Ezekieli 10:1-22, Ezekieli 11:1-25, Ezekieli 12:1-28 NEN

Ezekieli 10:1-22

Utukufu Unaondoka Hekaluni

10:1 Kut 23:10; Eze 1:22; Ufu 4:2-3; Mwa 3:24Nikatazama, nikaona juu ya ile nafasi iliyokuwa juu ya vichwa vya wale makerubi kulikuwa na kitu mfano wa kiti cha enzi cha yakuti samawi. 10:2 Eze 1:15; 9:2; Ufu 8:5; 2Sam 22:9Bwana akamwambia mtu yule aliyekuwa amevaa nguo ya kitani, “Ingia katikati ya yale Magurudumu yaliyo chini ya makerubi. Ukaijaze mikono yako makaa ya mawe ya moto kutoka katikati ya makerubi na uyatawanye juu ya mji.” Nilipokuwa nikiangalia, akaingia ndani.

Basi wale makerubi walikuwa wamesimama upande wa kusini wa Hekalu wakati yule mtu alipoingia ndani, wingu likaujaza ule ukumbi wa ndani. 10:4 Kut 24:16; Eze 44:4; 1:28Kisha utukufu wa Bwana ukainuka kutoka juu ya wale makerubi ukaenda kwenye kizingiti cha Hekalu. Wingu likajaza Hekalu, nao ukumbi ukajawa na mngʼao wa utukufu wa Bwana. 10:5 Ay 40:9; Eze 1:24; 3:15Sauti ya mabawa ya wale makerubi ingeweza kusikika mpaka kwenye ukumbi wa nje, kama sauti ya Mungu Mwenyezi10:5 Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote). wakati anapoongea.

10:6 Dan 7:9Bwana alipomwamuru yule mtu aliyevaa nguo za kitani akisema, “Chukua moto toka katikati ya magurudumu, kutoka katikati ya makerubi,” yule mtu aliingia ndani akasimama pembeni mwa gurudumu. 10:7 Eze 5:4Ndipo mmoja wa wale makerubi akanyoosha mkono wake kwenye moto uliokuwa katikati yao. Akachukua baadhi ya moto na kuutia mikononi mwa yule mtu aliyevaa mavazi ya kitani, naye akaupokea akatoka nje. 10:8 Eze 1:8(Chini ya mabawa ya makerubi paliweza kuonekana kitu kilichofanana na mikono ya mwanadamu.)

10:9 Kut 28:20; Eze 1:15-21; 24:6Nikatazama, nikaona magurudumu manne kando ya makerubi, moja kando ya kila kerubi. Magurudumu hayo yalimetameta kama kito cha zabarajadi. Kule kuonekana kwake, yote manne yalifanana kila gurudumu lilikuwa kama linazunguka ndani ya lingine. 10:11 Eze 1:17Yalipozunguka, yalikwenda kokote katika pande nne walikoelekea wale makerubi. Magurudumu hayakugeuka wakati makerubi yalipokwenda. Makerubi walikwenda upande wowote kichwa kilikoelekea pasipo kugeuka walipokuwa wakienda. 10:12 Ufu 4:6-8; Eze 1:15-21; 24:6Miili yao yote, pamoja na migongo yao, mikono na mabawa yao yote yalikuwa yamejaa macho kabisa kama yalivyokuwa yale magurudumu yao manne. Nikasikia magurudumu yakiitwa, “Magurudumu ya kisulisuli.” 10:14 1Fal 7:36; Eze 41:19; Dan 9:21; Ufu 4:7Kila mmoja wa wale makerubi alikuwa na nyuso nne: Uso mmoja ulikuwa kama vile wa kerubi, uso wa pili ulikuwa wa mwanadamu, uso wa tatu ulikuwa wa simba na uso wa nne ulikuwa wa tai.

10:15 Isa 6:2; Eze 1:3-5; Za 137:1Kisha makerubi wakapaa juu. Hawa ndio wale viumbe walio hai niliowaona kando ya Mto Kebari. 10:16 Eze 1:19Wakati makerubi walipokwenda, magurudumu yaliyoko kando yao yalikwenda na wakati makerubi walipotanda mabawa yao wapate kupaa juu kutoka ardhi, magurudumu yale hayakuondoka pembeni mwao. 10:17 Eze 1:20-21; 3:13Makerubi yaliposimama kimya, nayo pia yalitulia kimya, nao makerubi yalipoinuka juu, magurudumu nayo yaliinuka juu pamoja nao, kwa sababu roho ya vile viumbe hai ilikuwa ndani yake.

