Kutoka 35:1-35, Kutoka 36:1-38 NEN

Kutoka 35:1-35

Masharti Ya Sabato

35:1 Kut 34:32Mose akakusanya jumuiya yote ya Waisraeli na kuwaambia, “Haya ndiyo mambo ambayo Bwana amewaamuru ninyi mfanye: 35:2 Law 23:3; Mwa 2:3; Kut 34:21; Kum 5:13-14; Kut 31:14, 15; Hes 15:32; Lk 13:14Kwa siku sita, mtafanya kazi, lakini siku ya saba itakuwa takatifu kwenu, Sabato ya kupumzika kwa Bwana. Yeyote atakayefanya kazi yoyote siku hiyo ni lazima auawe. 35:3 Kut 16:23Msiwashe moto mahali popote katika makazi yenu siku ya Sabato.”

Vifaa Kwa Ajili Ya Maskani Ya Mungu

(Kutoka 25:1-9)

35:4 Kut 25:1, 2Mose akaiambia jumuiya yote ya Waisraeli, “Hili ndilo Bwana aliloamuru: 35:5 Kut 25:2; 2Kor 9:7Toeni sadaka kwa Bwana kutoka mali mliyo nayo. Kila mmoja aliye na moyo wa kupenda atamletea Bwana sadaka ya dhahabu, fedha na shaba; nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani safi; singa za mbuzi; ngozi za kondoo dume zilizopakwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo;35:7 Pomboo hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili. mbao za mshita; 35:8 Kut 25:6mafuta ya zeituni kwa ajili ya taa; vikolezi kwa ajili ya mafuta ya upako, pamoja na uvumba wa harufu nzuri; vito vya shohamu, na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kisibau na kile kifuko cha kifuani.

35:10 Kut 31:6; 39:43; 1Fal 7:14; Isa 28:26“Wote wenye ujuzi miongoni mwenu inawapasa kuja na kutengeneza kila kitu Bwana alichoamuru: 35:11 Kut 26:1-37; 36:8-38; Mdo 7:44, 45; Ebr 8:2, 5; 9:2-11; Ufu 21:3Maskani pamoja na hema lake na kifuniko chake, vibanio, mihimili, mataruma, nguzo na vitako; 35:12 Kut 25:10-22; 37:1-9; 26:33Sanduku la Agano pamoja na mipiko yake, kifuniko cha kiti cha rehema na pazia linalokizuia; 35:13 Kut 25:23-30; 37:10-16meza na mipiko yake pamoja na vyombo vyake vyote, mikate ya Wonyesho; 35:14 Kut 25:31kinara cha taa kwa ajili ya mwanga pamoja na vifaa vyake vyote, taa na mafuta kwa ajili ya mwanga; 35:15 Kut 30:1-6; 37:26-28; 30:34-38; 26:36; 1Sam 2:28; 1Nya 23:13; 2Nya 29:11; Lk 1:9madhabahu ya kufukiza uvumba pamoja na mipiko yake, mafuta ya upako na uvumba wenye harufu nzuri; pazia la mlangoni mahali pa kuingilia ndani ya maskani; 35:16 Kut 27:1-8; 38:1-7; 30:18madhabahu ya sadaka za kuteketeza pamoja na wavu wake wa shaba, mipiko yake pamoja na vyombo vyake vyote; sinia la shaba pamoja na tako lake; 35:17 Kut 27:9; 38:9-20pazia la eneo la ua pamoja na nguzo zake na vitako vyake, pazia la ingilio la kwenye ua; 35:18 Kut 27:19; 38:20vigingi vya hema kwa ajili ya maskani pamoja na ua na kamba zake; 35:19 Kut 28:2; 31:10; 39:1mavazi yaliyofumwa yanayovaliwa wakati wa huduma katika mahali patakatifu, yaani mavazi matakatifu kwa ajili ya kuhani Aroni, na mavazi kwa ajili ya wanawe watakapokuwa wakihudumu katika kazi ya ukuhani.”

