Kutoka 37:1-29, Kutoka 38:1-31 NEN

Kutoka 37:1-29

Sanduku La Agano

(Kutoka 25:10-22)

37:1 Kut 31:2; 30:6; 39:35; Kum 10:3; Kut 35:30; 25:10Bezaleli akatengeneza Sanduku la mbao za mshita: urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu,37:1 Dhiraa moja na nusu ni sawa na mita 1.13. upana wake dhiraa moja na nusu, na kimo chake dhiraa moja na nusu. Akalifunika kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulizungushia ukingo wa dhahabu. Akasubu pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine. 37:4 Hes 4:6Kisha akatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu. 37:5 Hes 1:50; 2Sam 6:3Akaiingiza hiyo mipiko kwenye zile pete katika pande mbili za Sanduku ili kulibeba.

37:6 Kut 26:34; 31:7; Ebr 9:5; Kut 25:17Akatengeneza kifuniko cha upatanisho kwa dhahabu safi: urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu. 37:7 Eze 41:18Kisha akatengeneza makerubi wawili wa dhahabu iliyofuliwa katika miisho ya hicho kifuniko. Akatengeneza kerubi mmoja kwenye mwisho mmoja, na kerubi mwingine kwenye mwisho mwingine; akawatengeneza kuwa kitu kimoja na hicho kifuniko katika miisho hiyo miwili. 37:9 Ebr 9:5; Kum 10:3; Mwa 3:24; Kut 25:22; 1Fal 6:23; 2Nya 3:10; Za 80:1; Eze 1:5-28; 10:1; Yn 1:51; Flp 2:10; 1Tim 3:16; 1Pet 1:12Makerubi hao walikuwa wametandaza mabawa kuelekea juu, wakitia kivuli hicho kifuniko. Makerubi hao walielekeana, wakitazama hicho kifuniko.

Meza

(Kutoka 25:23-30)

37:10 Kum 31:8; Ebr 9:2; Kut 15:23; Mal 1:7, 12Akatengeneza meza ya mbao za mshita yenye urefu wa dhiraa mbili,37:10 Dhiraa mbili ni sawa na sentimita 90. upana wa dhiraa moja,37:10 Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45. na kimo cha dhiraa moja na nusu. Kisha akaifunika kwa dhahabu safi, na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. Pia akatengeneza upapi wenye upana wa nyanda nne,37:12 Nyanda nne ni sawa na sentimita 8. na kuufanyia ule upapi ukingo wa dhahabu kuuzunguka pande zote. Akasubu pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na kuzifungia kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne. 37:14 Ebr 9:4Pete hizo ziliwekwa karibu na ukingo ule ili kuishikilia ile mipiko iliyotumika kuibebea hiyo meza. Mipiko hiyo ya kubebea meza ilitengenezwa kwa mti wa mshita, na ilikuwa imefunikwa kwa dhahabu. 37:16 Kut 25:29Vyombo vyote vya mezani vilitengenezwa kwa dhahabu safi: yaani sahani zake, masinia, na bakuli na bilauri zake kwa ajili ya kumiminia sadaka za vinywaji.

Kinara Cha Taa

(Kutoka 25:31-40)

37:17 Ebr 9:2; Ufu 1:12; Kut 25:31; Law 24:4; 1Nya 28:15; Zek 4:2; Mt 5:15, 16; Yn 5:35; Flp 2:15; 1Pet 2:9; Ufu 1:20Akatengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi iliyofuliwa vizuri katika kitako chake na ufito wake; vikombe vyake vilivyofanana na ua, matovu na maua vilikuwa kitu kimoja. Matawi sita yalitokeza kuanzia ule ufito wa katikati wa kinara cha taa: matawi matatu upande mmoja na matatu upande mwingine. Vikombe vitatu vya mfano wa maua ya mlozi yenye matovu na maua vilikuwa katika tawi moja, vikombe vitatu katika tawi jingine, na vivyo hivyo kwa matawi yote sita yaliyotokeza kwenye kile kinara cha taa. 37:20 Hes 17:8; Yer 1:11Juu ya kinara chenyewe kulikuwepo na vikombe vinne vya mfano wa maua ya mlozi yakiwa na matovu yake na maua yake. Tovu moja lilikuwa chini ya jozi ya kwanza ya matawi yaliyotokeza kwenye kinara cha taa, tovu la pili chini ya jozi ya pili, nalo tovu la tatu chini ya jozi ya tatu, yaani, matawi sita kwa jumla. 37:22 Hes 8:4Matovu na matawi yote yalikuwa kitu kimoja na kile kinara cha taa, yakiwa yamefuliwa kwa dhahabu safi.

