Kutoka 4:1-31, Kutoka 5:1-23, Kutoka 6:1-12 NEN

Kutoka 4:1-31

Ishara Za Mose

4:1 Kut 3:18Mose akamjibu, “Itakuwaje kama hawataniamini au kunisikiliza, waseme, ‘Bwana hakukutokea’?”

4:2 Mwa 38:18; Kut 7:19; 8:5; 14:16, 21; 17:5-9; Hes 17:2; 20:8; Yos 8:18; Amu 6:21; 1Sam 14:27; 2Fal 4:29Ndipo Bwana akamwambia, “Ni nini hicho kilicho mkononi mwako?”

Akajibu, “Fimbo.”

4:3 Kut 7:8-15Bwana akasema, “Itupe chini.”

Mose akaitupa chini hiyo fimbo nayo ikawa nyoka, naye akaikimbia. Kisha Bwana akamwambia, “Nyoosha mkono wako umkamate mkiani.” Basi Mose akanyoosha mkono akamkamata yule nyoka, naye akabadilika tena kuwa fimbo mkononi mwake. 4:5 Kut 3:6; 14:31; 19:9Bwana akasema, “Hivi ndivyo Waisraeli watakavyoamini kuwa Bwana, Mungu wa baba zao, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo, amekutokea wewe.”

4:6 Law 13:2, 11; Hes 12:10; Kum 24:9; 2Fal 5:1; 2Nya 26:21Kisha Bwana akamwambia, “Weka mkono wako ndani ya joho lako.” Basi Mose akaweka mkono wake ndani ya joho lake, naye alipoutoa, ulikuwa na ukoma, mweupe kama theluji.

4:7 2Fal 5:14; Mt 8:3; Lk 17:12-14Mungu akamwambia, “Sasa urudishe tena huo mkono ndani ya joho lako.” Basi Mose akaurudisha mkono wake ndani ya joho lake na alipoutoa, ulikuwa mzima, kama sehemu zingine za mwili wake.

4:8 Kut 3:8; Amu 6:17; 1Fal 3:3; Isa 7:14; Yer 44:28-29Ndipo Bwana akamwambia, “Kama hawatakuamini wewe, au kutojali ishara ya kwanza, wataamini ishara ya pili. 4:9 Kut 7:17-21Lakini kama hawataamini ishara hizi mbili au hawatawasikiliza ninyi, chukua kiasi cha maji kutoka Mto Naili uyamimine juu ya ardhi kavu. Maji mtakayotoa mtoni yatakuwa damu juu ya ardhi.”

4:10 Kut 3:11Mose akamwambia Bwana, “Ee Bwana, kamwe sijapata kuwa msemaji kwa ufasaha wakati uliopita wala tangu ulipoanza kuzungumza na mtumishi wako. Ulimi wangu ni mzito kuzungumza.”

4:11 Kut 3:11; Lk 1:20, 64; Za 94:9; Mt 11:5; Yn 10:21Bwana akamwambia, “Ni nani aliyempa mwanadamu kinywa? Ni nani aliyemfanya mtu kuwa kiziwi au bubu? Ni nani anayempa mtu kuona au upofu? Je, si mimi, Bwana? 4:12 Kut 3:10; Hes 23:5; Kum 18:15-18; Isa 50:4; 51:16; Mt 10:19-20; Mk 13:11; Lk 12:12Sasa nenda, nitakusaidia kusema, nami nitakufundisha jambo la kusema.”

4:13 Yon 1:1-3Lakini Mose akasema, “Ee Bwana, tafadhali mtume mtu mwingine kufanya kazi hiyo.”

4:14 Hes 11:1; 12:9; 16:15; 22:22; 24:10; 32:13; Kum 7:25; Ay 17:8; Yos 7:1; 1Sam 10:2-5Ndipo hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Mose, akamwambia, “Vipi kuhusu ndugu yako, Aroni Mlawi? Ninajua yeye anaweza kuzungumza vizuri. Naye yuko tayari njiani kukulaki, na moyo wake utafurahi wakati atakapokuona. 4:15 Hes 23:5, 12-16; Kum 18:18; Isa 51:16; 59:21; Yer 1:9; 31:33Utazungumza naye na kuweka maneno kinywani mwake. Nitawasaidia ninyi wawili kusema, nami nitawafundisha jambo la kufanya. 4:16 Kut 7:1-2; Yer 15:19; 36:6; Hes 33:1; Za 77:20; 105:26; Mik 6:4Aroni ataongea na watu badala yako na itakuwa kwamba yeye amekuwa kinywa chako nawe utakuwa kama Mungu kwake. 4:17 Kut 7:9-21; 8:5; 9:22; 10:12-15, 21-23; 14:15-26; 17:6; Hes 14:11; Kum 4:34; Za 74:9; 78:43; 105:27Lakini chukua fimbo hii mkononi mwako ili uweze kuitumia kufanya ishara hizo za ajabu.”

