Kutoka 6:13-30, Kutoka 7:1-25, Kutoka 8:1-32 NEN

Kutoka 6:13-30

Orodha Ya Jamaa Ya Mose Na Aroni

6:13 Kut 3:10Ndipo Bwana akanena na Mose na Aroni kuhusu Waisraeli na Farao mfalme wa Misri, naye akawaamuru wawatoe Waisraeli kutoka Misri.

6:14 Kut 13:3; Hes 1:1; 26:4; Mwa 29:32Hawa walikuwa wakuu wa jamaa zao:

Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli walikuwa Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi. Hawa walikuwa ndio koo za Reubeni.

6:15 Mwa 29:33Wana wa Simeoni walikuwa Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli mwana wa mwanamke Mkanaani. Hawa walikuwa ndio koo za Simeoni.

6:16 Mwa 29:34; 46:11; Hes 3:17; Yos 21:7; 1Nya 6:1, 16Haya ndiyo majina ya wana wa Lawi kufuatana na orodha zao: Gershoni, Kohathi na Merari. Lawi aliishi miaka 137.

6:17 Hes 3:18; 1Nya 6:17Wana wa Gershoni kwa koo, walikuwa Libni na Shimei.

6:18 Hes 3:19, 27; 1Nya 6:18; 23:12Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. Kohathi aliishi miaka 133.

6:19 1Nya 6:19; 23:21; Hes 3:20, 33Wana wa Merari walikuwa Mahli na Mushi.

Hizi ndizo zilizokuwa koo za Lawi kufuatana na orodha zao.

6:20 Kut 2:1-2; 1Nya 23:13; Hes 26:59Amramu akamwoa Yokebedi, shangazi yake, ambaye alimzalia Aroni na Mose. Amramu aliishi miaka 137.

6:21 1Nya 6:38Wana wa Ishari walikuwa Kora, Nefegi na Zikri.

6:22 Law 10:4; Hes 3:30; 2Nya 29:13Wana wa Uzieli walikuwa Mishaeli, Elisafani na Sithri.

6:23 Rut 4:19-20; 1Nya 2:10; 6:3; 24:1; Hes 2:3; 3:2, 32; 4:28; 16:37-39; 26:60; Kum 10:6; Kut 24:1; Law 10:1-6; 10:12-16Aroni akamwoa Elisheba binti wa Aminadabu ndugu yake Nashoni, naye akamzalia Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

6:24 Hes 16:1; 1Nya 6:22, 37Wana wa Kora walikuwa Asiri, Elikana na Abiasafu. Hawa walikuwa ndio koo za Kora.

6:25 Hes 25:7; 31:6; Yos 24:33; Za 106:30Eleazari mwana wa Aroni akamwoa mmoja wa binti za Putieli, naye akamzalia Finehasi.

Hawa walikuwa ndio wakuu wa jamaa za Walawi, ukoo kwa ukoo.

6:26 Kut 3:10; 7:4; 12:17, 41, 51Hawa walikuwa Aroni na Mose wale wale ambao Bwana aliwaambia, “Watoeni Waisraeli katika nchi ya Misri kwa vikosi vyao.” Ndio hao hao waliozungumza na Farao mfalme wa Misri kuhusu kuwatoa Waisraeli Misri. Ilikuwa ni huyo Mose na huyo Aroni.

Aroni Kuzungumza Badala Ya Mose

Bwana aliponena na Mose huko Misri, akamwambia, “Mimi ndimi Bwana. Mwambie Farao mfalme wa Misri kila kitu nikuambiacho.”

6:30 Kut 3:11Lakini Mose akamwambia Bwana, “Kwa kuwa mimi huzungumza kwa kigugumizi, Farao atanisikiliza mimi?”

Read More of Kutoka 6

Kutoka 7:1-25

7:1 Kut 4:15, 16; Mdo 14:12Kisha Bwana akamwambia Mose, “Tazama, nimekufanya kuwa kama Mungu kwa Farao, naye Aroni, huyo ndugu yako, atakuwa nabii wako. Utasema kila kitu nitakachokuagiza, naye Aroni ndugu yako atamwambia Farao awaachie Waisraeli watoke katika nchi yake. 7:3 Kut 3:20; 4:21; Rum 9:18; Mdo 7:36Lakini nitaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu. Ingawa nitazidisha ishara na maajabu katika Misri, 7:4 Kut 3:20; 6:26; 8:15-19; 9:12; 11:9; Mdo 7:36hatawasikiliza. Kisha nitaupeleka mkono wangu juu ya Misri, na kwa matendo makuu ya hukumu nitavitoa vikundi vyangu, watu wangu Waisraeli. 7:5 Kut 3:20; 6:2; Za 138:7; Eze 6:14; 25:13Nao Wamisri watajua kuwa Mimi ndimi Bwana nitakapounyoosha mkono wangu dhidi ya Misri na kuwatoa Waisraeli watoke humo.”

