Kutoka 27:1-21, Kutoka 28:1-43 NEN

Kutoka 27:1-21

Madhabahu Ya Sadaka Ya Kuteketezwa

(Kutoka 38:1-7)

27:1 Kut 20:24; 40:6; 1Fal 8:64“Jenga madhabahu ya mbao za mti wa mshita, kimo chake kiwe dhiraa tatu;27:1 Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35. itakuwa mraba, urefu wake dhiraa tano,27:1 Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25. na upana wake dhiraa tano. 27:2 Kut 29:12; 30:2; 37:25; Law 4:7; 1Fal 1:50; 2:28; Za 118:27; Yer 17:1; Eze 43:15; Amo 3:14; Zek 9:15Tengeneza upembe kwenye kila pembe ya hizo pembe nne, ili zile pembe na madhabahu ziwe zimeungana, na ufunike madhabahu kwa shaba. 27:3 Hes 7:13; 1Fal 7:40-45; 2Fal 12:13; Hes 4:14; 1Nya 28:17; Yer 52:18Tengeneza vyombo vyake vyote kwa shaba: vyungu vyake vya kuondolea majivu, masepetu, mabakuli ya kunyunyizia, uma za nyama, na vyombo vya kuchukulia moto. Kisha tengenezea hayo madhabahu wavu wa shaba, na utengeneze pete za shaba kwenye kila moja ya hizo pembe nne za huo wavu. Weka wavu huo chini ya ukingo wa madhabahu ili ufikie nusu ya kimo cha madhabahu. 27:6 Kut 25:13-14, 28Tengeneza mipiko ya mti wa mshita kwa ajili ya madhabahu, na uifunike kwa shaba. 27:7 Hes 4:15; Isa 52:11Hiyo mipiko itaingizwa kwenye zile pete ili iwe pande mbili za madhabahu inapobebwa. 27:8 Kut 25:9, 40; Ebr 8:5; Mdo 7:44Tengeneza madhabahu yawe na uvungu ndani yake ukitumia mbao. Utaitengeneza sawasawa na vile ulivyoonyeshwa mlimani.

Ua Wa Kukutania

(Kutoka 38:9-20)

27:9 Kut 35:17; 40:8, 33; Law 6:16, 26; Eze 40:14; 42:1“Tengeneza ua kwa ajili ya Hema la Kukutania. Upande wa kusini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja,27:9 Dhiraa 100 ni sawa na mita 45. na utakuwa na mapazia ya kitani iliyosokotwa vizuri, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo. Upande wa kaskazini utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja, nao utakuwa na mapazia, pamoja na nguzo ishirini na vitako vya shaba ishirini, pamoja na kulabu na tepe za fedha juu ya hizo nguzo.

“Upande wa magharibi wa ua utakuwa na upana wa dhiraa hamsini,27:12 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5. nao utakuwa na mapazia, na nguzo kumi na vitako vyake kumi. Upande wa mwisho wa mashariki jua linakochomoza, ua pia utakuwa na upana wa dhiraa hamsini. Mapazia yenye urefu wa dhiraa kumi na tano yatakuwa upande mmoja wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu. Kutakuwepo tena na mapazia ya dhiraa kumi na tano27:15 Dhiraa 15 ni sawa na mita 6.75. kwa upande mwingine wa ingilio, pamoja na nguzo tatu na vitako vitatu.

27:16 Kut 40:33; 36:37“Kuhusu ingilio la ua, weka pazia lenye urefu wa dhiraa ishirini27:16 Dhiraa 20 ni sawa na mita 9. la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. Pazia hilo litashikiliwa na nguzo nne na vitako vinne. Nguzo zote zinazozunguka ua zitakuwa na tepe na kulabu za fedha, na vitako vya shaba. Ua wa kukutania utakuwa na urefu wa dhiraa mia moja na upana wa dhiraa hamsini, ukiwa na mapazia ya kitani yaliyosokotwa vizuri yenye urefu wa dhiraa tano kwenda juu na vitako vya shaba. Vyombo vingine vyote vinavyotumika katika maskani kwa shughuli yoyote, pamoja na vigingi vyote na hata vile vya ua, vitakuwa vya shaba.

Mafuta Ya Kinara Cha Taa

(Walawi 24:1-4)

27:20 Kut 25:6; Law 24:2“Utawaamuru Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili zile taa ziwake mfululizo. 27:21 Kut 28:43; 29:42; 30:36; 33:7; Law 6:26; 8:3, 31; Hes 31:54; Yos 18:1; 1Fal 1:38-39; Kut 16:34; 25:37; 29:9; 30:21; Law 3:17; 16:34; 17:7; Hes 18:23; 19:21; 1Sam 30:25Katika Hema la Kukutania, nje ya pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, Aroni na wanawe watahakikisha kuwa taa hizo zinawaka kuanzia jioni mpaka asubuhi mbele za Bwana. Hili litakuwa agizo la milele miongoni mwa Waisraeli kwa vizazi vyote vijavyo.

