Ezekieli 1:1-28, Ezekieli 2:1-10, Ezekieli 3:1-27 NEN

Ezekieli 1:1-28

Viumbe Hai Na Utukufu Wa Bwana

1:1 Kum 21:10; Mt 3:16; Eze 11:24-25; Mdo 7:56; Kut 24:10Katika mwaka wa thelathini, mwezi wa nne, siku ya tano ya mwezi, wakati nilipokuwa miongoni mwa hao waliokuwa uhamishoni kando ya Mto Kebari, mbingu zilifunguka nami nikaona maono ya Mungu.

1:2 2Fal 24:15; 24:15; 24:12Katika siku ya tano ya mwezi, ilikuwa mwaka wa tano wa kuhamishwa kwa Mfalme Yehayakini, 1:3 2Fal 3:15; Isa 8:11; 2Pet 1:21; Eze 24:24; 3:14, 22; 33:22neno la Bwana lilimjia Ezekieli kuhani, mwana wa Buzi, kando ya Mto Kebari, katika nchi ya Wakaldayo. Huko mkono wa Bwana ulikuwa juu yake.

1:4 Yer 1:14; 23:19; Eze 8:2; Ay 38:1Nilitazama, nikaona dhoruba kubwa ikitoka kaskazini, wingu kubwa sana pamoja likiwa na umeme wa radi likiwa limezungukwa na mwanga mkali. Katikati ya huo moto kulikuwa kama rangi ya manjano ya chuma kinapokuwa ndani ya moto. 1:5 Isa 6:2; Ufu 4:6; Dan 7:13Katika ule moto kulikuwa na kitu kinachofanana na viumbe vinne vyenye uhai. Katika kuonekana kwake vilikuwa na umbo mfano wa mwanadamu, 1:6 Eze 10:14lakini kila kimoja kilikuwa na nyuso nne na mabawa manne. 1:7 Dan 10:6; Ufu 1:15; Eze 40:3Miguu yao ilikuwa imenyooka, nyayo za miguu yao zilikuwa kama kwato za miguu ya ndama, nazo zilimetameta kama shaba iliyosuguliwa. 1:8 Eze 10:8; 10:18, 21Chini ya mabawa yao katika pande zao nne walikuwa na mikono ya mwanadamu. Wote wanne walikuwa na nyuso na mabawa, 1:9 Eze 10:22; 10:11; 1:11nayo mabawa yao yaligusana. Kila mmoja alikwenda kuelekea mbele moja kwa moja, hawakugeuka walipokuwa wanatembea.

1:10 Eze 10:4; Ufu 4:7; Hes 2:10Kuonekana kwa nyuso zao kulikuwa hivi: Kila mmoja wa wale wanne alikuwa na uso wa mwanadamu na kwa upande wa kulia kila mmoja alikuwa na uso wa simba, upande wa kushoto alikuwa na uso wa ngʼombe pia kila mmoja alikuwa na uso wa tai. 1:11 Isa 6:2Hivyo ndivyo zilivyokuwa nyuso zao. Mabawa yao yalikunjuliwa kuelekea juu, kila mmoja alikuwa na mabawa mawili ambayo kila moja liligusa bawa la mwenzake kila upande na mabawa mengine mawili yakifunika mwili wake. 1:12 Eze 10:16-19; 10:22Kila mmoja alikwenda kuelekea mbele moja kwa moja. Popote roho alipotaka kwenda, ndipo walipokwenda pasipo kugeuka. 1:13 Ufu 4:5; Mt 28:3; 2Sam 22:9Kuonekana kwa vile viumbe hai katikati kulikuwa kama makaa ya mawe yanayowaka au kama mienge. Moto ule ulikuwa ukienda mbele na nyuma katikati ya vile viumbe, ulikuwa na mwangaza mkali na katikati ya ule moto kulitoka kimulimuli kama umeme wa radi. 1:14 Zek 4:10; Za 29:7; Amu 13:20Vile viumbe vilipiga mbio kwenda na kurudi, kama vimulimuli vya umeme wa radi.