7:6 Mwa 6:22Mose na Aroni wakafanya sawasawa kama vile Bwana alivyowaagiza. 7:7 Kum 31:2; 34:7; Mdo 7:23-30Mose alikuwa na umri wa miaka themanini na Aroni alikuwa na umri wa miaka themanini na mitatu walipozungumza na Farao.

Fimbo Ya Aroni Yawa Nyoka

Bwana akamwambia Mose na Aroni, 7:9 Kum 6:22; 2Fal 19:29; Za 78:43; 105:27; Isa 7:11; 37:30; 38:7-8; 55:13; Yn 2:11; Kut 4:2-5“Farao atakapowaambia, ‘Fanyeni muujiza,’ basi mwambie Aroni, ‘Chukua fimbo yako na uitupe chini mbele ya Farao,’ nayo fimbo itakuwa nyoka.”

Ndipo Mose na Aroni wakaenda kwa Farao wakafanya sawasawa kama vile Bwana alivyoagiza. Aroni akaitupa ile fimbo yake chini mbele ya Farao na maafisa wake, nayo ikawa nyoka. 7:11 Kut 22:18; Kum 18:10; 1Sam 6:12; 2Fal 21:6; Isa 2:6; 47:12; Yer 27:9; Mal 3:5; Mwa 41:8; 2Tim 3:8; Mt 24:24Farao naye akawaita watu wenye maarifa na wachawi na waganga wa Kimisri, nao wakafanya vivyo hivyo kwa siri ya uganga wao. Kila mmoja alitupa fimbo yake chini, nayo ikawa nyoka. Lakini fimbo ya Aroni ikazimeza zile fimbo zao. 7:13 Kut 4:21Hata hivyo moyo wa Farao ukawa mgumu, naye hakuwasikiliza Mose na Aroni, sawasawa kama vile Bwana alivyokuwa amesema.

Pigo La Kwanza: Damu

7:14 Kut 7:22; 9:7; 10:20-27; 8:15, 32Kisha Bwana akamwambia Mose, “Moyo wa Farao ni mgumu, anakataa kuwaachia watu kuondoka. Nenda kwa Farao asubuhi wakati anapokwenda mtoni. Ngoja ukingoni mwa Naili ili uonane naye, na uchukue mkononi mwako fimbo ile iliyobadilishwa kuwa nyoka. 7:16 Kut 3:18Kisha umwambie, ‘Bwana, Mungu wa Waebrania, amenituma nikuambie: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu jangwani. Lakini hadi sasa hujasikiliza. 7:17 Kut 4:9; 6:2; 14:25; Ufu 11:6; 16:4Hili ndilo Bwana asemalo: Kwa hili utajua kuwa Mimi ndimi Bwana: Fimbo iliyo mkononi mwangu nitapiga nayo maji ya Naili nayo yatabadilika kuwa damu. 7:18 Isa 19:6; Za 78:44Samaki waliomo katika Mto Naili watakufa, nao mto utanuka vibaya, Wamisri hawataweza kunywa hayo maji yake.’ ”

7:19 Kut 4:2; 14:21; 2Fal 5:11Bwana akamwambia Mose, “Mwambie Aroni, ‘Chukua ile fimbo yako unyooshe mkono wako juu ya maji ya Misri, juu ya chemchemi na mifereji, juu ya madimbwi na mabwawa yote,’ navyo vitabadilika kuwa damu. Damu itakuwa kila mahali katika Misri, hata kwenye vyombo vya miti na vya mawe.”

7:20 Kut 17:5; Za 78:44; 105:29; 114:3; Hab 3:8Mose na Aroni wakafanya kama vile Bwana alivyokuwa amewaagiza. Akainua fimbo yake machoni pa Farao na maafisa wake na kuyapiga maji ya Mto Naili, na maji yote yakabadilika kuwa damu. Samaki katika Mto Naili wakafa, nao mto ukanuka vibaya sana kiasi kwamba Wamisri hawakuweza kunywa maji yake. Damu ilikuwa kila mahali katika nchi ya Misri.