Mose Anarudi Misri

Kisha Mose akarudi kwa Yethro mkwewe akamwambia, “Niruhusu nirudi kwa watu wangu Misri kuona kama yuko hata mmoja wao ambaye bado anaishi.”

Yethro akamwambia, “Nenda, nami nakutakia mema.”

4:19 Kut 2:15, 23; Mt 2:20Basi Bwana alikuwa amemwambia Mose huko Midiani, “Rudi Misri kwa maana watu wote waliotaka kukuua wamekufa.” 4:20 Kut 2:22; 18:3; Mdo 7:29Basi Mose akamchukua mkewe na wanawe, akawapandisha juu ya punda na kuanza safari kurudi Misri. Naye akaichukua ile fimbo ya Mungu mkononi mwake.

4:21 Kut 3:19, 20; 7:3, 13; 8:15, 32; 9:12, 17, 35; 10:20-27; 11:10; 14:4, 8; Kum 2:30; Yos 11:20; Za 105:25; Isa 6:10; 63:17; Yn 12:40; Rum 9:18Bwana akamwambia Mose, “Utakaporudi Misri, hakikisha kwamba utafanya mbele ya Farao maajabu yote niliyokupa uwezo wa kuyafanya. Lakini nitafanya moyo wake kuwa mgumu ili kwamba asiwaruhusu watu waende. 4:22 Mwa 10:15; Kum 32:6; Isa 9:6; 63:16; 64:8; Yer 3:19; 31:9; Hos 11:1; Mal 2:10; Rum 9:4; 2Kor 6:18Kisha mwambie Farao, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Israeli ni mwanangu mzaliwa wa kwanza, 4:23 Kut 3:18; 5:1; 7:16; 11:5; 12:12, 29; Mwa 49:3; Hes 8:17; 33:4; Za 78:51; 105:36; 135:8; 136:10nami nilikuambia, “Ruhusu mwanangu aondoke, ili aweze kuniabudu mimi.” Lakini ukakataa kumruhusu kwenda, basi nitaua mwana wako mzaliwa wa kwanza.’ ”

4:24 Hes 22:22Mose alipokuwa mahali pa kulala wageni akiwa njiani kurudi Misri, Bwana akakutana naye, akataka kumuua. 4:25 Kut 2:21; Mwa 17:14; Yos 5:2-3Lakini Sipora akachukua jiwe gumu, akakata govi la mwanawe na kugusa nalo miguu ya Mose. Sipora akasema, “Hakika wewe ni bwana arusi wa damu kwangu.” Sipora alipomwita Mose, “Bwana arusi wa damu,” alikuwa anamaanisha ile tohara. Baada ya hayo Bwana akamwacha.

4:27 Kut 3:1; Mwa 27:27; 29:13Bwana akamwambia Aroni, “Nenda jangwani ukamlaki Mose.” Basi akakutana na Mose kwenye mlima wa Mungu, akambusu. Kisha Mose akamwambia Aroni kila kitu Bwana alichomtuma kusema, vilevile habari za ishara na maajabu alizokuwa amemwamuru kufanya.

4:29 Kut 3:16Mose na Aroni wakawakusanya wazee wote wa Waisraeli, naye Aroni akawaambia kila kitu Bwana alichokuwa amemwambia Mose. Pia akafanya ishara mbele ya watu, 4:31 Kut 2:25; 3:18; Mwa 16:11; 24:26nao wakaamini. Nao waliposikia kuwa Bwana anajishughulisha nao, na kwamba ameona mateso yao, walisujudu na kuabudu.

