Kutoka 9:1-35, Kutoka 10:1-29 NEN

Kutoka 9:1-35

Pigo La Tano: Vifo Vya Mifugo

9:1 Kut 8:1Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Nenda kwa Farao ukamwambie, ‘Hili ndilo Bwana, Mungu wa Waebrania asemalo: “Waachie watu wangu waende ili wapate kuniabudu.” Kama ukikataa kuwaachia waende, nawe ukiendelea kuwashikilia, 9:3 Kut 7:4; 1Sam 5:6; Ay 13:21; Za 32:4; 39:10; 78:50; Mdo 13:11; Law 26:25; Amo 4:10mkono wa Bwana utaleta pigo baya kwa mifugo yako, juu ya farasi wako, punda, ngamia, ngʼombe wako, kondoo na mbuzi. 9:4 Kut 8:23Lakini Bwana ataweka tofauti kati ya mifugo ya Israeli na ile ya Misri, kwamba hakuna mnyama wa Mwisraeli atakayekufa.’ ”

Bwana akaweka wakati na kusema, “Kesho Bwana atalitenda hili katika nchi.” 9:6 Kut 11:5; 12:29; Za 78:48-50Siku iliyofuata Bwana akalitenda: Mifugo yote ya Wamisri ikafa, lakini hakuna hata mnyama mmoja wa wana wa Israeli aliyekufa. 9:7 Kut 7:14, 22; 8:32Farao akatuma watu kuchunguza, nao wakakuta kuwa hakuna hata mnyama mmoja wa Waisraeli aliyekufa. Lakini moyo wa Farao haukukubali kuwaachia watu waende.

Pigo La Sita: Majipu

Kisha Bwana akamwambia Mose na Aroni, “Chukueni majivu ya tanuru, naye Mose ayarushe angani mbele ya Farao. 9:9 Law 13:18-19; 2Fal 20:7; Ay 2:7; Isa 38:21; Ufu 16:2Yatakuwa vumbi jepesi juu ya nchi yote ya Misri, pia yatatokea majipu yenye kufura juu ya watu na wanyama katika nchi yote.”

Basi wakachukua majivu kwenye tanuru na kusimama mbele ya Farao. Mose akayarusha hewani, nayo majipu yenye kufura yakatokea miilini mwa watu na wanyama. 9:11 Kut 8:18Waganga hawakuweza kusimama mbele ya Mose kwa sababu ya majipu yale yaliyokuwa miilini mwao na juu ya miili ya Wamisri wote. 9:12 Kut 4:21; 7:4Lakini Bwana akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, naye hakuwasikiliza Mose na Aroni, sawasawa kama vile Bwana alivyokuwa amemwambia Mose.

Pigo La Saba: Mvua Ya Mawe

9:13 Kut 3:18Kisha Bwana akamwambia Mose, “Amka mapema asubuhi, usimame mbele ya Farao, umwambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Waebrania: Waachie watu wangu waende, ili kwamba waweze kuniabudu, 9:14 Kut 8:10; 15:11; 1Sam 2:2; 2Sam 7:22; 1Fal 8:23; 1Nya 17:20; Za 35:10; 71:19; 86:8; 89:6; Isa 46:9; Yer 10:6; Mik 7:18au wakati huu nitaleta mapigo yangu yenye nguvu dhidi yako, maafisa wako na watu wako, ili upate kujua kuwa hakuna mwingine kama Mimi katika dunia yote. 9:15 Kut 3:20Kwa kuwa mpaka sasa ningelikuwa nimenyoosha mkono wangu na kukupiga wewe na watu wako kwa pigo ambalo lingekufutilia mbali juu ya nchi. 9:16 Mit 16:4; Kut 14:4, 17, 31; Za 20:6; 25:11; 68:28; 71:18; 106:8; 109:21; Rum 9:17Lakini nimekuinua wewe kwa kusudi hili hasa, ili nipate kukuonyesha uwezo wangu, na ili Jina langu lipate kutangazwa duniani yote. Bado unaendelea kujiinua juu ya watu wangu, wala hutaki kuwaachia waende. 9:18 Yos 10:11; Za 78:47-48; 105:32; 148:8; Isa 30:30; Eze 38:22; Hag 2:17; Kut 9:24; 10:6Kwa hiyo, kesho wakati kama huu nitaleta mvua mbaya sana ya mawe ambayo haijapata kunyesha katika nchi ya Misri, tangu siku ilipoumbwa mpaka leo. Sasa toa amri urudishe wanyama wote watoke malishoni na chochote ambacho kipo mashambani waje mpaka mahali pa usalama, kwa sababu mvua ya mawe itanyesha juu ya kila mtu na kila mnyama ambaye hajaletwa ndani ambao bado wako nje mashambani, nao watakufa.’ ”