7:22 Mwa 41:8; Mt 24:24; Kut 8:19; Za 105:28Lakini waganga wa Misri kwa kutumia siri ya uganga wao wakafanya vivyo hivyo, nao moyo wa Farao ukawa mgumu, hakuwasikiliza Mose na Aroni, kama vile Bwana alivyokuwa amesema. Badala yake, Farao akageuka, akaenda kwenye jumba lake la kifalme, wala hakulitia hili moyoni. Nao Wamisri wote wakachimba kandokando ya Mto Naili kupata maji ya kunywa, kwa sababu hawakuweza kunywa maji ya mto.

Pigo La Pili: Vyura

Zilipita siku saba baada ya Bwana kuyapiga maji ya Mto Naili.

Read More of Kutoka 7

Kutoka 8:1-32

8:1 Kut 3:12; 4:23; 5:1; 9:1Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Nenda kwa Farao ukamwambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu. 8:2 Za 78:45; 105:30; Ufu 16:13Kama ukikataa kuwaruhusu kuondoka, basi nitaipiga nchi yako yote kwa kuwaletea vyura. 8:3 Kut 10:6; 12:34Mto Naili utafurika vyura. Watakuja kwenye jumba lako la kifalme na katika chumba chako cha kulala na kitandani mwako, katika nyumba za maafisa wako na kwa watu wako, vyura hao wataingia katika meko yenu na kwenye vyombo vya kukandia unga. Vyura watapanda juu yako, juu ya watu wako na maafisa wako wote.’ ”

8:5 Kut 4:2, 17; 7:9-23; 10:13, 21-22; 14:27Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Mwambie Aroni, ‘Nyoosha mkono wako ukiwa na ile fimbo yako juu ya vijito, mifereji na madimbwi, fanya vyura waje juu ya nchi ya Misri.’ ”

8:6 Za 78:45; 105:30Ndipo Aroni akaunyoosha mkono wake juu ya maji ya Misri, nao vyura wakatokea na kuifunika nchi. 8:7 Kut 7:11; Mt 24:24Lakini waganga wakafanya vivyo hivyo kwa siri ya uganga wao, nao pia wakafanya vyura kuja juu ya nchi ya Misri.

8:8 Kut 9:28; 10:8, 17; Hes 21:7; 1Sam 12:19; 1Fal 13:6; Yer 42:2; Mdo 8:24Ndipo Farao akamwita Mose na Aroni na kusema, “Mwombeni Bwana awaondoe vyura kutoka kwangu na kwa watu wangu, nami nitawaachia watu wenu waende kumtolea Bwana dhabihu.”

8:9 Kut 9:5Mose akamwambia Farao, “Ninakupa heshima ya kuamua ni wakati gani wa kukuombea wewe, maafisa wako na watu wako ili kwamba vyura watoke kwenu na kwenye nyumba zenu. Isipokuwa wale walio katika Mto Naili.”

8:10 Kut 9:14; 15:11; Kum 3:24; 4:35; 33:26; 2Sam 7:22; 1Fal 8:23; 1Nya 17:20; 2Nya 6:14; Za 71:19; 86:8; 89:6; Isa 40:18; 42:8; 46:9; Yer 49:19; Mik 7:18Farao akasema, “Kesho.”

Mose akamjibu, “Itakuwa kama unavyosema, ili upate kujua kwamba hakuna yeyote kama Bwana Mungu wetu. Vyura wataondoka kwako na katika nyumba zako, kwa maafisa wako na kwa watu wako, ila watabakia katika Mto Naili tu.”

Baada ya Mose na Aroni kuondoka kwa Farao, Mose akamlilia Bwana kuhusu vyura aliokuwa amewaleta kwa Farao. 8:13 Yak 5:16-18Naye Bwana akafanya lile Mose alilomwomba. Vyura wakafia ndani ya nyumba, viwanjani na mashambani. Wakayakusanya malundo, nchi nzima ikanuka. 8:15 Mhu 8:11; Kut 7:14Lakini Farao alipoona pametokea nafuu, akaushupaza moyo wake na hakuwasikiliza Mose na Aroni, kama vile Bwana alivyokuwa amesema.