Read More of Kutoka 4

Kutoka 5:1-23

Matofali Bila Nyasi

5:1 Kut 3:18; 4:23Baadaye Mose na Aroni wakaenda kwa Farao, wakamwambia, “Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: ‘Waruhusu watu wangu waende, ili waweze kunifanyia sikukuu huko jangwani.’ ”

5:2 Amu 2:10; Ay 21:15; Mal 3:14; Kut 3:19Farao akasema, “Huyo Bwana ni nani, hata nimtii na kuruhusu Israeli uende? Simjui huyo Bwana wala sitawaruhusu Israeli waende.”

5:3 Mwa 30:36; Law 26:25; Hes 14:12; Kum 28:21; 2Sam 24:13Ndipo Mose na Aroni wakasema, “Mungu wa Waebrania amekutana nasi. Sasa turuhusu tuwe na safari ya siku tatu ya jangwani ili tukamtolee Bwana Mungu wetu dhabihu, la sivyo aweza kutupiga sisi kwa tauni au kwa upanga.”

5:4 Kut 1:11; 6:6-7Lakini mfalme wa Misri akasema, “Mbona ninyi Mose na Aroni mnawachukua watu waache kazi zao? Rudini kwenye kazi zenu!” 5:5 Mwa 12:2Kisha Farao akasema, “Tazama, sasa watu hawa ni wengi, nanyi mnawazuia kufanya kazi.”

5:6 Mwa 15:13Siku iyo hiyo Farao akatoa amri hii kwa viongozi wa watumwa na wasimamizi wa watu akawaambia: 5:7 Mwa 11:3“Tangu sasa msiwape hawa watu nyasi za kutengenezea matofali. Wao wakusanye nyasi zao wenyewe. 5:8 Kut 10:11Lakini watakeni kutengeneza matofali kiasi kile kile cha mwanzo, kiwango kisipunguzwe. Wao ni wavivu, ndiyo sababu wanalia, wakisema, ‘Turuhusiwe twende kumtolea Mungu wetu dhabihu.’ Fanyeni kazi kuwa ngumu zaidi kwa watu hao ili kwamba wakazane na kazi na kuacha kusikiliza uongo.”

Basi viongozi wa watumwa na wasimamizi wakaenda kuwaambia watu, “Hivi ndivyo Farao asemavyo: ‘Sitawapa tena nyasi. Nendeni mkatafute nyasi wenyewe popote mnapoweza kuzipata, lakini kazi yenu haitapunguzwa hata kidogo.’ ” Basi watu wakatawanyika kote nchini Misri kukusanya mabua ya kutumia badala ya nyasi. Viongozi wa watumwa wakasisitiza, wakisema, “Timizeni kazi mnayotakiwa kwa kila siku, kama wakati ule mlipokuwa mkipewa nyasi.” 5:14 Isa 10:24Wasimamizi wa Kiisraeli waliochaguliwa na viongozi wa watumwa wa Farao walipigwa na kuulizwa, “Kwa nini hamkutimiza kiwango chenu cha kutengeneza matofali jana na leo, kama mwanzoni?”

Ndipo wasimamizi wa Kiisraeli wakaenda kumlilia Farao, wakisema: “Mbona umewatendea watumishi wako hivi? Watumishi wako hawapewi nyasi, hata hivyo tumeambiwa, ‘Tengenezeni matofali!’ Watumishi wako wanapigwa, lakini kosa ni la watu wako wenyewe.”

Farao akasema, “Ninyi ni wavivu ndiyo sababu mnasema, ‘Turuhusu twende tukamtolee Bwana dhabihu.’ 5:18 Mwa 15:13Sasa nendeni kazini. Hamtapewa nyasi zozote, nanyi ni lazima mtengeneze matofali.”

Wasimamizi wa Kiisraeli walitambua kuwa wako taabani walipoambiwa, “Hamtakiwi kupunguza idadi ya matofali mliotakiwa kutengeneza kila siku.” Walipoondoka kwa Farao, wakawakuta Mose na Aroni wakingojea kukutana nao, 5:21 Mwa 34:30; 16:5; Kut 1:13; 14:11; 16:3; Hes 14:3; 20:3wakawaambia Mose na Aroni, “Bwana na awaangalie awahukumu ninyi! Mmetufanya tunuke kwa Farao na maafisa wake, nanyi mmeweka upanga mikononi mwao ili kutuua sisi.”

