Kutoka 33:7-23, Kutoka 34:1-35 NEN

Kutoka 33:7-23

Hema La Kukutania

33:7 Kut 27:21; Mwa 25:22; 1Fal 22:5; Kut 29:42-43; 2Sam 21:1Basi Mose alikuwa na desturi ya kuchukua hema na kuliweka wakfu nje ya kambi umbali kiasi, akaliita “Hema la Kukutania.” Kila aliyekuwa akiulizia shauri kwa Bwana, angelikwenda katika Hema la Kukutania nje ya kambi. 33:8 Hes 16:27Wakati wowote Mose alipokwenda kwenye Hema, watu wote waliinuka na kusimama kwenye maingilio ya mahema yao, wakimwangalia Mose mpaka aingie kwenye Hema. 33:9 Kut 13:21; 19:9; Kum 31:15; 1Kor 10:1; Kut 29:42; 31:18; Za 99:7Kila mara Mose alipoingia ndani ya hema, nguzo ya wingu ingeshuka chini na kukaa kwenye ingilio, wakati Mungu akizungumza na Mose. Kila mara watu walipoona hiyo nguzo ya wingu ikiwa imesimama kwenye ingilio la hema, wote walisimama wakaabudu, kila mmoja kwenye ingilio la hema lake. 33:11 Hes 12:8; Kum 5:4; 34:10; Kut 17:9; Mwa 32:30; Kut 24:13Bwana angezungumza na Mose uso kwa uso, kama vile mtu azungumzavyo na rafiki yake. Kisha Mose angerudi kambini, lakini msaidizi wake kijana Yoshua mwana wa Nuni hakuondoka mle Hemani.

Mose Na Utukufu Wa Bwana

33:12 Kut 3:10; 15:17; Isa 43:1; 45:3; 49:1; Yn 10:14-15; 2Tim 2:19; Mwa 6:8Mose akamwambia Bwana, “Umekuwa ukiniambia, ‘Ongoza watu hawa,’ lakini hujanifahamisha ni nani utakayemtuma pamoja nami. Umesema, ‘Ninakujua wewe kwa jina lako, nawe umepata kibali mbele zangu.’ 33:13 Za 25:4; 27:11; 51:13; 86:11; 103:7; 143:8; Kut 3:7; Kum 9:26-29; Za 77:15; Yoe 2:17Ikiwa umependezwa nami, nifundishe njia zako ili nipate kukujua, nami nizidi kupata kibali mbele zako. Kumbuka kuwa taifa hili ni watu wako.”

33:14 Kut 13:21; Kum 4:37; Isa 63:9; Hag 1:13; 2:4; Kum 12:9-10; 25:19; Yos 1:13; 11:23; 21:44; 22:4; 1Fal 8:56; Isa 63:14; Yer 31:2; Mt 11:28; Ebr 4:1-11Bwana akajibu, “Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.”

33:15 Kut 34:9; 2Fal 13:23; 17:18; 23:27; 24:20; Za 51:11; 80:3, 7; Yer 7:15; 52Kisha Mose akamwambia, “Kama Uso wako hauendi pamoja nasi, usituondoe hapa. 33:16 Kut 34:5; 40:34-35; Hes 9:15; 14:14; Kut 34:10; Law 20:24-26; Hes 23:9; Kum 4:7, 32, 34; 32:9; 33:28Mtu yeyote atajuaje kuwa mimi pamoja na watu wako tumepata kibali mbele zako, usipokwenda pamoja nasi? Ni nini kingine kitakachoweza kututofautisha mimi na watu wako miongoni mwa watu wengine wote walio katika uso wa dunia?”

33:17 Kut 34:28; Kum 9:18, 25; 10:10; Yak 5:16; Mwa 6:8Bwana akamwambia Mose, “Nitakufanyia jambo lile uliloomba, kwa sababu ninapendezwa nawe, nami ninakujua kwa jina lako.”