9:20 Mit 13:13Wale maafisa wa Farao ambao waliliogopa neno la Bwana wakafanya haraka kuwaleta watumwa wao na mifugo yao ndani. 9:21 Mwa 19:14; Eze 33:4-5Lakini wale waliopuuza neno la Bwana wakawaacha watumwa wao na mifugo yao shambani.

Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Nyoosha mkono wako kuelekea angani ili kwamba mvua ya mawe inyeshe juu ya Misri yote, juu ya watu, wanyama na juu ya kila kitu kiotacho katika mashamba ya Misri.” 9:23 Kut 20:18; 1Sam 12:17; Za 18:13; 29:3; 68:33; 77:17; 104:7; Ufu 8:7; 16:21Mose alipoinyoosha fimbo yake kuelekea angani, Bwana akatuma ngurumo na mvua ya mawe, umeme wa radi ulimulika hadi nchi. Kwa hiyo Bwana akaifanya mvua ya mawe kunyesha juu ya nchi ya Misri, mvua ya mawe ikanyesha na radi ikamulika pote. Ikawa dhoruba ya kutisha ambayo haijakuwako katika nchi ya Misri, tangu nchi hiyo iwe taifa. 9:25 Za 105:32-33; Eze 13:13Mvua ya mawe ikaharibu kila kitu katika nchi ya Misri kilichokuwa katika mashamba, watu na wanyama, ikaharibu kila kitu kinachoota mashambani na kuvunja kila mti. 9:26 Isa 32:18-20; Kut 10:23; 11:7; 12:13; Amo 4:7Mahali pekee ambapo mvua ya mawe haikunyesha ni nchi ya Gosheni, ambako Waisraeli waliishi.

9:27 Kut 10:16; Hes 14:40; Kum 1:41; Yos 7:11; Amu 10:10; 1Sam 15:24; 24:17; 26:21; Za 11:7; 116:5; 119:135; 129:4; 145:17; Yer 12:1; Mao 1:18Ndipo Farao akawaita Mose na Aroni akawaambia, “Wakati huu nimetenda dhambi. Bwana ni mwenye haki, mimi na watu wangu ni wakosaji. 9:28 Kut 8:8; Mdo 8:24Mwombeni Bwana, kwa kuwa tumepata ngurumo na mvua za mawe za kututosha. Nitawaachia mwondoke; hamtahitaji kungoja zaidi.”

9:29 1Fal 8:22; Ay 11:13; Za 77:2; 88:9; 143:6; Isa 1:15; Kut 19:5; Ay 41:11; Za 24:1; 50:12; 1Kor 10:26Mose akamjibu, “Nitakapokuwa nimetoka nje ya mji, nitanyoosha mikono yangu juu kumwomba Bwana. Ngurumo zitakoma na hapatakuwepo mvua ya mawe tena, ili upate kujua kuwa, nchi ni mali ya Bwana. 9:30 Kut 8:29Lakini ninajua kuwa wewe na maafisa wako bado hammwogopi Bwana Mungu.”

9:31 Kum 8:8; Rut 1:22; 2:23; 2Sam 14:30; 17:28; Isa 28:25; Eze 4:9(Kitani na shayiri viliharibiwa, kwa kuwa shayiri ilikuwa na masuke, na kitani ilikuwa katika kutoa maua. 9:32 Isa 28:25Hata hivyo, ngano na jamii nyingine ya ngano hazikuharibiwa kwa sababu zilikuwa hazijakomaa bado.)

Kisha Mose akaondoka kwa Farao akaenda nje ya mji. Mose akanyoosha mikono yake kuelekea kwa Bwana, ngurumo na mvua ya mawe vikakoma, mvua haikuendelea tena kunyesha nchini. Farao alipoona kwamba mvua ya mawe na ngurumo zimekoma, akafanya dhambi tena. Yeye na maafisa wake wakafanya mioyo yao kuwa migumu. 9:35 Kut 4:2Kwa hiyo moyo wa Farao ukawa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waende, kama vile Bwana alivyokuwa amesema kupitia Mose.