Ndipo jumuiya yote ya Waisraeli ilipoondoka mbele ya Mose, 35:21 Kut 25:2; 36:2; 1Nya 28:2, 9; 29:9; Ezr 7:27; 2Kor 8:12; 9:7na kila mmoja aliyependa na ambaye moyo wake ulimsukuma alikuja na kuleta sadaka kwa Bwana, kwa ajili ya kazi katika Hema la Kukutania, kwa ajili ya huduma yake yote na kwa ajili ya mavazi matakatifu. Wote waliokuwa na utayari, wanaume kwa wanawake, wakaja wakaleta vito vya dhahabu vya kila aina: vipini, vipuli, pete na mapambo. Wote wakatoa dhahabu zao kama sadaka ya kuinuliwa kwa Bwana. 35:23 Kut 39:1; 1Nya 29:8Kila mmoja aliyekuwa na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, au za rangi nyekundu au kitani safi, au singa za mbuzi, ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, au ngozi za pomboo, wakavileta. Wale waliotoa sadaka ya fedha au shaba wakavileta kama sadaka kwa Bwana, na kila aliyekuwa na mti wa mshita kwa ajili ya kazi yoyote ile akauleta. 35:25 Kut 28:3; 31:6; 36:1; 2Fal 23:7; Mit 31:19-24Kila mwanamke aliyekuwa na ujuzi alisokota kwa mikono yake na alileta kile alichosokota, iwe ni nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, au za rangi nyekundu au kitani safi. 35:26 Kut 25:2; 1Nya 29:6-8Wanawake wote waliopenda na waliokuwa na ujuzi wakasokota singa za mbuzi. Viongozi wakaleta vito vya shohamu pamoja na vito vingine vya thamani kwa ajili ya kuweka kwenye kisibau na kwenye kifuko cha kifuani. 35:28 Kut 25:6Wakaleta pia vikolezi na mafuta ya zeituni kwa ajili ya mwanga, kwa ajili ya mafuta ya upako na kwa ajili ya uvumba wenye harufu nzuri. 35:29 Kut 25:2-7; 36:3; 2Fal 12:4Waisraeli wote waume kwa wake waliokuwa wanapenda wakaleta mbele za Bwana kwa hiari yao wenyewe sadaka kwa ajili ya kazi yote ya Bwana aliyokuwa amewaagiza kuifanya kupitia kwa Mose.

Bezaleli Na Oholiabu

(Kutoka 31:1-11)

Kisha Mose akawaambia Waisraeli, “Tazameni, Bwana amemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, 35:31 2Nya 2:7, 14naye amemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, na uwezo na ujuzi katika aina zote za ufundi, ili kubuni michoro ya kupendeza katika ufundi wa dhahabu, fedha na shaba, kuchonga vito na kuvitia mahali, kufanya ufundi kwa mbao, na kujishughulisha na aina zote za ufundi wa kupendeza. 35:34 Kut 31:6; 2Nya 2:14Tena amempa yeye pamoja na Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, uwezo wa kufundisha wengine. 35:35 Kut 31:3, 6; 36:1, 2; 1Fal 7:14; 1Nya 2:14; Isa 28:26; Yak 1:5Amewajaza ustadi wa kufanya kazi za aina zote zifanywazo na mafundi, na wenye kubuni michoro, pia na watarizi kwa rangi za buluu, zambarau, nyekundu na kitani safi, na wafumaji: wote wakiwa mafundi na wabunifu hodari.

Read More of Kutoka 35

Kutoka 36:1-38

36:1 Kut 28:3; 25:8; Ay 32:8; Isa 28:26; Mit 2:6; Kut 25:8; Law 4:6; 19:30; Hes 18:5; 30:8; 1Fal 6:16; Za 96:6; 134:2; Isa 63:18; Eze 5:11; Dan 8:13, 14; Ebr 9:1, 2Kwa hiyo Bezaleli, Oholiabu na kila mtu Bwana aliyempa ustadi na uwezo wa kujua jinsi ya kufanya kazi zote za kujenga mahali patakatifu wataifanya hiyo kazi kama vile Bwana alivyoagiza.”

36:2 Kut 31:2, 6; 25:2; 35:2, 26; 1Nya 29:5Ndipo Mose akawaita Bezaleli na Oholiabu na kila mtu mwenye ustadi ambaye Bwana alikuwa amempa uwezo na mwenye kupenda kuja na kufanya kazi. 36:3 Kut 35:29Wakapokea kutoka kwa Mose sadaka zote ambazo Waisraeli walikuwa wameleta ili kuifanya kazi ya ujenzi wa Mahali Patakatifu. Nao watu wakaendelea kuleta sadaka za hiari kila asubuhi. Ikafika wakati mafundi wote wenye ujuzi waliokuwa wakiifanya kazi yote ya mahali patakatifu wakasimamisha kazi zao, 36:5 2Nya 24:14; 31:10; 2Kor 8:2-3wakaja na kumwambia Mose, “Watu wanaleta vitu vingi kuliko tunavyohitaji kwa ajili ya kazi hii ambayo Bwana ameagiza ifanyike.”

Ndipo Mose akatoa agizo, nao wakapeleka neno hili katika kambi yote: “Mtu yeyote mwanaume au mwanamke asilete tena kitu chochote kwa ajili ya sadaka ya mahali patakatifu.” Hivyo watu wakazuiliwa kuleta zaidi, 36:7 1Fal 7:47kwa sababu walivyokuwa navyo tayari vilitosha na kuzidi kuifanya kazi yote.

