Kutoka 31:1-18, Kutoka 32:1-35, Kutoka 33:1-6 NEN

Kutoka 31:1-18

Bezaleli Na Oholiabu

(Kutoka 35:30–36:1)

Ndipo Bwana akamwambia Mose, 31:2 Kut 36:1-2; 37:1; 38:22; 1Nya 21:20; 2Nya 1:5; Kut 17:10“Tazama, nimemchagua Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda, 31:3 Kut 28:3; 1Fal 7:14; 1Kor 12:4; Kut 35:31; Isa 28:26nami nimemjaza Roho wa Mungu, pamoja na ustadi, uwezo na ujuzi katika aina zote za ufundi, ili kubuni michoro ya kupendeza katika ufundi wa dhahabu, fedha na shaba, kuchonga vito na kuvitia mahali, kufanya ufundi kwa mbao, na kujishughulisha na aina zote za ufundi. 31:6 Kut 36:1-2; 38:23; 1Fal 7:14; 2Nya 2:14Tena nimemteua Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila la Dani, ili kumsaidia. Pia mafundi wote nimewapa ustadi wa kutengeneza kila kitu nilichokuamuru wewe: 31:7 Kut 36:8-38; 37:1-6; 40:20Hema la Kukutania, Sanduku la Ushuhuda pamoja na kiti cha rehema juu yake, pia na vifaa vyote vya kwenye hema, 31:8 Kut 37:10-24; Law 24:4; Kut 37:25-28meza na vifaa vyake, kinara cha taa cha dhahabu safi na vifaa vyake vyote, madhabahu ya kufukizia uvumba, 31:9 Kut 38:3; Hes 4:14; Kut 30:18madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, sinia na kinara chake, 31:10 Kut 28:2; 39:1, 41pamoja na mavazi matakatifu yaliyofumwa ya kuhani Aroni, na mavazi kwa ajili ya wanawe wakati wanahudumu katika kazi ya ukuhani, 31:11 Kut 30:22-32; 37:29; 25:6-9pia mafuta ya upako na uvumba wenye harufu nzuri kwa ajili ya Mahali Patakatifu. Watavitengeneza sawasawa kama vile nilivyokuagiza wewe.”

Sabato

Kisha Bwana akamwambia Mose, 31:13 Kut 20:8; Isa 56:4; Eze 20:12, 20; Kut 29:42; Law 11:44; 20:8; Eze 37:28“Waambie Waisraeli, ‘Ninyi ni lazima mzishike Sabato zangu. Hii itakuwa ni ishara kati yangu na ninyi kwa ajili ya vizazi vijavyo, ili mpate kujua kwamba Mimi Ndimi Bwana, niwafanyaye ninyi watakatifu.

31:14 Kut 35:2; Hes 15:32-36“ ‘Mtaishika Sabato, kwa sababu ni takatifu kwenu. Yeyote atakayeinajisi lazima auawe, yeyote atakayefanya kazi siku hiyo lazima akafie mbali na watu wake. 31:15 Kut 20:8-11; 35:2; Law 16:29; 23:3; Hes 29:7; Mwa 2:3Kwa siku sita, mtafanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika, takatifu kwa Bwana. Yeyote afanyaye kazi yoyote siku ya Sabato ni lazima auawe. 31:16 Kut 20:8Waisraeli wataishika Sabato, kuiadhimisha kwa vizazi vijavyo kuwa Agano la milele. 31:17 Mwa 2:2-3; Kut 20:9; Isa 56:2; 58:13; 66:23; Yer 17:21-22; Eze 20:12, 20Itakuwa ishara kati yangu na Waisraeli milele, kwa kuwa kwa muda wa siku sita Bwana aliumba mbingu na dunia, na siku ya saba akaacha kufanya kazi, akapumzika.’ ”

31:18 Kut 19:11; 24:12; 2Kor 3:3; Ebr 9:4; Kut 32:15-16; 34:1; 28; Kum 4:30; 9:10Bwana alipomaliza kusema na Mose juu ya Mlima Sinai, Mungu akampa vile vibao viwili vya Ushuhuda, vibao vya mawe vilivyoandikwa kwa kidole cha Mungu.