Read More of Kutoka 9

Kutoka 10:1-29

Pigo La Nane: Nzige

10:1 Kut 4:21; 3:19; 7:3; Yos 24:17; Neh 9:10; Za 74:9; 105:26-30Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Nenda kwa Farao, kwa kuwa nimeufanya moyo wake kuwa mgumu na mioyo ya maafisa wake ili kwamba nipate kutenda ishara hizi zangu za ajabu miongoni mwao 10:2 Kut 12:26-27; 13:8, 14; Kum 4:9; 6:20; 32:7; Yos 4:6; Za 71:18; 78:4-5; Kut 6:2ili upate kuwaeleza watoto wako na wajukuu wako jinsi nilivyowatendea Wamisri kwa ukali na jinsi nilivyofanya ishara zangu miongoni mwao, nanyi mpate kujua kuwa Mimi ndimi Bwana.”

10:3 1Fal 21:29; 2Fal 22:19; 2Nya 7:14; 12:7; 33:23; 34:27; Ay 42:6; Isa 58:3; Dan 5:22; Yak 4:10; 1Pet 5:6Kwa hiyo Mose na Aroni wakaenda kwa Farao na kumwambia, “Hili ndilo Bwana, Mungu wa Waebrania, asemalo: ‘Utaendelea hata lini kukataa kunyenyekea mbele yangu? Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu. 10:4 Kut 8:2; 9:2; Kum 28:38; Za 105:34; Mit 30:27; Yoe 1:4; Ufu 9:3Kama ukikataa kuwaachia waende, kesho nitaleta nzige katika nchi yako. 10:5 Kut 9:32; Yoe 1:4Nao watafunika uso wa ardhi hata usionekane. Watatafuna mabaki machache yaliyobakizwa baada ya ile mvua ya mawe, yaani pamoja na kila mti unaoota katika mashamba yenu. 10:6 Yoe 2:9; Kut 9:18Nzige hao watajaza nyumba zako, za maafisa wako wote na za Wamisri wote. Jambo ambalo baba zenu wala babu zenu hawajapata kuona tangu siku ile walipoanza kuishi katika nchi hii mpaka leo hii.’ ” Ndipo Mose akageuka na kumwacha Farao.

10:7 Kut 23:33; 34:12; Kum 7:16; 12:30; 20:18; Yos 23:13; Amu 2:3; 8:27; 16:5; 1Sam 18:21; Za 106:36; Mhu 7:26; Mwa 20:3; Kut 8:19Maafisa wa Farao wakamwambia, “Mpaka lini huyu mtu atakuwa tanzi kwetu? Waachie hao watu waende zao, ili wapate kumwabudu Bwana Mungu wao. Je, bado hutambui kuwa Misri imeangamia?”

10:8 Kut 8:8Ndipo Mose na Aroni wakaletwa kwa Farao. Farao akawaambia, “Nendeni, mkamwabudu Bwana Mungu wenu. Lakini ni nani hasa watakaokwenda?”

10:9 Kut 3:18Mose akajibu, “Tutakwenda na vijana wetu na wazee, pamoja na wana wetu na binti zetu, pia pamoja na kondoo zetu, ngʼombe, mbuzi, farasi na punda kwa sababu tutaadhimisha sikukuu kwa Bwana.”

Farao akasema, “Bwana awe pamoja nanyi, kama nikiwaruhusu mwondoke pamoja na wanawake wenu na watoto wenu! Ni wazi kwamba mna makusudi mabaya. La hasha! Wanaume peke yao na waende, wakamwabudu Bwana, kwa kuwa hilo ndilo mmekuwa mkiomba.” Kwa hiyo Mose na Aroni wakaondolewa mbele ya Farao.

10:12 Kut 7:19Basi Bwana akamwambia Mose, “Nyoosha mkono wako juu ya Misri ili kundi la nzige liweze kuingia juu ya nchi na kutafuna kila kitu kiotacho katika mashamba na kila kitu kilichosazwa na ile mvua ya mawe.”