Mungu Anaahidi Ukombozi

5:22 Kut 1:12; Yos 7:7; Hes 11:11Mose akarudi kwa Bwana na kumwambia, “Ee Bwana, mbona umewaletea watu hawa taabu? Kwa nini basi ukanituma mimi? 5:23 Yer 4:10; 20:7; Eze 14:9Tangu nilipomwendea Farao kuzungumza naye kwa jina lako, amewaletea taabu watu hawa, nawe kamwe hujawakomboa watu wako.”

Read More of Kutoka 5

Kutoka 6:1-12

6:1 Kut 3:20; 11:1; 12:31-39; Kum 5:15Kisha Bwana akamwambia Mose, “Sasa utaona kitu nitakachomfanyia Farao: Kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawaachia watu waende; kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawafukuza waondoke nchini mwake.”

6:2 Kut 3:14-15; 7:5; 8:22; 10:2; 12:12; 14:4, 18; 16:12; Law 11:44; 18:21; 20:7; Isa 41:20; 43:11; 49:23; 60:16; Eze 13:9; 25:17; 36:38; 37:6, 13; Yoe 2:27Pia Mungu akamwambia Mose, “Mimi ndimi Bwana. 6:3 Mwa 7:1; 2Sam 7:26; Za 48:10; 61:5; 68:4; 83:18; 99:3; Isa 52:6; Kut 3:14, 15; Yn 8:58Nilimtokea Abrahamu, Isaki na Yakobo kama Mungu Mwenyezi,6:3 Mungu Mwenyezi hapa ni jina la Kiebrania, El-Shaddai (yaani Mungu Mwenye utoshelevu wote). ingawa sikuwajulisha Jina langu, Yehova, Mimi mwenyewe sikujitambulisha kwao. 6:4 Mwa 6:18; 12:7; 15:18; 17:8; Mdo 7:5; Rum 4:13; Gal 3:16; Ebr 11:8-10Pia niliweka Agano langu nao kuwapa nchi ya Kanaani, ambako waliishi kama wageni. 6:5 Kut 2:23; Mdo 7:34; Mwa 9:15Zaidi ya hayo, nimesikia kilio cha huzuni cha Waisraeli ambao Wamisri wamewatia utumwani, nami nimelikumbuka Agano langu.

6:6 Kut 3:8, 19-20; 12:17, 51; 15:13; 16:6; 20:2; 29:46; Law 22:33; 26:13; Kum 6:12; 7:8; 9:26; Za 9:16; 19:14; 34:22; 74:2; 77:15; 81:10; 105:27; 136:11; Yer 2:6; 15:21; 31:11; 50:34; Hos 13:4; Amo 2:10; Mik 6:4; 1Nya 17:21; Isa 29:22; 35:9; 44:23; 48:20; Mdo 13:17“Kwa hiyo, waambie Waisraeli: ‘Mimi ndimi Bwana, nami nitawatoa mtoke katika kongwa la Wamisri. Nitawaweka huru mtoke kuwa watumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyooshwa pamoja na matendo makuu ya hukumu. 6:7 Mwa 17:7; Kut 34:9; Eze 11:19-20; 39:6; Rum 9:4; 1Fal 20:13, 28; Isa 43:10; Yoe 3:17Nitawatwaa mwe watu wangu mwenyewe, nami nitakuwa Mungu wenu. Ndipo mtajua kuwa mimi ndimi Bwana Mungu wenu, niliyewatoa chini ya kongwa la Wamisri. 6:8 Mwa 12:7; 14:22; Kut 3:8; Yer 11:5; Eze 20:6; Ufu 10:5-6; Za 136:21-22; Law 18:21Nami nitawaleta mpaka nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kumpa Abrahamu, Isaki na Yakobo. Nitawapa iwe milki yenu. Mimi ndimi Bwana.’ ”

6:9 Mwa 34:30; Kut 2:23Mose akawaarifu Waisraeli jambo hili, lakini hawakumsikiliza kwa sababu ya maumivu makuu ya moyoni na utumwa wa kikatili.

Ndipo Bwana akamwambia Mose, 6:11 Kut 3:18“Nenda, mwambie Farao mfalme wa Misri awaachie Waisraeli waondoke nchini mwake.”

6:12 Kut 3:18; 4:10Lakini Mose akamwambia Bwana, “Ikiwa Waisraeli hawatanisikiliza, kwa nini yeye Farao anisikilize mimi, ambaye huzungumza kwa kigugumizi?”

Read More of Kutoka 6