37:23 Kut 40:4, 25; Ufu 1:20; 4:5Akatengeneza taa zake saba, na pia mikasi ya kusawazishia tambi, pamoja na masinia, zote kwa dhahabu safi. Akatengeneza kinara hicho cha taa pamoja na vifaa vyake vyote kutumia talanta37:24 Talanta moja ya dhahabu ni sawa na kilo 34. moja ya dhahabu safi.

Madhabahu Ya Kufukizia Uvumba

(Kutoka 30:1-5)

37:25 Kut 30:34-36; Lk 1:11; Ebr 9:4; Ufu 8:3; Kut 27:2; Ufu 9:13; 1Fal 9:25; 1Nya 29:6, 7; Isa 60:6; Mal 1:11; 1Pet 2:5Akatengeneza madhabahu ya kufukizia uvumba kwa mbao za mshita. Ilikuwa ya mraba, urefu na upana wake dhiraa moja, na kimo cha dhiraa mbili, nazo pembe zake zilikuwa kitu kimoja nayo. Akafunika hayo madhabahu juu na pande zote na pia zile pembe zake kwa dhahabu safi, na akayafanyizia ukingo wa dhahabu kuizunguka. Akatengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili ya madhabahu chini ya huo ukingo, zikiwa mbili kila upande, za kushikilia hiyo mipiko iliyotumika kuyabebea madhabahu. 37:28 Kut 25:13Akatengeneza mipiko kwa miti ya mshita na kuifunika kwa dhahabu.

37:29 Kut 31:11; 30:1, 25; 39:38; Isa 61:1; 11:2; Za 133:2; 1Yn 2:20; Za 141:2; Wim 4:14; Mal 1:11; Ebr 5:7; 7:25; Ufu 5:8; 8:3, 4Pia akatengeneza mafuta matakatifu ya upako, na uvumba safi wenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato.

Read More of Kutoka 37

Kutoka 38:1-31

Madhabahu Ya Sadaka Ya Kuteketezwa

(Kutoka 27:1-8)

38:1 Kut 27:1; 2Nya 29:23, 24; Za 51:15-19; Isa 61:8; Eze 44:11; 45:17; Ebr 9:14; 13:10Akatengeneza madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa mbao za mti wa mshita, kimo chake dhiraa tatu;38:1 Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35. nayo ilikuwa mraba, urefu wake dhiraa tano, na upana wa dhiraa tano38:1 Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25. 38:2 2Nya 1:5; 1Fal 7:45Akatengeneza upembe kwenye kila pembe ya hizo pembe nne, ili zile pembe na madhabahu zikawa zimeungana, akafunika madhabahu kwa shaba. 38:3 Kut 31:9; 35:16Akatengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, uma za nyama na vyombo vya kuchukulia moto. Akatengeneza wavu wa shaba chini ya ukingo wa madhabahu ili ufikie nusu ya kimo cha madhabahu. Akasubu pete za shaba za kushikilia ile mipiko kwa ajili ya zile pembe nne za huo wavu wa shaba. Akatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuifunika kwa shaba. Akaiingiza ile mipiko kwenye zile pete, ili iwe pande mbili za madhabahu kwa ajili ya kuibeba. Akaitengeneza madhabahu yenye uvungu ndani yake akitumia mbao.

Sinia La Kunawia

(Kutoka 30:18)

38:8 Kut 30:18; 40:7; Kum 23:17; 1Sam 2:22; 1Fal 14:24; 2Fal 16:17; 2Nya 4:2; Za 26:6; Zek 13:1; Eze 36:25; 2Kor 7:1; Ebr 10:22; 1Yn 5:6Akatengeneza sinia la shaba lenye kitako cha shaba kutoka kwa vioo vya shaba vilivyotolewa na wanawake waliohudumu pale ingilio la Hema la Kukutania.

Ua Wa Hema La Kukutania

(Kutoka 27:9-19)

38:9 Kut 27:9; Za 84:2; 92:13Kisha akatengeneza ua. Upande wa kusini ulikuwa na urefu wa dhiraa mia moja,38:9 Dhiraa 100 ni sawa na mita 45. na ulikuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. Upande wa kaskazini ulikuwa na urefu wa dhiraa mia moja, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.