1:15 Eze 3:13; 10:2; Dan 7:9Nilipokuwa nikitazama vile viumbe hai, niliona gurudumu moja juu ya ardhi kando ya kila kiumbe kikiwa na nyuso zake nne. 1:16 Dan 10:6; Kut 28:20Hivi ndivyo ilivyokuwa kuonekana kwa hayo magurudumu na muundo wake: yalingʼaa kama zabarajadi, nayo yote manne yalifanana. Kila gurudumu lilikuwa na gurudumu jingine ndani yake. 1:17 Eze 1:12; 1:19Yalipokwenda yalielekea upande wowote wa pande nne walipoelekea wale viumbe, magurudumu hayakuzunguka wakati viumbe vile vilipokwenda. 1:18 Mit 15:3; Eze 10:12; Ufu 4:6Kingo zake zilikuwa ndefu kwenda juu na za kutisha, nazo zote nne zilijawa na macho pande zote.

1:19 Eze 1:16, 17Vile viumbe hai vilipokwenda, magurudumu yaliyokuwa kando yao yalisogea na wakati hivyo viumbe hai vilipoinuka kutoka ardhini magurudumu nayo yaliinuka. 1:20 Eze 1:12; 10:17Mahali popote roho alipokwenda wale viumbe nao walikwenda, nayo magurudumu yaliinuka pamoja navyo, kwa sababu roho ya vile viumbe hai alikuwa ndani ya hayo magurudumu. 1:21 Eze 10:9, 12, 17Wakati viumbe vile viliposogea, nayo magurudumu yalisogea, viumbe viliposimama kimya, nayo pia yalisimama kimya, viumbe vilipoinuka juu ya nchi magurudumu yaliinuliwa pamoja navyo kwa kuwa roho ya hivyo viumbe hai alikuwa ndani ya hayo magurudumu.

1:22 Eze 10:1, 5Juu ya vichwa vya hao viumbe hai palikuwa na kitu mfano wa eneo lililokuwa wazi, lililokuwa angavu kabisa na lenye kutisha. Chini ya hiyo nafasi mabawa yao yalitanda moja kuelekea jingine, kila mmoja alikuwa na mabawa mengine mawili yaliyofunika mwili wake. 1:24 2Fal 7:6; Ufu 14:2; Dan 10:6; Za 18:13; 46:3; Eze 10:5; 43:2; Ufu 19:6Viumbe wale waliposogea nilisikia sauti ya mabawa yao, kama ngurumo ya maji yaendayo kasi, kama sauti ya Mwenyezi,1:24 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania. kama makelele ya jeshi. Waliposimama kimya walishusha mabawa yao.

Ndipo ikaja sauti toka juu ya ile nafasi ya wazi iliyokuwa juu ya vichwa vyao, waliposimama mabawa yao yakiwa yameshushwa. 1:26 Kut 24:10; Eze 10:1; Ufu 1:13; Isa 6:1; 1Fal 22:19; Yer 3:17Juu ya ile nafasi ya wazi iliyokuwa juu ya vichwa vyao kulikuwa na kitu mfano wa kiti cha enzi cha yakuti samawi. Na juu ya kile kiti cha enzi kulikuwa na umbo mfano wa mwanadamu. 1:27 Eze 8:2Nikaona kwamba kutokana na kile nilichoona kama kiuno chake kuelekea juu alionekana kama chuma inayowaka kana kwamba imejaa moto na kuanzia kiuno kwenda chini alionekana kama moto na mwanga mkali ulimzunguka. 1:28 Mwa 9:13; Ufu 10:1; 4:2; 1:17; Hes 12:8; Kut 24:16; Dan 8:17; Hes 14:5; Lk 2:9; Kut 16:7Kama vile kuonekana kwa upinde wa mvua mawinguni siku ya mvua, ndivyo ulivyokuwa ule mngʼao uliomzunguka.

Hivi ndivyo ilivyokuwa kuonekana kwa utukufu wa Bwana. Nilipouona, nikaanguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mtu anaongea.

Read More of Ezekieli 1

Ezekieli 2:1-10

Wito Wa Ezekieli

2:1 Dan 10:11; Mdo 26:16; Ay 25:6; Za 8:4; Eze 1:26; Mdo 9:6; 14:10Akaniambia, “Mwanadamu, simama kwa miguu yako nami nitasema nawe.” 2:2 Eze 3:24; Dan 8:18; Amu 13:25Alipokuwa akiongea nami, Roho akanijia na kunisimamisha wima, nikamsikia akisema nami.