10:13 Kut 4:17; 8:5, 17; 9:23; 14:15-16, 26-27; 17:5; Hes 20:8; 1Fal 8:37; Za 78:46; 105:34; Amo 4:9; Nah 3:16Kwa hiyo Mose akanyoosha fimbo yake juu ya Misri, Bwana akauleta upepo wa mashariki ukavuma katika nchi yote mchana wote na usiku kucha, kufikia asubuhi upepo ukawa umeleta nzige. 10:14 Kum 28:38; Za 78:45; Isa 33:4; Yoe 1:4; 2:1-11, 25; Amo 4:9Wakaivamia Misri yote na kukaa kila eneo la nchi kwa wingi. Kamwe hapajapata kuwepo pigo la nzige kama hilo, wala halitakuwepo tena. 10:15 Kum 28:38; Za 105:34-35; Yoe 1:4; Amo 7:2; Mal 3:11Wakafunika ardhi yote mpaka ardhi ikawa nyeusi. Wakatafuna kile chote kilichokuwa kimebakizwa na ile mvua ya mawe, kila kitu kiotacho mashambani pamoja na matunda kwenye miti. Hakuna kitu chochote cha kijani kilichosalia katika miti au mmea katika nchi yote ya Misri.

10:16 Kut 8:25; 9:27Farao akawaita Mose na Aroni kwa haraka na kuwaambia, “Nimetenda dhambi dhidi ya Bwana Mungu wenu na dhidi yenu pia. 10:17 1Sam 15:25; Kut 8:8Sasa unisamehe dhambi yangu mara moja tena na umwombe Bwana Mungu wako aondoe pigo hili baya kwangu.”

10:18 Kut 8:30Kisha Mose akaondoka kwa Farao akamwomba Bwana. Naye Bwana akaugeuza upepo ukavuma kutoka magharibi, wenye nguvu nyingi, ambao uliwaondoa wale nzige na kuwapeleka kwenye Bahari ya Shamu. Hakuna nzige hata mmoja aliyebaki popote katika nchi ya Misri. 10:20 Kut 4:21; 11:10Lakini Bwana akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waondoke.

Pigo La Tisa: Giza

10:21 Kum 28:29Kisha Bwana akamwambia Mose, “Nyoosha mkono wako kuelekea angani ili giza litande katika nchi ya Misri, giza ambalo watu wanaweza kulipapasa na kulihisi.” 10:22 Za 105:28; Isa 13:10; 45:7; 50:3; Ufu 16:10Kwa hiyo Mose akaunyoosha mkono wake kuelekea angani, na giza nene likafunika pote katika nchi ya Misri kwa muda wa siku tatu. 10:23 Kut 8:22; Amo 4:7Hakuna mtu yeyote aliyeweza kumwona mwenzake, wala kuondoka mahali alipokuwa kwa muda wa siku tatu. Lakini Waisraeli wote walikuwa na mwanga katika maeneo yao waliyokuwa wanaishi.

10:24 Kut 8:8; Mwa 45:10Ndipo Farao akamwita Mose na kusema, “Nendeni, mkamwabudu Bwana. Hata wanawake na watoto wenu mwaweza kwenda nao pia, lakini kondoo, mbuzi na ngʼombe wenu waacheni.”

10:25 Mwa 8:20; Kut 18:12Lakini Mose akasema, “Huna budi kuturuhusu tuwe na dhabihu na sadaka za kuteketezwa za kutoa mbele za Bwana Mungu wetu. Sisi ni lazima tuondoke na mifugo yetu pia, wala hakuna ukwato utakaoachwa nyuma. Inatupasa kutumia baadhi ya hiyo mifugo katika kumwabudu Bwana Mungu wetu, kwa kuwa mpaka tutakapofika huko hatutakuwa tumefahamu ni nini tutakachotumia katika kumwabudu Bwana.”

10:27 Kut 4:21; 10:20Lakini Bwana akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, hakuwa radhi kuwaachia waondoke. Farao akamwambia Mose, “Ondoka mbele yangu! Hakikisha kuwa hutakuja mbele yangu tena! Siku ile utakapouona uso wangu utakufa.”

10:29 Kut 11:8; Ebr 11:27Mose akamjibu, “Iwe kama ulivyosema! Kamwe sitauona uso wako tena.”

Read More of Kutoka 10