Upande wa mwisho wa magharibi ulikuwa na upana wa dhiraa hamsini38:12 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5. na ulikuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. Upande wa mwisho wa mashariki jua linakochomoza, pia ulikuwa na upana wa dhiraa hamsini. Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano38:14 Dhiraa 15 ni sawa na mita 6.75. yalikuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yalikuwa upande mwingine wa ingilio la ua, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. Mapazia yote yaliyozunguka ua yalikuwa ya kitani iliyosokotwa vizuri. Vitako vya nguzo vilikuwa vya shaba. Kulabu na tepe juu ya nguzo zilikuwa za fedha, na ncha zake zilifunikwa kwa fedha. Kwa hiyo nguzo zote za ua zilikuwa na tepe za fedha.

38:18 2Nya 3:14Pazia la ingilio la ua lilikuwa la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini kama zile za kwenye ua, na kimo chake kilikuwa dhiraa tano, likiwa na nguzo nne na vitako vinne vya shaba. Kulabu zake na tepe zake zilikuwa za fedha, na ncha zake zilikuwa zimefunikwa kwa fedha. 38:20 Kut 35:18; 38:20; 27:10; 2Nya 3:9; Ezr 9:8; Isa 22:23; Efe 2:21, 22Vigingi vyote vya maskani na vya ua ulioizunguka vilikuwa vya shaba.

Vifaa Vilivyotumika

38:21 Hes 1:50-53; 8:24; 9:15; 10:11; 17:7; 1Nya 23:32; 2Nya 24:6; Mdo 7:44; Ufu 15:5; Hes 4:28-33Ifuatayo ni orodha ya vifaa vilivyotumika kwa ajili ya ujenzi wa maskani, maskani ya Ushuhuda, ambavyo vilitayarishwa na Walawi kama alivyoagiza Mose, chini ya usimamizi wa Ithamari, mwana wa kuhani Aroni. 38:22 Kut 31:2(Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, alifanya kila kitu Bwana alichomwamuru Mose, 38:23 Kut 31:6akiwa pamoja na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, fundi stadi wa kutia nakshi, kubuni michoro, mtarizi kwa rangi ya buluu, ya zambarau, nyekundu na kitani safi.) 38:24 Kut 30:12-16; 12:37; Hes 3:47Jumla ya dhahabu iliyopatikana kutokana na sadaka ya kuinuliwa kwa ajili ya kazi ya mahali patakatifu ilikuwa na uzito wa talanta 29 na shekeli 730,38:24 Talanta 29 na shekeli 730 ni sawa na tani moja. kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.

38:25 Kut 12:37; 30:12Fedha iliyopatikana kutokana na jumuiya ya watu waliohesabiwa ilikuwa yenye uzito wa talanta mia moja na shekeli 1,775,38:25 Talanta 100 na shekeli 1,775 za fedha ni sawa na tani 3.4. kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. 38:26 Kut 30:12-16; 12:36-37; Hes 1:46Kila mtu alitoa beka moja, ambayo ni sawa na nusu shekeli ya fedha, kwa kazi ya mahali patakatifu, kutoka kwa kila mtu aliyekuwa amehesabiwa mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi, ambao jumla yao walikuwa wanaume 603,550. 38:27 Kut 26:19Talanta hizo 100 za fedha zilitumika kusubu vile vitako mia moja kwa ajili ya mahali patakatifu na pazia: vitako mia moja kwa talanta mia, yaani, talanta moja kwa kila kitako. Akatumia zile shekeli hizo 1,775 kutengeneza kulabu za nguzo, kufunika ncha za nguzo na kutengeneza vitanzi vyake.

Shaba iliyopatikana kutokana na sadaka ya kuinuliwa ilikuwa na uzito wa talanta 70 na shekeli 2,400.38:29 Talanta 70 na shekeli 2,400 ni sawa na tani 2.4. Akaitumia hiyo shaba kutengeneza vitako vya ingilio la Hema la Kukutania, madhabahu ya shaba pamoja na ule wavu wake na vyombo vyake vyote, 38:31 Kut 27:19; 2Nya 3:9; Ezr 9:8; Isa 22:23; Efe 2:21, 22vile vitako vya ule ua uliozunguka na vile vya ingilio, na vigingi vyote vya Maskani pamoja na ule ua uliozunguka.

Read More of Kutoka 38