33:18 Kut 16:7; Yn 1:12; 12:41; 1Tim 6:16; Ufu 15:8Kisha Mose akasema, “Basi nionyeshe utukufu wako.”

33:19 1Fal 19:11; Kut 6:3; 34:5-7; Rum 9:15Ndipo Bwana akasema, “Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza Jina langu, Bwana, mbele ya uso wako. Nitamrehemu yeye nimrehemuye, na pia nitamhurumia yeye nimhurumiaye.” 33:20 Mwa 16:13; Kut 3:6; Kum 5:26; Yn 1:18; Isa 6:5Lakini Mungu akasema, “Hutaweza kuuona uso wangu, kwa kuwa hakuna mtu yeyote awezaye kuniona akaishi.”

Kisha Bwana akasema, “Kuna mahali karibu nami ambapo unaweza kusimama juu ya mwamba. 33:22 Mwa 49:24; 1Fal 19:9; Za 27:5; 31:20; 62:7; 91:1; Isa 2:21; Yer 4:29; Isa 49:2; 51:16; Za 91:4Utukufu wangu unapopita, nitakuweka gengeni kwenye mwamba na kukufunika kwa mkono wangu mpaka nitakapokwisha kupita. Kisha nitaondoa mkono wangu nawe utaona mgongo wangu; lakini kamwe uso wangu hautaonekana.”

Read More of Kutoka 33

Kutoka 34:1-35

Vibao Vipya Vya Mawe

(Kumbukumbu 10:1-5)

34:1 Kut 24:12; Kum 10:2-4; Kut 32:19Bwana akamwambia Mose, “Chonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza, nami nitaandika juu yake maneno yale yaliyokuwa kwenye vile vibao vya kwanza, ulivyovivunja. 34:2 Kut 19:11Uwe tayari asubuhi, kisha upande juu ya Mlima Sinai. Uje mbele zangu kukutana nami huko juu ya mlima. 34:3 Kut 19:13Mtu yeyote asije pamoja nawe, wala asionekane mtu popote juu ya mlima, wala kondoo na mbuzi au ngʼombe wasilishe karibu mbele ya huo mlima.”

34:4 Kum 10:3; Kut 32:15Kwa hiyo Mose akachonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza, naye akapanda juu ya Mlima Sinai asubuhi na mapema, kama Bwana alivyokuwa amemwagiza, akachukua vile vibao viwili vya mawe mikononi mwake. 34:5 Kut 13:21; 19:9; 6:3; 33:19Kisha Bwana akashuka katika wingu akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina lake, Bwana. 34:6 Kut 22:27; Hes 14:20; Za 86:15; 78:18; Rum 2:4; Yer 15:15; Mwa 19:16; Za 61:7; Yoe 2:13; Mao 3:23; Yak 5:11; Hes 14:18Bwana akapita mbele ya Mose, akitangaza, “Bwana, Bwana, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu, 34:7 Kut 20:5-6; Kum 5:10; 1Fal 8:30; Za 86:5; 103:3; 130:4-8; Isa 43:25; Dan 9:9; 1Yn 1:9; Kut 23:7; Yos 24:19; Ay 7:20-21; 10:14; Mik 6:1-16; Nah 1:3akidumisha upendo kwa maelfu, pia akisamehe uovu, uasi na dhambi. Lakini haachi kuadhibu mwenye hatia; huwaadhibu watoto na watoto wao kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata katika kizazi cha tatu na cha nne.”

Mara Mose akasujudu na kuabudu. 34:9 Kut 33:13-15; Hes 11:15; Kut 32:9; Hes 14:19; 1Fal 8:30; 2Nya 6:21; Za 19:12; 25:11; Yer 33:8; Hos 14:2; Kut 6:7; 19:5; Kum 4:20; 7:6; 9:26-29; 14:2; 26:18; 32:9; 1Sam 10:1; 2Sam 14:16; 1Fal 8:51, 53; Za 28:9; 33:12; 74:2; 79:1; 94:14; 106:5, 40; Isa 19:25; 63:17; Yer 10:16; 51:19; Mik 7:18; Zek 2:12Mose akasema, “Ee Bwana, kama nimepata kibali mbele zako, basi Bwana uende pamoja nasi. Ingawa watu hawa ni wenye shingo ngumu, samehe uovu wetu na dhambi yetu, tuchukue kuwa urithi wako.”