Maskani Ya Mungu

(Kutoka 26:1-37)

36:8 Kut 26:1; Ay 32:8; Mit 10:8; 15:14; 21:1; Mwa 3:24; 1Fal 6:23; 2Nya 3:10; Eze 1:5-28; 10:1Watu wote wenye ustadi miongoni mwa wafanyakazi wote wakatengeneza maskani kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi akatirizi makerubi kwenye mapazia hayo. Mapazia yote yalitoshana kwa ukubwa: kila moja lilikuwa na urefu wa dhiraa ishirini na nane,36:9 Dhiraa 28 ni sawa na mita 12.6. na upana wa dhiraa nne36:9 Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8. Wakayaunganisha mapazia matano pamoja, pia wakafanya vivyo hivyo kwa hayo mengine matano. Kisha wakatengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, pia wakafanya vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho. 36:12 Kut 26:5Wakatengeneza pia vitanzi hamsini katika pazia mmoja, na vitanzi vingine hamsini kwenye pazia la mwisho la fungu hilo lingine, nazo vitanzi vyote vikaelekeana. Kisha wakatengeneza vifungo hamsini vya dhahabu, na wakavitumia kufunga na kuunganisha zile fungu mbili za mapazia pamoja ili maskani ipate kuwa kitu kimoja.

36:14 Kut 26:7Wakatengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika maskani. Mapazia hayo kumi na moja yalikuwa na kipimo kimoja, yaani urefu wa dhiraa thelathini,36:15 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5. na upana wa dhiraa nne. Wakaunganisha mapazia matano kuwa fungu moja, na hayo mengine sita kuwa fungu lingine. Kisha wakatengeneza vitanzi hamsini kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu moja, na vivyo hivyo kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu hilo lingine. Wakatengeneza vifungo hamsini vya shaba ili kukaza hema pamoja kuwa kitu kimoja. 36:19 Kut 26:14Kisha wakatengeneza kifuniko cha hema kwa ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo.36:19 Pomboo hapa ina maana ya mnyama mwenye ngozi laini aishiye kwenye milima yenye misitu, au pengine nguva au sili.

36:20 Kut 26:15; 25:5, 10; Hes 25:1; Kum 10:3; Yos 2:1Wakatengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani. Kila mhimili ulikuwa na urefu wa dhiraa kumi,36:21 Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5. na upana wa dhiraa moja na nusu,36:21 Dhiraa moja na nusu ni sawa na sentimita 67.5. zikiwa na ndimi mbili zilizokuwa sambamba kila mmoja na mwingine. Wakatengeneza mihimili yote ya maskani jinsi hii. Wakatengeneza mihimili ishirini kwa ajili ya upande wa kusini wa maskani, na wakatengeneza vitako arobaini vya fedha vya kuweka chini ya hiyo mihimili, vitako viwili kwa kila mhimili, kimoja chini ya kila ulimi. Kwa upande wa kaskazini wa maskani wakatengeneza mihimili ishirini na vitako arobaini vya fedha, viwili chini ya kila mhimili. Wakatengeneza mihimili sita kwa mwisho ulio mbali, yaani upande wa magharibi wa maskani, na mihimili miwili ikatengenezwa kwa ajili ya pembe za maskani za upande uliokuwa mbali. 36:29 Kut 26:24; Za 133:1; Mdo 2:46; 1Kor 1:10Katika pembe hizi mbili mihimili yake ilikuwa miwili kuanzia chini mpaka juu, na ikaingizwa kwenye pete moja; mihimili ya pembe hizi mbili ilifanana. Kwa hiyo kulikuwa na mihimili minane, na vitako kumi na sita vya fedha, viwili chini ya kila mhimili.

36:31 Kut 26:26Wakatengeneza pia mataruma kwa mti wa mshita: matano kwa ajili ya mihimili ya upande mmoja wa maskani, matano kwa ajili ya mihimili ya upande mwingine, na matano kwa ajili mihimili ya upande wa magharibi, mwisho kabisa mwa maskani. Wakatengeneza taruma la katikati, likapenya katikati ya mihimili kutoka mwisho mmoja hadi mwisho mwingine. Wakaifunika hiyo mihimili kwa dhahabu, na wakatengeneza pete za dhahabu za kushikilia hayo mataruma. Pia wakayafunika hayo mataruma kwa dhahabu.

36:35 Kut 39:38; Mt 27:51; Lk 23:45; Ebr 9:5; 6:19; 10:20Wakatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, naye fundi stadi akatirizi makerubi kwenye hilo pazia. Wakatengeneza nguzo nne za mti wa mshita kwa ajili yake na kuzifunika kwa dhahabu. Wakatengeneza kulabu za dhahabu kwa ajili ya nguzo hizo, na kusubu vitako vinne vya fedha. 36:37 Kut 27:16; Law 16:2Kwa ajili ya ingilio la hema wakatengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. 36:38 1Fal 7:16; 2Nya 4:12; Yer 52:22Pia wakatengeneza nguzo tano zenye kulabu. Wakafunika ncha za juu za hizo nguzo pamoja na tepe zake kwa dhahabu, na pia wakatengeneza vitako vyake vitano vya shaba.

Read More of Kutoka 36