Pigo La Tatu: Viroboto

8:16 Kut 4:2Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Mwambie Aroni, ‘Nyoosha fimbo yako uyapige mavumbi ya ardhi,’ nayo nchi yote ya Misri mavumbi yatakuwa viroboto.” 8:17 Za 105:31Wakafanya hivyo, Aroni aliponyoosha mkono wake wenye fimbo na kuyapiga mavumbi ya nchi, viroboto wakawajia watu na wanyama. Mavumbi yote katika nchi ya Misri yakawa viroboto. 8:18 Kut 7:11; 9:11; Dan 5:8Lakini waganga walipojaribu kutengeneza viroboto kwa siri ya uganga wao, hawakuweza. Nao viroboto walikuwa juu ya watu na wanyama.

8:19 Kut 7:5, 13-15; 10:7; 12:33; 31:18; 1Sam 6:9; Neh 9:6; Za 8:3; 33:6; Lk 11:20Waganga wale wakamwambia Farao, “Hiki ni kidole cha Mungu.” Lakini moyo wa Farao ukawa mgumu naye hakuwasikiliza, kama vile Bwana alivyosema.

Pigo La Nne: Mainzi

8:20 Kut 7:15; 9:13; 3:18Kisha Bwana akamwambia Mose, “Amka mapema asubuhi na usimame mbele ya Farao wakati anapokwenda mtoni nawe umwambie, ‘Hili ndilo Bwana asemalo: Waachie watu wangu waende, ili wapate kuniabudu. Kama hutawaachia watu wangu waondoke nitakupelekea makundi ya mainzi juu yako, kwa maafisa wako, kwa watu wako na kwenye nyumba zenu. Nyumba za Wamisri zitajazwa mainzi, hata na ardhi yote ya Misri.

8:22 Mwa 45:10; Kut 7:5; 9:4-6, 26, 29; 10:23; 11:7; 12:13; 19:5; Kum 4:20; 7:6; 14:2; 26:18; 1Fal 8:36; Ay 36:11; Za 33:12; 135:4; Mal 3:17“ ‘Lakini siku ile nitafanya kitu tofauti katika nchi ya Gosheni, ambapo watu wangu wanaishi, hapatakuwepo na makundi ya mainzi, ili mpate kujua kwamba Mimi, Bwana, niko katika nchi hii. 8:23 Kut 9:4-6; 10:23; 11:7; 12:23-27Nitaweka tofauti kati ya watu wangu na watu wenu. Ishara hii ya ajabu itatokea kesho.’ ”

8:24 Za 78:45; 105:31Naye Bwana akafanya hivyo. Makundi makubwa ya mainzi yalimiminika katika jumba la kifalme la Farao na katika nyumba za maafisa wake, pia nchi yote ya Misri ikaharibiwa na mainzi.

8:25 Kut 9:27; 10:16; 12:31Ndipo Farao akamwita Mose na Aroni na kuwaambia, “Nendeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu katika nchi hii.”

8:26 Mwa 43:32Lakini Mose akamwambia, “Hilo halitakuwa sawa. Dhabihu tutakazomtolea Bwana Mungu wetu zitakuwa chukizo kwa Wamisri. Kama tukitoa dhabihu ambazo ni chukizo mbele yao, je, hawatatupiga mawe? 8:27 Mwa 30:36; Kut 3:18Ni lazima twende mwendo wa siku tatu mpaka tufike jangwani ili tumtolee Bwana Mungu wetu dhabihu, kama alivyotuagiza.”

8:28 Yer 37:3; Mdo 8:24Farao akamwambia, “Nitawaruhusu mwende kumtolea Bwana Mungu wenu dhabihu huko jangwani, lakini hamna ruhusa kwenda mbali sana. Sasa mniombee.”

8:29 Kut 9:30; 10:11; Isa 26:10Mose akajibu, “Mara tu nitakapoondoka, nitamwomba Bwana na kesho mainzi yataondoka kwa Farao, kwa maafisa wake na kwa watu wake. Hakikisha tu kwamba Farao hatatenda kwa udanganyifu tena kwa kutokuwaachia watu waende kumtolea Bwana dhabihu.”

8:30 Kut 9:33; 10:18Ndipo Mose akamwacha Farao na kumwomba Bwana, naye Bwana akafanya lile Mose alilomwomba. Mainzi yakaondoka kwa Farao, kwa maafisa wake na kwa watu wake, wala hakuna hata inzi aliyebakia. 8:32 Kut 7:14Lakini wakati huu pia Farao akaushupaza moyo wake, wala hakuwaruhusu Waisraeli waondoke.

Read More of Kutoka 8