Kufanya Agano Upya

(Kutoka 23:14-19; Kumbukumbu 7:1-5; 16:1-17)

34:10 Mwa 6:18; 9:15; 15:15, 18; Kum 5:2-3; Kut 3:20; 33:16Kisha Bwana akasema: “Tazama ninafanya Agano mbele ya watu wako wote. Mbele ya watu wako wote nitafanya maajabu ambayo hayajafanyika katika taifa lolote katika ulimwengu wote. Watu wale mnaoishi miongoni mwao wataona jinsi ilivyo ya kushangaza ile kazi nitakayowafanyia mimi Bwana wenu. 34:11 Kum 6:25; Yos 11:15; Kut 23:28; 32:2Tii yale ninayokuamuru leo. Tazama nawafukuza mbele yako Waamori, Wakanaani, Wahiti, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. 34:12 Amu 2:2; Kut 10:7; 23:32-33Uwe mwangalifu, usifanye agano na wale wanaokaa katika nchi ile unayoiendea, la sivyo watakuwa mtego katikati yako. 34:13 Kut 23:24; Hes 33:52; Kum 7:5; 12:3; Amu 6:26; 1Fal 15:13; 2Nya 15:16; 17:6; 34:3-4; Mik 5:4Bomoa madhabahu yao, vunja mawe yao ya kuabudia na ukatekate nguzo zao za Ashera. 34:14 Kut 20:3-4; Isa 9:6; Kum 4:24Usiabudu mungu mwingine, kwa kuwa Bwana, ambaye jina lake ni Wivu, ni Mungu mwenye wivu.

34:15 Law 17:7; Hes 25:2; Kum 32:17; Za 106:37; Law 27:29; Kum 13:5; 17:2-5; 18:20; 2Nya 15:1334:15 Kum 23:6; Ezr 9:12; Kut 22:20; 32:8; Kum 31:16; Amu 2:17; 2Nya 17:8; 1Nya 17:8; 5:25; 2Nya 11:15; Amo 2:4; Kut 32:6; 1Kor 8:4“Uwe mwangalifu usifanye agano na wale watu wanaoishi katika nchi, kwa maana wakati wanapojifanyia ukahaba kwa miungu yao na kuwatolea kafara, watakualika wewe nawe utakula sadaka za matambiko yao. 34:16 Kum 7:3; 17:17; Yos 23:12; Amu 3:6; 14:2-3; 1Fal 11:1-2; 16:31; Ezr 9:2; 10:3; Neh 10:30; 13:25-26; Kum 7:4; 12:31; 20:18; 1Fal 11:4; 2Fal 21:3-15; Za 106:34-41; Mal 2:11Unapowachagua baadhi ya binti zao kuwa wake wa wana wenu na binti hao wakajifanyia ukahaba kwa miungu yao, watawaongoza wana wenu kufanya vivyo hivyo.

34:17 Kut 20:4; 32:8“Usijifanyie sanamu za kusubu.

34:18 Kut 12:17; Mt 26:17; Lk 22:1; Mdo 12; Kut 12:15; 12:2“Utaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu, kama nilivyokuamuru. Fanya hivi kwa wakati ulioamriwa, katika mwezi wa Abibu, ndio mwezi wa nne, kwa kuwa katika mwezi huo ndipo wewe ulipotoka Misri.

34:19 Kut 13:2“Mzaliwa wa kwanza wa kila tumbo ni mali yangu, pamoja na wazaliwa wa kwanza wote wa kiume wa mifugo yako, ikiwa ni wa ngʼombe au wa kondoo au mbuzi. 34:20 Kut 13:13; 13:2; 22:29; Kum 16:16; Eze 46:9Utakomboa mzaliwa wa kwanza wa punda kwa mwana-kondoo, lakini kama humkomboi, utavunja shingo yake. Utakomboa wazaliwa wako wa kwanza wote wa kiume.