Read More of Kutoka 27

Kutoka 28:1-43

Mavazi Ya Kikuhani

(Kutoka 39:1-7)

28:1 Law 8:30; Za 99:9; Ebr 5; 4; Kut 6:23; 24:9; Law 8:2; 21:1; Hes 18:1-7; Kum 18:5; 1Sam 2:28; Ebr 5:1“Mtwae Aroni ndugu yako aliyeletwa kwako kutoka miongoni mwa Waisraeli, pamoja na wanawe Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. 28:2 Kut 29:5; 31:10; 35:19; Law 8:7-9; 16:32; Hes 20:26-28Mshonee Aroni ndugu yako mavazi matakatifu ili yampe ukuu na heshima. 28:3 Kut 31:6; 35:10, 25, 35; 36:1; 31:3; Kum 34:9; Isa 11:2Waambie mafundi stadi wote niliowapa hekima katika shughuli hiyo wamtengenezee Aroni mavazi hayo, ili awekwe wakfu, anitumikie katika kazi ya ukuhani. 28:4 Kut 25:7; Law 10:5Haya ndiyo mavazi watakayoshona: kifuko cha kifuani, kisibau, kanzu, joho lililorembwa, kilemba na mshipi. Mavazi haya yatashonwa kwa ajili ya ndugu yako Aroni na wanawe ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. 28:5 Kut 25:4-7; 25:4-7Waambie watumie dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani safi.

Kisibau

28:6 Kut 39:2; Law 8:7“Tengeneza kisibau cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa, kazi ya fundi stadi. Kitakuwa na vipande viwili vya mabegani vilivyoshikizwa kwenye pembe zake mbili ili kufungia kisibau. 28:8 Kut 29:5Mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi utafanana nacho: utakuwa kitu kimoja na hicho kisibau, nao utengenezwe kwa dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kwa kitani iliyosokotwa vizuri.

28:9 Wim 8:6; Isa 44:16; Hag 2:23“Chukua vito viwili vya shohamu, na uchore juu yake majina ya wana wa Israeli kufuatana na walivyozaliwa: majina sita katika kito kimoja, na mengine sita katika kito kingine. Yachore majina ya wana wa Israeli juu ya vito hivyo viwili kama vile sonara anavyochonga muhuri. Kisha uvitie vito hivyo katika vijalizo vya dhahabu, 28:12 Kum 33:12; Ay 31:36; Kut 30:16; Hes 10:10; 31:54; Yos 4:7; Zek 6:14; Kut 39:7; Mwa 9:12-17; Kut 12:14; Mk 14:9; Mdo 10:4; 1Kor 11:24, 25na uvifungie juu ya vipande vya mabega ya kisibau yawe kama vito vya ukumbusho kwa wana wa Israeli. Aroni atavaa majina hayo mabegani mwake kama kumbukumbu mbele za Bwana. Tengeneza vijalizo vya dhahabu na mikufu miwili ya dhahabu safi iliyosokotwa kama kamba, na uifunge mikufu hiyo kwenye vijalizo.

Kifuko Cha Kifuani

(Kutoka 39:8-21)

28:15 Kut 25:7; 39:8; Law 8:8; Isa 59:17; 1The 5:7; Efe 6:14“Fanyiza kifuko cha kifuani kwa ajili ya kufanya maamuzi, kazi ya fundi stadi. Kitengeneze kama kile kisibau: cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa. Kitakuwa cha mraba, chenye urefu wa shibiri moja28:16 Shibiri moja ni sawa na sentimita 22. na upana wa shibiri moja, na kikunjwe mara mbili. 28:17 Eze 28:13; Ufu 21:19-20; Kut 30:10; Mal 3:17Kisha weka safu nne za vito vya thamani juu yake. Safu ya kwanza itakuwa na akiki, yakuti manjano na zabarajadi; katika safu ya pili itakuwa na almasi, yakuti samawi na zumaridi; safu ya tatu itakuwa na hiakintho, akiki nyekundu na amethisto; 28:20 Eze 1:16; 10:9; Dan 10:6na safu ya nne itakuwa na krisolitho, shohamu na yaspi. Yote yatiwe kwenye vijalizo vya dhahabu. 28:21 Yos 4:8; Ufu 21:12; Hes 1:5; 2:3; Ufu 7:4-8; 21:12Patakuwa na vito kumi na viwili, kila kimoja kwa jina mojawapo la wana wa Israeli, kila kimoja kichorwe kama muhuri kikiwa na jina mojawapo la yale makabila kumi na mawili.

