaa. Nitawaambia ninyi, “Ukuta umebomoka na vivyo hivyo wale walioupaka chokaa, 13:16 Isa 57:21; Yer 6:14; 8:11; Eze 7:25wale manabii wa Israeli waliotabiri juu ya Yerusalemu na kuona maono ya amani kwa ajili yake wakati kulipokuwa hakuna amani, asema Bwana Mwenyezi.” ’

13:17 Kut 15:20; Ufu 2:20; Isa 3:16; Eze 4:7; 25:2; 28:21“Sasa, mwanadamu, kaza uso wako dhidi ya binti za watu wako wanaotabiri mambo kutoka mawazo yao wenyewe. Tabiri dhidi yao 13:18 2Pet 2:14na useme, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ole wao wanawake washonao hirizi za uchawi juu ya viwiko vyao vyote na kutengeneza shela za urefu wa aina mbalimbali kwa ajili ya kufunika vichwa vyao kwa makusudi ya kuwanasa watu. Je, mtatega uhai wa watu wangu lakini ninyi mponye wa kwenu? 13:19 Yer 44:26; Eze 22:26; 20:39; Mit 28:21; Mik 3:11; Rum 14:15Ninyi mmeninajisi miongoni mwa watu wangu kwa ajili ya konzi chache za shayiri na chembe za mkate. Kwa kuwaambia uongo watu wangu, wale ambao husikiliza uongo, mmewaua wale watu ambao wasingekufa na kuwaacha hai wale ambao wasingeishi.

13:20 Za 124:7“ ‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi niko kinyume na hizo hirizi zenu za uchawi ambazo kwa hizo mnawatega watu kama ndege, nami nitazirarua kutoka mikononi mwenu, nitawaweka huru watu wale mliowatega kama ndege. 13:21 Za 91:3Nitazirarua shela zenu na kuwaokoa watu wangu kutoka mikononi mwenu, nao hawatakuwa tena mawindo ya nguvu zenu. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana. 13:22 Yer 23:14; Eze 18:21; Mit 19:27; Isa 9:21; Eze 33:14-16Kwa sababu mliwavunja moyo wenye haki kwa uongo wenu, wakati mimi sikuwaletea huzuni na kwa kuwa mliwatia moyo waovu ili wasiziache njia zao mbaya na hivyo kuokoa maisha yao, 13:23 Eze 12:24; Mik 3:6; Eze 14:8; Neh 6:12; Za 72:14kwa hiyo hamtaona tena maono ya uongo wala kufanya ubashiri. Nitawaokoa watu wangu kutoka mikononi mwenu. Nanyi ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.’ ”

Read More of Ezekieli 13

Ezekieli 14:1-23

Waabudu Sanamu Walaumiwa

14:1 Eze 8:1; 20:1Baadhi ya wazee wa Israeli walinijia na kuketi mbele yangu. Ndipo neno la Bwana likanijia kusema: 14:3 Eze 7:19; Ufu 2:14; Isa 1:15; Eze 20:31; Mit 15:8; Eze 6:4“Mwanadamu, watu hawa wameweka sanamu katika mioyo yao na kuweka vitu viovu vya kukwaza mbele ya macho yao. Je, kweli niwaruhusu waniulize jambo lolote? Kwa hiyo sema nao uwaambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Wakati Mwisraeli yeyote anapoweka sanamu moyoni mwake na kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akaenda kwa nabii, Mimi Bwana nitamjibu peke yangu sawasawa na ukubwa wa ibada yake ya sanamu. 14:5 Ebr 3:12-19; Kum 32:15; Hos 5:7; Yer 2:11; Eze 16:45; Zek 11:8Nitafanya jambo hili ili kukamata tena mioyo ya watu wa Israeli, ambao wote wameniacha kwa ajili ya sanamu zao.’

14:6 Isa 2:20; 30:22; Neh 1:9; Yer 3:12; 35:15“Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Tubuni! Geukeni kutoka kwenye sanamu zenu na mkatae matendo yenu yote ya machukizo!

14:7 Kut 12:48; 20:10; Mt 6:24; Yer 2:13; Isa 8:14; Mwa 25:22; Hos 4:5“ ‘Mwisraeli yeyote au mgeni yeyote anayeishi katika Israeli anapojitenga nami na kujiwekea sanamu katika moyo wake na kwa hivyo kuweka kitu kiovu cha kukwaza mbele ya macho yake na kisha akamwendea nabii kuuliza shauri kwangu, mimi Bwana nitamjibu mwenyewe. 14:8 Eze 15:7; Za 102:8; Hes 26:10; Eze 5:15; Yer 42:20; Hes 16:38Nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo na kumwadhibu na kumfanya ishara kwa watu. Nitamkatilia mbali kutoka watu wangu. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.

14:9 Yer 14:15; Isa 63:17; Yer 4:10; 2Nya 18:22; Zek 13:3; 1Fal 22:23“ ‘Naye nabii kama atakuwa ameshawishika kutoa unabii, Mimi Bwana nitakuwa nimemshawishi nabii huyo, nami nitaunyoosha mkono wangu dhidi yake na kumwangamiza kutoka miongoni mwa watu wangu Israeli. Watachukua hatia yao, nabii atakuwa na hatia sawa na yule mtu aliyekuja kuuliza neno kwake.