10:18 Za 78:60; 18:10; Eze 7:20-22; 1Sam 4:21Kisha utukufu wa Bwana ukaondoka pale kwenye kizingiti cha Hekalu na kusimama juu ya wale makerubi. 10:19 Eze 11:1-22; 43:4Nilipokuwa nikitazama, makerubi yakatanda mabawa yao na kuinuka kutoka ardhini, nao walipokuwa wakienda, yale magurudumu yakaenda pamoja nao. Wakasimama kwenye ingilio la lango la mashariki la nyumba ya Bwana, nao utukufu wa Mungu wa Israeli ukawa juu yao.

10:20 Eze 1:1-8Hawa walikuwa ndio viumbe hai niliokuwa nimewaona chini ya Mungu wa Israeli kando ya Mto Kebari, nami nikatambua ya kuwa hao walikuwa makerubi. 10:21 Eze 1:6, 8Kila mmoja alikuwa na nyuso nne, mabawa manne, chini ya mabawa yao kulikuwa na kile kilichoonekana kama mikono ya mwanadamu. 10:22 Eze 1:10, 12Nyuso zao zilifanana kama zile nilizokuwa nimeziona kando ya Mto Kebari. Kila mmoja alikwenda mbele moja kwa moja.

Read More of Ezekieli 10

Ezekieli 11:1-25

Hukumu Juu Ya Viongozi Wa Israeli

11:1 Eze 8:16; 43:4-5; 3:12-14; Yer 5:5Ndipo Roho akaniinua na kunileta mpaka kwenye lango la nyumba ya Bwana linalotazama upande wa mashariki. Pale kwenye ingilio la lango kulikuwepo wanaume ishirini na watano, nami nikaona miongoni mwao Yaazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, viongozi wa watu. 11:2 Isa 29:20; Nah 1:11Bwana akaniambia, “Mwanadamu, hawa ndio wafanyao hila na kutoa mashauri potovu katika mji huu. 11:3 Yer 1:13; Eze 24:3; 12:22, 27; Mik 3:3Wao husema, ‘Je, hivi karibuni hautakuwa wakati wa kujenga nyumba? Mji huu ni chungu cha kupikia, nasi ndio nyama.’ 11:4 Eze 3:4, 17Kwa hiyo toa unabii dhidi yao, tabiri, Ewe mwanadamu.”

11:5 Ebr 4:11; Za 26:2; Yer 17:10Kisha Roho wa Bwana akaja juu yangu, naye akaniambia niseme: “Hili ndilo Bwana asemalo: Hili ndilo ninyi mnalosema, ee nyumba ya Israeli, lakini ninajua mnalowaza mioyoni mwenu. 11:6 Eze 7:23; 22:6Mmewaua watu wengi katika mji huu na kujaza barabara zake maiti.

11:7 Mik 3:2-3; Eze 24:3-13; Yer 1:13“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi: maiti ulizozitupa huko ni nyama na mji huu ni chungu, lakini nitawaondoa mtoke huko. 11:8 Mit 10:24; Isa 66:4; Law 26:25; Yer 42:16Mnaogopa upanga, nao upanga huo ndio nitakaouleta juu yenu, asema Bwana Mwenyezi. 11:9 Za 106:41; Eze 5:8; Kum 28:36Nitawaondoa mtoke katika mji na kuwatia mikononi mwa wageni nami nitawaadhibu. 11:10 Yer 39:6; 2Fal 14:25Mtaanguka kwa upanga, nami nitatimiza hukumu dhidi yenu katika mipaka ya Israeli. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana. 11:11 Eze 24:6Mji huu hautakuwa chungu kwa ajili yenu, wala hamtakuwa nyama ndani yake. Nitatoa hukumu dhidi yenu katika mipaka ya Israeli. 11:12 Law 18:4; Eze 18:9; 8:10; 6:7Nanyi mtajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana, kwa kuwa hamkufuata amri zangu wala kuzishika sheria zangu, bali mmefuata mwenendo wa mataifa yanayowazunguka.”

11:13 Eze 9:8; Amo 7:2Basi nilipokuwa ninatoa unabii, Pelatia mwana wa Benaya akafa. Ndipo nikaanguka kifudifudi, nikalia kwa sauti kuu nikasema, “Ee Bwana Mwenyezi! Je utaangamiza kabisa mabaki ya Israeli?”

Neno la Bwana likanijia kusema: 11:15 Eze 33:24“Mwanadamu, ndugu zako, ndugu zako ambao ni wa uhusiano wa damu na nyumba yote ya Israeli, ndio wale ambao watu wa Yerusalemu wamesema, ‘Wako mbali na Bwana; nchi hii tulipewa sisi kuwa milki yetu.’