Read More of Kutoka 31

Kutoka 32:1-35

Ndama Wa Dhahabu

(Kumbukumbu 9:6-29)

32:1 Mwa 7:4; Kum 9:9-12; Kut 13:21; 24:18; Mdo 7:40Watu walipoona kuwa Mose amekawia sana kushuka kutoka mlimani, walimkusanyikia Aroni na kumwambia, “Njoo, tutengenezee miungu itakayotutangulia. Kwa maana huyu jamaa yetu Mose aliyetupandisha kutoka Misri, hatujui jambo lililompata.”

32:2 Kut 35:22; Amu 8:24-27Aroni akawajibu, “Vueni vipuli vya dhahabu ambavyo wake zenu, wana wenu na binti zenu wamevaa, mkaniletee.” Kwa hiyo watu wote wakavua vipuli vyao, wakavileta kwa Aroni. 32:4 Kut 20:23; Amu 17:3-4; Isa 30:22; Kum 9:16; Neh 9:18; Za 106:19; Mdo 7:41; Kut 20:23; Isa 42:17; 1Fal 12:28; 14:9; 2Fal 10:29; 17:16; 2Nya 13:8; Hos 8:6; 10:5Akavichukua vile vitu walivyomkabidhi, akavifanyiza kwa kusubu sanamu yenye umbo la ndama, akaichonga kwa kutumia chombo. Kisha wakasema, “Hii ndiyo miungu yenu, ee Israeli, iliyowapandisha kutoka Misri.”

32:5 Law 23:2, 37; 2Fal 10:20; Yoe 2:15Aroni alipoona hili, akajenga madhabahu mbele ya yule ndama na kutangaza, “Kesho kutakuwa na sikukuu kwa Bwana.” 32:6 Kut 20:24; 34:15; Law 3:1; 4:10; 6:12; 9:4; 22:21; Hes 6:14; 25:2; Kum 27:7; Amu 20:26; Eze 43:27; Mdo 7:14; Amu 19:4; Rut 3:3; 1Sam 1:9; 2Sam 11; 11; 1Fal 13:23; 18:42; Neh 8:12; Mhu 5:18; Yer 16:8; 1Kor 10:7Kwa hiyo siku iliyofuata watu wakaamka asubuhi na mapema na kutoa sadaka za kuteketeza na sadaka za amani. Baadaye watu wakaketi kula na kunywa, nao wakasimama, wakajizamisha katika sherehe.

32:7 Kut 33:1; Mwa 6:11-12; Kut 20:8Kisha Bwana akamwambia Mose, “Shuka, kwa sababu watu wako, uliowatoa Misri, wamepotoka. 32:8 Yer 7:26; 16:12; Mal 2:8; 3:7; Kut 20:4; 22:20; 1Fal 12:28; Eze 23:8Wamekuwa wepesi kugeuka na kuacha niliyowaamuru, na wamejitengenezea sanamu ya kuyeyusha yenye umbo la ndama. Wameisujudia na kuitolea dhabihu, nao wamesema, ‘Hii ndiyo miungu yenu, ee Israeli iliyokupandisha kutoka Misri.’ ”

32:9 Kut 33:3-5; 34:9; Kum 9:6, 13; 10:16; 31:27; Amu 2:19; 2Fal 17:14; 2Nya 30:8; 36:13; Neh 9:16; Za 78:8; Mit 29:1; Isa 46:12; 48:4; Yer 7:26; Eze 2:4; Hos 4:16; Mdo 7:51Bwana akamwambia Mose, “Nimeona watu hawa, nao ni watu wenye shingo ngumu. 32:10 1Sam 2:25; Yer 11:14; 7:16; 14:11; Kut 22:24; 33:3-5; Hes 16:21; Kum 9:14-19; Za 106:22; Yer 14:12; Eze 20:13; Hes 14:12; Dan 9:14Sasa niache ili hasira yangu ipate kuwaka dhidi yao, nami nipate kuwaangamiza. Kisha nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa.”