“Mtu yeyote asije mbele zangu mikono mitupu.

34:21 Mwa 2:2-3; Neh 13:15; Isa 56:2; 58; 13; Lk 13:14“Kwa siku sita utafanya kazi, lakini siku ya saba utapumzika, hata ikiwa ni majira ya kulima au ya kuvuna lazima upumzike.

34:22 Kut 23:19; Law 2:12-14; 7:13; 23:10, 17; Hes 28:26; Kut 23:14-16; 34:23“Utaadhimisha Sikukuu ya Majuma kwa malimbuko ya mavuno ya ngano, na Sikukuu ya Mavuno mwishoni mwa mwaka. 34:23 Kut 23:14Mara tatu kwa mwaka wanaume wako wote watakuja mbele za Bwana Mwenyezi, Mungu wa Israeli. 34:24 Kut 23:28; Kum 12:20; 19:8; Ay 12:23; Za 78:55Nitawafukuza mataifa mbele yako na kupanua mipaka ya nchi yako, wala hakuna mtu yeyote atakayeitamani nchi yako wakati unapokwenda mara tatu kila mwaka kuonana na Bwana Mungu wako.

34:25 Kut 23:18; 12:8-10“Usinitolee damu ya dhabihu pamoja na kitu chochote chenye chachu, wala usibakize dhabihu yoyote ya Sikukuu ya Pasaka mpaka asubuhi.

34:26 Kut 22:29; Hes 18:12; Kut 23:19“Leta matunda ya kwanza yaliyo bora zaidi ya ardhi yako katika nyumba ya Bwana Mungu wako.

“Usimchemshe mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.”

34:27 Kut 17:14; Mwa 6:18; 15:18; Kut 24:4; Kum 31:9; Isa 30:8Kisha Bwana akamwambia Mose, “Andika maneno haya, kwa maana kulingana na maneno haya, nimefanya Agano na wewe pamoja na Israeli.” 34:28 Mwa 7:4; Mt 4:2; Lk 4:2; Kum 9:9, 18; Kut 24:18; Ezr 10:6; Kut 31:18; Kum 4:13; 10:4Mose alikuwa huko pamoja na Bwana kwa siku arobaini usiku na mchana bila kula chakula wala kunywa maji. Naye akaandika juu ya vibao maneno ya Agano, yaani zile Amri Kumi.

Mngʼao Wa Uso Wa Mose

34:29 Kut 19:11; 32:15; Za 34:5; Isa 60:5; Mt 17:2; 2Kor 3:7, 13Mose alipoteremka kutoka Mlima Sinai akiwa na vile vibao viwili vya Ushuhuda mikononi mwake, hakujua kuwa uso wake ulikuwa ukingʼaa, kwa sababu alikuwa amezungumza na Bwana. Aroni na Waisraeli wote walipomwona Mose, kuwa uso wake unangʼaa, waliogopa kumkaribia. 34:31 Kut 16:22Lakini Mose akawaita, kwa hiyo Aroni na viongozi wote wa jumuiya wakarudi, naye akazungumza nao. 34:32 Kut 21:1; 35:1-4Baadaye Waisraeli wote wakamkaribia, naye akawapa amri zote Bwana alizompa katika Mlima wa Sinai.

34:33 2Kor 3:13Mose alipomaliza kuzungumza nao, akaweka utaji kwenye uso wake. Lakini kila wakati Mose alipoingia mbele za Bwana kuzungumza naye, aliondoa ule utaji mpaka alipotoka nje. Naye alipotoka nje na kuwaambia Waisraeli lile ambalo ameagizwa, waliona kuwa uso wake unangʼaa. Kisha Mose angeliweka tena utaji juu ya uso wake mpaka alipokwenda kuzungumza na Bwana.

Read More of Kutoka 34