Ahadi Ya Kurudi Kwa Israeli

11:16 Za 31:20; Isa 8:14; Za 91:9; Isa 4:6“Kwa hiyo sema, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ingawa niliwapeleka mbali miongoni mwa mataifa na kuwatawanya katika nchi mbalimbali, lakini kwa kitambo kidogo mimi nimekuwa mahali patakatifu kwao katika nchi walizokwenda.’

11:17 Neh 1:9; Yer 24:5-6; 3:18; 31:16; Eze 20:41; 28:25; 34:13“Kwa hiyo sema: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitawakusanyeni kutoka mataifa na kuwarudisha kutoka nchi ambazo mmetawanywa, nami nitawarudishia nchi ya Israeli.’

11:18 Eze 5:11; 37:2311:18 Eze 5:11; 37:23“Watairudia nchi na kuondoa vinyago vyote vya upotovu na sanamu zote za machukizo. 11:19 Za 86:11; Yer 32:36; Zek 7:12; Yer 24:7; Rum 2:5; 2Kor 3:3; Eze 36:26; 18:31; 2Nya 30:12Nitawapa moyo mmoja na kuweka roho mpya ndani yao, nitaondoa kutoka ndani yao moyo wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama. 11:20 Za 105:45; Kut 6:7; Ebr 8:10; Yer 11:4; 32:38; Eze 36:26-28Kisha watafuata amri zangu na kuwa waangalifu kutii sheria zangu. Watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao. 11:21 Yer 16:11; Eze 16:43; Ebr 3:12; Eze 9:10Lakini kwa wale ambao mioyo yao imeambatana na vinyago vyao vya upotovu na sanamu zao za machukizo, nitaleta juu ya vichwa vyao yale waliyotenda asema Bwana Mwenyezi.”

11:22 Eze 9:3; 10:19; Kut 24:16Ndipo wale makerubi, wenye magurudumu pembeni mwao, wakakunjua mabawa yao, nao utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao. 11:23 Eze 1:28; 8:4; Zek 14:4; Eze 10:4Basi utukufu wa Bwana ukapaa juu kutoka mji, ukatua juu ya mlima ulio upande wa mashariki ya mji. 11:24 2Kor 12:2; Eze 8:3Roho akaniinua na kunileta mpaka kwa watu wa uhamisho huko Ukaldayo nikiwa katika yale maono niliyopewa na Roho wa Mungu.

Ndipo maono niliyokuwa nimeyaona yakanitoka, 11:25 Eze 3:4, 11; Mdo 20:20nami nikawaeleza wale watu wa uhamisho kila kitu Bwana alichokuwa amenionyesha.

Read More of Ezekieli 11

Ezekieli 12:1-28

Kutekwa Kwa Yuda Kwaelezewa

Neno la Bwana likanijia kusema: 12:2 Isa 6:10; Mk 8:18; Yer 5:21; Mt 13:15; Za 78:40; Yer 42:21; Mk 4:12“Mwanadamu, unaishi miongoni mwa watu waasi. Wana macho ya kuona, lakini hawaoni na masikio ya kusikia lakini hawasikii, kwa kuwa ni watu waasi.

12:3 Yer 36:3; 26:3; Eze 3:27; 2Tim 2:25-26“Kwa hiyo, mwanadamu, funga mizigo yako kwa kwenda uhamishoni tena wakati wa mchana, wakiwa wanakutazama, toka nje na uende mahali pengine kutoka hapo ulipo. Labda wataelewa, ingawa wao ni nyumba ya kuasi. 12:4 2Fal 25:4; Yer 39:4Wakati wa mchana, wakiwa wanakutazama, toa nje mizigo yako iliyofungwa kwa ajili ya kwenda uhamishoni. Kisha wakati wa jioni, wakiwa wanakutazama toka nje kama wale waendao uhamishoni. 12:5 Yer 52:7; Amo 4:3Wakiwa wanakutazama, toboa ukuta utolee mizigo yako hapo. 12:6 Isa 8:18; 20:3Beba mizigo hiyo begani mwako wakikuangalia uichukue nje wakati wa giza la jioni. Funika uso wako ili usione nchi, kwa maana nimekufanya ishara kwa nyumba ya Israeli.”

12:7 Eze 24:18; 37:10Basi nikafanya kama nilivyoamriwa. Wakati wa mchana nilitoa vitu vyangu nje vilivyofungwa tayari kwa uhamishoni. Kisha wakati wa jioni nikatoboa ukuta kwa mikono yangu. Nikachukua mizigo yangu nje wakati wa giza la jioni, nikiwa nimeibeba mabegani mwangu huku wakinitazama.