32:11 Kum 9:18; 2Sam 21:1; 2Nya 15:2; Za 9:10; 34:4; 106:23; Isa 9:13; Yer 15:1; Kum 9:26; 1Sam 7:9; Neh 1:10; Za 136:12Lakini Mose akamsihi Bwana Mungu wake, akasema, “Ee Bwana, kwa nini hasira yako iwake dhidi ya watu wako, wale uliowatoa Misri kwa uweza mkuu na mkono wenye nguvu? 32:12 Hes 14:13-16; Kum 9:28; Kut 33:13Kwa nini Wamisri waseme, ‘Ni kwa nia mbaya aliwatoa Misri, ili awaue milimani na kuwafuta usoni mwa dunia’? Achilia mbali hasira yako kali, waonee huruma na usilete maafa juu ya watu wako. 32:13 Kut 2:24; 33:14; Mwa 22:16; Ebr 6:13; Mwa 15:5; 22:17; 12:7; 26:4Wakumbuke watumishi wako Abrahamu, Isaki na Israeli, ambao uliwaapia kwa nafsi yako mwenyewe: ‘Nitawafanya uzao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa wazao wako nchi hii yote ambayo niliwaahidia, nayo itakuwa urithi wao milele.’ ” 32:14 Kum 9:19; 1Sam 15:11; 2Sam 24:16; 1Fal 21:29; 1Nya 21:15; Za 106:45; Yer 18:8; 26:3; Amo 7:3; Yn 3:10Kisha Bwana akawaonea huruma, wala hakuleta juu ya watu wake maafa aliyokuwa amekusudia.

32:15 Kut 31:18; 19:18; Ebr 9:4; Kut 34:4, 29; Kum 9:15; 2Kor 3:3Mose akageuka, akashuka kutoka mlimani akiwa na vibao viwili vya Ushuhuda mikononi mwake. Vilikuwa vimeandikwa pande zote mbili, mbele na nyuma. 32:16 Kut 24:12; 31:18Vibao hivyo vilikuwa kazi ya Mungu; maandishi yalikuwa mwandiko wa Mungu, yaliyochorwa kama muhuri juu ya vibao.

32:17 Kut 17:9; 31:18Yoshua aliposikia sauti za watu wakipiga kelele, akamwambia Mose, “Kuna sauti ya vita kambini.”

Mose akajibu:

“Si sauti ya ushindi,

wala si sauti ya kushindwa;

ni sauti ya kuimba ninayosikia.”

32:19 Kum 9:16; 1Kor 10:7; Ezr 9:3; Za 119:53, 158; Kut 34:1; Kum 9:17Mose alipoikaribia kambi na kuona yule ndama na ile michezo, hasira yake ikawaka, akatupa vile vibao vilivyokuwa mikononi mwake, akavipasua vipande vipande pale chini ya mlima. 32:20 Kut 7:25; 12:3; Yos 7:1; 2Fal 23:6; 1Nya 14:12; 2Nya 34:7; Mik 1:7; Kum 9:21Kisha akamchukua yule ndama waliokuwa wamemtengeneza na kumchoma kwenye moto, kisha akamsaga kuwa unga, akanyunyiza kwenye maji na kuwafanya Waisraeli wanywe.

Mose akamwambia Aroni, “Watu hawa walikufanyia nini, hata ukawaongoza kufanya dhambi kubwa hivyo?”

32:22 Mwa 18:30; Kum 9:24; 28:20; 2Fal 21:15; Ezr 9:13; Neh 9:28; Yer 4:4; 44:3; Eze 6:9Aroni akamwambia, “Usikasirike bwana wangu. Unajua jinsi watu hawa walivyo tayari kwa maovu. 32:23 Mdo 7:40Wao waliniambia, ‘Tufanyie miungu itakayotuongoza. Kwa kuwa huyu jamaa yetu Mose aliyetupandisha kutoka Misri, hatufahamu yaliyompata.’ Kwa hiyo nikawaambia, ‘Yeyote aliye na kito chochote cha dhahabu avue.’ Kisha wakanipa hiyo dhahabu, nami nikaitupa motoni, akatokea huyu ndama!”

32:25 Mwa 38:23Mose akaona kuwa watu wameasi, kwa kuwa Aroni alikuwa amewaacha waasi, na hivyo kuwa kichekesho kwa adui zao. Kwa hiyo Mose akasimama kwenye ingilio la kambi, akasema, “Yeyote aliye upande wa Bwana, aje upande wangu.” Walawi wote wakamjia.