14:11 Eze 48:11; 11:19-20; 37:23; Isa 13:19; 51:16“ ‘Ndipo watu wa Israeli hawataniacha tena, wala kujitia unajisi tena kwa dhambi zao zote. Ndipo watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

Hukumu Isiyoepukika

Neno la Bwana likanijia kusema, 14:13 Law 26:26; Eze 5:16; 5:16; 6:14; Mit 13:21; Eze 15:8“Mwanadamu, kama nchi itanitenda dhambi kwa kutokuwa waaminifu nami nikinyoosha mkono wangu dhidi yake kukatilia mbali upatikanaji wake wa chakula na kuipelekea njaa na kuua watu wake na wanyama wao, 14:14 Mwa 6:8-9; Dan 6:13; Ay 42:9; Eze 28:3; 18:20; 3:19hata kama watu hawa watatu: Noa, Danieli na Ayubu wangekuwa ndani ya nchi hiyo, ndio hao tu wangeweza kujiokoa wenyewe kwa uadilifu wao, asema Bwana Mwenyezi.

14:15 Hes 21:6; Eze 5:17; Law 26:22“Au kama nikipeleka wanyama pori katika nchi hiyo yote na kuifanya isiwe na watoto, nayo ikawa ukiwa kwamba hakuna mtu apitaye katika nchi hiyo kwa sababu ya wanyama pori, 14:16 Mwa 19:29; Eze 18:20hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hata kama watu hawa watatu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kuokoa wana wao wala binti zao. Wao peke yao wangeokolewa, lakini nchi ingekuwa ukiwa.

14:17 Law 26:25; Yer 25:27; Eze 25:13; 5:12; Yer 42:16“Au kama nikileta upanga dhidi ya nchi hiyo na kusema, ‘Upanga na upite katika nchi yote,’ nami nikiua watu wake na wanyama wao, 14:18 Eze 14:14hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hata kama watu hawa watatu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kuokoa wana wao wala binti zao. Wao wenyewe tu wangeokolewa.

14:19 Yer 14:12; Eze 38:22; Ufu 16:3-6; Eze 7:8; Isa 34:3“Au kama nikipeleka tauni katika nchi hiyo na kumwaga ghadhabu yangu juu yake kwa njia ya kumwaga damu, kuua watu wake na wanyama wao, 14:20 Eze 14:14hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hata kama Noa, Danieli na Ayubu wangekuwa humo ndani yake, wasingeweza kumwokoa mwana wala binti. Wao wangeweza kujiokoa wenyewe tu kwa uadilifu wao.

14:21 Eze 5:17; Amo 4:6-10; Ufu 6:8; Hes 33:4; Isa 31:8; 34:6; Eze 21:3; 2Sam 24:13“Kwa maana hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Itakuwa vibaya kiasi gani nitakapopeleka dhidi ya Yerusalemu hukumu zangu nne za kutisha, yaani, upanga, njaa, wanyama pori na tauni, ili kuua watu wake na wanyama wao! 14:22 Eze 12:16; 20:43; Yer 41:16; Eze 31:16; 32:31Lakini watakuwepo wenye kuokoka, wana na binti wataletwa kutoka nje ya nchi hiyo. Watawajia ninyi, nanyi mtakapoona mwenendo wao na matendo yao, mtafarijika kuhusu maafa niliyoleta juu ya Yerusalemu, kwa ajili ya yale yote niliyoleta juu yake. 14:23 Yer 22:8-9; Eze 8:6-18Mtafarijika wakati mtakapoona mwenendo wao na matendo yao, kwa kuwa mtajua kwamba sikufanya lolote ndani yake bila sababu, asema Bwana Mwenyezi.”

Read More of Ezekieli 14

Ezekieli 15:1-8

Yerusalemu Mzabibu Usiofaa

Neno la Bwana likanijia kusema: 15:2 Za 80:8-16; Yn 15:2; Yer 2:21; Isa 27:2-6; 5:1-7; Hos 10:1“Mwanadamu, je, ni vipi mti wa mzabibu unaweza kuwa bora zaidi kuliko tawi la mti mwingine wowote ndani ya msitu? 15:3 Yer 13:10; Isa 22:23Je, mti wake kamwe huchukuliwa na kutengeneza chochote cha manufaa? Je, watu hutengeneza vigingi vya kuningʼinizia vitu kutokana na huo mti wake? 15:4 Eze 17:3-10; Yn 15:6; Eze 19:14Nao baada ya kutiwa motoni kama nishati na moto ukateketeza ncha zote mbili na kuunguza sehemu ya kati, je, unafaa kwa lolote? Kama haukufaa kitu chochote ulipokuwa mzima, je, si zaidi sana sasa ambapo hauwezekani kufanyishwa chochote cha kufaa baada ya moto kuuchoma na kuuunguza?

“Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kama nilivyoutoa mti wa mzabibu miongoni mwa miti ya msituni kuwa nishati kwa ajili ya moto, hivyo ndivyo nitakavyowatendea watu waishio Yerusalemu. 15:7 Yer 21:10; Law 26:17; Za 34:16; Isa 24:18; Amo 9:1-4; Eze 14:8; 5:2-4Nitaukaza uso wangu dhidi yao. Ingawa watakuwa wameokoka kwenye moto, bado moto utawateketeza. Nami nitakapoukaza uso wangu dhidi yao, ninyi mtajua kwamba Mimi ndimi Bwana. 15:8 Eze 14:13; 17:20; Amo 5:19; Eze 18:24Nitaifanya nchi kuwa ukiwa kwa sababu wamekuwa si waaminifu, asema Bwana Mwenyezi.”

Read More of Ezekieli 15