2:3 Yer 3:25; Eze 24:3; 20:8-24Akaniambia: “Mwanadamu, ninakutuma kwa Waisraeli, kwa taifa asi ambalo limeniasi mimi, wao na baba zao wananikosea mimi hadi leo. 2:4 Kut 32:9; Isa 9:9; Eze 3:7; Amo 7:15Watu ambao ninakutuma kwao ni wapotovu na wakaidi. Waambie, ‘Hivi ndivyo anavyosema Bwana Mwenyezi.’ 2:5 Eze 3:11; 3:27; Yn 15:22; Eze 33:33; Yer 5:3Kama watasikiliza au hawatasikiliza, kwa kuwa wao ni nyumba ya kuasi, watajua nabii amekuwa miongoni mwao. 2:6 1Pet 3:14; Yer 1:8, 17; Hes 33:55; Mik 7:4Nawe mwanadamu, usiwaogope wao wala maneno yao, usiogope, ingawa michongoma na miiba vinakuzunguka na unaishi katikati ya nge. Usiogope yale wasemayo wala usitishwe nao, ingawa wao ni nyumba ya uasi. 2:7 Yer 7:27; 42:21; Eze 3:10-11; Mt 28:20Wewe lazima uwaambie maneno yangu, ikiwa wanasikiliza au hawasikilizi, kwa kuwa wao ni watu waasi. 2:8 Isa 8:11; 50:5; Ufu 10:9; Za 81:10; Hes 20:10-13; Yer 15:16Lakini wewe mwanadamu, sikiliza ninalokuambia. Usiwe mwenye kuasi kama hiyo nyumba ya kuasi. Fungua kinywa chako na ule nikupacho.”

2:9 Eze 8:3; Yer 1:9; Za 40:7; Yer 36:4; Ufu 5:1-5; 10:8-10Ndipo nikatazama, nami nikaona mkono ulionyooshwa kunielekea. Nao ulikuwa na ukurasa wa kitabu, 2:10 Isa 3:11; Ufu 8:13ambao aliukunjua mbele yangu. Pande zote mbili ulikuwa umeandikwa maneno ya maombolezo, vilio na ole.

Read More of Ezekieli 2

Ezekieli 3:1-27

3:1 Eze 2:8, 9Naye akaniambia, “Mwanadamu, kula kile kilichoko mbele yako, kula huu ukurasa wa kitabu, kisha uende ukaseme na nyumba ya Israeli.” 3:2 Hes 11:25; Amu 13:25; Neh 9:30Ndipo nikafungua kinywa changu, naye akanilisha ule ukurasa wa kitabu.

3:3 Yer 15:16; Za 19:10; Ufu 10:9-10; Za 19:10Ndipo akaniambia, “Mwanadamu, kula ukurasa huu wa kitabu ninaokupa ujaze tumbo lako.” Kwa hiyo nikaula, ulikuwa mtamu kama asali kinywani mwangu.

Kisha akaniambia, “Mwanadamu, sasa nenda katika nyumba ya Israeli ukaseme nao maneno yangu. 3:5 Isa 28:11; Yn 1:2Hukutumwa kwa taifa lenye maneno ya kutatiza na lugha ngumu, bali kwa nyumba ya Israeli. 3:6 Yn 3:5-10; Mt 11:21-23Sikukutuma kwa mataifa mengi yenye maneno ya kutatiza na lugha ngumu ambao maneno yao hutayaelewa. Hakika ningekutuma kwa watu hao, wangekusikiliza. 3:7 Isa 48:4; Yn 15:20-23; Yer 7:27; Eze 2:4Lakini nyumba ya Israeli haitakusikiliza kwa kuwa hawako radhi kunisikiliza mimi, kwa kuwa nyumba yote ya Israeli ni wenye vipaji vya nyuso vigumu na mioyo ya ukaidi. 3:8 Yer 1:18; 15:20Tazama nimefanya uso wako mgumu dhidi ya nyuso zao na kipaji cha uso wako kigumu dhidi ya vipaji vya nyuso zao. 3:9 Isa 50:7; 48:4; Mik 3:8; Eze 2:6; 4:6; Yer 5:3Kama vile almasi ilivyo ngumu kuliko gumegume, ndivyo nilivyokifanya kipaji cha uso wako. Usiwaogope wala usiwahofu, ijapokuwa ni nyumba ya kuasi.”

3:10 Ay 22:22Naye akaniambia, “Mwanadamu, sikiliza kwa makini na uyatie moyoni mwako maneno yote nitakayosema nawe. 3:11 Eze 43:5; Mdo 8:39; Eze 8:3Kisha nenda kwa watu wa taifa lako walio uhamishoni, ukaseme nao. Waambie, ‘Hivi ndivyo Bwana Mwenyezi asemavyo,’ kwamba watasikiliza au hawatasikiliza.”