Asubuhi neno la Bwana likanijia kusema: 12:9 Eze 20:49; 24:19; 7:12“Mwanadamu, je, nyumba ile ya kuasi ya Israeli haikukuuliza, ‘Unafanya nini?’

12:10 Mal 1:1“Waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Neno hili linamhusu mkuu aliye katika Yerusalemu na nyumba yote ya Israeli ambao wako huko.’ 12:11 2Fal 25:7; Yer 15:2; Isa 8:18; Zek 3:8; Yer 52:15Waambie, ‘Mimi ndiye ishara kwenu.’

“Kama vile nilivyotenda, basi litatendeka vivyo hivyo kwao. Watakwenda uhamishoni kama mateka.

12:12 Yer 39:4; 52:7“Naye mkuu aliye miongoni mwao atabeba mizigo yake begani mwake kwenye giza la jioni na kuondoka na tundu litatobolewa ukutani kwa ajili yake ili kupitia hapo. Atafunika uso wake ili kwamba asiweze kuiona nchi. 12:13 Ay 19:6; Eze 32:3; Hos 7:12; Isa 24:17-18; Mao 4:20; Yer 39:7; 24:8; Eze 17:20; 19:8; 17:16Nitatandaza wavu wangu kwa ajili yake, naye atanaswa kwenye mtego wangu, nitamleta mpaka Babeli, nchi ya Wakaldayo, lakini hataiona, naye atafia huko. 12:14 Eze 5:10; 2Fal 25:5; Yer 21:7; Eze 17:21Wote wanaomzunguka nitawatawanya pande zote, watumishi wake na majeshi yake yote, nami nitawafuatilia kwa upanga uliofutwa.

12:15 Za 9:16; Eze 6:7, 14; 11:10“Wao watajua kwamba Mimi ndimi Bwana, nitakapowatawanya miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi zote. 12:16 Yer 4:27; 22:8-9; Eze 36:20; 6:8-10; 14:22Lakini nitawaacha wachache wao waokoke na upanga, njaa na tauni, ili kwamba katika mataifa watakakokwenda waweze kutambua matendo ya machukizo waliotenda. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Bwana.”

Neno la Bwana likanijia kusema: 12:18 Mao 5:9; Eze 4:16“Mwanadamu, tetemeka wakati ulapo chakula chako, tetemeka kwa hofu wakati unywapo maji yako. 12:19 Yer 10:22; Zek 7:14; Eze 4:16; 6:6-14; Mik 7:13Waambie watu wa nchi: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kuhusu hao wanaoishi Yerusalemu na katika nchi ya Israeli: Watakula chakula chao kwa wasiwasi na kunywa maji yao kwa kufadhaika, kwa kuwa nchi yao itanyangʼanywa kila kitu chake kwa sababu ya udhalimu wa wote wanaoishi humo. 12:20 Isa 7:23-24; Yer 4:7; 25:9Miji inayokaliwa na watu itaharibiwa na nchi itakuwa ukiwa. Ndipo mtakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana.’ ”

Neno la Bwana likanijia kusema: 12:22 Isa 5:19; 2Pet 3:4; Za 37:13; 49:4; Eze 3:11; Amo 6:3“Mwanadamu, ni nini hii mithali mlio nayo katika nchi ya Israeli: ‘Siku zinapita na hakuna maono yoyote yanayotimia?’ 12:23 Yoe 2:1; Sef 1:14; Eze 7:7; 18:3; Za 37:13Waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitaikomesha mithali hii, nao hawataitumia tena katika Israeli.’ Waambie, ‘Siku zimekaribia wakati kila maono yatakapotimizwa. 12:24 Mik 3:6; Zek 13:2-4; Mao 2:14; Yer 14:14; Eze 13:23Kwa maana hapatakuwepo tena na maono ya uongo wala ubashiri wa udanganyifu miongoni mwa watu wa Israeli. 12:25 Hes 14:28-32; Dan 9:12; Hab 1:5; Hes 11:23; Eze 13:6; Isa 14:24; Yer 15:9Lakini Mimi Bwana nitasema neno nitakalo, nalo litatimizwa bila kuchelewa. Kwa maana katika siku zako, wewe nyumba ya kuasi, nitatimiza kila nisemalo, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

Neno la Bwana likanijia kusema: 12:27 Dan 10:14; Mt 24:48-50; Isa 5:19; Eze 11:3“Mwanadamu, nyumba ya Israeli inasema, ‘Maono yale anayoyaona ni kwa ajili ya miaka mingi ijayo, naye hutabiri kuhusu siku zijazo zilizo mbali.’

“Kwa hiyo, waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Hakuna maneno yangu yatakayocheleweshwa tena zaidi, lolote nisemalo litatimizwa, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

Read More of Ezekieli 12