32:27 Hes 25:3-5; Kum 33:9; Eze 9:5Ndipo alipowaambia, “Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Kila mmoja wenu ajifunge upanga wake kiunoni aende huku na huko kambi yote mwisho hadi mwisho mwingine, kila mmoja amuue ndugu yake, na rafiki yake na jirani yake.’ ” Walawi wakafanya kama Mose alivyoamuru, siku ile wakafa watu wapatao 3,000. Kisha Mose akasema, “Leo mmewekwa wakfu kwa Bwana, kwa kuwa mlikuwa kinyume na wana wenu wenyewe na ndugu zenu, naye Mungu amewabariki leo.”

32:30 1Sam 12:20; Za 25:11; 85:2; Law 4:20; 5:6-13; 6:7; Hes 25:13Siku iliyofuata Mose akawaambia watu, “Mmefanya dhambi kubwa. Lakini sasa nitapanda juu kwa Bwana, labda nitaweza kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi yenu.”

32:31 Kut 34:9; 9:18; 20:23Hivyo Mose akarudi kwa Bwana na kumwambia, “Lo! Hawa watu wamefanya dhambi kubwa namna gani! Wamejitengenezea miungu ya dhahabu. 32:32 Hes 14:19; Rum 9:3; Za 69:28; Eze 13:9; Dan 7:10; 12:1; Mal 3:16; Lk 10:20; Efe 4:3Lakini sasa nakusihi, wasamehe dhambi yao; lakini kama sivyo, basi nifute kutoka kwenye kitabu ulichoandika.”

32:33 Kut 17:14; Ay 21:20; Ufu 3:5; Za 9:5Bwana akamjibu Mose, “Yeyote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta kutoka kwenye kitabu changu. 32:34 Kut 15:17; 3:17; 14:19; Mwa 50:19; Kum 32:35; Za 89:32; 94:23; 99:8; 109:20; Isa 27:1; Yer 5:9; 11:22; 23:20; 44:13, 29; Hos 12:2; Rum 2:5-6Sasa nenda, uongoze hao watu mpaka mahali nilipokuambia, naye malaika wangu atakutangulia. Pamoja na hayo, wakati utakapofika wa mimi kuwaadhibu, nitawaadhibu kwa ajili ya dhambi yao.”

32:35 2Sam 12:9Ndipo Bwana akawapiga watu kwa ugonjwa wa tauni kwa sababu ya yale waliyoyafanya kwa ndama yule ambaye alitengenezwa na Aroni.

Read More of Kutoka 32

Kutoka 33:1-6

Amri Ya Kuondoka Sinai

33:1 Kut 13:11; Hes 14:23; Ebr 6:13; Mwa 12:7Kisha Bwana akamwambia Mose, “Ondoka mahali hapa, wewe pamoja na hao watu uliowapandisha kutoka Misri, mpande mpaka nchi niliyomwahidi Abrahamu, Isaki na Yakobo kwa kiapo, nikisema, ‘Nitawapa wazao wenu nchi hii.’ 33:2 Kut 14:19; 23:28; Kum 7:22; Yos 24:11Nitamtuma malaika mbele yenu, naye atawafukuza Wakanaani, Waamori, Wahiti, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. 33:3 Kut 3:8; 32:9-10; Mdo 7:51; Kum 9:6Pandeni mwende katika nchi itiririkayo maziwa na asali. Lakini mimi sitakwenda pamoja nanyi, kwa sababu ninyi ni watu wenye shingo ngumu, nisije nikawaangamiza njiani.”

33:4 Hes 14:39; Ezr 9:3; Es 4:1; Za 119:53; 2Sam 19:24Watu waliposikia habari hizo za huzuni, wakaanza kuomboleza wala hakuna mtu aliyevaa mapambo yoyote. 33:5 Kut 32:9-10Kwa kuwa Bwana alikuwa amemwambia Mose, “Waambie Waisraeli, ‘Ninyi ni watu wenye shingo ngumu. Kama ningefuatana nanyi hata kwa muda mfupi, ningewaangamiza. Sasa vueni mapambo yenu, nami nitaamua nitakalowatendea.’ ” Hivyo Waisraeli wakavua mapambo yao katika Mlima wa Horebu.

Read More of Kutoka 33