“Kwa ajili ya kile kifuko cha kifuani, tengeneza mikufu ya dhahabu safi, iliyosokotwa kama kamba. Tengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili yake, uzifungie kwenye pembe mbili za hicho kifuko cha kifuani. Funga ile mikufu miwili ya dhahabu kwenye hizo pete zilizo katika pembe za hicho kifuko cha kifuani, nazo zile ncha nyingine za mkufu zifunge kwenye vile vijalizo viwili, na uzishikamanishe na vile vipande vya mabega vya kile kisibau upande wa mbele. Tengeneza pete mbili za dhahabu, uzishikamanishe kwenye pembe mbili za chini, upande wa ndani wa kifuko cha kifuani karibu na kisibau. Tengeneza pete nyingine mbili za dhahabu, na uzishikamanishe sehemu ya chini ya vipande vya mabega upande wa mbele wa kile kisibau, karibu na pindo juu kidogo ya mshipi wa kiunoni wa kisibau. Pete za kifuko cha kifuani zitafungwa kwenye pete zile za kisibau kwa kamba ya buluu, ziunganishwe na ule mshipi wa kiunoni, ili kifuko cha kifuani kisisogee kutoka kwenye kile kisibau.

28:29 Wim 8:6; Isa 49:15, 16; Ebr 9:24“Wakati wowote Aroni aingiapo Mahali Patakatifu, atakuwa na yale majina ya wana wa Israeli moyoni mwake juu ya kile kifuko cha kifuani cha uamuzi kama kumbukumbu ya kudumu mbele za Bwana. 28:30 Law 8:8; Hes 27:21; Kum 33:8; 1Sam 28:6; Ezr 2:63; Neh 7:65Pia weka Urimu na Thumimu28:30 Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha. ndani ya kifuko cha kifuani, yawe juu ya moyo wa Aroni kila mara aingiapo mbele za Bwana. Kwa hiyo siku zote Aroni atakuwa na uwezo kufanya maamuzi kwa ajili ya wana wa Israeli mbele za Bwana.

Mavazi Mengine Ya Kikuhani

(Kutoka 39:22-31)

28:31 Kut 39:22; Law 8:7; 2Sam 6:14; Hos 3:4“Shona joho la kisibau lote kwa kitambaa cha rangi ya buluu tupu, na katikati uweke nafasi ya kuingizia kichwa. Kutakuwa na utepe uliofumwa, unaofanana na ukosi kuizunguka nafasi hiyo, ili isichanike. 28:33 Hes 13:23; 1Sam 14:2; 1Fal 7:18; Wim 4:3; Yer 52:22; Yoe 1:12; Hag 2:19Tengeneza makomamanga ya nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu kuzunguka pindo la hilo joho, na uweke pia vikengele vya dhahabu kati ya hayo makomamanga. Hivyo vikengele vya dhahabu na makomamanga vitapishana kuzunguka upindo wa joho lile. Ni lazima Aroni alivae anapofanya huduma. Sauti ya hivyo vikengele itasikika anapoingia na kutoka Mahali Patakatifu mbele za Bwana, ili asije akafa.

28:36 Kut 29:6; Law 8:9; Zek 14:20; Kut 39:30; 1Nya 16:29; Za 29:2; 93:5; Ebr 4:15; 7:26“Tengeneza bamba la dhahabu safi na uchore juu yake maneno haya kama vile muhuri huchorwa: Mtakatifu kwa Bwana. Lifunge hilo bamba kwa kamba ya buluu kwenye kilemba, nalo ni lazima liwe mbele ya kilemba. 28:38 Law 5:1; 10:17; 16:22; 22:9, 16; Hes 18:1; Isa 53:5-11; Eze 4:4-6; Ebr 9:28; 1Pet 2:24; Mwa 32:20; Law 22:20, 27; 23:11; Isa 56:7Aroni alivae bamba hilo kwenye paji la uso wake, naye atachukua hatia kuhusu sadaka takatifu za Waisraeli wanazoweka wakfu, sadaka za aina yoyote. Litakuwa kwenye paji la uso wa Aroni daima ili zikubalike kwa Bwana.

28:39 Kut 29:6; Law 16:4; Eze 24:17-23; 44:18“Fuma koti la kitani safi na ufanye kilemba cha kitani safi. Mshipi uwe ni kazi ya mtarizi. 28:40 Kut 29:8-9; 39:41; 40:14; Law 8:13; Eze 44:17Watengenezee wana wa Aroni makoti, mishipi na kofia, ili kuwapa ukuu na heshima. 28:41 Kut 40:13; 29:7; Law 6:20; 10:7; 21:12; Hes 35:25; Kut 29:7-9; 30:30; 40:15; Law 4:3; 6:22; 8:1-36; Hes 3:3; Ebr 7:28Baada ya kumvika Aroni ndugu yako pamoja na wanawe nguo hizi, watie mafuta na kuwabariki. Waweke wakfu ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.

28:42 Law 6:10; 16:4, 23; Eze 44:18“Watengenezee nguo za ndani za kitani zitakazofunika mwili, kutoka kiunoni hadi mapajani. 28:43 Kut 27:21; 30:20-21; Law 16:13; 22:9; Hes 1:51; 4:15-20; 18:22Aroni na wanawe ni lazima wavae haya kila wanapoingia katika Hema la Kukutania au wanaposogelea madhabahu wakati wa kutoa huduma katika Mahali Patakatifu, ili wasije wakafanya kosa wakafa.

“Haya yawe maagizo ya kudumu kwa Aroni na vizazi vyake.

Read More of Kutoka 28