3:12 Eze 3:14; 8:3; 43:5Ndipo Roho akaniinua, nikasikia sauti kubwa nyuma yangu ya ngurumo. (Utukufu wa Bwana na utukuzwe katika mahali pa makao yake!) 3:13 Eze 1:24; 10:5, 16-17; 1:15Ilikuwa ni sauti ya mabawa ya wale viumbe hai yakisuguana moja kwa jingine, sauti kama ya ngurumo. 3:14 1Fal 18:12; Isa 8:11; Eze 37:1Ndipo Roho aliponiinua na kunipeleka mbali. Nikaenda nikiwa na uchungu na hasira moyoni mwangu, nao mkono wa Bwana ukiwa juu yangu. 3:15 Mwa 50:10; Ay 2:13Nikafika kwa wale watu waliokuwa uhamishoni huko Tel-Abibu karibu na Mto Kebari. Nikakaa miongoni mwao kwa muda wa siku saba, nikiwa nimejawa na mshangao.

Onyo Kwa Israeli

3:16 Yer 42:7Mwishoni mwa hizo siku saba neno la Bwana likanijia kusema: 3:17 Isa 52:8; Yer 6:17; Wim 5:7; Eze 11:4; Yer 1:17; Isa 58:1“Mwanadamu, nimekufanya uwe mlinzi wa nyumba ya Israeli, kwa hiyo sikia neno nisemalo, ukawape onyo litokalo kwangu. 3:18 Eze 33:6; Rum 1:16; Mwa 2:17; Yn 8:21Nimwambiapo mtu mwovu, ‘Hakika utakufa,’ na wewe usipomwonya mtu huyo au kumshauri aache njia zake mbaya ili kuokoa maisha yake, huyo mtu mwovu atakufa katika dhambi yake na damu yake nitaidai mkononi mwako. 3:19 2Fal 17:13; 1Tim 4:14-16; Za 7:12; Yer 42:16; Eze 14:14-20; Mdo 18:6Lakini ukimwonya mtu mwovu naye akakataa kuacha uovu wake na njia zake mbaya, atakufa katika dhambi yake, lakini wewe utakuwa umejiokoa nafsi yako.

3:20 2Pet 2:20; Za 125:5; Eze 18:24; Yer 34:16; Isa 8:14; Law 26:37“Tena, mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda maovu, nami nikaweka kikwazo mbele yake mtu huyo atakufa. Kwa kuwa hukumwonya, atakufa katika dhambi yake. Mambo ya haki aliyotenda, hayatakumbukwa, damu yake nitaidai mkononi mwako. 3:21 Mdo 20:31; Rum 2:7Lakini ukimwonya mwenye haki asitende dhambi na akaacha kutenda dhambi, hakika ataishi kwa sababu alipokea maonyo na utakuwa umejiokoa nafsi yako.”

3:22 Eze 8:4; Mdo 9:6Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu huko, naye akaniambia, “Simama uende mpaka sehemu tambarare, nami nitasema nawe huko.” 3:23 Mwa 17:3; Eze 1:28Kwa hiyo niliinuka nikaenda mpaka mahali pa tambarare. Utukufu wa Bwana ulikuwa umesimama huko, kama utukufu ule niliouona kando ya Mto Kebari, nami nikaanguka kifudifudi.

3:24 Eze 2:2; Yer 15:17Ndipo Roho akaja ndani yangu akanisimamisha kwa miguu yangu. Akasema nami akaniambia: “Nenda ukajifungie ndani ya nyumba yako. 3:25 Eze 4:8Nawe, ee mwanadamu, watakufunga kwa kamba, watakufunga ili usiweze kutoka na kuwaendea watu. 3:26 Eze 33:22; Hos 4:4; Eze 24:27; Za 22:15; Eze 2:5Nitaufanya ulimi wako ushikamane kwenye kaa la kinywa chako, ili uwe kimya usiweze kuwakemea, wajapokuwa ni nyumba ya kuasi. 3:27 Eze 24:27; 29:21; Ufu 22:11; Eze 12:3; 33:22Lakini nitakaposema nawe, nitafungua kinywa chako nawe utawaambia, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo.’ Yeyote atakayesikiliza na asikilize, na yeyote atakayekataa na akatae; kwa kuwa wao ni nyumba ya kuasi.

Read More of Ezekieli 3